Sheria ya uchaguzi yakataza malalamiko ya kampeni kwenda mahakama za kawaida

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Hili angalizo nimeona nilitoe mapema baada ya Mwenyekiti wa NCCR-MAGEUZI, Bw. Mbatia, kuitishia Chadema kuipeleka mahakamani kwa madai ya fidia ya TSHS 3 bilioni kwa kile alichodai kudhalilishwa na chama hicho kwenye kampeni za Kawe.

Na pia Bw. Mbatia kutishia kuwaburuza TAMWA mahakamani kwa kumsingizia kuwa anamdhalilisha dada yetu Mpendwa Halima Mdee ambaye wanachuana vikali kulinyakua jimbo hilo la Kawe.

Tatizo la Bw. Mbatia ni jazba kwa sababu kama angelijipanga vizuri na kuipitia kwa utaratibu sheria ya uchaguzi angelibaini ya kuwa haitoi mwanya kwa Mahakama zetu za kawaida kuwanyang'anya Msajili wa vyama vya siasa na Tume ya uchaguzi kuwa mihimili ya mwisho kwenye malalamiko yatokanayo na kampeni za uchaguzi.

Bw. Mbatia anapaswa afuate sheria ya uchaguzi kwa kuwakilisha malalamiko yake kwa Msajili wa vyama vya siasa au Tume ya uchaguzi ambao wao wamepewa mamlaka ya kutatua migogoro itokanayo na kampeni. Na endapo hataridhika na utatuzi wao basi ndiyo afikirie kujitwika zigo la kushawishi mahakama zetu kuingilia migogoro itokanayo na kampeni za uchaguzi kinyume na matakwa ya sheria hiyo ya uchaguzi ambayo imevipa vyombo tajwa sauti ya mwisho juu ya migogoro hiyo.

Hivyo njozi za Bw. Mbatia za kunyakua kitita cha mabilioni zitabakia ni za alinacha wakati mahakama zetu za kawaida zitakapomjulisha ya kuwa hazina mamlaka ya kutatua migogoro itokanayo na kampeni za uchaguzi na majukumu hayo wanayo akina John Tendwa na mwenzie Jaji Mstaafu .....Lewis Makame(?).....ambaye ndiye Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi
 
Back
Top Bottom