Sheria za Kazi inasemaje kuhusu Mfanyakazi katika Kuhama Kituo cha kazi.

stanluva

Senior Member
Apr 7, 2009
153
32
Wajuzi wa sheria naomba kusaidiwa hili! Hivi sheria inasemaje kuhusu uhamisho wa mfanyakazi kutoka Kituo kimoja hadi kingine hasa kama anafuata familia yake! Je kuna sehemu yeyote inayo mlazimisha mfanyakazi kutafuta wa kubadilishana naye kituo ndipo ahame?

Maana wengine tunapoteza haki zetu ya mfanyakazi kwa kutojua sheria! (Maana waajiri wamekua mstari wa mbele kuzuia wafanyakazi kudai haki zao).

Kwa ujumla, sisi kama wafanyakazi tunapoomba uhamisho ili kuwa karibu na familia familia zetu, wanaohusika na idara fulani fulani wanasema lazima tutafute wa kubadilishana nao la sivyo hatutaweza kuhama.

Je sheria ina lolote kuhusu habari hii?
 
Asante mkuu....lkn kama unaweza kuidadavua pia itakuwa ni vyema sana.

Hakuna kipengele cha mke au mme kumfuata mwenzi wake wa ndoa kwenye kituo chake cha kazi. Jitafiti ufanye maamuzi magumu kwani si lazima wote muwe kwenye ajira "Master and Servant relationship"
 
Back
Top Bottom