Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 93,479
- 119,309
Hivi hawa wabunge wetu wanaijua kweli kazi yao? Wanaujua wajibu wao? Wakati mwingine mtu unaingiwa na shaka kama kweli hata wanajua wapo humo bungeni kufanya nini!
Kuona mbunge analalamika kwenye mitandao ya kijamii kuwa eti sheria yetu na madini ni mbaya na anadiriki kusema kuwa "Kama Magufuli ana nia njema angeanza na sheria. Hajaanza na sheria, hana nia njema" ni kilele cha ujinga.
Magufuli aanze na sheria kwani yeye ndo mtunga sheria? Hivi hawa wabunge wetu wakoje lakini?
Bunge ndo chombo cha kutunga sheria nchini. Magufuli hatungi sheria. Huyo Magufuli ataanzaje na sheria?
Kwa nini huyo Lissu na wenzake wasiwasilishe muswada wa kutunga sheria mpya ya madini au kufanyia marekebisho iliyopo kama wanaiona ni mbaya?
Kinachomshinda huyo Lissu kufadhili na kuwasilisha hoja ya muswada wa kutunga sheria mpya ya madini ni kitu gani?
Kama hili suala si la kichama, kama suala ni la kitaifa zaidi, sioni kwa nini iwe shida kwa mbunge yeyote yule, awe wa CCM, CHADEMA, CUF, ACT, na kadhalika kuwasilisha hoja ya sheria mpya na kushawishi wabunge wenzake wamuunge mkono ili waibadili hiyo sheria iliyo mbaya.
Mimi ningependa kuona hao wabunge wanaopenda sana kuongea kwa hisia kuhusu mambo mbalimbali wakijikusanya na kuwa pamoja bila kujali itikadi zao za kisiasa na kufadhili hoja ya muswada wa kutunga sheria mpya ya madini.
Waache kulialia ili kujipatia visifa vya rejareja na waanze kutenda sasa. Wao ndiyo watunga sheria. Magufuli hatungi sheria.