Sheria yavunjwa na aliyeapa kulinda, ateua msajili kuwa Mkurugenzi, CCM, watanzania wamelala tu

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
14,047
20,409
Watumishi wa Umma wanaongozwa na Sheria zifuatazo:

1/Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini namba 6 ya Mwaka 2004 sura ya 366

2/Sheria ya Utumishi wa Umma ya mwaka 2003.

3/Sheria ya Vyama vya Siasa namba 5 ya mwaka 1992 sura ya 258

4/Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma za mwaka 2009( Standing Order for the Public Services).

5/Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

Kuna orodha ya Watumishi wa Umma ambao hawaruhusiwi kuwa wanachama wa Chama chochote cha Siasa wala kujihusisha na siasa ( strictly prohibited from joining or having any political affiliation) ingawa watakuwa na haki ya kupiga kura tu ( suffrage/right to vote ) .

Watu hao /watumishi hao wametajwa kama Ifuatavyo;

Kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 ibara ya 147(3)(4) ambao ni askari polisi, magereza, Usalama wa Taifa, JWTZ, Mgambo, Nk. Ibara hiyo imewapiga marufuku kabisa.

Orodha nyingine imetajwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 ibara ya 113A ambayo imetaja kuwa ni Msajili wa Mahakama, Hakimu wa ngazi yoyote, Jaji wa Mahakama Kuu /rufani.

Katiba pia imeorodhesha kwenye ibara ya 74(14)(15) ambao imewataja kuwa ni Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Wakurugenzi wa Tume ya Uchaguzi, Wakurugenzi wa Wilaya, miji ,Manispaa na Majiji pamoja na watendaji wa vijiji na Kata.

Watu wengine wametajwa vizuri sana kwenye Sheria ya Utumishi wa Umma kama vile maafisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Pamoja na wafanyakazi wa ofisi ya Bunge yaani Katibu wa Bunge na sekretariet yake.

Katika uendeshaji wa shughuli za Utumishi wa Umma na kutafsiri Sheria ya Utumishi wa Umma, zilitungwa Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma za 2009 (Standing Orders for the Public Services 2009) .

Katika Kanuni hizo, kanuni ya F20(1),(2) imeorodhesha watumishi wasiotakiwa kujihusisha na siasa kabisa ambao kwa kifupi ni hawa

Askari Polisi

Askari Magereza

Maafisa wa PCCB

Maafisa wa Jeshi la Zimamoto

Maafisa wa Bunge

Askari wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)

Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)

Askari wa Mgambo (Militia)

Majaji wa Mahakama Kuu/Rufani

Msajili wa Mahakama

Msajili wa Vyama vya Siasa

Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo, Wilaya na Hakimu Mkazi

Lakini watumishi ambao hawajatajwa au kuorodheshwa hapo wanaruhusiwa kujiunga na kujihusisha na vyama vya siasa. Yaani wafuatao wanaruhusiwa ni Pamoja na Walimu, madaktari, mainjinia, Wanasheria (mawakili), wauguzi, nk.

Lakini pamoja na kuwa wameruhusiwa kufanya siasa au kujishughulisha na siasa kuna masharti yaliyowekwa waziwazi katika utekelezaji wa hilo. Masharti hayo yameorodheshwa katika Kanuni ya F(21)(a) -(h) .Masharti hayo ni pamoja na

1/Kutotoa huduma kwa umma kwa ubaguzi wa kiitikadi za kisiasa.Mfano,kujiepusha na kuwatenga wanafunzi ambao wazazi wao au wao wenyewe ni wa chama kinzani na cha kwako mwalimu. Au Daktari wa Chama fulani kukataa kumtibu mgonjwa wa chama fulani cha Siasa.

2/Kutovaa mavazi ya Chama eneo la Kazi. Mfano kuvaa magwanda ya CHADEMA au CCM hospitali au shuleni ni *kosa* .

3/Kufanya siasa muda wa kazi. Muda wa kazi kwa mujibu wa sheria ni 1:30 - 3:30 yaani masaa 8(saa 8). Hivyo ni ruhusa kufanya siasa kuanzia saa 10 jioni mpaka saa 12 asubuhi.

4/ Ni kosa kutumia nyaraka za taasisi unayofanyia kazi kwa maslahi ya kisiasa. Mfano, shuleni kuna Ufisadi wa mali za shule, mwalimu usichukie hizo taarifa ukaenda kuzitumia jukwaani wewe mwenyewe kujipatia umaarufu wa kisiasa (political mileage). Unachopaswa kufanya ni kuwapa wengine taarifa hizo

5/Usitoe kauli au maneno ya kuidhalilisha serikali kwa kiwango kitakachopunguza hadhi au heshima ya serikali kwa

*NOTE* :eneo la Kazi la Mtumishi wa Umma limefafanuliwa vizuri na sheria ya Vyama vya Siasa namba 5 ya mwaka 1992 sura 258 kifungu cha 12(2)(3) cha sheria.
 
Ndo akili zako zinapoishia, Hata Bashiru Ally anaeza kuteuliwa kuwa mkurugenzi wa tume ya uchaguzi isipokua atakubali na kukoma kuwa mwanachama wa chama chake..
Same to Lissu anaeza kuteuliwa kuwa jaji isipokua atabid akikane chama chake, acha kukurupuka
 
Back
Top Bottom