Shida na matatizo tuliyonayo watanzania kwa sasa ni haki yetu-tusilalamike | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shida na matatizo tuliyonayo watanzania kwa sasa ni haki yetu-tusilalamike

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mambomoto, Jan 14, 2012.

 1. m

  mambomoto JF-Expert Member

  #1
  Jan 14, 2012
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 327
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Nalazimika kusema hivyo kwa kuwa Watanzania tumekuwa watu wa kulalamika na kusahau na siku zinasonga mbele. Mtanzania ni mtu ambaye anaamini kila mtu ataubeba mzigo wake peke yake. Ndiyo maana hata linapotokea jambo muhimu lenye maslahi kwa taifa bila kujali chama, dini, kabila, rangi nk Watanzania tumekuwa wagumu sana sana kuungana na kuwa kitu kimoja. Isitoshe tumekuwa watu wa kulalamika chinichini na mwishowe tunanyamaza na siku zinasonga mbele katika hali mbaya na ya kukatisha tamaa mno. Maisha ndugu zangu yanapanda kila siku tena kwa makusudi utafikiri tunakisa nayo. Jambo la kujiuliza kweli watanzania miaka 50 tangu tupate uhuru hakuna afadhali ya maisha chini ya chama cha CCM???. Mbona wao wananeemeka na sisi tunateseka? Kweli ndugu zangu bila kujali tofauti zetu tunahitaji mabadiliko kama kweli tunataka kupona sisi na vizazi vyetu. Wakati wa uchaguzi wengi hatuna umakini wa nini tufanye. Kilio kingine ni baadhi ya wanawake wa Tanzania ambao ndiyo janga tulilo nalo kwa sasa katika kuikomboa nchi hii. Wanawake/ Mama zetu/ Dada zetu kweli mmekuwa mkituangusha sana wakati wa uchaguzi kwa Khanga, Vitambaa, T-shirt, Vilemba, Pilau amabazo mkishapewa tu mnaimba na kuimba kutwa nzima mwishoni mnauza uhuru wenu. Je leo hii matatizo ugumu wa maisha tulionao tumlilie nani?? Hii ni haki yetu hatupaswi kulalamika
   
 2. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #2
  Jan 14, 2012
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,659
  Likes Received: 4,755
  Trophy Points: 280
  Swadakta!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 3. K

  Kubingwa JF-Expert Member

  #3
  Jan 14, 2012
  Joined: Apr 23, 2010
  Messages: 502
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Waambie wengine wamo humu humu wa pilau,kofia,khanga na posho
   
Loading...