Sheria ya Usalama ya Mwaka 1996 Ibara ya 5:29(10) Imeiua Tanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheria ya Usalama ya Mwaka 1996 Ibara ya 5:29(10) Imeiua Tanzania?

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by DSN, Apr 21, 2011.

 1. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #1
  Apr 21, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Naaamini daima mlinzi wa mwisho wa nchi yoyote dunia ni USALAMA WA TAIFA wa TAIFA LOLOTE DUNIANI.

  USALAMA WA TAIFA
  ndio roho ya mwisho ya TAIFA kujua MAADUI WA TAIFA na NDIO washauri wa muhimu kutoa MIKAKATI ya njia gani zitumike kupambana na adui awe ni wa ndani ya nchi ama nje ya nchi.

  Kwa mujibu wa sheria ya USALAMA WA TAIFA ya mwaka 1996 Ibara ya 5:2(1), kipengele hiki kinatamka HAITAKUA KAZI YA USALAMA WA TAIFA KUHAKIKISHA KUWA HATUA ZA KIUSALAMA ZINATEKELEZWA[kwa mujibu wa Kisima cha Mjadala]

  Jamani kama kifungu hiki ndio sheria halali, basi kumbe hapa tulipofika USALAMA WA TAIFA SIO waliotufikisha hapa tulipo bali WATAWALA WETU NA BUNGE HILO LILOKAA NA KUTUNGA SHERIA HIYO.

  Ni jukumu sasa la wao kama Walinzi wa MWISHO WA UHAI WA TAIFA wawe tayari kuivunja sheria hiyo,aiwezekana anaelinda nchi amjue adui yake [naamanisha adui wa USALAMA WA TAIFA] kisha azuiwe kujua ni jukumu la nani, njia zipi na wakati gani adui yake atashughulikiwa kumuepusha kumuua yeye kama TAIFA.

  Manake hapa tulipofika sasa bila busara za walinzi wa nchi kutumika ipasavyo, nchi hii iko kwenye hatua ambayo ni bomu wakati wowote likipata mlipuaji linalipuka manake, wananchi wanaitaji majibu ya mafumbo mengi sana na ambayo wenye majibu hayo wapo bado na hawawatosherezi kwa majibu wanayotoa.

  Kwa kuwa wapo na ni jukumu na wajibu wao kuwajua na kupambana [Wajibu wa walionyanganya na bunge mwaka 1996]na maadui zetu. Waludishe wajibu wao wa KUPAMBANA na maadui zetu wa ndani na nje ya nchi.

  TAIFA litakapoingia kwenye matatizo wao pia ni watanzania nao watakuwa ni sehemu ya waathiliwa wa tatizo,mbaya zaidi ni DHAMBI MBAYA kwao na kwa vizazi vyao kwa KUISALITI MAMA NCHI NA WANA WA NCHI kwa kushindwa kutekeleza jukumu la kuilinda na kusimamia USTAWI WA TAIFA ambao kwao ni dhamana waliyokabidhiwa na WATANZANIA.

  Wanaitajika kulingana na nyakati za sasa kuwa mabadiliko kutoka kuwa IDARAna hadi TAASISI [INSTITUTE] yenye IDARA toshelezi na yenye kujitegemea kwa kila jambo hata kama watatumia mabilioni ya shilingi kwani ghalama ya kujenga Taifa jipya na kuludisha uhai wa watakao potea kwa Taifa kuingia matatani, nini kulinganisha na mabilioni hayo. Watanzania wanalipa kodi ili Serikali iwatumikie wapate ustawi binafsi na hatimae ustawi wa Taifa zima na kwa ujumla wake. Na USALAMA WA TAIFA ndio walinzi wakuu kusimamia UHAI HUO WA WANANCHI KAMA TAIFA.

  Sio vyema na sio sahihi leo wananchi wanajadiliana kuwa amani ya Taifa iko hatiani wakati wowote amani inaweza kutoweka, kisa UFISADI na tofauti kubwa ya kipato kati ya Matajiri na Maskini.

  Jibu lipatikane ili gumzo la maisha ya kila siku ya watanzania wajadiliane jinsi gani Taifa lao kipato chake kimeongezeka na wajadiliane mambo ya msingi juu ya mafanikio mema ya utawala uliopo au utakao kuja. Wajadiliane dhidi ya sera zipi za Chama Tawala [Ruling Party] ama Upinzani [Opposition] ni bora kwao na kama zinastahiki kupewa nafsi ya kupewa nafsi ya kutekelezwa ili zilete ustawi.

