‘Sheria zinakataza kampuni kuomba kazi isiyotangazwa’ Ni mangapi wamepeana bila Tenda? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

‘Sheria zinakataza kampuni kuomba kazi isiyotangazwa’ Ni mangapi wamepeana bila Tenda?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by dosama, May 27, 2012.

 1. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #1
  May 27, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  MAMLAKA ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) imesema sheria ya ununuzi wa umma hairuhusu kampuni kuomba kazi kwenye Taasisi ya Umma bila zabuni ya kazi husika kutangazwa. Katika taarifa yake jana, Ofisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, Dk Ramadhan Mlinga, alisema nunuzi wowote wa umma, unapaswa kufuata sheria na kanuni zinazoongoza sekta hiyo na si vinginevyo.

  Dk Mliga alikuwa akijibu maswali ya Mwananchi, kuhusu utata uliogubika katika mchakato wa kutafuta mzabuni wa kuhamasisha umma, kushiriki katika sensa ya watu na makazi, kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na Ofisi ya Taifa ya Sensa.

  “Sheria ya ununuzi katika sekta ya umma na kanuni zake haijaweka mazingira yanayoiruhusu kampuni kuomba kazi kwenye taasisi ya umma bila taasisi hiyo kutangaza zabuni au kazi husika,” ilisema Dk Mliga katika taarifa yake. Utata uliotokea katika Ofisi ya Taifa ya Takwimu, unatokana na taasisi hiyo ya umma, kutaka kuipa kazi ya uhamasishaji wa wananchi, kampuni ya Campaign International Marketing Ltd bila kazi hiyo kutangazwa katika zabuni kama sheria zinavyoelekeza.

  Mpango huo uliotaka kufanywa kwa njia mfumo wa ununuzi wa huduma ya moja kwa moja kutoka kwa mzabuni na kutumia mpango wa ushirikiano wa sekta ya umma na binafsi, ulizua mvutano ndani ya ofisi hiyo.

  Kufuatia majibu ya PPRA yaliyokuwa na mwelekeo unaobainisha kwamba njia hizo ni batili, wakuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, walipeleka suala hilo katika Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu (UNFPA) ofisi za Tanzania, ambako mchakato wa kumpata mzabuni unaendelea. Katika maelezo yake, Dk Mliga alikiri kwamba Ofisi yake ilipokea barua kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu kuomba mwongozo kuhusu ushirikiano wa Sekta ya Umma na Binafsi, kuhusu kuhamasisha wananchi kushiriki katika sensa. Alisema katika barua yake, ofisi hiyo pia ilisema imepokea maombi kutoka Kampuni ya Campaign International Marketing Ltd, kutaka iruhusiwe kufanyakazi hiyo. Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Campaign International Marketing, Peter Bilal. alikiri jana kwamba kampuni yake iliomba kushirikiana na ofisi hiyo, katika kazi ya kuhamasisha umma kuhusu sense.

  Hata hivyo, alisema hafahamu chochote kuhusu mvutano wao wa ndani. “Sisi kama kampuni tuliomba kazi kama wewe unavyoweza kuomba kazi sehemu yoyote, sasa kama utaratibu ni wa kutangaza zabuni hiyo ni juu yao wale wanaotoa kazi, lakini pia kama walivutana hilo nililisoma kwenye gazeti tu na sifahamu lolote, niko huku kwangu (ofisini) kama wewe ulivyo kwenye ofisi yako,”alisema Bilal.
  Dk Mlinga alisema taasisi yake iliielekeza Ofisi ya Taifa ya Takwimu, njia za kufuata kama inataka kutumia mfumo wa PPP kama zilivyoainishwa kwenye kanuni namba 74 ya ununuzi katika sekta ya umma.


  “Single source haiwezi kuja kwa sura ya PPP, kwa sababu hizo ni njia mbili tofauti za ununuzi na zenye taratibu tofauti za kuzifuata. Pia njia hizi hutumika katika mazingira tofauti na kiwango cha ukomo cha thamani ya ununuzi ni tofauti,”alisema Dk Mliga katika taarifa yake. Dk Mliga alisema ikiwa sababu zilizopo zinaruhusu kutumia kauni husika, basi bodi ya zabuni ya taasisi husika ndiyo inayopaswa kuidhinisha njia ya ununuzi.


  Wiki iliyopita Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dk Albina Chuwa, alikiri kuwa kazi ya ununuzi wa huduma za uhamasishaji na ushawishi wakati wa sense, imerejeshwa UNFPA na kwamba hatua hiyo imetokana na ofisi yake kutokuwa na uwezo wa kutekeleza majukumu yote kwa pamoja.

  My concern
  Hivi hizi sheria zinatumika pale tu mpinzani anapokosea? Ni mangapi wamepeana bila kutangaza?
   
Loading...