Sheria ya VOTE OF NO CONFIDENCE irekebishwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheria ya VOTE OF NO CONFIDENCE irekebishwe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by RUBERTS, Apr 24, 2012.

 1. RUBERTS

  RUBERTS Senior Member

  #1
  Apr 24, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 136
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wana-JF, mi naona hii sheria ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na serikali ifanyiwe marekebisho kwa kuondoa kipengelea kinachotaka majina na sahihi za wabunge 20%. Badala ya wabunge kujiorodhesha na kutia sahihi zao, wapige kura ya siri bungeni kwanza kama process ya awali ikiwa mbunge yoyote atapeleka hoja ya kutokuwa na imani na serikali. Ikiwa zaidi ya 50% watapiga kura ya ku-favour hoja basi hoja hiyo ndo mchakato wake uendelee kwa mtoa hoja kuweka utetezi wake mezani ni kwa nini anataka serikali iondolewe madarakani. Hitimisho lake pia liamuliwe kwa kura za siri za kutokuwa na imani na serikali. Hii ya kujiorodhesha hadharani inawafanya wabunge wawe waoga wa kushughulikiwa. Na tayari tumeishaambiwa hao wabunge waliosaini kwenye karatasi ya Zitto wametishiwa maisha yao. Kura ya siri inamhakikishia mbunge usalama wake, na ndiyo demokrasia ya kweli.

  Naomba kuwasilisha.
   
 2. Eng. Y. Bihagaze

  Eng. Y. Bihagaze Verified User

  #2
  Apr 24, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 1,481
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Heshima Kiongozi..

  nadhani ungeenda mbele na kupanua jiografia ya ubongo wako ukafikiri zaidi kwenye mambo matatu hivi..

  1. Mwoga ni Mtu mbaya sana ..sana hasa kwenye ujenzi wa taifa changa kama letu.. Kiongozi mwoga hawezi kukemea maovu, Kiongozi mwoga hawezi kusimamia sheria, kiongozi mwoga hawezi kutetea walioonewa.. Kiumbe mwoga daima ni wa kumwogopa zaidi ya ugonjwa wa namna yoyote ile.. Mtu mwoga hajiamini hata kwa kauli za mdomo wake, mtu mwoga daima ni mnafiki anaependa kuonekana ni mwema kwenye makundi tofauti ndani ya jamii moja. mtu mwoga hana HESHIMA.

  2. mawazo yako yana Ubinafsi wa hali ya juu.. kama ziada ya wabunge wawe wakipiga kura zao uvunguni mwa mapaja yao, je unamaaanisha mtoa hoja peke yake ndiye aonekane mbaya mbele ya jamii. Mbona mtoa hoja humzungumzii? labda ungesema na mtoa hoja awe anaitolea uvunguni mwa kiti cha madam speaker. tukifikia hapo basi na ripoti zote za kamati za kudumu za bunge ziwe zinawekwa uvunguni, tutaenda mbali zaidi na maswali yawe yanapitia uvunguni manake mengine yanawananga wahusika moja kwa moja.. tukienda mbali zaidi nadhani hatuta kuwa na bunge..

  3. Michango, Hoja, maswali na Vuguvugu kama hili ndilo linaloleta uhai wa Bunge.. Lazima wabunge, mawaziri, watendaji wakubwa na wadogo wa serikali wawe makini na kazi zao wakijua kwamba makosa kidogo yatasababisha matatizo si kwa jamii tu bali pia kuyeyuka wa ajira zao. na hii ndio tafsiri ya kuwajibika. kama kamsemo ketu kazi ni dhamana...

  Mwisho usiwe mchoyo wa kufikiria, Wabunge hawa hawapigi kura kwa dhamira ya chuki binafsi, kisasi, choyo, wivu au linginelo juu ya Kaka Mizengo Peter Pinda.. Wanamuheshimu, Wanampenda na kumkubali. wala sio kwamba Pinda kama Pinda kakosea hapa au pale, ni Dhana zima ya Uwajibikaji. hata mawaziri nao sio kwamba moja kwa moja wanahusika na kukwiba, bali ni dhana ile ile ya uwajibikaji kwamba ulipaswa kumwangalia mtoto kama kajinyea kabla ya kumleta kwenye ubwabwa ni Nundu tu anapaparika mimi hata simuelewi mbaba wa watu, nahisi huyu mtu kuna kitu kweli kakwiba huyu....
  ndio maana wabunge hawa kama umekuwepo dom, baada ya bunge huku sahihi zinaendelea huku wanasalimiana kama kawaida..

  IMG_9256.JPG   
 3. RUBERTS

  RUBERTS Senior Member

  #3
  Apr 24, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 136
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mimi sijasema mtoa hoja ndiye atakayezungumza peke yake. Baada ya kuwasilisha hoja kwa Spika na hoja hiyo kupata kibali cha kujadiliwa kwa njia ya kura, ni wazi kwamba kila mbunge atatoa mchango wake, na mawaziri watatoa utetezi wao. Haiwezi kuwa hoja ya mtu mmoja ndo ikatosha kuiondoa serikali madarakani. Mijadala yote ya kutupiana mawe itahitimishwa kwa kura ya siri tena. Kwa vyovyote vile kura ya siri ni muhimu ktk kufanya maamuzi ya haki. Uwoga upo mwingi kwa watu hasa kwenye serikali zisizokubali mabadiliko kama hii yetu. Mabadiliko wanayaongea mdomoni kufurahisha wafadhili lkn moyoni hayamo. Hii yote ni kwa sababu wameiba sana wanaogopa serikali nyingine kuwasulubu. Hakuna mtu ambaye yuko tayari kutoa uhai wake kwa ajili ya kutetea umma. Tukubali tusikubali uwoga bado ni tatizo kubwa hapa kwetu. Haitoshi tu kuwasuta waoga au kuelezea hasara za uwoga. Inabidi kutafuta mbinu mbadala ya kufanikisha malengo watu wote wakiwa salama.
   
 4. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #4
  Apr 24, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Itakuwa fujo sasa maana ukikosana tu na Waziri unakuja na VoNC motion. Bunge litakuwa linapiga kura kila siku.
   
Loading...