Shibuda aachiwa na Polisi na kusema "CCM wamenipa Umaarufu"

Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga limemwachia huru mgombea Ubunge wa jimbo la Maswa Magharibi kupitia CHADEMA, John Shibuda baada ya upepelezi wa wali kukosa ushahidi wa kumhusisha moja kwa moja na vurugu zilizotokea Maswa mara baada ya mkutano wa kampeni za kisiasa, kampeni zilizosababisha kifo cha Steven Kwilasa ambaye alikuwa dereva wa mgombea wa CCM, kwa jimbo hilo.

Polisi pia wamethibitisha kuwa lilimshikilia mgombea wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM, Simon Kisena, kwa tuhuma za kumshambulia Mkuu wa Polisi Maswa kwa muda na kumwachia huru mara baada ya mahojiano.

Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai, Robert Manumba amesema watu kumi na mmoja walioswekwa rumande kutokana na vurugu hizo wamepandishwa kizimbani na kusomewa mashitaka yanayowakabili



SORCE: Jeshi la polisi lawaachia huru Shibuda na Kisena -
Na mimi polisi akinichokoza nampiga maana adhabu zake ni kuhojiwa tu na kurudi kuja kulala home
 
Ni habari njema kwa Decmocracy na haki za binadamu. DCI Manumba alitia timu Maswa kufuatia kifo cha mwana-CCM kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ni mapigano na wana-CHADEMA. Nasikitika kuwa yawapata wiki mbili watu saba nadhani Karatu walifariki kwa kuchomwa moto sikumsikia DCI anaruka huko. Napata shida kudhani kuwa incident ya Maswa ilikuwa muhumu zaidi....
 
Sasa tuwe makini na hao washtakiwa wasijekuwa mamluki. wanaweza kusema kwenye ushahidi wao kuwa walihamasishwa na Shibuda kufanya hayo waliyoshtakiwa.
Naamini akina Makamba sio wehu kupiga kambi kule

Mkuu you can do that kwenye case nyingine lakini si mauaji, ili jaji ahukumu inatakiwa kweli iwe beyond reasonable doubt. Unakumbuka kesi ya Zombe na wenzake??? Pamoja na kwamba kulikuwa na kila dalili kwamba walihusika na vifo vya wale jamaa wa Mahenge lakini ushahidi ulishindikana sembuse iwe ya kusinghiziwa
 
Ukifuatilia alivyoongea RPC shinyanga na DCI utaona kuwa iko kazi ktk utekelezaji wa majumu. Wakati RPC anasema anamshikiria SHIBUDA kuona amehusika kwa kiasi gani (meaning there was no doubt kuwa amehusika) ili wamfungulie mashitaka kulinga na alivyohusika. Na kwamba swala la OCD kupigwa lilikuwa ni dogo, kwamba issue kubwa ni kuwa mtu amekufa (sikatai). RPC alikwisha fanya judgement kuwa Shibuda amehusika.
 
Jeshi la polisi limemwachia huru mgombea ubunge wa jimbo la maswa magharibi kwa tiketi ya CHADEMA,John Shibuda,kwa madai hakuhusika na mauaji yaliyosababishwa na vurugu zilizotokea katika kijiji cha kizungu,wilayani humo.(Tanzania Daima,26 October 2010 u.k 1)

My take

Katika hili jeshi la polisi limeonyesha ukomavu wa hali ya juu na linahitaji pongezi,kwa kuwa haki imetendeka bila kuingiliwa na hila za kisiasa.
 
Hiyo ni habari njema, Ahsante kwa taarifa. Sasa ndiyo umashuhuri umeongezeka, hapo atajizolea kura kilaini za kumpa pole na yaliyomsibu.
 
............Katika hili jeshi la polisi limeonyesha ukomavu wa hali ya juu na linahitaji pongezi,kwa kuwa haki imetendeka bila kuingiliwa na hila za kisiasa.

Hawajaonesha ukomavu kwa hiari yao. Mimi nampongeza sana Kamanda manumba, kama umeshasikiliza kesi nyingi za aina hii, hajawahi kutimuka haraka na kufanya upelelezi wa haraka namna hii
Wameona athari zake, Lakini Manumba nadhani katoa mchango wake mkubwa, ukijaribu kuchek utaona kuna watu tayari walishatwisha chadema kosa lile. Sasa ona kumbe hawana kosa kwa uchunguzi wa awali.
Kwa Kifupi CCM ndo walioua dereva wa mgombea wao kwa kumsakizia kwenda kufanya vurugu kwa Chadema jambo ambalo kwao ni mpango wa mwaka huu, ili chadema waonekane hawahubiri amani

Hongera Manumba sasa endelea kwa speed ya hivyo, siyo iwe mwisho kwa Shibuda.
 
Heko manumba, amesema wazi, shibuda hakuhusika na fujo na kifo cha dereva wa ccm. Kamanda siasi alijua hilo lkn aliendelea kumshikilia shibuda.
 
