Shibuda awashukia vikali mawaziri wa Rais Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shibuda awashukia vikali mawaziri wa Rais Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jun 27, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jun 27, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=3]Na Rashid Mkwinda,Dodoma

  MBUNGE wa Jimbo la Maswa Magharibi (CHADEMA) Bw.John Shibuda, amesema utendaji mzuri wa Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, unavurugwa na baadhi ya
  mawaziri aliodai ni mzigo ambao hawana utashi na ari ya kuwatumikia wananchi na taifa kwa ujumla.

  Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili mjini hapa, Bw.Shibuda alisema Bw. Pinda ana wakati mgumu katika kipindi cha uongozi wake kutokana na watendaji wabovu wasioitakia mema nchi.

  Alisema uwajibikaji ni sera nzuri iliyoasisiwa na Baba wa Taifa Marehemu Mwalimu Julius Nyerere, lakini viongozi waliopo wanatumia msemo huo kama wimbo ambao wanashindwa kuutekeleza kutokana na kugubikwa na ubinafsi.

  "Baadhi ya wasaidizi wa huyu mtoto wa mkulima ni mzigo kwa taifa letu, hawafai kabisa kuwa viongozi walipaswa kufukuzwa na kuondolewa katika uongozi..hawana nia njema na nchi yetu,"alisema Bw.Shibuda na kuongeza;

  "Nchi hii inatakiwa kuongozwa na viongozi waadilifu wenye utashi na uchungu na nchi yetu,"alisema Bw. Shibuda.

  Alifafanua kuwa baadhi viongozi kuanzia wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa,mawaziri na watendaji wengine serikalini walipaswa kutimuliwa uongozi kwa kuwa hakuna wanachokifanya.

  Alisema kuwa bashasha ya waziri mkuu inapotea siku hadi siku, kutokana na kugubikwa na mawazo ya ugumu wa kazi zinazomkabili mbele yake kwa kuwa baadhi ya wasaidizi wake wamemtupia majukumu peke yake.

  Akitolea mfano kauli hiyo Bw.Shibuda alisema kuna sera ya Kilimo Kwanza iliyorithiwa kutokana na falsafa za Kilimo ni Uti wa Mgongo , Siasa ni Kilimo na mengineyo mfano wa haya, lakini hakuna hata kiongozi mmoja ndani ya CCM ambaye anamuunga mkono waziri mkuu katika kupigania
  wakulima hali inayomfanya muda wote kukosa raha.

  "Suala hili la kilimo limetelekezwa kwa Rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu Bw.Pinda, wengine ni propaganda kisiasa, wanachokijua ni kupiga vita maandamano ya CHADEMA," alisema na kuongeza kuwa, wakulima wanataka kusikia maneno yenye tija kuhusu kukosekana kwa pembejeo za kilimo,na namna ambavyo serikali imejipanga kuwapatia wakulima pembejeo kwa njia rahisi.

  Akitolea mfano wa ziara za CCM zinazofanywa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Bw.Nape Nnauye, kwamba zimelenga kuendelea kuwapumbaza wananchi juu ya kile kinachozungumzwa kuwa wapo viongozi mafisadi ambao hata hivyo hawachukuliwi hatua za kisheria zaidi ya
  kuzungumza majukwaani.

  Bw.Shibuda ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya Bunge Mambo ya Nje,Ulinzi na Usalama alisema kuwa iwapo zingefuatwa sheria kama zile zinazofuatwa China na kwingineko,watu hawa wangepigwa risasi na kutoweka kabisa duniani na suala la kuzungumzia ufisadi lingekoma na kugeuka historia kwani hakuna mtu ambaye angethubutu kuhujumu mali za wavuja jasho.

  Alisema ziara za CCM kwa wananchi hazigusi matatizo yatokanayo na ukosefu wa pembejeo na jinsi serikali ilivyojipanga kupatia ufumbuzi tatizo la wakulima, bali kinachozungumzwa ni propaganda za kukipiga vita CHADEMA kutokana na jitihada zake za kuwaamsha wananchi kujua
  mustakabali wao.
  [/h]
   
 2. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #2
  Jun 27, 2011
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Yetu macho kwa sasa
   
 3. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #3
  Jun 27, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Na masikio pia
   
 4. Mwendabure

  Mwendabure JF-Expert Member

  #4
  Jun 27, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,051
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Khaa! Ndo alikuwa anateta hayo kama nilivyowaona (Shibu na Pinda) ktk gazeti la Mwananchi la leo!! Kuumbeeee! Kweli PM wetu ni lialia.
   
 5. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #5
  Jun 27, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Yakweli haya?kunamtoto wa mkulima kweli katika viongozi wetu?viongozi gani hao wabuvu na mzigo kwa taifa si awataje nini kufumbiana katika zama za uwazi na ukweli?mbona wabunge hamjiamini?taja watu wabovu tuwajue,mbo dr slaa anawataja nyinyi mnashindwa nini?kumbuka ndege wafananao huruka pamoja so wewe uko wapi?
   
 6. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #6
  Jun 27, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Chibuda kasema, hizo ndio zake, lakini wengine wanataka kumlazimisha kusema wakati hayupo tayari kusema. sasa kazungumza.
   
Loading...