Shibuda awa mwenyekiti mpya CHADEMA mkoa wa Shinyanga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shibuda awa mwenyekiti mpya CHADEMA mkoa wa Shinyanga

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Molemo, Apr 28, 2011.

 1. M

  Molemo JF-Expert Member

  #1
  Apr 28, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Jana Baraza kuu la CHADEMA Mkoa wa Shinyanga limemtangaza John Magale Shibuda kuwa Kaimu Mwenyekiti wa mkoa wa Shinyanga (Soma majira la leo).Habari hizi zilinishtua kidogo nikawa na maswali machache:
  Kweli Shibuda ametubu na kuutii uongozi wa Taifa chini ya Mh Mbowe.??
  Je,Shibuda ataacha kutofautiana na viongozi wenzake hasa wabunge??
  Si ni Shibuda huyuhuyu aliyekashifu wabunge wa Chadema bungeni??
  Si ni Shibuda huyuhuyu aliyesema Mh Wenje hana adabu??
  Si ni Shibuda huyu huyu aliyesema Chadema ni mkusanyiko wa wanaharakati wasio wanasiasa??
  Je,Shibuda si alileta vurugu kwenye vikao vya wabunge wa Chadema huko Bagamoyo??
  Ikumbukwe Shibuda ni mbunge pekee wa jimbo ambaye hakupewa wizara kivuli bungeni.

  Nimeeleza yote haya si kwa chuki na Shibuda bali changamoto kwake kwamba alikuwa amepoteza imani na wanachama wengi kwa matendo yake yasiyotabirika na anapaswa kurejesha heshima yake kwa kutii viongozi wa chama na wabunge wa chama chake...
   
 2. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #2
  Apr 28, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  ...serious?? je, uteuzi huo wa baraza la mkoa utahitaji endorsement ya kamati kuu? anyway, Mpiganaji Slaa (PhD) na viongozi wengine wa CDM wamo humu JF wata-clerify hii kitu. Binafsi simfagilii Shibuda, namuona kama ni gamba kwa CDM?
   
 3. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #3
  Apr 28, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Cha ajabu ni majira tuu ndio wameandika habari hiyo magazeti mengine hawajaandika kitu,
   
 4. m

  mama kubwa JF-Expert Member

  #4
  Apr 28, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 2,414
  Likes Received: 1,974
  Trophy Points: 280
  hata mie presha inashuka huyu ni rahisi sana hata kuhadaiwa pia uswahili umemjaa sana anaweza kufanya lolote wakati wowote
   
 5. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #5
  Apr 28, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  majira bado wanasherehekea sikukuu ya wajinga duniani.
   
 6. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #6
  Apr 28, 2011
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mpe mchawi akulelee mtoto bwana
   
 7. L

  LAT JF-Expert Member

  #7
  Apr 28, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  dont worry ..... ana kaimu tu mpaka uchaguzi utakapo fanyika...... hii ni kilemba cha ukoka
   
 8. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #8
  Apr 28, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Hata mi nimeshtuka sana,
  hili lijamaa ni ccm damu, sijui wamefikiria nini hao watu wa shinyanga? Ok tusubiri maelezo!
   
 9. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #9
  Apr 28, 2011
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Siku zote Shibuda huwa haaminiki kwani mara nyingi anachoongea huwa tofauti na kilicho moyoni mwake au matendo yake, huyu bwana alikuwa/au bado ni UWT sasa vipi kupewa nafasi nyeti ndani ya CDM? ni sawa na leo umchukue Mbowe awe mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kilimanjaro kweli hiyo itakuwa imetulia? kwa mtindo huu wasiwasi yangu ni kupoteza majimbo yote ya Shinyanga, WHY NOT MPENDAZOE OR OTHERS THAN SHIBUDA?...Dr Slaa alikuwepo, Mbowe alikuwepo sasa tunaomba ufafanuzi wenu!
   
 10. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #10
  Apr 28, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  CDM hawana viongozi zaidi ya wakina Shibuda, sasa wakimtoa Shibuda unataka ww ndio uwe mwenyekiti ili hali huwezi? Hongera Shibuda , wavue magamba na wenzako kwa kuwaambia ukweli
   
 11. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #11
  Apr 28, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wewe jipe moyo tu, ndio imetoka hiyo mkuu !
   
 12. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #12
  Apr 28, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  kama viongozi wa mkoa wamemuona anafaa basi anafaa:A S 39:
   
 13. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #13
  Apr 28, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,250
  Likes Received: 3,863
  Trophy Points: 280
  Kimsi cdm ni makini! Ukiona unakabidhiwa uongoz ujue upo active! Ppz powerrrrrr!
   
 14. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #14
  Apr 28, 2011
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Mpiganaji naungana na wewe.

  Shibuda ni mtu hatari kwa uhai na mstakaballi wa CDM. Hivyo ni vizuri kukaa naye kwa uangalifu mkubwa!
  Shibuda kwa sehemu kubwa anaonekana amehama KIMWILI toka CCM lakini AKILI/MAWAZO yote bado viko CCM. Matendo yake yanadhihirisha hivo. Juzi tu nilisikia akimshambulia Mbunge mwenzake wa CHADEMA jimbo la Ilemera kuwa aache kuto vitisho baada ya Mbunge huyo kutoa siku 90 kwa JWTZ kuhama maeneo fulani wanayoyakalia pale Mwanza mjini.

  Kwa hiyo Shibuda anaonekana kuwa bado ni vuvuzela la CCM.Ni vizuri kama ataishia kukaimu hiyo nafasi tu. Itakuwa ni hatari sana kama atapewa hiyo nafasi moja kwa moja. Shibuda pamoja na kushinda Ubunge bado hajaweza kumfikia marehemu Shelembi hata kwa robo pc kwa umahiri na uongozi bora ambao umeijenga CHADEMA katika mkoa wa Shinyanga.

  CHADEMA high authority zingatieni hilo. Tusije tukajikuta tunakiangamiza Chama chetu na kusambaratisha base yote aliyoijenga Mhe. Shelembi(RIP).
   
 15. Dullo

  Dullo JF-Expert Member

  #15
  Apr 28, 2011
  Joined: Oct 24, 2009
  Messages: 252
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani wana CDM mnakuwa na wasiwasi wa bure tu, huyu jamaa hata kabla hajaingia CDM viongozi wa juu walimjadili sana na wakagundua faida na hasara ya kuwa naye katika chama.

  Lakini viongozi wa juu wakagundua kunafaida kubwa ya kuwa na Shibuda katika CDM hivyo mie nina imani naye sana na ni mtu ambaye yuko active sana. CDM wanachoangalia ni mtu kuwa muadilifu na ndiyo silaha kubwa kwa CDM. Mie naamnini kazi yake mtaiona na viongozi wa mkoa wa Shinyanga wanamkubali sana Shibuda, tumpeni muda akijenge chama kwani fitna za siasa za mkoa wa shinyanga anazifahamu sana..Poeplesssssssssssssss Power.
   
 16. mangi waukweli

  mangi waukweli JF-Expert Member

  #16
  Apr 28, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 246
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  (ukaskazini unakusumbua)tatizo lenu chadema mnataka viongozi wote watokee kaskazini (moshi na arusha) yani watu kama kina zitto na shibuda wanapata tabu kweli kwenye hiki chama,sasa kama chadema kikitaka kife na kionekane ni chama cha wachaga basi wamstopishe shibuda kua mwenyekiti wa shinyanga chadema.nasikia mchezo mzima ameucheza zitto kabwe mwana mapinduzi kijana ambaye ndiyo roho ya uhai wa chadema
   
 17. Avanti

  Avanti JF-Expert Member

  #17
  Apr 28, 2011
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 1,209
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Hapo penye nyekundu nakukumbusha tu ni Wenje yule yule aliwaambia wenzake wana uroho wa kula nyama kwenye sherehe
   
 18. Josephine

  Josephine Verified User

  #18
  Apr 28, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 787
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Tutafika.Hofu siyo fungu letu na hakuna gumu litakalomshinda Mungu.
   
 19. E

  ESAM JF-Expert Member

  #19
  Apr 28, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 962
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Hivi marehemu Shelembi alikuwa mchaga kutoka Kilimanjaro au Mmasai, mmeru ... kutoka Arusha??? Kazi kweli kweli
   
 20. M

  Marytina JF-Expert Member

  #20
  Apr 28, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,034
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Hapo blue craaaaaaaaaaaaap
  Mimi wa Songea nipo tayari kukifia CDM
  Zitto hana uwezo wa kumburuza Dr.Slaa hata siku mmoja.Zitto alikosea na sasa anajirudi atakuwa kwenye form yake ya makali with time.
  Shibuda ameisumbua CDM ila hakuleta mpasuko (minors have no effect) kwa hiyo hakuna kinachozuia kupewa ukaimu mwenyekiti.
   
Loading...