Sheria ya utumishi wa umma ya mwaka 2009 inaruhusu mwajiri kumfukuza mtumishi akiwa kwenye uchunguzi?

Sep 4, 2021
5
45
Khabari za mchana wanandugu wote humu ndani. Napenda kushare nanyi jambo moja ambalo linanitatiza sana na sijapata bado sijalipatia suluhisho kabisa

Jambo lenyewe ni kuwa nna jamaa yangu alikuwa mtumishi katika ofisi mija ya serikali akapata chagamoto wakamsimamisha kisha akaachishwa lakini jambo lilikuwa pia polisi ingawa mwajiri aliamua kuwafanyia mtimanyongo kwa kuwaundia timu nyengine ya uchunguzi. Wakiwa bado wako polisi wakaongezwa watumishi wengine ila walipkuja hawa watumishi hawakuundiwa tume ya ndani na mwajiri.

Polisi wakaamua kuwapeleka mahakamani wote na wakapata dhamana ila cha kushangaza mmoja anatokea kazini kwenda mahakamani na mwengine anatokea nyumbani na wote wako kwenye hati moja ya mashtaka. Nimejiuliza sana na sijapata jawabu mpaka sasa au inawezekana huyu jamaa yangu ikawa ananificha bado yuko kazini ila amesimamishwa tu?

Kwani kwenye sheria ya utumishi wa umma ya mwaka 2009 inaruhusu mwajiri kumfukuza mtumishi akiwa kwenye uchunguzi. Mana ninajua na nimesoma kwenye vyombo vya habari kuwa ole sabaya bado ni mtumishi na ana kesi ambayo imeshaanza kuongea na washafunga ushahidi kwa upande wa jamhuri, na pia mwakibibi mkurugenzi wa zamani wa temeke ana kesi na bado ni mtumishi, sasa inakuwaje kunakuwa na uonevu kama huu kwa hawa jamaa zetu

Kama wana malalamiko juu ya mwajiri wao ni sehemu gani sahihi kwa sasa ambapo wanaweza kupata haki zao huku wakiwa wanaendelea na kesi mahakamani ambayo nayo upepelezi haujakamilika mwaka wa tano huu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom