Shibuda matatani....atuhumiwa kukashifu............

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,468
911,173
Mwenyekiti CCM atishia kumshitaki Shibuda kwa kumkashifu

Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 8th December 2010 @ 21:25


MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja, ameonya kuwa atamfikisha mahakamani Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda (Chadema), iwapo ataendelea kumkashifu.

Mbali ya hatua hiyo, amewataka wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kupuuza maneno na tuhuma zinazotolewa dhidi yake kwa kuwa hazina ukweli na kwamba anataka kujipatia umaarufu kupitia jina lake.

“Namuonya aache kunikashifu hadharani, kama anataka tufanye siasa na sio kutoa matusi.

Akiendelea na kashfa hizo nitamfikisha mahakamani,” alisema Mgeja na kuwa anashangazwa na maneno yanayotolewa na mbunge huyo na ambayo yanaonesha ana chuki binafsi.

“Kwa sasa namsamehe kwa kuwa ukubwa ni jalala, lakini akitoa kashfa nyingine dhidi yangu namfikisha mahakamani,” alionya Mgeja.

Mapema wiki hii, Shibuda alikaririwa akisema katika mkutano wa hadhara mjini Kahama kuwa CCM ya sasa siyo ile iliyoachwa na Mwalimu Nyerere na kuwa kwa Shinyanga anayesababisha isifanye vizuri ni Mgeja.

Mgeja alisema kwa sasa CCM inajipanga kufanya tathmini kuhusu hali ilivyokuwa katika Uchaguzi Mkuu na imejikita kutekeleza ahadi kama ilivyotoa kwenye Ilani huku kubwa ikiwa ni kutatua kero za wananchi.

Kuhusu madai kuwa CCM ya sasa siyo aliyoiacha Nyerere, Mgeja alisema CCM ya sasa ndiyo ile ile iliyoachwa na Mwalimu na kuwa mambo mengi ya msingi aliyokuwa akipigania muasisi huyo, yametekelezwa kwa kiwango cha hali ya juu.

“Mwalimu alipigania elimu, afya, muungano, kujitegemea….mambo hayo yanatekelezwa kwa vitendo na kwa kasi kubwa. Wanafunzi wanaoanza elimu ya msingi, wanaoingia sekondari na

vyuo vikuu wameongezeka maradufu, huduma ya afya, miundombinu na nyinginezo zimeimarishwa, achilia mbali amani na utulivu uliopo,” alisema Mwenyekiti huyo.

Alisema CCM ndiyo ile ile na fikra ndizo zile zile zinazoendelezwa za kujali maslahi ya wananchi, na ndiyo maana wamekichagua na kukipa ridhaa ya kuongoza Dola.

Kuhusu madai ya CCM Mkoa wa Shinyanga kupoteza majimbo, Mgeja alisema hilo sio jambo la kushangaza katika siasa za ushindani wa vyama vingi na kutoa mfano wa hivi karibuni ambapo chama tawala cha Democratic cha Marekani kilipoteza Jimbo kwa Republican na kwa Tanzania, siyo Shinyanga pekee yake iliyopoteza majimbo, bali ipo mikoa mingine.
 
nahisi, Shibuda bado anaimezea mate CCM ijapokuwa amekihama chama hicho! Inawezeka yupo tayari hata kurudi huko pale maslahi yakiwa mazuri. Chadema kuweni makini nae yupo mguu nje mguu ndani si mwenzenu huyu.
 
Kama ana facts ni haki yake kwenda mahakamani. Wengi wanadhani mahakamani nia sehemu ya kwenda kumfunga tu wakisahau kwamba mahakaa husikiliza pande zote.
 
Back
Top Bottom