Sheria yetu ya ndoa kila kukicha inazidi kupitwa na wakati

Tella Mande

JF-Expert Member
Jun 2, 2018
333
500
Sheria yetu ya ndoa kila kukicha inazidi kupitwa na wakati na teknoligia. Hebu tutizame mifano ifuatayo inayoonyesha mapungufu ninayoongelea.

1. Kumekuwa na ongezeko la watu wenye ndoa kufunga ndoa ya pili bila kutambulika. Mtu akiwa ndani ya dini moja akihama dini hiyo anafunga ndoa kwenye dini hiyo mpya. Anapewa cheti cha ndoa cha dini ba cha serikali kwa majina mapya. SULUHISHO: Vyeti vya ndoa haswa vya serikali viwe na picha na fingerprint. Hii itakuwa rahisi kumtambua mwanandoa anayetaka kufunga ndoa ya 2 kinyemela.

2. Sheria ya ndoa iwe na kufungu kinachoitaka serikali iwe na database ya wanandoa walio na vyeti vya serikali vikiwa na fingerprint na picha ili iwe rahisi kusearch. Kabla ndoa kufungwa wafungaji ndoa walazimike kupata printout ya search kama tunavyofanya kwenye ardhi/ viwanja vilivyopimwa.

3. Sheria ya sasa haitambui watu wenye majina zaidi ya 1. Zipo ndoa feki ambazo watu wamefunga na wanaume/ wanawake kwa kutumia majina waluotumia shule baada ya kurudia. Wengine walibadili dini ukubwani hivyo kuwa na majina zaidi ya moja ambayo tayari yapo kwenye vyeti. Wengine wana majina ya utotoni ambayo ni maarufu kuliko ya shule.vyeti vya ndoa vitoe nafasi ya kuyatambua majina yote maarufu ya mwanandoa mtarajiwa.

4. Wanandoa wengi wanadanganya umri wakati wanaingia kwenye ndoa. Kuwe na utaratibu wa kisheria wa kuthibisha umri.

5. Umri wa kuolewa uzingatie mazingira halisi ya wahusika. Vijana sasahivi wanamaliza la saba na umri mdogo na wanapevuka mapema sana. Sasa ukisema mpaka miaka 18 wakati keshamaliza la saba na miaka 13 ni kuwaadhibu wazazi bure maana kukaa na mtoto wa kike anayetaka kuolewa miaka 5 bila sababu ni shughuli. Kuwe na utaratibu wa kisheria wa kuthibitisha kuwa hasomi na hakupata hiyo fursa na haozwi kwa nguvu kutafuta mali.

6.sheria itambue status ya ndoa na sio kuziacha plain. Kama ndoa ni ya mke wa 2,3 nk isomeke kwenye cheti cha ndoa. Au kama mtu kafiwa na mke/ mume hivyo kuifanya hiyo ndoa ya 2 ,3 nk badi kuwe na sehemu ya kuonyesha.

7. Sheria itambue ndoa za mikataba na hizi ziseme wazi kuwa sio za kidini ila watambulike kisheria. Bado ndoa hizi zisiwe za jinsia moja. Sheria itoa nafasi ya muda wa ndoa na utaratibu wa kugawana kilichochumwa ndani ya hiyo ndoa kwa wanandoa.

8. Sheria itambua na kuainisha haki na wajibu wa watoto wa wazazi wanaoingia kwenye ndoa wakiwa na watoto. Haswa walioko chini ya miaka 18 na wanaosoma. Hapa nalenga wazazi waoachana au kufiwa na wenzi wao na kuamua kuanza maisha mapya ya ndoa.

9. Ndoa baina ya raia wa Tanzania na wageni au ndoa baina ya wageni na Raia wa Tanzania, haswa ndoa zinazofungwa nje ya Tanzania. Sheria ilazimishe kuandikishwa ndoa hizo ili kulinda haki za mwanandoa mtanzania. Hapa ni muhimu kuoanisha sheria za uhamiaji na ndoa kwani zao la ndoa yaani mali na watoto vilindwe.

10. Kumekuwa na kesi nyingi za haki ya kuzika mwanandoa anapifariki baina ya mwanandoa aliyebaki na ndugu wa marehemu. Huu ni upungufu wa sheria. Sheria itoe haki kwa mwanandoa aliyebaki na watoto wake.

11. Sheria ya ndoa na mirathi zioanishwe. Itoe haki na angalizo. Endapo mwanandoa atathibitika kusababisha kifo cha mwenzi wake kwa makusudi au kumnyima matunzo stahiki , basi kiwe kigezo cha kumnyima usimamizi wa mirathi. Na endapo atakuwa mrithi na akiamua kuoa au kuolewa basi mali ugawanywe kwa watoto kwanza yeye aingie kwenye ndoa mpya na ile sehemu yake stahiki na sio mali zote.

12. Sheria itamke na iweke utaratibu wa watoto wanaokuwa adopted kwa wanandoa wasioweza pata watoto kabisa au wanaotaka kuchanganya jinsia. Utaratibu ujumuishe uhuru wa kuadopt ndani na nje ya nchi.

13. Sheria iangalie uwezekano wa kukataa baadhi ya ndoa. Kama ilivyo kwa ndoa za jinsia moja, ndoa za watoto pia ndoa zenye tofauti mkubwa wa umri zipitie mchakato fulani wa kisheria...ikiwezekana kuwe na hearing... kusihekuwa na kutapeliana. Mmoja akijidai mapenzi kumbe mali.

UNASEMAJE MDAU.
NA WEWE ONGEZA LA KWAKO
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom