Shida na kero ya ukosefu wa maji safi na salama katika maeneo mengi katika nchi yetu

Apr 12, 2018
71
33
Kwa ujumla kutokea tupate uhuru shida na uhaba wa maji safi na salama kwa matumizi ya binadamu na mifugo yetu ni moja ya changamoto kubwa na hili halina ubishi.

Kutokea tupate Uhuru serikali imepata mafanikio kiasi katika baadhi ya sector kama vile mwenye sector ya elimu kwani idadi ya wasiojua kusoma na kuandika imepungua na elimu ya msingi inatolewa bure kwa sasa. Pia sector ya afya kunamafanikio yamepatika kwani huduma zimesogezwa kW wananchi ingawa bado kunachangamoto .

NB; Ikumbukwe tu kuwa mafanikio katika sector zingine yanakwamiahwa kwa kiasi kikubwa na ukosefu wa maji safi na salama kwa matumizi ya binadamu na mifugo yetu kwani mtu hukikuta akitumia mda mwingi sana kutafuta maji takribani 2/3 ya siku na baadhi ya sehemu mfano nitokeapo Mimi huwa tinatumia siku nzima kutafuta maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na kwaajili ya mifugo.

Kwa maana hiyo kupitia ukosefu wa maji safi na salama ndio maana tunashindwa kutokomeza magonjwa mengi yatokanayo matumizi ya maji yasiyo safi na salama Na hii huathiri afya za watu na huenda moja kwa moja kuathiri elimu na uchumi wa watu na badae umaskini kuendelea . Kwa hiyo swala hili la ukosefu wa maji safi na salama lafaa kuagaziwa kwa mapana na kuvhukuliwa kwa mkazo wa hili ya juu sana kuliko ilivyokuwa au ilivyo sasa kwani inaadhari kubwa sana kwa MTU mmoja mmoja na kwa taifa kwa ujumla .

Kwa miaka yote hii tokea Uhuru shida hii ya maji haijaweza kutatuliwa ingawa serikali imejitahidi sana kujaribu kuitafutia ifumbuzi kero hii lakini bado tatizo ni kubwa sana.

Wanasiasa wengi sana wamekuwa wakitoa ahadi ya kutatua kero hii bila mafanikio. Nadhani wengi wetu ni mashahidi wa hili katika maeneo tunapo ishi .

TUJADILI KWA PAMOJA SWALI LIFUATALO KARIBUNI SANA

Je, ni nini kifanyike ili kuweza kulitatua tatizo hili ambalo limetuchukua taktibani nusu karne bila kulipatia ufumbuzi .
 
Back
Top Bottom