  Tufike sehemu watanzania wawe gumzo duniani kuwa AFRICA kuna Taifa limeingia kwenye DEVELOP NATION, Why Not?

  Nampenda Mwl JK pamoja na msimamo wake ambao ni udikteta kwa Maslahi ya wengi ulijenga picha ya Tanzania kuwa Taifa la aina yake [Unique] ambayo ni heshima.

  Mimi ni mfuasi wa IMANI Kuwa kila jambo linaloendeshwa na binadamu yoyote duniani linawezekana kwa mwingine pia. Naamini watanzania wanaweza kuwa TAIFA la kupigiwa mfano. Tunakila kitu kutufikisha hapo kuwa Taifa lenye maendeleo, tuna madini, maliasili, ardhi safi na bora, na hata maliasili watu.

  Tunaitaji silaha moja USALAMA WA TAIFA kuwa na nguzo BORA na IMARA pekee kuliokoa TAIFA na kusimamia mikakati yote kwa jicho Chanya [Positive] la Ujenzi wa Taifa na kupambana na wahujumu chanya [Negative] dhidi ya Taifa.

  Katika dhama hizi za leo kuendelea kuamini lolote linalohusu Usalama ni SIRI,jamani nikupoteza Taifa linaloitwa Tanzania. Ndio ni kweli Lazima yanayoendelea Ndani ya Idara [ambayo napenda kuona siku moja soon ikibidi inakua TAASISI] yanaendelea kuwa SIRI, na hata ikibidi baadae miaka Ishirini lilokuwa SIRI linaachiwa kuwa sio siri tena,kwani inasaidia kuleta tafakari baadae ni kwanini uamuzi huo ulichukuliwa, kwa faida ya Taifa. Kwani kama idara [Taasisi] nao ni watu wanaitaji kupumua kwani kikombe kikijaa maji ama chai umwagika.

  Je tumefika hapa tulipo kwa Sheria za kibabe kama hiyo hapo juu ya Usalama wa Taifa 1996 ibara ya5:2(1) ili kuua nchi ama kujenga nchi?
   
 2. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #2
  Apr 21, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Mada yako ni nzuri. Sio jukumu la Idara ya Usalama wa taifa kujitungia sheria yenyewe na kisha kuzitekeleza, ni wajibu wetu na bunge letu kujadili na kuona mapungufu ya sheria hiyo.

  Ni changamoto kwa bunge letu kupitia sheria hiyo na kuangalia upya kama ina ulinzi wa kutosha kwa jamii yetu. TISS kama TISS inapokea sheria kutoka bunge letu na kutekeleza.

  Tukumbuke kuwa upungufu katika sheria zozote za nchi ni upungufu katika ulinzi na usalama wetu. Sheria zipo ili kuanzishwa na kurekebishwa kutokana na mahitaji ya wakati.
   
 3. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #3
  Apr 21, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Katika fani ya sheria kuna wakati ni makosa kuilaimu sheria kwa sababu inawezekana wakati inatungwa ilikuwa ni muhimu kufanya hivyo, kwa mfano sheria ya kuwaweka watu kizuizini au uhujumu uchumi ambapo wapo wanasema ni sheria mbaya na wengine wanaosema ni nzuri.

  Ili kulisaidia bunge letu na TISS yenyewe tukijadili kipengere hicho hasa kwa kuangalia ni maneno gani mbadala yangetumika kwa wakati huu ili kukipa nguvu kipengere hiki na zaidi kuingozea nguvu TISS.
   
 4. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #4
  Apr 21, 2011
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  je ni hii?

  5.-(1) Subject to the control of the Minister, the functions of the Functions

  Service of TISS shall be-

  (a) to obtain, correlate, and evaluate intelligence relevant to security, and to communicate any such intelligence to the Minister and to persons whom, and in the manner which, the Director-General considers it to be in the interests of security;

  (b) to advise Ministers, where the Director-General is satisfied that it is necessary to do so, in respect of matters -relevant to security, so far as those matters relate to departments or portfolios of which they are in charge;

  (c) to cooperate as far as practicable and necessary with such other organs of state and public authorities within or outside Tanzania as are capable of assisting the Service in the performance of its functions.

  (d) to inform the President, and any other person or authority which the Minister may so direct, of any new area of potential espionage, sabotage, terrorism or subversion in respect of which the Director-General has considered it necessary to institute surveillance.

  (2) It shall not be a function of the Service-
  (a) to enforce measures for security; or
  (b) to institute surveillance of any person or category of persons by reason only of his or their involvement in lawful protest, or dissent in respect of any matter affecting the Constitution, the laws or the Government of Tanzania.

   
 5. koo

  koo JF-Expert Member

  #5
  Apr 21, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 258
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hakuna haja ya kuongeza nguvu kwa taasisi iliyokosa umakini wa kujitegemea ikajikuta inatumika kwa maslai ya kikundi kidogo cha watu tunahitaji kutizama upya katika katiba itakayo undwa kuhakikisha taasisi hii inaripot kwa kamati maalumu ya usalama itakayo kua chini ya bunge na kujumuisha wabunge wa chama vyote ili kamati hiyo ya usalama iwe na nguvu za kufuatilia utendaji na uwajibikaji wa TISS ilikama watapotoka iwe rahisi kuwawajibisha hata kwa kuzui pesa za walipa kodi kutumika kuwachakachua walipa kodi hao hao
   
 6. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #6
  Apr 21, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Awali TISS ilikuwa haiongozwi na sheria za wazi na haikuundwa kisheria hadi 1996.

  Inaelezwa kwamba kukosekana kwa sheria hizo kulisababisha chombo hicho kufanya kazi nje ya misingi iliyowekwa na bunge lakini pia hakikuwa na mipaka ya utendaji kazi wake. Kwa kuzingatia hilo TISS iliweza kufanya lolote bila mipaka ya kisheria jambo ambalo ni hatari kwa taifa lolote. Waliokuwepo wakati huo waliona ipo haja ya kuunda chombo hicho kisheria na sisi tuna fursa ingine kuboresha sheria hiyo.

  Inawezekana kutokana na hali hiyo, sheria ya kuunda TISS ya mwaka 1996 iliangaliwa kwa wastani tu ili kukidhi mahitaji ya wakati huo na sio sasa. Sheria ya Usalama wa Taifa ya mwaka 1970 haikuwa ya kuundwa kwa TISS bali inaeleza wajibu wake kwa usalama wa Taifa. Hata hivyo, ndani ya sheria hizo kuna mambo mengi mazuri kuliko yale yasiyokidhi mahitaji ya kizazi kipya.
   
 7. T

  Taso JF-Expert Member

  #7
  Apr 21, 2011
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,653
  Likes Received: 458
  Trophy Points: 180
  Hiki kipengele ni kizuri sana.

  Marekani, kwa mfano, wamewapa CIA uwezo wa kijeshi, kuua mpaka raia, hata nchi za watu. Kosa kubwa.

  Sisi hatutaki TISS wafanye kazi hiyo kwa sababu "kutekeleza hatua za kiusalama" hakutakiwi kufanywa na chombo cha kisiri.

  Zamani, Usalama wa Taifa ya Nyerere ilikuwa inaua watu kisiri. Ina arrest, ina tesa, ina detain, inaua, inahamisha watu na kuwafungia kijijini. Makosa makubwa. Kwa sababu majeshi kama polisi au magereza yana sheria zinazodhibiti mamlaka yao kiusalama, na tunajua polisi akikukamata anaruhusiwa kukufanya nini. Hata kama anakuchunguza kuhatarisha usalama, lazima tujue wanakufanya nini.

  Hayo yakifanywa kwa siri, "wakikutekelezea hatua za kiusalama" halafu ukafa, tutajuaje?
   
 8. A

  Ame JF-Expert Member

  #8
  Apr 21, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Imani yako inabidi uibadili ama sivyo utaishi kwakutojiamini katika dunia hii ambapo mwenye nguvu humla asiye na nguvu. Sisi wengine tunaamini katika ulinzi wa yule aonaye hadi ndani ya moyo wa mwanadamu ambao ni kama msitu mnene wenye giza. Huomba macho yetu yapewe nguvu ya ziada kuona hadi ndani ya hao ili sisi wenyewe tuwe walinzi wa taifa letu na tuko jinsi tulivyo.

