Shibuda amwagia sifa kemkem Jemadari Freeman Mbowe amesema "Mizengo Pinda ni Mpambe nuksi"

Phillemon Mikael

JF-Expert Member
Nov 5, 2006
9,767
2,000
Kuna wasemao shibuda ni TISS ati
Tena Senior
Kimsingi TISS inatakiwa kuwa kila mahali maana wao wako kwa ajili ya Taifa iwe nchi iko chini ya CCM ; Chadema ; Kijeshi Au hata chini ya Jaji Mkuu .... kote huko lazima kuuwe na options in any scenario that may happen even in a worst scenario
Wana jukumu la kuhakikisha sustainability ya nchi kwenye Kila hali .... na ndio Maana unakuta wapinzani wanashinda Mfano alafu hawatangazwi Lakini ipo siku wakisharidhika na uimara wao ccm itaweza kujikuta inatoswa na system ...na ndio doctrine ya Mwalimu Nyerere “ nataka tujenge Vyama Angalau viwili mbadala ambapo chochote kinaweza kushinda urais na “tulakiamini” kitawale “
Mwalimu Nyerere alikua akivutiwa Sana na mfumo wa USA ( Democrats na Republican ) au UK ( Labour na Conservatives) Kutawala kwa zamu na ndio imekua Ndoto yake inayoishi

Ukiacha kuhumiza uhai wa ccm na kukitaka kuenda na wakati ; Mwalimu baada ya kusoma katiba za Vyama vyote Pamoja na waanzilishi wake tena wakati NCCR Ina nguvu hata Mwanaye na Jimbo la kusoma vijijini kwenda NCCR ; bado aliitabiria CHADEMA kikiwa Chama Cha Tano kwa ukubwa Wakati Huo kuja kuwa Chama kikubwa; aliwaambia ccm
“ nimeangalia vyaka vyote Lakini kati ya vyote itazameni Sana Chadema kitakuja kuwa chama kikubwa kitakachowasumbua Sana “
Pengine alivutiwa na sera zake Lakini zaidi kilianzishwa Na maafisa waandamizi serikalini waliokua na mtazamo wa Kibepari katika serikali yake na ya Mwinyi
Kwa hiyo kimsingi tunakua na Vyama viwili vikubwa CCM inayoamini sera za kulia ( rightist ) na Chadema ( leftist ) na kuna nafasi ya Chama Cha Tatu anbacho kitakua kinatumika kufanya coalitions ( mseto) Pale Vyama viwili vikubwa vinapofungana kitaweza kuunga mkono Chama kimoja wapo na kikashinda ...( ie CUF au ACT ) Vyama vingine vyote vilivyobaki Vitakua vidogo
Utabiri wa Nyerere hauko Mbali kutimiaa


Sent from my iPhone using JamiiForums
 

Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
6,925
2,000
Kwa hiyo kimsingi tunakua na Vyama viwili vikubwa CCM inayoamini sera za kulia ( rightist ) na Chadema ( leftist ) na kuna nafasi ya Chama Cha Tatu anbacho kitakua kinatumika kufanya coalitions ( mseto)
Ulishaharibu huko juu, lakini hapa ndipo umeanguka kabisa!

Oooh, na-'edit' kwa kuongezea mstari huu: nilikuwa sijatambua mwandishi wa bandiko hili! Ni mkuu 'Philemon Michael'? Imekuwaje sasa mkuu, mbona ni kama umechanganya?
 

Omulasil

JF-Expert Member
May 5, 2015
3,544
2,000
Ulishaharibu huko juu, lakini hapa ndipo umeanguka kabisa!

Oooh, na-'edit' kwa kuongezea mstari huu: nilikuwa sijatambua mwandishi wa bandiko hili! Ni mkuu 'Philemon Michael'? Imekuwaje sasa mkuu, mbona ni kama umechanganya?
Mi namuona hajachanganya kabisa tena anaonesha kutokaa upande mmoja na huo ndio ukweli. TISS wanatakiwa kuwa kotekote ili usalama wa taifa uwepo la sivyo tutakuwa pabaya. Huyo Shibuda(boxer) wa Moshi Tech ni kweli alipata vetting na wao, baadae ........ kabla hata hawa General tyre, na baadae.... ndio hivyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom