Sheria Zetu ni nguzo ya ufisadi na ulinzi kwa wakubwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheria Zetu ni nguzo ya ufisadi na ulinzi kwa wakubwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by tenende, Aug 17, 2012.

 1. t

  tenende JF-Expert Member

  #1
  Aug 17, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah

  1. ......Sheria ya Takukuru ya mwaka 2007 ni mbovu kwa kuwa inambana na kumfanya ashindwe kuwafikisha watuhumiwa wa rushwa kubwa mahakamani.

  2. sheria hiyo inamruhusu kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wadogo wa rushwa na wale wakubwa inamtaka apeleke kwanza jalada kwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP), jambo ambalo linafanya aonekane hafanyi kazi yake ipasavyo.

  3. Alisema anajua matarajio ya wananchi ni makubwa kwa Takukuru, lakini akasema sheria hiyo imewafunga mikono kwa kuwa hawawezi kuchukua uamuzi dhidi ya kesi kubwa za ufisadi bila ushauri wa DPP.

  4. "Sheria yetu imetufunga mikono kwa kuwa kumpeleka mtu mahakamani siyo uamuzi wangu, bali wa DPP." (a) Kifungu cha 37 hakimruhusu kutaja majina ya watuhumiwa wa rushwa; (b) Kifungu cha 57 inamzuia kuwapeleka mahakamani watuhumiwa wakubwa wa rushwa, mpaka awafikishe kwa DPP. (c) Kifungu hicho cha 57 (1) kinasema kuwa shtaka lolote la kosa lililoelezwa kwenye Sheria ya Takukuru lazima lifunguliwe kwa ruhusa ya maandishi kutoka kwa DPP. (d) Kifungu cha 57 (2) kinamtaka DPP ndani ya siku 60 kutoa au kukataa ruhusa ya kushtakiwa.

  5. wananchi wasubiri mabadiliko ya kiutendaji kama sheria itabadilika na kumruhusu kufanya hivyo.

  6. "Tusaidieni sheria hii ibadilishwe ili iweze kuturuhusu kufanikisha kupambana na rushwa nchini,"

  7. Dk Hoseah alisema ofisi yake inazo taarifa kuna mabilioni ya fedha yamefichwa Uswisi na kwamba taasisi yake inayafuatilia.

  Source: Mwananchi:Thursday, 16 August 2012
   
 2. U

  Ubungo JF-Expert Member

  #2
  Aug 17, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Sheria irekebishwe haraka, wananchi wanaumia kwa wizi wa fedha za umma.
   
 3. t

  tenende JF-Expert Member

  #3
  Aug 17, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  ORGANISED CRIME:......... The involvement in organized crime is the justification of corruption as the normal business. That is the participation of the government officials in corruption and treating it as a normal business." At the surface level they campaign against it but in actual sense they organize it and create mechanism to protect themselves against the wrath of the law. ................ Source: GS for A - Level.
   
 4. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #4
  Aug 17, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Hizi sheria za 2007 zilipitishwa makusudi na serikali ya kifisadi ili kujilinda wenyewe na maswahiba wao. Zitahitaji kubadilishwa haraka mara tutakapokuwa na bunge linalowakilisha maslahi ya watanzania.
   
 5. Sungurampole

  Sungurampole JF-Expert Member

  #5
  Aug 17, 2012
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 987
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kama haya asemayo Hosea ni kweli - Anachotuambia ni kwamba wapowapo tu lakini tusitegemee chochote.

  Swali ni je, haya kayajua lini na je, kwa nini asiachie ngazi kuliko kuendelea kuigiza kufuatailia mafisadi wakati anajua hakuna kitu?
   
 6. mangikule

  mangikule JF-Expert Member

  #6
  Aug 17, 2012
  Joined: Jun 11, 2012
  Messages: 3,176
  Likes Received: 1,257
  Trophy Points: 280
  Rushwa ni Taasisi!! Kweli tuna kazi kumbe Hosea yuko chini wa DPP!! Ndiyo maanaaaa!!!
   
 7. s

  samakimbichi New Member

  #7
  Aug 17, 2012
  Joined: Aug 17, 2012
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wahuni watupu,serikali hii ni ya viongozi dhidi ya wananchi kwa kutumia kigezo cha sheria.Tuliona Africa kusini tukapiga makelele kwelkweli,leo kwetu walewale tunaona sawa tu mradi hatujagombana na ukiuliza unahatarisha amani kama ilivyokuwa kule.Inabidi wananchi waunde serikali yao itakayo wajali na viongozi wa leo wabaki na yao watafunane,hapo ndo kwenye suluhisho
   
 8. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #8
  Aug 17, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Ili tuendelee tunahitaji vitu vinne
  Watu
  Ardhi
  Siasa safi
  Uongozi

  Adui yetu mkuu ni CCM. Ameleta ujinga, maradhi na dhulma (Ufisadi). Darasa la saba hajui kusoma? Duhhh
   
 9. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #9
  Aug 17, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,323
  Likes Received: 1,788
  Trophy Points: 280
  Alikaa kimya muda wote amengundua ipo siku watu watamdai yeye kama Hosea kwamba ndiye aliyeshindwa kazi.
   
Loading...