  Twajua yote bila msaada wa hao walinzi wenye macho ya damu na nyama. Why waste time on such inferior ways of securing your country? Njoo this side where we see things before they happen we know before they tell us and are always at our watch post to see nothing shall hurt us.
   
 9. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #9
  Apr 22, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Tanzania tunaitaji mabadiliko ndio maana nikasema iwe TAASISI [INSTITUTE] kwa misingi hata Mkurugenzi [DG] wake, atakapoteuliwa na Rais lakini mthibitishaji wake awe ni BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO,ndio wawe wathibitishaji kwa vigezo vya rekodi ya mteule huyo au kwa kupambanisha majina ambayo Rais ataona yanafaha kupigiwa kura na kati ya hayo,moja kuibuka kama jina thibitishwa kuwa Director General [DG] wa Taasisi.

  Itakapokuwa Taasisi mambo mengi nimatumaini yangu yatapewa kipaumbele na mfumo mzima wa TAASISI hiyo kuingia katika zama za kisasa zaidi na kuendeshwa kwa sheria bora na utawala bora zenye kuzingatia nyakati na zama za ulimwengu wa sasa ulimwengu wa Sayansi na teknolojia.Ambako kwa kuwa na Taasisi hiyo itakayosimamia kutambua maadui wetu wa ndani na nje ya nchi katika nyanja ya KIUCHUMI,KISAYANSI,UONGOZI NA UTAWALA,KIJAMII NA KIUTAMADUNI NK, nakutoa majibu na mbinu za kutatua matatizo hayo,chini ya ulinzi wa jicho la Kamati Maalumu [KAMATI YA USALAMA YA TAIFA] yenye muundo wa wakilishi [Wajumbe] ambao wanatokana na mihimili mitatu ya nchi. [Bunge, Mahakama na Rais].Na KAMATI YA USALAMA YA TAIFA hiyo itakua inawajibika kutoa majibu ndani ya BUNGE TUKUFU pindi inapobidi na kusimamia MAADILI na MWENENDO MZIMA WA TAASISI [Watchdog].

  Tunaingia kwenye East Africa Community tunaitaji matayarisho ya kweli kweli ya kitaasisi yenye kukidhi mahitaji na matakwa ya kileo [Usasa] yenye changamoto za kisasa na kila mmoja katika nchi husika kuvutia upande wake.
   
 10. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #10
  Jul 29, 2012
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Kaaz kweli kweli
   
 11. Superbrand

  Superbrand JF-Expert Member

  #11
  Apr 29, 2013
  Joined: Apr 6, 2013
  Messages: 508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Habari wana jamvi;

  kuna kashfa nyingi zikiendelea kuhusu idara nyeti ya usalama wa taifa na wasemaji wengi ni wanasiasa, najiuliza enzi za kuanzia awamu ya tatu kurudi nyuma idara ya usalama wa taifa ilikuwa inajulikana kwa jina tu na utendaji wake wa kazi ulikuwa kimya kimya na sijawahi kusikia kashfa.

  Leo hii unaweza ukawataja wafanyakazi ngazi ya juu asilimia zaidI ya 40% na kuwahusisha na matukio kwa nini hamna hatua kwa hao watendaji?hatuoni kuwa tunaanika mambo yetu hadharani na tunahatarisha usalama wa nchi.
   
 12. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #12
  Apr 29, 2013
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,512
  Likes Received: 5,628
  Trophy Points: 280
  Yapo mambo ya kufanya siri ndugu yangu,kuna wengine wanatamani hata hilo jina la TISS liwe siri khaa!!!
   
 13. v

  vegas JF-Expert Member

  #13
  Apr 29, 2013
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 985
  Likes Received: 405
  Trophy Points: 80
  kama CIA na Scotland Yard wanajulikana why not Tiss?
   
 14. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #14
  Apr 29, 2013
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Wako baadhi ya maofisa hawatakiwi kujilikana na wanajiheshimu. Sio hao!
   
 15. stroke

  stroke JF-Expert Member

  #15
  Apr 29, 2013
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 13,394
  Likes Received: 6,578
  Trophy Points: 280
  ya Ngoswe muachieni Ngoswe..hii idara inadhalilishwa na Chadede, nashangaa kuishi nchi ambayo amani yake inalindwa na the same people that you accuse
   
 16. Erythrocyte

  Erythrocyte JF-Expert Member

  #16
  Apr 29, 2013
  Joined: Nov 6, 2012
  Messages: 44,592
  Likes Received: 25,527
  Trophy Points: 280
  Kama wakifuata malengo yaliyowafanya waitwe TISS hakuna atakayehangaika nao , lakini kinyume na hapo wategemee hata kuburuzwa Mahakamani siku za Mbele , Haiwezekani TISS kumshughulikia mtu , kisa Nyumba ndogo ya kiongozi ! Watajadiliwa tu .
   
 17. H

  Haki Yetu Senior Member

  #17
  Apr 29, 2013
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 162
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi kwani tuna Usalama wa Taifa hivi sasa? Kama usalama wa taifa wanashiriki kwenye kuhujumu uchaguzi wa Rais nchini, hapo tunaweza kujigamba kuwa tuna usalama wa taifa? Watu wanaoshiriki kwenye kuwatesa na kuwang'oa wananchi kucha, meno na macho, tutatamba mbele za mataifa mengine kuwa tuna usalama wa taifa hapo? Kama haya mambo si ya kweli mbona wanaoyasema hawachukuliwi hatua zozote?

  Nilikua nasikiliza leo asubuhi Power Breakfast ya Clouds FM, kwenye suala la uzalendo alikua anaongea nadhan ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, akawa anashangaa kwa viongozi wa siasa kushutumu idara ya usalama wa taifa. Lakini sikutegemea mtu kama huyo azungumze tofauti na yale aliyoyazungumza.

  Kama Usalama wa Taifa wangejikita kwenye kutekeleza majukumu yao ya msingi, hata hao wanasiasa wanaowashutumu wangewasifia. Lakini hivi sasa, inaonekana yeyote anayetaka kuwania uongozi wa nchi hii kwa njia za kidemokrasia kabisa nje ya chama tawala anaonekana kama ni adui wa taifa. Kwa hali hii, mimi pia naona ni vyema na haki kwa wanasiasa kuwataja viongozi wa usalama wa taifa. Kwani wao ni nani bana?
   
 18. omujubi

  omujubi JF-Expert Member

  #18
  Apr 29, 2013
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 4,144
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  kikawaida mkuu wa mkoa naye anakuwa au anahusiana na usalama wa taifa, lakini akitokea akafanya kama yele ya Arusha ya juzi unadhani watu watendelea kuheshimu kutowataja?
  Hiyo miaka ya awamu ya tatu na kurudi nyuma walikuwa wanajitahidi sana
   
 19. D

  Dr Willibrod Slaa Verified User

  #19
  Apr 29, 2013
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 675
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  MTAZAMO,

  Tatizo letu ni la uvivu wa kufikiri. Siku hizi huhitaji kutembea kufuata library. Hata kwenye simu yako ya Mkono unaweza kufanya utafiti japo ndogo tu. Usalama wa Taifa sio Mungu. Fungua simu yako uone Taasisi za usalama za nchi zingine zinavyofanya kazi.

  Kinachopigiwa kelele si siri za kiusalama Bali utendaji kazi wa hovyo wa Taasisi yetu, wanavyoshiriki kwenye majukumu yasiyo ya kiusalama na kujihusisha na kutoa watu kucha na meno Kama walivyofanya kina Ramadhan Ighondu au kununua maofisa wa vyama na kuwadhinikiza kutengeneza ushahidi feki. Katika desturi za usalama Mkuu wa Usalama angelikuwa amejiuzulu kitambo na Kama hafanyi hivyo Mkuu wake angelikuwba ameisha kumtimua kazi iwapo yeye siyo sehemu ya njama.

  Hivyo, kinachoelezwa hapa ni kuwafanya Usalama wa Taifa Kama Miungu watu. Tunaojua haki zetu, tunaofuatilia matumizi mabaya ya fedha za Umma katika Idara ya Usalama wa Taifa tutaendelea kupiga kelele "Mpaka Kieleweke". Kama wewe au na kundi lako hamjui haki zenu, au ndio hao hao wanaotoa watu kucha au vijana wao, au ni uvivu tu wa kutokujua majukumu ya Usalama wa Taifa, basi ni vema ukakaa kimya kuliko kupotosha na kutosha watu bila sababu.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #20
  Apr 29, 2013
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Me like like like ! Umemaliza mkuu
   
Loading...