Sheria ya utumishi wa umma ikoje juu ya umri wa Dkt. Slaa?

Dickson Ng'hily

JF-Expert Member
Oct 22, 2010
451
485
By the way, hili la Dakta Slaa vipi kuhusu umri ? Coz nakumbuka kuna kipindi Mabalozi walistaafishwa baada kuufikia umri huo wa kustaafu.

Sasa dakta Slaa ni vipi! Na kwani umri wa kustaafu Mabalozi si ni sawa na watumishi umma wengine! Maana dakta Slaa alizaliwa 29/10/1948 so ana miaka 69 sasa....Hapa imekaaje! Najaribu kuwaza tu na wala simuonei 'wivu' dakta Slaa......
 
Tofautisheni vitu hivi:-

1.Utumishi wa umma wa kuajiriwa( mfano ualimu, uuguzi, uaskari n.k) huu una ukomo wa kisheria wa utumishi na kustaafu.

2. Utumishi wa kuteuliwa, huu hauzingatii umri wa kusheria kustaafu, mfano mkuu wa wilaya, mkoa, waziri, balozi n.k

Rais yupo sahihi, kwa hiyo pambaneni na hali zenu wajomba!!
 
Saguda47,

Nadhani wewe ndo unachanganya mambo hapa
...Ubalozi sio nafasi za kisiasa...Ni utumishi wa Umma.
Wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa, mawaziri hizo ndo nafasi za kisiasa.

Pia kuteuliwa hakumaanishi hujaajiliwa...Mfano Nafasi nyingi katika utumishi wa umma ni teuzi toka kwa rais....

Wakurugenzi, maafisa tawala, makatibu wakuu nk. Hawa ni waajiliwa wa serikali na huwa kuna process katika kuwaachisha kazi... Tofauti na nafasi za kisiasa....
 
jidanganye.. kama balozi nao wamehakikiwa vyeti kama watumishi wa ualimu, uuguzi n.k..

mtumishi yeyote wa kuteuliwa na rais sio level ya walimu


Kwa ufahamu wangu mimi Ubalozi unaangukia kwenye utumishi kama ualimu, uuguzi, n.k. Hivyo muda wa kustaafu ni miaka 60.
 
Back
Top Bottom