Sheria zinasemaje juu ya kugawana mali kwa wanandoa wanaotalakiana?

Brooklyn

JF-Expert Member
Mar 17, 2009
1,459
284
Wadau kuna issue imeibuka hapa, dada mmoja kaniomba ushauri juu ya mambo yafuatayo;

1. Je iwapo mahakama ikatoa kibali cha kutolewa talaka, mtalakiwa (mke) ana haki ya kugawana mali ambayo mtalaka (mume) aliichuma kabla ya ndoa yao kufungwa?

2. Kama mtalakiwa alikuwa ni mama wa nyumbani (hafanyi kazi yoyote inayomwingizia kipato), je ana haki ya kugawana nusu kwa nusu mali yote ambayo ilipatikana wakati wakiwa wanandoa (wanaishi pamoja)?

3. Je mtalakiwa ana haki ya kugawana mali ambazo zimechumwa na mtalaka katika kipindi ambacho tayari mtalakiwa alikuwa haishi na mtalaka lakini kabla ya ndoa yao kuvunjwa rasmi mahakamani? (i.e. ni miaka miwili imepita toka mke aondoke kwa mume, je mali iliyochumwa katika kipindi ambacho mume alikuwa peke yake lakini kabla ya kutolewa talaka)

Naomba mwongozo wa kisheria wadau ili niweze kumsaidia huyu dada.
 
Na hili nalo ni neno, wewe mwache mkeo tu, hakuna cha kuwa alikuwa mama wa nyumbani au mfanyakazi, hakuna cha mali ulitafuta mwenyewe, mgao ni pasu bin pasu, kama nimekosea wanasheria naomba msaada wenu.
 
ninavyojua mali ambazo watakuwa na haki ya kugawana n zile zlzochumwa pamoja wakiwa bado wako kwenye ndoa.
Kuhusu mali ambazo zmechumwa kabla mnaweza kugawana lakn wakati mwingne hamwez kugawana, mfano mwanamke akiwa alisain prenup. Lakn kesho ntarud na jb lenye ushahd wa ksheria na vfungu.
 
Back
Top Bottom