Sheria zitungwe na wananchi badala ya Wabunge

The Bliss

JF-Expert Member
Oct 16, 2021
213
435
Habari zenu wadau wa JF.
Leo nimeona niangazie upande wa sheria zetu Tanzania ambazo hutungwa na wabunge ambao wengi wao hawajachaguliwa na wananchi kihalali bali wamechaguliwa na jopo la viongozi wao wachache ili kulinda maslahi ya viongozi hao hapo baadae wakishapata madaraka.

Suala la utungaji wa sheria limekuwa changamoto sana kwa nchi zetu za Kiafrika ambapo watunga sheria ni wabunge ambao wamekuwa wakitunga sheria za kueakandamiza binadamu wengine huku wao wakijiwekea kinga dhidi ya kushtakiwa kwa makosa mbalimbali.

Sheria nyingi zinazotungwa katika nchi za Kiafrika hasa Tanzania huwa zinampendelea mtawala na kumkandamiza mtawaliwa. Wabunge hutunga sheria zenye kuwalinda waendelee kubaki madarakani wao na viongozi wao wakubwa na sio kwaajili ya kuleta haki na usawa kwa wananchi wote.

Mimi kwa mawazo yangu, sheria zingetungwa na wananchi masikini, wenye vipato duni na ambao wanaishi katika maisha ya uhalisia huku mitaani badala ya kutungwa na watu wanaokaa magorofani huku wakitumia raslimali za umma kuishi maisha ya anasa.

Utungaji huu ushirikishe watumishi wenye mishahara ya chini kabisa, pamoja na kundi la vijana wasio na ajira (Mawakili na wanasheria). Wafanyabiashara na viongozi wa dini wanaoaminika katika jamii zao. Baada ya hapo tutapata sheria ambazo zitaweza kuwawajibisha viongozi wetu hasa wa kisiasa pindi wanapofanya maamuzi yasiyokuwa na tija kwa umma.

Pia TAKUKURU,JESHI LA POLISI na MAHAKAMA ziaangaliwe upya utendaji wake, ikibidi ziwekwe chini ya watu wazalendo hasa wanajeshi, viongozi wa kidini wenye maadali na wahukumu kwa kutumia Torati pamoja na sheria nyingine tutakazojitungia kama wananchi ili waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Tofauti na hivi hii nchi itaendelea kuliwa na kuchezewa na watu wachache sana. Kwa hali pia inayoonekana sasa hivi ni kwamba watu wanajimilikisha nafasi za uongozi kwa kufuata familia zao na sio vigezo vya mtu binafsi.

NB: Ni mawazo yangu, nipo tayari kukosolewa.
 
Hapo ni hadi Wananchi wenyewe waamke kutoka usingizini ndio itawezekana hivi hivi watu hawatokubali kupoteza ugali wao.
 
Back
Top Bottom