Shibuda achangia bajeti ya waziri mkuu; ataka posho ziongezwe kwa jina jipya

Kumbe posho kiswahili sanifu ni ujira wa mwiha, dah! Shibuda ni noma...
 
amemaliza kwa kumpongeza lowasa na kusema wanaomkosoa wana chuki binafsi..na kuongezeaa UJIRA WA MWIHA usifutwe na uwahishwe walipwe mapema! anashangiliwa kwa vigelegele..!
 
Shibuda sioni sababu ya yeye kufika 2015 CDM wamfute uanachama then wafanye uchaguzi upya huko Maswa Magharibi ana maneno ya kifala sana huyo mwendawazimu.

Mlafi wa nyama mkubwa huyo.
 
Hilo gamba no. 1! Kwani sie tunaochangia harusi, misiba n.k., tunalipwa huo 'ujira wa mwiha'?
 
Katika mjadala wa bunge jioni hii Mbunge John Shibuda apendekeza posho iongezwe kwani inayotolewa sasa haitoshi. Shibuda amesikika katika mchango wake akisema posho inayotolewa iongezwe ikiwezekana ifikie laki tano na iitwe UJIRA WA MWIHA kama ambavyo ilikuwa ikiitwa wakati wa Mkoloni.
 
Kweli wachina wanafalsafa yakipekee! Wanasema kama ktk maendeleo pakiwa na watu watatu halafu wote wakawa wanamsikiliza mtu mmoja,hakika maendeleo yatachelewa! Ndicho nilicho shuhudia Mh John Shibuda akipigania posho kwa mahairi yenye vina huku akimuomba Mungu ziongezwe mpaka 500000/
Nini tafsri yake ktk hili?
 
huyu jamaa bwana..yani leo alichopanga kuongea ni posho tu! hata hivyo nimependa mchango wake kuhusu upinzani kukandamizwa na kutosikilizwa
 
MBUNGE WA MASWA JOHN SHIBUDA, akichangia hotuba ya waziri mkuu jioni hii amesema kiswahili sanifu cha posho ni 'UJIRA WA MWIHA' na kuomba iongezwe ikiwezekana hata laki tano kwa siku. Kasema kutofautiana mawazo ni demokrasia. Kweli Shibuda yuko CDM kwa bahati mbaya.
 
Mwenyekiti unasubiri nini kuwmfuta huyo ambaye ni mwiba kwetu? Mfute uanachama na uchaguzi uitishwe upya. I hate papeti kama huyu.
 
Uzalendo wa mtu kwa wakati wa sasa ni pesa na si maneno.

Kama huwezi kugawa na wenzio kwa kidogo kilichopo hata uimbe ngonjera ya maneno matamu vipi ni bure.

Anasema habari ya posho iongezwe huku akijiita mzalendo na anajua kilichopo wengine hakiwafikii .ama kweli hapo cdm wamepoteza
 
What the f***??seriously mtu anasema hivyo kabisa.hawa wanafanya mchezo na kodi zetu
 
Puppet wa ccm huyu mzee, Ndio maana wenje alimwambia ni mlafi wa nyama...Chadema inabidi wa mteme.
 
Back
Top Bottom