mteeq
Member
- Sep 8, 2014
- 43
- 16
Mtanzania mwanamme au mwanamke aliyeoa au aliyeolewa na raia wa kigeni ananyanyasika kisaikolojia na hata kifedha pale anapotaka kumuombea mzazi mwezie uraia wa Tanzania. Raia wa kigeni aliyeolewa au aliyeoa Mtanzania pamnoja na kwamba anakuwa ni sehemu ya Tanzania kwa vile aidha ana watoto na Mtanzania au anategemea watoto na mtanzania, lakini anajikuta katika wakati mgumu pale anaopotaka kujihalalisha kisheria (Spouse) na kuchukuwa uraia wa Tanzania. Kwanini raia wa namna hii au kwanini mzazi wa namna hii abaguliwe na kupewa mazingira sawa na yale ambayo raia yeyote wa kigeni anayapewa akitaka kuununua uraia wa Tanzania….!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!?????????????
Kulingana na shereia ya uraia inayotumika hivi sasa ni kwamba raia yeyote wa kigeni anayetaka kuwa raia wa Tanzania anatakiwa alipie US $ 5,000 (Tsh. 11,000,000), bila ya kujali kwamba ameolewa na Mtanzania au amemuoa Mtanzania au ni Mchina au ni Mvietnam aliyekuja kutafuta maisha tu hapa nchini..!!! Wote hawa wamechanganywa kwenye kundi moja na wanatakiwa walipe kiasi hicho cha Tsh. 11,000,000 ndipo waweze kupewa uraia wa Tanzania. Kwanini mtu ambaye ana mahusiano ya kisheria na Mtanzania (Mzazi Mwenza au Mzazi Mtarajiwa) apewa mazingira sawa na raia yeyote wa kigeni ambaye anautafuta uraia kwa maslahi yake binafsi. Nasema raia wa kigeni anautafuta uraia wa Tanzania kwa maslahi yake binafsi kwa vile hana sababu zozote za kijamii zinazomsukuma aombe uraia wa Tanzania zaidi ya kujijengea mazingira mazuri ya kufanya shughuli zake za kibiashara; tofauti na raia wa kigeni ambaye aidha ameolewa au amemuoa Mtanzania na aidha wana watoto au wanatarajia watoto. Raia wa kigeni wa namna hii anazo sababu za kimsingi na za kijamii na kibinadamu zinazomlazimisha awe raia wa Tanzania; kwa vile tayari yeye ni sehemu ya Tanzania kimawazo na hata kijamii (Kidamu). Raia huyu ana watoto wenye damu ya Kitanzania na hivyo ni damu hii ndiyo hasa inayomsukuma atake kuwa raia wa Tanzania.
Kama tutazingatia ukweli huo, basi tunaona kwamba wabunge walioipitisha sheria hii ya uraia hawakuwa makini wa kuangalia tatizo hili kwa mapana na marefu na huku wakishindwa kuwajali wale wote walioolewa au waliooa Watanzania. Wabunge walitakiwa sheria ya uraia waigawanywe kwenye vifungu mbalimbali kulingana na aina ya wageni wanaoutaka uraia wa Tanzania. Inakuwa siyo busara wala ubinadamu kumlazimisha raia mgeni mwenye watoto wa Kitanzania alipe pesa sawa na raia wa kigeni ambaye amekuja nchini kwa makusudi tu ya kutafuta maisha. Kwanini mume wangu au mke wangu ambaye ni raia wa kigeni na pia ni mzazi mwenzangu alipie Tsh. 11,000,000 ili apate haki ya kuwa raia na kuishi na watoto wake wa Kitanzania..!? Sheria hii ya uraia ni gandamizi na inaonyesha wazi kwamba wabunge wetu wengi ni wabinafsi ambao hawakutaka kuyaangalia maslahi mapana ya watanzania waliooa au walioolewa na raia wa kigeni.
Mimi binafsi nilikuwa nashauri kwamba Serikali iifanyie marekebisho makubwa sheria nzima ya uraia ili wageni wote wanaoomba uraia wa Tanzania wagawanywe kwenye makundi mbalimbali yanayozingatia maslahi ya taifa na ubinadamu pia. Kama mimi ni mtoto wa Kitanzania ambaye nimezaliwa na mmoja wa mzazi wangu ni raia wa kigeni; ni kwanini mzazi wangu abaguliwe kwa kutozwa mamilioni mengi ya pesa ndipo apate haki ya kuishi na mimi hapa Tanzania..!? Mimi kama mtoto sikuchagua kwamba nizaliwe na wazazi wa mataifa mawili tofauti kama ambavyo hakuna mtoto anayeweza kujichagulia kwamba azaliwe kwenye ndoa ya dini gani. Sitaki kusema kwamba raia wa kigeni mwenye mahusiano ya kisheria na Mtanzania (Spouse) awe raia wa Tanzania bila kulipa pesa yoyote, hapana, bali ninachosisitiza hapa ni kwamba kiasi cha Tsh. 11,000,000 ni kikubwa mno na kinaonyesha wazi kwamba kiasi hicho kimewekwa kama vile kuwakomoa watanzania wote wenye mahusiano ya karibu na raia wa kigeni.
Nihitimishe makala hii kwa kuiomba Serikali ya awamu ya tano kuiangalia upya sheria ya uraia wa Tanzania na kuhakikisha kwamba kuwapa haki ya kimsingi na kibinadamu watanzania wote wenye mahusiano ya karibu na raia wa kigeni ili kuhakikisha kwamba raia hao wanaishi na familia zao katika mazingira ya upendo na amani bila ya kubaguliwa au kunyanyaswa kwa vigezo pesa. Mimi naamini kwamba kama mwanao uliyemzaa na raia wa kigeni anatambulika kama Mtanzania, basi ni kwanini mmoja wa mzazi wake naye asitambulike kama Mtanzania pale atakapotaka kuwa Mtanzania tena kwa bei Poa….!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Dr. Noordin Jella