Shida sio kuvaa Masks: aina namna...

unprejudiced

JF-Expert Member
Jan 27, 2017
2,752
2,000
Nawasalimu kwa jina la JMT. Kazi na iendelee.

Naona huko nyumbani wakubwa wanajitajidi kuvaa masks. Na Pia kama Leo katika kikao cha RJMT na wazee, masks zilitamalaki. Hongereni Ni hatua as Long as mnapenda kulindana hasa wazee wetu.

Huku ulaya namna ya watu walivyojua kuhusu masks mwaka Jana na Leo Ni tofauti. Sasa mambo ya vitambaa marufuku na hata Hizo masks tulizozoea kwenda NAzo ICU. Hii imetokana na maambukizi kutokupungua na wanasayansi wakagundua sababu mojawapo ni uimara na quality ya masks. Sasa Ni lazima kuvaa masks zenye prescribed standard. Ambazo ni gharama hata kwa Sisi wa huku kama itabidi uvae Daily.

Lakini la ziada, likagunduliwa Pia umbali Kati ya mtu na mtu katika kupunguza uwezekano wa maambukizi. Sasa Ni 2 meters Social distancing na inapendeza mnaokaa pamoja, basi muwe wa Familia moja Na sio mwingine wa kivule mwingine wa masaki.

Ugumu kwa nchi kama yetu, Ni gharama za masks na Pia aina ya maisha ya wengi wetu hasa makazi na kipato. Ni ngumu sana kuweza kupambana na corona kwa mtindo wa wazungu. La msingi kila mtu anayejihisi na hali ndivyo sivyo ajitahidi kuwalinda wengine, na Kazi ziendelee.

Msipende kuiga mana haitawezekana. Watu watakufa kwa njaa wakati corona inategemea vitu vya ziada mwilini kuweza kukuondoa. Na Ukiwa na njaa na hiyo corona itapita tu na wewe.

Tanzania kwanza. Tuipende nchi yetu. Adui wa Tz. Ni adui yetu.
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
8,805
2,000
Sasa hivi tunasubiria ripoti ya wataalamu mama kishasema iko karibu.

Haya ya kina nyungu, maombi na juice juice tusameheane kwanza.

Inaweza kuwa huu ugonjwa hauwahusu wanaopiga kelele za kudunisha hatari yake.

Ujerumani vizingiti vyote vya Corona sasa haviwahusu wale waliokwisha pata chanjo na maisha yanasonga.

Maisha ni pamoja na kujifunza kwa wengine na hasa waliotutangulia.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom