Shetani apoteza form za Mchungaji Rwakatare:-) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shetani apoteza form za Mchungaji Rwakatare:-)

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by SURUMA, Jun 16, 2011.

 1. S

  SURUMA JF-Expert Member

  #1
  Jun 16, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Habari hii imenistua kiasi kikubwa na imetoka katika gazeti Mwananchi la jana (15/06/2011)...Kwa mwendo huu tutafika jamani wa Tanzania wenzangu? Mh anajitetea kwa kusema SHETANI KAPOTEZA FORMS...

  Tafakari

  Mchungaji Rwakatare atoampya Baraza la Maadili

  Wednesday, 15 June 2011 22:25

  Nora Damian

  MBUNGE wa Viti maalum (CCM), Mchungaji Getrude Rwakatare jana alitoa mpya mbele ya Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma alikofikishwa kujieleza kwa nini hakujaza fomu ya kutangaza mali zake, baada ya kudai kuwa shetani ndiye amepoteza fomu hizo.

  Dk Rwakatare alisema hayo wakati akihojiwa na mwanasheria wa baraza hilo Getrude Cynacus.Katika utetezi wake, Dk Rwakatare alitumia maneno kama pepo, shetani na Mungu yalitawala.Mchungaji huyo alijitetea kuwa yeye alijaza fomu hizo na kuziwasilisha katika ofisi za bunge lakini hajui nini kilichotokea hadi fomu hizo zisifike kunakohusika.

  "Mambo mengine ni shetani tu, shetani ana nguvu sana kila mahali yuko,"alisema Mchungaji huyo na kuongeza kuwa:"Kazi yenyewe ya kujaza fomu ni ya dakika 10 tu sio kwamba unafanya mtihani Cambridge hivyo halikuwa zoezi kubwa kwangu hadi mimi nishindwe kujaza,"alisema.Alisema yeye hakuwa na wasiwasi kabisa kwamba angeweza kuwa mmoja wa watu ambao hawakujaza fomu hizo kwasababu alizijaza na kuzirejesha Ofisi ya Bunge.

  Dk Rwakatare pia alionyesha nakala ya fomu hiyo anayodai kuijaza na kudai kuwa ana uzoefu wa muda mrefu katika fomu hizo na kwamba kila mwaka amekuwa akizijaza."Tutaamini vipi kama nakala hiyo ni halali pengine ulikuwa nayo nyumbani na jana ukaitoa copy.

  Je hukusaini kokote wakati uliporudisha fomu hizo?" alihoji mwanasheria wa baraza hilo Getrude Cynacus.Akijibu swali hilo Dk Rwakatare alisema wakati wa kuchukua fomu hizo ilikuwa lazima kusaini lakini kurudisha haikuwa lazima.

  Baadhi ya mahojiano baina ya Mchungaji huyo na Mwanasheria huyo wa baraza yalikuwa hivi:Mwanasheria: Unasema ulijaza fomu, mbona hazikufika kwetu?Rwakatare: Hilo litakuwa ni pepo tu. Mimi nilirejesha na Mungu ni shahidi.Mwanasheria: Umeng'ang'ania shetani hivi huyo shetani ni nani?

  Rwakatare: Ni roho chafu ambaye kazi yake ni kuharibu na kufanya mambo yaende vibaya.Mwanasheria: Sasa huoni kama anakupeleka pabaya?Baada ya swali hilo, Mchungaji Rwakatare hakujibu kitu alikaa kimya.

  Mwanasheria huyo aliliomba baraza hilo litupilie mbali utetezi wa Mchungaji huyo kwa sababu amekiri kutofanya ufuatiliaji.Hata hivyo akizungumza nje ya baraza hilo na waandishi wa habari, Dk Rwakatare alisema tangu uanze mchakato wa fomu hizo, hajasafiri kwenda mahali kokote na kwamba anashangaa kwanini hawakumpigia simu kumuuliza kama alijaza au la.

  "Mimi sijasafiri kwenda kokote na wala nilikuwa sina wasiwasi kabisa kwa sababu nilijaza fomu na kuzirejesha, wangeweza kunipigia simu na ningeweza kuja,"alisema.

  Alipoulizwa na waandishi wa habari haoni kama kuna haja ya kuwakemea mashetani, Mchungaji huyo hakujibu kitu aliamua kuingia kwenye gari yake na kuondoka.Katika hatua nyingine, Mbunge wa Mpanda Vijijini kupitia CCM, Moshi Kakoso naye alifikishwa kwenye baraza hilo jana na kuitupia lawama ofisi ya bunge kwa madai kuwa alijaza fomu na kuzikabidhi kwa wahudumu wa ofisi hiyo."Sijafurahia kuitwa katika baraza hili ni kitendo ambacho si kizuri.

  Naomba nipewe nafasi ya kujaza fomu nyingine ili nitekeleze sheria za nchi,"alisema Kakoso.Alisema yeye hana mali za kutisha kiasi cha kumfanya ashindwe kujaza fomu hizo na kulalamikia ofisi ya bunge kuwa haiko makini katika utunzaji wa kumbukumbu.

  Mbunge huyo pia alipoulizwa na Mwenyekiti wa baraza hilo Jaji Damian Lubuva kuhusu kumpa muhudumu wa ofisi ya bunge nyaraka muhimu kama hizo, alijitetea kuwa hilo ni bunge lake la kwanza na kwamba alidhani kuwa alikuwa sahihi kumpa muhudumu huyo.

  "Hata mawasiliano ya barua kuja Mpanda yanachukua muda mrefu sana na kutufanya sisi wengine tuonekane tumekiuka sheria,"alisema Kakoso. Baada ya kusikiliza utetezi wa wabunge hao, Jaji Lubuva alisema watatoa uamuzi na mapendekezo yao kwenye mamlaka zinazohusika.

  Baraza hilo litaendelea leo ambapo Mbunge wa Mbinga Magharibi John Komba, diwani kutoka Geita Elias Okomu na Hakimu wa Mahakama ya Sumbawanga Edwin

  SOURCE:
  Mchungaji Rwakatare atoampya Baraza la Maadili
   
 2. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #2
  Jun 16, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Wapewe tu form zingie basi, siasa nyiiiiingi.
   
 3. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #3
  Jun 16, 2011
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Akemee azirudishe!
   
 4. M

  Mbwambo JF-Expert Member

  #4
  Jun 16, 2011
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 626
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Mama Rwekatare kwa kumtaja shetani kwamba ndiye kapoteza form zake ni kumfanya shetani aone kwamba ana nguvu na uwezo kuliko Mungu. Yeye angesema tu kwamba yawezekana ni uzembe au bahati mbaya ofisi husika ya Bunge kupoteza form yake maana kama ni shetani yeye kama mkristo na mchungaji amepewa mamlaka na Mungu ya kumkemea.... kwa jina la YESU.

  Ni kweli shetani yupo kila mahali lakini tusimsingizie kila mara maana hata yeye wakati mwingine anashangaa matendo yetu sisi wanadamu mengine hajatushawishi yeye. Mwisho ajaze nyingine kama anayo copy mbona ni rahisi kiasi hicho watu wa Mungu...........
   
 5. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #5
  Jun 16, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  Hata yeye shetani anamzidi kete!!
  sisi wengine itakuwaje?!!
   
 6. s

  sativa saligogo Senior Member

  #6
  Jun 16, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 126
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiyo si dalili nzuri kwa mchungaji kama yeye!! Je sadaka zake shetani kachukua?? Asituzingue hilo na anguko la aibu na bado!!
  MONEY CAN BUY A CHURCH NOT WoRSHIP!!!!:A S-baby:
   
Loading...