Shibuda kufukuzwa CHADEMA

Faty

Member
Mar 28, 2012
11
0
Ni vizuri akaonywa kwa mara nyingine na aeleze lengo hasa ni nini? je ni chama gani makini unaweza kufanya vitu ambavyo ni nje ya katiba ya chama.................. ikiwa ni vipi avalishwe gamba.
 
May 18, 2012
30
0
jamani lakini kuna vitu viwili tunatakiwa kutofautisha shibuda kama shibudas anawezaa kuongea mawazo yake binafsi nini anwazia katika ulimwengu wa siasa.
ila shibuda kama mbunge ni lazima aongee vitu vinavyo kwenda sambamba na chama chake
suali kwenu jee shibuda aliongea kama nani? chadema muwe makini sana wanajamii wasiwapotee malengo
 

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,864
1,225na Nasra Abdallah

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kuwa kitaunda kamati maalum ya kushughulikia tuhuma dhidi ya Mbunge wa Maswa Mashariki, John Shibuda (CHADEMA), ambapo akipatikana na hatia atakabiliwa na adhabu nzito ikiwemo kuvuliwa uanachama.


Habari za kuaminika kutoka ndani ya chama hicho na kuthibitishwa na mmoja wa maafisa wake waandamizi, zimesema kuwa kamati hiyo inayotarajiwa kukutana wakati wowote kuanzia sasa inaongozwa na mjumbe wa Kamati Kuu, Prof. Abadallah Safari.

Imedaiwa kuwa kamati hiyo maalumu itamhoji Shibuda kabla ya kutoa mapendekezo yake katika kikao cha baraza kuu ambapo kuna habari kuwa litachukua uamuzi mzito na mgumu dhidi ya mbunge huyo, ingawa imedaiwa kuwa naye atakuwa na haki ya kukata rufaa.


Hii itakuwa mara ya pili kwa kamati hiyo kumjadili Shibuda kutokana na kupingana mara kadhaa na msimamo wa CHADEMA katika masuala ya msingi ya sera na itikadi, likiwemo suala la nidhamu.


Hivi karibuni, akiwa mjini Dodoma, Shibuda alikiuka utaratibu wa chama chake na kukidhalilisha hadharani mbele ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM waliokuwa katika semina, akidai kuwa hajaona chama kinachoweza kuongoza nchi zaidi ya chama tawala.


Katika Bunge la bajeti la mwaka jana wakati wabunge wote wa CHADEMA wakipinga na kususia posho, Shibuda alipingana nao ndani na nje ya Bunge, akidai kuwa ilikuwa ni halali yao kupokea posho hizo alizozibandika jina la ‘ujira wa mwina’


Akizungumza na Tanzania Daima, mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Arusha na Mjumbe wa Baraza Kuu, Samson Mwigamba, alisema kuwa kitendo alichokifanya Shibuda hakikubaliki kwa mujibu wa katiba yao, ingawa anaweza kudai ni haki yake ya Kikatiba.


Mwigamba alisema katiba inamtaka kila mwanachama wao kukipigania, kukitetea na kukieneza chama chao kwa lengo la kushika dola.


Hivyo kitendo cha Shibuda kudai kwamba mpaka sasa hajaona chama kinachoweza kushika dola, ni kukiuka katiba jambo ambalo linaweza kumfukuzisha moja kwa moja uanachama.


Kwa mujibu wa katiba ya chama hicho Shibuda alipaswa kupinga mapendekezo hayo ndani ya vikao vya chama ambapo ndipo hoja ilipoamuliwa badala ya kulizungumzia nje wakati ndani alikuwa nao pamoja.


Tanzania Daima ilimtafuta kwa njia ya simu msemaji wa chama hicho, John Mnyika, bila ya mafanikio ambapo simu yake ya mkononi ilikuwa ikiita muda mrefu bila ya kupokelewa.


Shibuda alikaririwa na vyombo vya habari juzi akieleza kuwa anataka kugombea urais kupitia CHADEMA na kumwomba Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, kuwa meneja wake.


Alipotakiwa kufafanua zaidi kauli yake hiyo aliyoitoa wakati akiwasilisha mada kwenye Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) mjini Dodoma, Shibuda alisema anataka kuwa Rais wa Watanzania wote hivyo, hata kura za CCM anazihitaji ndiyo maana akatangaza mbele ya jukwaa lao.


Shibuda alisema hakuna mwanachama wa CHADEMA anayeweza kuwa Rais wa nchi hii bila kupata kura za baadhi ya wanachama wa CCM na Watanzania wengine.


“Hata katika hayo majimbo ambayo CHADEMA tumeshinda, hatukupigiwa kura na wanachama wa CHADEMA pekee, bali walikuwepo hadi wa CCM wanaopenda mageuzi.


“Mimi ni Jemedari katika siasa. Ndiyo, nimetangaza mbele ya jukwaa la CCM kwa sababu nahitaji kura zao. Nahitaji kura ya Kikwete na wana CCM wengine, mimi siyo mtu mwoga wa kutangazia vichochoroni Kariakoo,” alisisitiza Shibuda. 

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,864
1,225
Vizuri wanaunda kamati kwanza chini ya Prof. Safari; Shibunda ni kiongozi wa Sura Mbili hatakiwi kuongoza nchi
 

EL MAGNIFICAL

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
938
195
anasema chama kinachoweza kushika nchi ni ccm wakati huo huo anasema ana mpango wa kugombea kupitia cdm sasa mbona kama anapanda mbegu zisizo ota.
 

Njoka Ereguu

JF-Expert Member
Apr 7, 2012
821
195
Ukweli ni kwamba Shibuda hajawahi kuhama CCM, alichokifanya ni kutafuta Ubunge kupitia CHADEMA, ndiyo maana hauwezi kumwona katika harakati madhubuti za CHADEMA kuikomboa nchi na kuzika magamba, aidha hakosekani katika dhifa za Magamba. Ni vyema kuwa makini sana na mtu wa namna hii hasa wakati huu ambapo ukombozi unakaribia kupatikana.
 

buzz

Member
Apr 4, 2012
31
70
Naungana na wazo lako 100% hakuna haja ya kumwekea vikao mnazidi kumpa umaarufu. Dawa yake BAVICHA tu basi.
 

Mwita Maranya

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
10,565
2,000
Sema yote kuhusu Shibuda lakini usimnyang'anye haki yake ya kuwa na influence hko kwao. CDM imebebwa na Shibuda huko Shinyanga na wasipo tumia busara safari ya kuelekea kwa NCCR ya kina Mrema na Marando.

Ndoto za aina hii mmekuwa mkiziota sana wanamagamba kila siku na kila mara, lakini mtambue kwamba chadema ni chama makini na imara mno, mambo ya nccr manunuzi na mrema lyatonga hayatuhusu waache wajifie wenyewe huko na viti maalum vyao.

Sisi tunaendelea kutanua mtandao wetu katika nchi na kujiimarisha kwa ajili ya kuiongoza Tanzania kuanzia November 2015.
 

mshikachuma

JF-Expert Member
Dec 2, 2010
2,853
0
Mfukuzeni muone! anamaono ya mbali sana. Hawezi kufungwa na minyororo ya ukabila. Nyinyi watu (hasa vijana) wa Mwanza, Shinyanga, Tabora, Mara na Rukwa, hebu jaribuni kuwa neutral (mawazo huru) mchambue hivi kweli cdm ni chama cha wanyonge wa nchi hii au mnatumiwa na hao wanaotaka kujitenga na kutangaza jamhuri yao. Ole wao wavivu wa kufikiri, watapiginia hata kitakachowaangamiza.
Kwa mawazo haya...wewe unatofauti gani na Shibuda? Naweza sema heri ya Shibuda kuliko wewe.
Chama tawala cha Zambia na utawala wa Gadaffi wa Libya walikuwepo mavuvuzela na wapambe kama wewe
lakini mwisho wa siku nguvu ya umma ilishinda na wote wamebaki na aibu...i mean hawaamini walichokishuhudia.
Time will tell!
 

Nurujamii

JF-Expert Member
Jun 14, 2007
414
195
Kama kuna kosa kubwa na la kiufundi CDM wanaweza kufanya ni kumfukuza Shibuda. Huwezi kuwa na wanachama wote wenye mawazo sawa kwenye chama chochote kile cha siasa duniani. Hata USA Republicans yupo Senetor wa Maine Susan Collins na mwenzake Olympia Snowe wanajulikana kama the most liberals in the party. Wamekuwa kikwazo kikubwa kwa chama chao kila inapofikia wakati wa kupiga kura za kuzuia fillibusters. Wameisaidia sana Democrats kwenye hizo kura. Lakini hata siku moja hawajatishiwa kufukuzwa chama.

Kama CDM wanataka kila mwanachama na kiongozi asiwe na mawazo tofauti, hata kama yanaonekana ni ya ukichaa, basi hilo ni tatizo kubwa kidemokrasia. Si busara kuwaandama kina Zitto na sasa Shibuda kwa kutofautiana na viongozi wao.

Shibuda simuungi mkono hata kidogo, lakini ni muhimu ashughulikiwe kwa hoja tu na sio vitisho vya kufukuzwa chama. Na hata kama ikibidi kumuondoa basi democrasia ichukue mkondo wake. Wasubiri harakati zijazo za kugombea ubunge wampambanishe na mwanachama mwingine wawapigie kura na atakayeshindwa ampishe mwenzake. Ndio machungu ya democrasia hayo.

CDM inatakiwa kuwa kinara wa demokrasia TZ na kuonyesha wana CCM kwamba CDM ina uwezo zaidi yao katika kuenzi na ku-practice democracy. Otherwise naanza kuogopa! Seriously!
 

Hofstede

JF-Expert Member
Jul 15, 2007
3,578
0
Kama kuna kosa kubwa na la kiufundi CDM wanaweza kufanya ni kumfukuza Shibuda. Huwezi kuwa na wanachama wote wenye mawazo sawa kwenye chama chochote kile cha siasa duniani. Hata USA Republicans yupo Senetor wa Maine Susan Collins na mwenzake Olympia Snowe wanajulikana kama the most liberals in the party. Wamekuwa kikwazo kikubwa kwa chama chao kila inapofikia wakati wa kupiga kura za kuzuia fillibusters. Wameisaidia sana Democrats kwenye hizo kura. Lakini hata siku moja hawajatishiwa kufukuzwa chama.

Kama CDM wanataka kila mwanachama na kiongozi asiwe na mawazo tofauti, hata kama yanaonekana ni ya ukichaa, basi hilo ni tatizo kubwa kidemokrasia. Si busara kuwaandama kina Zitto na sasa Shibuda kwa kutofautiana na viongozi wao.

Shibuda simuungi mkono hata kidogo, lakini ni muhimu ashughulikiwe kwa hoja tu na sio vitisho vya kufukuzwa chama. Na hata kama ikibidi kumuondoa basi democrasia ichukue mkondo wake. Wasubiri harakati zijazo za kugombea ubunge wampambanishe na mwanachama mwingine wawapigie kura na atakayeshindwa ampishe mwenzake. Ndio machungu ya democrasia hayo.

CDM inatakiwa kuwa kinara wa demokrasia TZ na kuonyesha wana CCM kwamba CDM ina uwezo zaidi yao katika kuenzi na ku-practice democracy. Otherwise naanza kuogopa! Seriously!

US Mbunge ni mali ya constintuent. Unaweza hama chama na ubunge wako. au ukaamua kutokuwa mwanachama wa chama chochote.

Kitu ambacho kinanifanya nisikubaliane na CDM kuhusu Shibuda ni kutaka kumdhibiti. Shibuda ameisha dhihirisha yeye kuwa ni CCM damu, japo anajulikana kuwa ni mbunge kwa ticket ya CDM. Hakuna haja ya kumfuatilia wamwache afanye atakavyo na wasimjibu kwani watanzania wote sasa wanajua kuwa Shibuda ni CCM.

Kumuwekea kamati na kumtishia kumfukuza ni kumuongezea profile yake bure bila sababu. Leave the guy alone na wala kina Heche wasishughulike nae kwani hana nafasi yoyote ya uongozi ndani ya CDM hivyo si threat kwa chama.
 

MpendaTz

JF-Expert Member
May 15, 2009
1,817
2,000
Sioni sababu ya CDM kulumbana na huyu jamaa because he is politically dead. Hana influence yeyote kwenye jamii hata katika jimbo lake la Maswa. Wamwache tu abwabwaje, baadae wanaMaswa watamwonyesha njia ya kutokea 2015. Endapo CDM wakianzisha malumbano yeyote na Shibuda kwa sasa, sanasana watampaisha katika vyombo vya habari, na anaweza kujenga influence. Wamwache tu maana hata CCM wanajua yule kwa ni insane...
Hapana hili lingekuwa sahihi endapo CDM ingeweza kufahamu kama itafika naye salama hiyo 2015. Anavyoelekea anazidi kuwa tatizo kwa CDM. Ninahakika hana nafasi kubwa ya kufahamu mambo ya ndani ya CDM, je akifahamu mikakati yote na wakati ambapo ni sensitive, anaweza sababisha matatizo makubwa. Huyu ni kupe, huwezi kaa na kupe mwilini ukingoja afe adondoke. Atakutia kichaaa!
 

KANYIMBI

JF-Expert Member
Nov 6, 2011
1,395
2,000
Huyu jamaa haina haja ya kamati. Afukuzwe tu. Hana tofauti na Mbatia, wote ni pandikizi ya Magamba. wapo kwa ajili ya kubomoa upinzani. Ameniudhi huyu hadi moyoni.
 

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
48,718
2,000
yan huyu mgonjwa ana tuumisha vichwa? ina bidi afukuzwe huyu moran.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom