Sheria za mikutano ya hadhara ni kwa vyama vya upinzani tu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheria za mikutano ya hadhara ni kwa vyama vya upinzani tu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sammosses, Feb 26, 2012.

 1. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #1
  Feb 26, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Hatari ninayoitabiri ambayo inaweza kuleta maangamizi kwa nchi yetu ni juu ya matumizi ya sheria mbalimbali zinazovunjwa na mhimili mmojawapo wa dola ili kukidhi matakwa yake binafsi au kuonyesha ubabe kutokana na upofu wa makusudi unaofanywa na waliopewa dhamana ya kusimamia utekelezaji wa sheria hizo.Ni mara nyingi imekuwa ikitokea ama viongozi wa mhimili mmoja wa dola ambao ni serikali kuvunja sheria makusudi labda kwa kuwa wao ndiyo wenye dhamana na vyombo hivyo vya dola au ni jeuri tu na ulevi wa madaraka uliokithiri kiasi cha kushindwa kusoma maono yajayo.Nachelea kusema hivi kutokana na matukio mbalimbali yanayojiari hivi sasa ndani ya nchi yetu kwa kusababishwa na vyombo vya dola kupendelea upande mmoja.Sipendi kuamini kama sheria zilitungwa ili zivunjwe kama wengi wanavyoamini,japokuwa ndo hali halisi kwa sasa na serikali imekaa kimya bila kutolea kauli juu ya ukiukwaji huo. Hatari hii,inaweza kutokea wakati wowote iwapo upande wa pili wa shilingi nao ukiaamua kuvunja sheria makusudi kwa kuona mhimili mmoja ambao ni serikali ndo mvunjifu mkubwa wa sheria hizo.Tunapozungumzia utawala wa sheria ina maana kwamba sheria zitekelezwe bila kujali huyu ni nani, ndo maana tukasema sheria ni msumeno haina upendeleo,inakata kote.Hakuna palipozungumzwa kiongozi fulani akivunja sheria aachwe hivi hivi.Waziri mkuu mh.Mizengo Pinda(mtoto wa mkulima) aliwahi kuvunja katiba kwa kutoa kauli iliyowataka wananchi kujichukulia sheria mkononi kwa kuwaadhibu wale wote watakao wauwa albino wakiwakamatwa nao wauwe.Hali iliyosababisha kumgharimu machozi mbele ya bunge letu tukufu,wabunge walimsamehe baada ya utetezi wake ambao kama si hisani yao leo tungekuwa na waziri mkuu mwingine.Tangu kutokea tukio hilo leo hii Waziri mkuu huyo huyo anafanya kosa lingine tena kwa kuamua kwa makusudi kuvunja sheria kwa kuzidisha muda katika mkutano wake wa hadhara mpaka saa 12.57 jioni huku askari polisi wakimwangalia bila kumchukulia hatua zozote.Ni mara ngapi viongozi wa upinzani hufikishwa kwenye vituo vya polisi kwa kosa la kuzidisha muda.Kama uwanja wa siasa upo fair basi uwe kote si kwa matabaka.Athari ya polisi kuwafumbia macho viongozi wa serikali ama chama tawala wanao vunja sheria huweza sababisha chuki na machafuko dhidi ya serikali yao pale upande wa pili ambao ni vyama vya upinzani utakapoamua nao kuvunja sheria na kuzidisha muda tena kwa kupata support ya wananchi kisha wakanyimwa fursa ile ile iliyotumiwa na serikali kuzidisha muda. Pia onyo kwa chombo chetu cha polisi kwa kushindwa kufanya kazi yao barabara,wawe thabiti katika kuhakikisha uvunjifu wa sheria unadhibitiwa bila upendeleo wowote.Polisi imekuwa chanzo cha machafuko mbalimabali hapa nchi,ama kwa kuelewa wao mdogo au kutumiwa na serikali kama chombo cha kuilinda serikali ya chama tawala ili kukidhi matakwa ya chama hicho bila kujali utawala wa sheria.Tuangalia yaliyotokea Misri,Tunisia na kwingine kote duniani ili wapate fundisho na kuhifadhi amani ya nchi yetu.Mwisho nakaribisha michango mbalimbali kuhusiana na thread hii kama kuna upungufu waongezee maboresho ili kuisaidia serikali yetu.Nawakilisha
   
Loading...