Shibuda kumshtaki Wenje kwa wazee.................... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shibuda kumshtaki Wenje kwa wazee....................

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Rutashubanyuma, Dec 12, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 12, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,887
  Likes Received: 416,601
  Trophy Points: 280
  Shibuda kumshtaki Wenje kwa wazee
  Saturday, 11 December 2010 21:01

  Mwandishi wetu
  MGOGORO ndani ya Chadema umechukua sura mpya baada ya Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda kuamua kumshtaki kwenye baraza la wazee wa Mwanza Mbunge mwenzake wa Nyamagana, Ezekiel Wenje kwa madai ya kumdhalilisha.

  Hatua hiyo ya Shibuda inakuja huku hali ndani ya chama hicho ikiwa bado tete iliyoibuka baada ya baadhi ya wabunge wa chama kushindwa kushiriki katika mgomo wa kususia hotuba ya Rais Jakaya Kikwete bungeni.

  Mgogoro huo ndio unaodaiwa kuwa ulisababisha juzi wabunge wa chama hicho kupiga kura ya kutokuwa na imani na Naibu Katibu Mkuu wake, Zitto Kabwe na kumvua wadhifa wa Naibu Kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni.

  Akizungumza na Mwananchi Jumapili jana, Shibuda alisema Wenje alimdhalilisha wakati wa kikao cha chama hicho kilichofanyika Bagamoyo mkoani Pwani na kujadili mambo mbalimbali likiwamo la baadhi ya wabunge wa chama hicho kutoonekana bungeni wakati wenzao walipotoka nje kususia hotuba ya Rais Kikwete.

  Shibuda ambaye hakuwepo bungeni wakati wabunge wengine wakitoka bungeni, baadaye akaonekana katika halfa ya kumpongeza Waziri Mkuu Pinda, alisema Wenje alimwambia kilichomfanya ahudhurie sherehe hiyo ilikuwa ni ulafi wake wa nyama.

  Alisema kitendo hicho kilimuudhi na akamwomba aliyekuwa Mwenyekiti wa kikao hicho, Freeman Mbowe amwonye Wenje aache kutumia lugha ambazo sio za kistarabu.

  Kwa mujibu wa Shibuda, Mbowe hakumwonya Wenje na hata Mnadhimu Mkuu wa kambi ya Upinzani bungeni ambaye Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lisu naye hakusema chochote huku baadhi ya wabunge wabunge katika kikao hicho wakishangilia kauli za Wenje.

  “Nitazungumza na baraza la wazee wa Mwanza nawajua, niwaeleze tabia na desturi za ulevi wa madaraka ya ubunge alizonazo Wenje za kugeuka mtambo wa kuzalishia matusi, kejeli na fedheha kwa wabunge wenzake,” alisema Shibuda na kuongeza.

  “Kwa mujibu wa mila na desturi za kiafrika, umri nilionao si wa kutukanwa matusi mazito na kijana mdogo anayelingana na mtoto wangu,” aliongeza Shibuda.

  Alieleza kwa asili yeye ni Msukuma anayetoka katika jamii ya wafugaji ambao chakula chao kikuu ni nyama, hivyo hawezi kuhudhuria sherehe kwa ajili ya ulafi wa nyama.

  Shibuda alisema aliamua kwenda kwenye sherehe hiyo ili kukutana na wabunge wenzake kubadilishana uzoefu wa kumaliza mtataizo ya wananchi katika majimbo yao.

  Hata hivyo, Wenje alipopigiwa simu kuelezea suala hilo alisema hangweza kuzungumza alikuwa kwenye kikao na kwamba apigiwe baadaye.

  Shibuda ambaye katika bunge lililopita alikuwa mbunge wa CCM, alimshangaa Wenje kuwa na tabia hiyo na kueleza kuwa hata wabunge wa Mwanza mjini yaani wa majimbo ya Ilemela na Nyamagana waliopita hawakuwa na hulka hiyo.

  Alisema alichokifanya mbunge mwezake ni kuvunja utaratibu wa Bunge ambao unamtaka mbunge kuwa na staha mbele ya wabunge wengine na umma kwa ujumla.

  Mbunge huyo alisema mbunge ni balozi wa chombo kinachosimamia maslahi ya wananchi ni vema akawa mstaarabu ili kulinda heshima ya chombo hicho.

  Alifafanua kuwa wananchi wa Mwanza wameonyesha kutokuwa ubaguzi wa aina yoyote kwa kuwachagua wabunge ambao si wenyeji wa mji huo akiwemo yeye (Wenje ), ambaye ni asili yake ni Tarime.

  Akamtaka katumia vyema heshima aliyopewa na wananchi wa Mwanza kuwakilisha matatizo yao bungeni badala ya kugeuka kuwa mtoa matusi kwa wabunge wenzake.

