Sheria ya Vyombo vya Habari kuanza kutumika Januari 2022

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa amewataka wamiliki wa vyombo vya habari na waandishi wa habari kuhakikisha wanajipanga ili kuendana na matwaka ya Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari (2016), itakayoanza kutumika Januari mwakani.

Wakati akizingumza na na wahariri na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, Bashungwa alisema sheria hiyo itakapoanza kutumika changamoto nyingi zitakwisha.

“Niwaambie tu, Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari ya mwaka 2016 ambayo imetoa muda mrefu wa media na waandishi kujiandaa ambao unaisha Desemba mwaka huu, tutaanza kuitumia rasmi Januari mwaka 2022, hivyo kama kuna ambao hawajakidhi matakwa ya sheria hiyo wahakikishe kabla ya Januari hiyo wanakuwa na vigezo, tukianza kuitumia itaondoa changamoto nyingi zinazowakabili,’’alisema Bashungwa.

Alisema kwa upande wa waandishi wa habari sheria hiyo inawataka ili kufanya kazi ya uandishi wa habari, lazima mhusika awe na sifa ya elimu angalau kuanzia ngazi ya stashahada kutoka vyuo vinavyotambulika na katika kuhakikisha kigezo hicho kinafikiwa, serikali ilitoa miaka zaidi ya minne kwa wasio na sifa kujiendeleza.

“Sheria inamtambua mwandishi wa habari kuwa ni yule mwenye sifa kuanzia ngazi ya Diploma, na kwa kutambua baadhi hawana, wana sifa za cheti tu ulitolewa muda wa mpito kujiandaa pamoja na wamiliki wa vyombo hivyo ili na yale wanayowahusu wahakikishe wanatimiza vigezo, tukianza hatuna mchezo,’’ alisema Bashungwa.

Akizungumzia maslahi ya wanahabari, Bashungwa alisema vyombo vingi nchini vinawatumia waandishi kama vibarua tu, wengine hawalipwi na wengi wao hawana mikataba ya ajira na hata wale waliyonayo masharti hayatekelezwi, hivyo kuanza kutumika kwa sheria hiyo kutasaidia kuondoa changamoto hizo.

Kanuni za sheria hiyo ambazo zitaenda sambamba na kuanza kutumika kwa sheria hiyo hapo mwakani, zitaondoa sitofahamu ya maslahi ya kundi hilo, lakini pia wamiliki na waandishi hao watawajibika kutekeleza wajibu kwa kuhakikisha wanafanya kazi hiyo kwa weledi mkubwa.

Alisema ni vyema kwa mwaka mmoja uliobaki, wamiliki na waandishi hao wakaisoma tena sheria hiyo ili kujua wajibu wao na kama kuna vigezo hawana wahakikishe wanavitimiza kabla ya kuanza kutumika kwa sheria.

“Sheria hii ni nzuri, inaonesha wajibu wenu na haki zenu na hayo mambo ya maslahi yapo humo kisheria, sasa ni vizuri kuipitia, kuisoma tena na kuangalia je, vigezo vya matakwa ya sheria hiyo mnavyo? kama bado fanyeni bidi mkamilishe ndani ya mwaka huu mmoja uliobaki,” alisema Bashungwa.

Chanzo: Habari Leo
 
Ni ngumu sana kwa mshahara wa 200k 150k au 100k hujala hujahudumia familia na upo na certificate ukasome mil 2 yani daaah hiyo kuipata tu miezi inapita hatari tupu.
 
Hiyo elimu ya diploma angalau itasaidia kuongeza uwezo wa waandishi kiakili, hata wakimfanyia mtu interview watajua ni maswali gani wanatakiwa kuuliza, sio hivi wanavyofanya sasa hivi unamuuliza mtu na heshima zake huwa ana "do" mara ngapi kwa siku.

Kwenye hilo la mikataba ya ajira wengi watakosa kazi, sidhani kama hayo mashirika yatakayowaajiri yatakuwa na uwezo wa kuwalipa mishahara watakayohitaji, biashara yenyewe siku hizi haiendi, magazeti hayanunuliwi.
 

"...tukianza kuitumia itaondoa changamoto nyingi zinazowakabili,’’alisema Bashungwa.
1937478154.jpg
 
Back
Top Bottom