Elections 2010 Shibuda kateleza au ni mazoea tu? hebu sikiliza video hii

Huyu jamaa ni mamluku,kiroho yuko CCM,kimwili yupo CHADEMA.Lakini anapaswa kuelewa CHADEMA ni chama makini,mamluki wote tutawajua na kuwashughulikia!!
 
Aliteleza. Kama ana matatizo yatajulikana maana tunaye kwenye peoples power
 
Huyu shibudabuda ni mamluki >>>nawataka wadau mkae mkao wakusikia siku moja akirudi sisiem na kuichamba chadema>>huyu pale chadema kaenda si kama mtetezi wa wanyonge bali kutimiza maslahi yake>>>viongozi wangu chadema..kaeni macho na huyu mtu

Mimi naona wanachadema mkae macho na huyu mageuzi 1992. ulikuwa wapi toka siku alipozungumza hivyo leo ndo unaibuka!!!!!!!!!!
 
Binafsi siwezi kuunga hoja kwa kusema eti ni mamluki, maana hakuna uthibitisho wa mimi kuutumia kujenga hoja yangu. Wanaodai yeye mamluki, basi watoe vithibitisho walivyonavyo hapa jamvini. Maana, kwenye video hapo juu, sikusika neo lolote la yeye kusema yu CCM. Hivyo, basi tutakuwa tayari kuiunga hoja ya umamluki wa mwanachama yeyote ndani ya CHADEMA chama cha wananchi kama wadau wataonyesha vithibitisho visivyo na ualakini.
 
Binafsi siwezi kuunga hoja kwa kusema eti ni mamluki, maana hakuna uthibitisho wa mimi kuutumia kujenga hoja yangu. Wanaodai yeye mamluki, basi watoe vithibitisho walivyonavyo hapa jamvini. Maana, kwenye video hapo juu, sikusika neo lolote la yeye kusema yu CCM. Hivyo, basi tutakuwa tayari kuiunga hoja ya umamluki wa mwanachama yeyote ndani ya CHADEMA chama cha wananchi kama wadau wataonyesha vithibitisho visivyo na ualakini.

"....Nasaha ambayo naweza nikaitoa kwa chama changu cha mapinduzi....."
 
Mbio za sakafuni siku zote huishia ukingoni. Tutaona mwisho wake mda si mrefu kama aliingia CDM ili ajihifadhi, lakini bado mapema mno kuanza kumuhukumu. Hebu tuangalie hapo bunge likianza mbivu na mbichi zitaonekana tu wanaCDM.
 
mimi nafikiri ni ulimi wa Mh Shibuda uliteleza hawezi kuongea kitu kama kile hadharani, ni kama kuna editing ya picha imefanywa hapa.

Lakini kwa upande mwingine sishangai kama ni kweli anayoyasema, maana binadamu tunasahau haraka mno.

Peoples Power
 
Don't be too serious with politicians!They are like player realy,you can play in one team and be a die fan of another team!!So Hawa Wanasiasa ni kuwabana watufanyie tunachokitaka,masuala yeye anapenda nini ama anaongea na nani si ya msingi endapo wanatimiza wajibu waliopewa na wananchi!
 
Ndiye mbunge pekee wa upinzani ambaye siku ya kuapishwa bungeni nilimuona akiwa anakwenda kuapa huku akiwa ana flag vidole viwili juu vya vema Chadema logo.jpg . Kama kuna mwingine aliyediliki kufanya hivyo naomba niambiwe!
pencil.png
 
Nilivyomsikia mimi ameitaja CCM si kwa kumaanisha kuwa bado yupo CCM bali ameitaja kama chama alichotoka au kilichomlea kwa muda mrefu, hivyo sioni kama ni tatizo akisema kwa chama changu cha CCM.... akaanza kuwapa wosia!!!!!!!!!!!! na kumalizia na PEOPLESSSSS POWER!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom