Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,495
- 9,275
Sheria zinazolinda na kuzuia ukatili wa kijinsia mitandaoni ni pamoja na;
• Sheria ya Maudhui ya Mitandaoni (Online Content Regulation) 2020 ambayo inakataza na kutoa adhabu kurusha maudhui ya udhalilishaji ikiwamo picha/video za utupu, lugha za udhalilishaji zinazokwenda kinyume na utamaduni wa Mtanzania.
• Sheria ya Kimakosa ya Mtandao 2015 (Cyber Crime Act) ambapo Kifungu cha 23 kinakataza na kupinga uonevu mtandaoni kuwa ni kosa kisharia kwa mtu yoyote kufanya uonevu wa aina yoyote kwa kutumia njia za kieleketroniki na kufanya huyo ni kosa kisharia, na yeyote atakayekutwa na kosa hili atatumikia kifungo kisichozidi miaka 3 jela au zaidi, au kulipa faini isyopungua million tano (5) au vyote kwa pamoja.
Je, kwanini ukatili wa mitandaoni unazidi kukithiri pamoja na sheria kuwepo Sababu zinazopelekea ukatili wa mitandaoni kuendelea kukithiri ni kama zifuatazo;
• Uelewa mdogo kwa wananchi juu ya sheria zinazozuia na kukataza ukatili wa kijinsia mitandaoni.
• Hofu ya kuendelea kudhalilika hasa pale kesi zinapotaka kwenda Mahakamani.
• Tamaduni ya jamii nyingi kwenye mitandao kukaa kimya badala ya kukemea wanapoona vitendo vya uaktili kwenye mitandao
Mapungufu katika utaratibu wa ripoti kwa vyombo husika.
• Hivyo basi, katika kipindi hiki cha Siku 16 za Uanaharakati, tunatumia kampeni hii kupaza sauti na kukemea ukatili wa kijinsia mitandaoni.