Sheria za Ajira Tanzania Zikoje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheria za Ajira Tanzania Zikoje?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kichuguu, Dec 2, 2008.

 1. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #1
  Dec 2, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Ukisafiri kati ya Nairobi na Dar kwa basi, utagundua kuwa zaidi ya asilimia 80 ya abiria wale ni wakenya wanaoishi Tanzania; ama wanakuwa wanakwenda Nairobi kusalimia ndugu zao au wanarudi Tanzania wanakopatia riziki zao. Yaani Tanzania inatoa green pastures kwa raia wa Kenya kuliko jinsi Kenya inavyoweza kutoa kwa raia wa Tanzania. Ukichunguza kazi zinazofanywa na wakenya walioko Tanzania, utasikitishwa kuona kuwa kazi hizo zingeweza kufanywa na watanzania lakini zimechukuliwa na wakenya hao. Ukipitia mahoteli mengi hapa Dar es salaama utakuta waajiriwa wengi ni raia wa Kenya. Kuna shule nyingi zinazoitwa academies au whatever fancy name zinafundishwa na raia wa Kenya tu. Katika makampuni mengi tuliyoletewa na viongozi wetu wakidai ni wawekezaji watatuleta ajira kebekebe kwa watanzania, raia wa Kenya ndio wamechukua ajira nyingi, nzuri nzuri, na hata pale ambapo watakuwa wanafanya kazi sawa na raia wa Tanzania, bado wale raia wa Kenya wanalipwa vizuri zaidi ya Watanzania. Juzi juzi nimesoma kuwa CEO mpya wa benki moja pale Tanzania ni mtoto wa mwanasiasa maarufu huko Kenya.

  Ni kutokana na ukweli huo kuwa utaona wakenya wanapigia kelele sana huu muungano wa Afrika Mashariki kwa vile wahenga walisema "Aisifuye mvua basi ujue amenyeshewa"

  Je Tanzania tuna sheria gani zinazodhibiti makampuni kutoajiri raia wa nje hovyo hovyo? Niliwahi kuruka kwa ndege kwenda Mwanza toka Dar wakati ATC ikiwa chini ya SAA, nikakutana na mhudumu kwenye ndege ile akiwa ni msauzi ambaye hata kiswahili alikuwa hajui. Kwa marekani, huwezi kumwajiri raia wa nje (hata yaya wa nyumbani) bila kupata kibali kutoka serikalini; na ili kupata kibali hicho ni lazima uonyeshe kuwa umeitangaza kazi hadharani, na hakuna raia aliyeiomba au aliyekuwa na sifa zitakiwazo, kwa hiyo ndipo unapoomba serikali ikuruhusu kuajiri raia wa nje.

  Pamoja na umaskini wetu na kuwa idadi kubwa ya raia wetu wasiokuwa na ajira, je serikali ya Tanzania inafanya lolote kutunza ajira kwa raia wake dhidi ya ushindani usiokuwa halali?

  Nikirudia maneno ya dharau yaliyotolewa na mwandishi GITAU WARIGI kwa Watanzania:

  (a) Kama Tanzania is dirt poor, its economy a fraction of Kenya’s. Further, it lacks the dynamism and skills to drive its economy forward at the pace of its neighbours. Even tiny Rwanda has a better capacity than can be said of Tanzania. kwa nini wakenya wanaing'ang'ania? je ni kutokana na upumbavu wetu kuwa tunawapa green pastures kirahisi? Wakati umefika kwa viongozi wetu kuangalia statements za namna kwa uzito wote.


  (b) Madai kuwa Mexico knows the immense benefits it reaps from the North America Free Trade Association (NAFTA) even though its economy can nowhere be compared with the United States’ or Canada’s. ni ya kipuuzi na wala hayalingani na mazingira tuliyonayo. Kama kweli uchumi wa Kenya ni imara kiasi hicho, ni dhahiri ungekuwa unavuta wafanya kazi kutoka nje, siyo kuwa wakenya ndio wangekuwa wanakimbilia kuja kufanya kazi Tanzania. Kwenye NAFTA ni wamexico wengi ndio wanaoingia kufanya Marekani, ndiyo maana OBAMA aliahidi kuiondoa Marekani kwenye NAFTA. Na vile vile NAFTA haikusema kuwa raia wavuke mpaka kirahisi kama Kenya wanavyotaka iwe, hata kutoka Kanada kuingia USA lazima upitia immigration kama kawaida, na kutoka Mexico kuingia USA ndiyo ngumu zaidi.

  Mimi naona kuwa dawa ni kwa serikali yetu kuweka utaratibu wa kulazimisha makampuni yote yanayofanyia shughuli zake Tanzania, hata kama ni makampuni ya Kenya, yasiajiri raia wa nje bila kuonyesha kuwa wamekosa watanzania kushika kazi hizo.

  Halafu pia watanzania tuamke, tuache upumbavu unaofanya watu kama bwana GITAU WARIGIP watutukane collectively namna hiyo. Siyo yeye tu anayesema kuwa watanzania ni wajinga; utashangaa kuwa hata wasomali, waganda, wanyarwanda, na warundi wote wanatusema vivyo hivyo.

  Saa ya kuamka ni sasa
   
 2. DMussa

  DMussa JF-Expert Member

  #2
  Dec 3, 2008
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 1,301
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Kichuguu
  Well said!.... i couldn't think of better ways. Lets learn from the past
   
Loading...