  Wabunge wa Chadema Tangu Desemba 9 hadi 10 mwaka huu walikuwa wakikutana mjini Bagamoyo kujadili mmabo mbalimbali ikiwamo kuteua wabunge watano ambao wataingia katika kikao cha kamati kuu.

  Joto la mgogoro lilianza Novemba 18, mwaka huu baada ya wabunge hao kususia kusikiliza hotuba ya Rais Jakaya Kikwete alipokuwa akihutubia kwa mara ya kwanza bunge la kumi.

  Wakiongozwa na Kiongozi wa kambi ya Upinzani Bungeni, Mbowe, wabunge hao waliinuka na kutoka nje ya ukumbi wa Bunge, kwa madai kuwa mfumo uliompa ushindi Rais Kikwete ni mbaya, hivyo wanataka katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.

  Hata hivyo, wabunge tisa wa chama hicho, akiwemo Zitto na Shibuda hawakuwepo bungeni siku hiyo, kitendo kilichotafsiriwa na uongozi wa chama hicho kuwa ni usaliti.
  Novemba 15, mwaka huu Chadema ilitoa msiamo wa kutotambua ushindi wa Rais Kikwete kwa maelezo kuwa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31 mwaka ulikuwa na kasoro kwa sababu katiba mbovu na kwamba uchaguzi huo ulijaa kasoro nyingi na kura zao zilichakachuliwa.

  Viongozi hao wa Chadema walitaka iundwe tume huru kuchunguza mwenendo mzima wa uchaguzi na namna Idara ya Usalama wa Taifa ilivyohusika katika uchaguzi huo.
   
 2. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #2
  Dec 12, 2010
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Shibuda rejea kauli ya JK...Kundi la MAJUHA
   
 3. s

  superfisadi JF-Expert Member

  #3
  Dec 12, 2010
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 552
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  sitaki nataka ww mmekubaliana ukakiuka unategemea afikirie nini maadam mnafahamiana na anajua weakness yako ni minofu akisema ni dharau , jiheshimu hy kijana atakuheshimu tu ila pole vijana wa sasa ndivyo walivyo
   
 4. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #4
  Dec 12, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,497
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Lkn Mzee Shibuda nawewe ulienda kufanyanini kule wakati chama kimesusa? Kweli ilikuwa sio kaulinzuri, uroho wa nyama?! tehetehetehe!, wenje bwana kumbe anamatusi ee! Lkn mzee J Shibuda ungeuchuna tu usingekimbilia kwenye media...ni kama unasambaza zaidi tusi.
   
 5. i

  ifolako Member

  #5
  Dec 12, 2010
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Genge la wahuni tuu hilo!
   
 6. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #6
  Dec 12, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  kweli kabisa, huwa hawaachi ujuha na ulafi wa nyama
   
 7. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #7
  Dec 12, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  the best quote....... Kumbe shibuda na umri wote ule bado ni mlafi wa nyama??

  Ukistaajabu ya JK utayaona ya Shibuda

  SHibuda nimeamua kununua kilo tano za nyma nikuletee wapi mze wangu na wewe ufaidi, ule na upige picha na uwapendao aisee?
   
 8. m

  mams JF-Expert Member

  #8
  Dec 12, 2010
  Joined: Jul 19, 2009
  Messages: 616
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Usingeenda kwenye sherehe usingeambiwa mroho wa minofu, wabunge wasingemshangilia Wenje, mwenyekiti Mbowe na Lissu wanguchukua hatua. Utakapo mshitaki kwa wazee wa Mwanza jaribu uanze na kwa nini ulienda kwenye sherehe tofauti na msimamo wa chama chako.
   
 9. 3D.

  3D. JF-Expert Member

  #9
  Dec 12, 2010
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,022
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wazee Baregu, Makani, Mtei inabidi wafanye kazi kubwa hapa. Nadhani wanapuuzia mambo mengi ambayo ni ya msingi. NItaandika barua rasmi kwa CHADEMA juu ya hili.
   
 10. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #10
  Dec 12, 2010
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Lol! kweli hiki ni kijiwe cha udaku...
   
 11. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #11
  Dec 12, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Pole Mzee Shibuda, lakini nina uhakika hata kule ccm ulikotoka mlikuwa na maamuzi ya chama, je, huku umehamia kwanye kichaka? Jadilini mabo ya msingi juu ya watanzania na si minofu ya nyama!
   
 12. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #12
  Dec 12, 2010
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,256
  Likes Received: 2,079
  Trophy Points: 280
  Aaah! Kubadishana mawazo?
  Vijana wa siku hizi wako wazi sana uwe makini, hawataki kuficha au kuogopa. Ukweli ni lazima usemwe.
  Du! Unataka kujadiliwa pia na wewe kwenye media kwa vikesi mbuzi kama hivyo?
   
Loading...