Hawajaonesha ukomavu kwa hiari yao. Mimi nampongeza sana Kamanda manumba, kama umeshasikiliza kesi nyingi za aina hii, hajawahi kutimuka haraka na kufanya upelelezi wa haraka namna hii
Wameona athari zake, Lakini Manumba nadhani katoa mchango wake mkubwa, ukijaribu kuchek utaona kuna watu tayari walishatwisha chadema kosa lile. Sasa ona kumbe hawana kosa kwa uchunguzi wa awali.
Kwa Kifupi CCM ndo walioua dereva wa mgombea wao kwa kumsakizia kwenda kufanya vurugu kwa Chadema jambo ambalo kwao ni mpango wa mwaka huu, ili chadema waonekane hawahubiri amani

Hongera Manumba sasa endelea kwa speed ya hivyo, siyo iwe mwisho kwa Shibuda.
mkuu nimesoma post yako huku chozi lanilenga. Unajua kuna ile sms ambayo ishaanza kusambaa kuhusu chadema na haya matatizo yaliyojitokeza.
Amini ushindi wa kweli dhidi ya ccm unakuja.
Jamani kama hata hamumpendi slaa basi mpigie kiongozi yeyote wa upinzani lakini kipaumbele cha kwanza ni dr. slaa.

Jeshi la polisi limemwachia huru mgombea ubunge wa jimbo la maswa magharibi kwa tiketi ya CHADEMA,John Shibuda,kwa madai hakuhusika na mauaji yaliyosababishwa na vurugu zilizotokea katika kijiji cha kizungu,wilayani humo.(Tanzania Daima,26 October 2010 u.k 1)

My take

Katika hili jeshi la polisi limeonyesha ukomavu wa hali ya juu na linahitaji pongezi,kwa kuwa haki imetendeka bila kuingiliwa na hila za kisiasa.
habari hii naamini haijawafurahisha ccm na genge lake.
Subiri hapo oktoba 31 ndipo mwisho wa ngoma yao ya kichawi iliyodumu miaka 5 ikulu
 
mkuu nimesoma post yako huku chozi lanilenga. Unajua kuna ile sms ambayo ishaanza kusambaa kuhusu chadema na haya matatizo yaliyojitokeza.
Amini ushindi wa kweli dhidi ya ccm unakuja.
Jamani kama hata hamumpendi slaa basi mpigie kiongozi yeyote wa upinzani lakini kipaumbele cha kwanza ni dr. slaa.

Binafsi mimi nilishaona mda mrefu na inaniuma sana kwa sababu watanzania walio wepesi kuamini ya ccm hata kama ya uwongo na huku wakiteseka kwa mambo kibao, wanaelewa hivyo.
Kibaya ni pale wanapomlipa mtu akajitoe kwenye mkutano wa watu wengine kama vile chama kimeanza mwaka huu. Ni dhambi sana! Siku ya juzi Dr. Yupo tanga, wamemfungia maspika dereva apigie kelele wana watanzania wanaomsikiliza rais wao Slaa. sasa si kumtoa kafara mtu huko!
Bahati watu nao washajua, wamebaki wale wenye hasira za ukweli kwa sababu wameshaumizwa sana na ccm.
Lakini mambo ya CCM mwaka huu yanaumiza sana, NATAMANI WADANGANYIKA WOTE WAAMKE USINGIZINI HALAFU DR. SLAA ASHINDE KWA 90%kinana na makamba watakufa ghafla
 
Heko manumba, amesema wazi, shibuda hakuhusika na fujo na kifo cha dereva wa ccm. Kamanda siasi alijua hilo lkn aliendelea kumshikilia shibuda.

Vipi Manumba kumwachia huru mshitakiwa aliyemkata ngwala OCD mbele za watu wengi tu tena hapo hapo kituo cha polisi? Ni ushahidi gani unaoendelea kutafutwa zaidi ya kumpeleka Mahakamani? au kwa vile mshitakiwa ni wa CCM basi anataka wayamalize kiaina hapo baada ya uchaguzi?
 
shibuda, hawamwezi kwenye uwanja wa siasa, kwenye mdahalo, kwenye jukwaa la kitaaluma ama hata kiunjanja.
Huyu mzee amatulia, anaongea kama anatania lakini ni mutu ya akili nyingi.

mungu ampe nguvu, ashinde maana timu hatakamilika bila yeye(maswa) ,mpendazoe, nyimbo(njome), mnyika(ubongo0, lema(arusha), mdee(kawe), mbilinyi/mr.ii(mbeya mjini), shitambala(mbeya vijijini), ........................timu ya matumaini, na zito pia.
 
CCM WAMWAGA DAMU MASWA
Katika kampeni za ubunge zinazoendelea Maswa magaribi kumetokea kifo cha dereva wa mgombea wa CCM (Robert Simon Kisena). Lakini hiki si kifo cha bahati mbaya ni kifo cha kupangwa na mgombea wa CCM anayeungwa mkono na Riziwani Kikwete, Makamba pamoja na Kikwete. Robert Kisena ambaye ni tapeli mkubwa anayejulikana kwa utapeli wake pia ni swahiba wa karibu wa Riziwani Kikwete.
Kulikuwa na mkutano wa CHADEMA uliokuwa unaendelea maswa magaribi huku gari moja ya chadema(land rover) ikiwa inazunguka maeneo ya karibu, ikiwa inawatangazia watu juu ya mkutano huo, ghafla ilitokea gari ya ccm(surf) ambayo ilitaka kuigonga gari ya chadema. Gari ya chadema katika kukwepa ikatoka barabarani na mmoja ya watu waliokuwemo katika gari hiyo ya chadema aliangusha kofia hapo, na ikabidi ashuke kuichukua. Chadema waliposimamisha gari yao kuokota kofia ndipo CCM waliposhuka na kuanza kuwashambulia CHADEMA. Watu wa CHADEMA kuona hivyo wakaanza kupiga kelele, wale CHADEMA waliokuwepo kwenye mkutano waliposikia wakaanza kuondoka kwenye mkutano kuelekea kwenye tukio. Huko kwenye tukio watu wa CHADEMA walianza kuwapiga mawe CCM mpaka wakakimbia na mmoja wao kukamatwa. Mgombea ubunge wa CHADEMA alitaarifiwa kuhusu kukamatwa kwa kada wa CCM na akawaambia watu wa CHADEMA wasimpige wampeleke kwake pale kwenye mkutano, na mwishowe alimkabidhi kwa polisi.
Cha ajabu yule dereva aliyekuwa anaendesha gari ya CCM iliyokimbia eneo la tukio, amefariki, na taarifa ya uongo inasema alikufa pale pale kwenye eneo la tukio. Lakini hii taarifa ya uongo inatokana na shinikizo la CCM kwa polisi na kwa vyombo vya habari. Ukweli ni kwamba yule dereva aliweza kuendesha gari mpaka kituo cha polisi na kuandika maelezo na baada ya hapo kupelekwa hospitali na kuekewa dripu ya maji. Gari ya CCM iliyoshiriki kwenye tukio ilikamatwa baadaye na kukutwa haina damu hata kidogo, kwahiyo kuna uwezekanao mawe hayakumpata dereva au hayakumuumiza kiasi cha kutoka damu. Lakini taarifa iliyotoka inasema alikufa kwa kupigwa mawe na kuchomwa na kitu cha ncha kali kisogoni. Ukumbuke dereva wa CCM akushuka kwenye gari na alikuwa amekaa kwenye kiti cha dereva chenye head-rest. Ni ngumu kuelewa hicho kitu cha ncha kali kiliweza kumfikia vipi kisogoni wakati amekaa kiti cha dereva. Na huwezi kuchomwa na kitu cha ncha kali kisogoni uendeshe gari mpaka kituo cha polisi kuandika maelezo. Inawezekana CCM walimmalizia huyu dereva ili kukuza hili jambo kiasi cha kufanya CHADEMA isiruhusiwe kushiriki uchaguzi maswa magharibi. Pia watu wanaomjua huyu Robert kisena (mgombea wa CCM) wanasema inawezekana kamtoa kafara dereva wake, hasa ukizingatia yeye Robert Kisena ni mshirikina sana.
Katika mazishi ya Dereva, ndugu wa dereva walimuomba Robert Kisena ushirikiano wa kifedha akawajibu mnataka kunigeuza mtaji. Ndugu wa marehemu walilikataa jeneza la CCM na kusema mgombea wa CCM kamtoa kafara ndugu yao. Riziwani Kikwete aliyekuwepo kwenye mazishi ya dereva huyo naye alipewa ukweli wake hapo kwenye mazishi, kuwa wanashirikiana na mgombea wa CCM kuwauzia watu bidhaa feki. Upo ushahidi wa picha wa haya yaliyosemwa hapa, pamoja na ushahidi wa picha unaonyesha mgombea wa CCM akimpiga OCD wa maswa. Mgombea wa CCM ni Mnyarwanda hivyo kukosa ubinadamu ni hulka yake na hana undugu na dereva aliyekufa. Dereva aliyekufa anamuita mgombea wa CHADEMA mjomba. CCM wanaogopa SHIBUDA asishinde ubunge kwa vile ataweka mfano m'baya ambao utawafanya wale wanaonewa CCM au ambao hawakubaliani na ufisadi, wahamie CHADEMA.
 
vipi yule mgombea mwingine wa ccm aliyemfyatua mitama ocd kisha rpc alipomwona makamba akafyata na kusema hay0 (ya kupigwa ocd) ni ya kawaida kiutendaji naye yuko huru?
huyu kutoka kwake kidogo itakuwa mbinde kapiga askari je raia?, si mtu salama huyu
 
Back
Top Bottom