Shibuda innocent | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shibuda innocent

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Chumvi1, Oct 28, 2010.

 1. C

  Chumvi1 Senior Member

  #1
  Oct 28, 2010
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 137
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mauaji Maswa: Shibuda aachiwa huru
  • Polisi yasema hakuhusika

  na Samwel Mwanga, Maswa


  [​IMG] JESHI la Polisi limemwachia huru mgombea ubunge wa Jimbo la Maswa Magharibi kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Shibuda, kwa madai hakuhusika na mauaji yaliyosababishwa na vurugu zilizotokea katika Kijiji cha Kizungu, wilayani humo.Akizungumza na waandishi wa habari mjini Maswa jana, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini, Robert Manumba, alisema wameamua kumwachia huru mgombea huyo kutokana na upelelezi wa awali kuonyesha kuwa hakuhusika na tukio hilo.

  Alisema upelelezi huo umeonyesha wazi kuwa hakuwepo katika eneo la tukio ambapo mauaji hayo yalipotokea baada ya wafuasi wa vyama vya CHADEMA na CCM waliposhambuliana na kusababisha kifo cha Stephen Kwilasa.
  “Unajua linapotokea tukio kama hilo la mauaji ni lazima tufanye upelelezi kwa makini, ili kuweza kutenda haki kwa pande zote na sisi kama polisi tupo hapa kwa ajili ya kulinda usalama wa raia, hasa katika matukio haya ya kampeni za kisiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu, ni lazima tufanye kazi kwa umakini mkubwa,” alisema. Alisema bado wanaendelea na upelelezi na iwapo itabainika kwa namna moja au nyingine alihusika na tukio hilo, atafikishwa mahakamani na kuongeza kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria.

  Aidha, alisema Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM wa Kata ya Nyalikungu, Abel Jombo, amelalamika katika Kituo cha Polisi Maswa dhidi ya Shibuda akidai kuwa alimpiga mateke alipopelekwa katika eneo la mkutano, ambapo alikuwa akihutubia mgombea huyo na kusisitiza kuwa upelelezi wa tukio hilo haujakamilika.
  Akizungumzia kitendo cha mgombea ubunge wa Jimbo la Maswa Magharibi kwa tiketi ya CCM, Robert Kisenha, kumpiga Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Maswa, SP Peter Ndunguru, alisema jeshi hilo linakamilisha upelelezi na litamfikisha mahakamani muda wowote pindi utakapokamilika. Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi Wilaya ya Maswa, limewafikisha mahakamani wafuasi 11 wa CHADEMA kwa tuhuma za mauaji.

  Waliofikishwa mahakamani ni Mohamed Juma (30), Constantine Zengo (20), Raphael James (20), Juvent William (30), Frank Gogadi (22), Emmanuel Bundalla (31) na Omari Iddi (26).
  Wengine ni Waziri Peter au Mrisho Shabani (40), Stephen Makondo (26), Emmanuel Edward (25) na Paschal Edward (19). Mbele ya Hakimu, Thomson Mtani, Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Hashimu Ngole, alidai kuwa Oktoba 10 majira ya saa 10 jioni katika Kijiji cha Kizungu, washitakiwa hao kwa pamoja walimuua Stephen Kwilasa (26) kufuatia mapambano kati ya wafuasi wa CHADEMA na CCM. Washitakiwa hawakutakiwa kujibu lolote kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi ya mauaji. Kesi itatajwa Novemba 8, mwaka huu, kwani upelelezi bado haujakamilika.


  SOURCE : TANZANIA DAIMA
   
 2. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  hili gazeti la lini jama?
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Oct 28, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Wenye akili zetu tulijua mapema kwamba hakuna kesi pale.
  Shibuda ni mjanja wa siku nyingi, na kesi ilikuwa inamfavor
   
 4. C

  Chumvi1 Senior Member

  #4
  Oct 28, 2010
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 137
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ni la tarehe 26 october mr. Speaker
   
Loading...