Sheria ya Uchaguzi ni mbovu! Kuendelea kuitumia sio Ujinga? Kuwabebesha masikini gharama za Uchaguzi sio Dhambi?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,337
113,178
Wanabodi,

Declaration of Interest
Mimi ni miongoni mwa Watanzania wazalendo wa nchi yangu, ambaye japo ni mwanachama wa chama cha siasa, lakini tunapokuja kwenye kutanguliza mbele maslahi ya taifa, mimi taifa kwanza ndipo chama kinafuata, kwa sababu siasa za vyama vingi za Tanzania, tunaziona katika baadhi ya maeneo kama ni ujinga ujinga fulani hivi, bora turejee kwenye chama kimoja.

Hivyo nawaomba sana univumilie, ninapoita baadhi ya siasa zetu ni kama siasa za ujinga ujinga fulani kwa baadhi ya vyama na baadhi ya wanasiasa, na nasisitiza, nimesema baadhi, nikimaanisha sii zote na sii wote!.

Tubishane kwa kutoa Hoja, kupangua Hoja, na sio Hoja kwa Viroja!

Hii ni opinion yangu tuu, and everybody has the right to his/her own opinion, hivyo tukitofautiana kwenye hili, tutofautiane kwa hoja, mimi nimeleta hoja zangu kuwa baadhi ya siasa zetu kwenye baadhi ya maeneo fulani fulani, likiwemo eneo la siasa za uchaguzi, kiukweli ni kama ujinga fulani, na zinavyoendeshwa, kuna maeneo zinaendeshwa kwa ujinga ujinga kabisa.

Hivyo naomba uzisome hoja zangu, ili tukitofautiana, tutofautiane kwa hoja, pangua hoja kwa hoja, kwa kupangua hoja zangu na ama kutetea ama kuleta hoja mbadala, nikiwasisitiza na kuwaomba tubishane kwa hoja na kushindanisha hoja kwa hoja, kupangua hoja kwa hoja mbadala na sio watu tumeleta hoja humu, halafu mtu anakuja kuibishia kwa viroja.

Ili tupate maendeleo ya kweli, Watanzania lazima tufanye siasa za ukweli, tuachane na siasa za ujinga ujinga. Nashauri kama ni kweli Tanzania tunataka maendeleo ya kweli ya taifa letu, ni lazima tufike mahali tufanye siasa za ukweli, the real politics na sio hizi siasa za blah blah tunazoendelea nazo.

Tufike mahali, sisi Watanzania, wazalendo wa kweli wa nchi hii, wenye nia njema na ya dhati ya maendeleo ya kweli ya taifa hili letu masikini, hatuwezi kukaa kimya na kunyamaza kwa kuendelea kukumbatia sheria mbovu za uchaguzi ambazo Makama Kuu ya Tanzania imeziita kuwa ni "bad laws" na kushauri, zifutwe, "scraped" kutoka katika vitabu vya sheria.

Lakini kwa vile sheria hizo mbovu, zinakinufaisha chama changu, then tunaendelea kuzing'ang'ania sheria hizo mbovu za uchaguzi, hata kama matumizi ya sheria hizo mbovu, ni kuwawabesha masikini wa Tanzania, mzigo mkubwa wa gharama za uchaguzi wa marudio, kwa sababu za kijinga jinga tuu kabisa, zinazotokana na siasa za ujinga ujinga.

Kitendo hiki cha masikini wa kutupwa wa Tanzania, wanaoishi kwenye lindi la umasikini uliotopea wa kipato cha chini ya dola moja kwa siku, halafu kuja kubebeshwa mzigo wa gharama za kugharimia uchaguzi za marudio, kutokana na diwani mmoja au mbunge mmoja kuhama chama hiki na kuhamia chama kile kwa sababu za kisiasa tuu, hizi ndizo siasa mimi ninazo ziita ni "siasa za ujinga ujinga", na sababu zenyewe zinazowafanya wabunge na madiwani hao kuhama chama kimoja kwenda chama kingine, naziita kuwa ni sababu za kijinga jinga na nyingine ni za kijinga kabisa.

Kwa maoni yangu, this, its not only ni nonsense, but also ni dhambi kwa Mungu, kuwabebesha, Watanzania masikini hawa wa kutupwa, gharama hizi za ziada za uchaguzi wa marudio, kutokana na wawakilishi wao kuhama vyama kwa sababu tuu za hizi siasa zetu za ujinga ujinga, mimi nauita huu pia ni ujinga fulani in the name of politics.

Kwanini Sheria yetu ya Uchaguzi ni Sheria Mbovu
Kifungu 21 cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kinatoa haki ya kila Mtanzania mwenye sifa, kuwa huru kushiriki katika siasa kuanzia serikali za mtaa hadi serikali kuu, bila ubaguzi wowote.

Uhuru wa kushiriki shughuli za umma Sheria ya 1984 Na.15 ib.6 Sheria ya 1994 Na.34 ya ib.4
21.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ya 5, ya 39 na ya 67 ya Katiba hii na ya sheria za nchi kuhusiana na masharti ya kuchagua na kuchaguliwa, au kuteua na kuteuliwa kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, ama moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi waliochaguliwa na wananchi kwa hiari yao, kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria.

Lakini kukatokea kikundi fulani cha watu, naomba kuwaita ni "wajinga fulani", wakaipindua katiba kwa sababu fulani za kijinga kabisa, wakainyofoa haki hiyo ya raia kushiriki uongozi kwa uhuru kabisa, na badala yake, kulazimisha ili mtu ushiriki uongozi fulani, au ugombee nafasi fulani fulani ya uongozi wa umma, ni lazima kwanza udhaminiwe na chama cha siasa! Kiukweli kabisa na ki haki, huu ni ujinga!, this is nonsense!. Katiba yetu haikusema hivyo.

Rev. Mtikila (Mungu amuweke pema peponi) alikipinga kifungu hiki na Mahakama Kuu ya Tanzania, ikatamka bayana kuwa kipengele hicho ni batili na kinakiuka katiba ya JMT hivyo kifutwe kwenye sheria, kila Mtanzania awe huru kugombea nafasi yoyote ya uongozi wa umma, au kwa kupitia vyama vya siasa, au bila kupitia chama chochote.

Lakini wajinga wale, wakaamua kuihalalisha batili ile, kwa kukipenyeza kipengele hicho batili ndani ya katiba yetu, ili kuuhalalisha ujinga wao, hivyo shurti la kudhaminiwa na chama sasa ni la kikatiba.

Jee Lengo la Kudhaminiwa na Chama ni Nini?, Huu Sii Ujinga Tuu?!.
Katiba ilisema kila Mtanzania yuko huru na ana haki ya kushiriki uongozi, toka serikali za mtaa hadi serikali kuu bila kuwa na chama chochote. Hili sherti la kumlazimisha kudhaminiwa na chama lilitoka wapi na kwa kwa nini watu walazimishwe kuwa wanachama wa vyama ili wadhaminiwe, ndipo waweze kugombea?

Mfano mimi naishi Kawe, ikitokea nina uwezo wa kuwatumikia wananchi wa eneo langu la Kawe na kuwaletea maendeleo bila kupitia chama chochote, kwa nini nizuiliwe?

Watanzania tusikubali na tupiganie milango ya wagombea huru na wagombea binafsi ifunguliwe, 2020, watu wenye uwezo wa uongozi, na wenye nia ya kugombea, ili kuwaletea wananchi maendeleo, bila kupitia hizi siasa vyama waingie, and you never know hata sisi kama mimi, tuingie, tushindane kwa hoja na sio kushindana kuhonga, kama hali inavyoendelea sasa!

Kiongozi akishachaguliwa, anakuwa ni Kiongozi wa watu, na sio Kiongozi wa Chama, kwasababu anachaguliwa na watu na Sio Chama!

Ujinga mwingine mkubwa kabisa wa siasa zetu za vyama, ni ujinga ni huu, hata kama mgombea amedhaminiwa na chama cha siasa kugombea, akiishapitishwa na Tume ya Uchaguzi kuwa Mgombea rasmi, japo anatambulika kama ni mgombea wa chama fulani, lakini anachaguliwa kwa kura za wananchi wa eneo lile wote wakiwemo wanachama wa chama chake.

Akiishachaguliwa, mwenyekiti wa mtaa, diwani, mbunge au rais, sasa anakuwa ni kiongozi wa umma na sio kiongozi wa chama kilichomdhamini, bali anakuwa ni kiongozi wa wananchi wa eneo lile waliomchagua, wasio mchagua hata wasiopiga kura, huyu sasa anakuwa ni kiongozi wa wote na sio kiongozi wa chama chake hata kama alidhaminiwa na chama fulani.

Mfano baada ya rais Magufuli kuchaguliwa kuwa rais kwa tiketi ya CCM, lakini hakuchaguliwa na wana CCM pekee, amechaguliwa na wananchi wote na Watanzania wote, na sasa sio kiongozi tuu wa CCM kwa sababu ndie Mwenyekiti wao, bali rais Magufuli ni kiongozi wa Watanzania wote, wa vyama vyote, wa watu wote.

Hali ni vivyo hivyo kwa wabunge, madiwani na viongozi wa serikali ya mtaa, kitendo cha kiongozi wa umma, kujitoa chama kilichomdhamini na kupoteza uongozi wa umma, ubunge, udiwani au uongozi wa umma, ni ujinga ambao haupaswi kuvumiliwa na kuendelea kukumbatiwa.

Nini muhimu zaidi kati ya umma na chama? Kuukosesha umma kiongozi waliemchagua kwa sababu za chama, sio tuu sio haki kwa wananchi waliomchagua, bali ni ujinga uliopitiliza!

Halafu wananchi masikini wa Tanzania, kuja kulipisha gharama za kugharimia uchaguzi wa marudio, sio tuu ni ujinga mwingine, bali ni dhambi kuwagharimisha wananchi hawa gharama za kurudia uchaguzi kwa sababu fulani amejiuzulu chama hiki na kitu cha ajabu kabisa, huyo huyo fulani aliyejiuzulu, ndio anakuja kugombea tena kupitia chama kingine.

Nini kifanyike
Kama nilivyowahi kushauri humu, ukosoaji wenye kujenga, huandamana na ushauri wa nini kifanyike kurekebisha kasoro hizi ili kuundoa ujinga huu unaoendelea nchini mwetu kwa sasa.

  1. Iwekwe faini maalum kwa kila kiongozi wa umma, atakayejiuzulu nafasi yake kwa sababu za kijinga jinga, ikiwemo kukatwa mafao yake na ikibidi kufilisiwa ili kugharimia gharama za uchaguzi wa marudio kwa kulitia hasara taifa.
  2. Viongozi wote wanaojiuzulu, wasiruhusiwe tena kugombea nafasi zile zile walizojiuzulu, kama sababu za kujiuzulu mimi nimeziita ni za kijinga, tusiwakubalie wajinga hawa kugombea tena, ili wasije kutuletea tena ujinga ule ule na kutugharimisha masikini sisi kugharimia uchaguzi wa marudio.
  3. Tubadili sheria yetu ya uchaguzi, kwa kufuta chaguzi zote ndogo, na tuanzishe mpango wa proportional representation na succession plan mgombea wa chama fulani aliyeshinda, tujenge hoja kuwa huyo aliyeshinda ameshinda kwa sababu ya chama c alichogombea hivyo wananchi wamekipa chama ridhaa, hivyo akijiuzulu, akisita kuwa mbunge, diwani, rais kwa sababu zozote zile, chama chake kiteue mwanachama mwingine kushika nafasi ile. Hili likifanyika, amini usiamini, hatutasikia tena kiongozi anajiuzulu kwa sababu za kijinga jinga.
  4. Kama tunaamini aliyechaguliwa ni mtu na sio chama, then diwani au mbunge awe huru kuhama na udiwani wake au ubunge wake kama nchini Kenya.
  5. Mbunge au diwani akijiuzulu au kufariki, tuanzishe kitu kinachoitwa "a proportional representation" kwa mwenye kura nyingi ndiye mshindi, lakini likitokea lolote, akasita kuwa Rais, mbunge au diwani, yule aliyemfuatia kwa wingi wa kura katika uchaguzi uliopita ndio anatangazwa mbunge, diwani, Rais, na kama hayupo anachukuliwa mtu wa tatu, hadi wa mwisho, kama wote hawapo, ndipo uchaguzi mdogo unafanyika.
  6. Kile kipengele cha kudhaminiwa na chama kiishie kwenye uteuzi tuu, kiongozi akiishachaguliwa, anakuwa kiongozi wa umma. kiongozi wa watu, anaweza kuhama chama bila kupoteza uongozi wake kama ilivyo nchini Kenya.
  7. Tubadili sheria yetu ya uchaguzi, kwa kuondoa kipengele cha kudhaminiwa na vyama ili kila Mtanzania mwenye sifa za kugombea uongozi wa nafasi yoyote, aruhusiwe, ila kwenye urais, tuweke vigezo vya ziada, ili asijetokea tajiri mmoja mwenye ukwasi wa kuwanunua Watanzania wote, tukajikuta tuna rais wa kununuliwa. Ila kwenye ubunge, udiwani na serikali za mtaa, kila mtu awe free kugombea, hivyo tuwe na wagombea huru, na hili likifanyika hata akina sisi tuliolazimika kujiunga vyama fulani vya siasa, tutaachana navyo na tutashiriki, as independent candidates mfano mimi, naweza kabisa kugombea jimbo fulani na kulitwaa kama kuokota embe dodo lililojiangukia, ambapo mbunge wa hapo, nitamsukuma kama nimesukuma mlevi!.
Hitimisho
Tanzania is too poor to spend billions on by elections!, nikimaanisha nchi yetu Tanzania ni masikini wa kutupwa, kuhalalisha matumizi ya mabilioni ya fedha kuendesha chaguzi ndogo marudio kwa sababu za kijinga ni ujinga!

Ili Taifa letu lipate maendeleo ya kweli, ni lazima sisi Watanzania tukubali kuwa wakweli toka ndani ya nafsi zetu, tusikubali ujinga huu wa kuhama vyama, uendelee kutugharimisha sisi masikini wa kutupwa, tunaoishi kwenye lindi la umasikini uliotopea, halafu kuendelea kugharimishwa kurudia uchaguzi kwa sababu tuu za kisiasa zilizosababishwa na ujinga usituumize sisi masikini wa Mungu ambao we have nothing.

Nawatakia Furahi Dei Njema.

Paskali
Rejea.
Rev. Mtikila ashida kesi ya kuruhusu mgombea binafsi mahakama ya ...
Mtikila: Shujaa wa Demokrasia, Mwanamapinduzi halisi na Shujaa ...
Mgombea binafsi Tanzania: Tatizo ni nini? | Page 9 | JamiiForums ...

Swali kwa Wana UKAWA: Is UKAWA for Real or Just A Marriage of ...
 
good analysis mzalendo mwenzangu! Nadhani taifa letu sasa linageuka kuwa taifa la wehu! sijajua sababu ni nini haswa!

Akili za wananchi wenzetu zinaenda kinyume, technology inaongezeka mataifa mengine wanakimbia kwenda mbele na technology yao sisi waTanzania tumegeuka tuna kimbilia nyuumaa!
 
Pascal Mayalla umesema vyema
Kwa nini Bunge lipo kimya na huu mwendelezo haramu?
Wanaohama vyama na kujivua ubunge wagharamie uchaguzi kama sivyo washindi wa pili kila jimbo lililoachwa wazi wapewe ubunge au yabaki wazi hadi 2020
Huu ni upuuzi na upumbavu kuwafanya Wananchi hasa walipa kodi kwamba pesa yao inaweza tumika vile mtu anapenda.
Wahame lakini walipe gharama zote awe ni ccm au upinzani hili linawahusu wasitufanye hamnazo.
 
Swali je hao waendekeza ujinga wakaugeuza ndio kazi yao ya kupatia riziki watakusikia kweli !!!???
 
Wanabodi,

Declaration of Interest.
Mimi ni miongoni mwa Watanzania wazalendo wa nchi yangu, ambaye sio mwanachama wa Chama chochote cha siasa, kwa sababu siasa za vyama za Tanzania, tunaziona kama ni ujinga Fulani hivi, hivyo nawaomba sana univumilie, ninapoita siasa za ujinga ujinga, hii ni opinion yangu, everybody has the right to his/her own opinion, hivyo tukitofautiana kwenye hili, tutofautiene kwa hoja, mimi nimeleta hoja zangu kuwa siasa zetu kwenye maeneo Fulani Fulani zikiwezo siasa za uchaguzi ni ujinga ujinga kwa hoja, naomba tubishane kwa hoja.

Watanzania Tufanye Siasa za Ukweli, Tuachane na Siasa za Ujinga Ujinga.
Tufike mahali sisi Watanzania, wazalendo, wenye nia njema na maendeleo ya taifa hili letu masikini, hatuwezi kukaa kimya kwa kuendelea kukumbatia sheria mbovu, bad laws, za uchaguzi, na kuendelea kuwawabesha masikini wa Tanzania, mzigo wa gharama za uchaguzi wa marudio, kwa sababu za kijinga jinga kabisa, zinazotokana na siasa za ujinga ujinga!. Kitendo hiki cha masikini wa kutupwa wa Tanzania, wanaoishi kwenye lindi la umasikini uliotopea wa kipato cha chini ya dola moja kwa siku, halafu kuja kubebeshwa mzigo wa kugharimia chaguzi za marudio kutokana na sababu za kisiasa za ujinga ujinga, na sababu zenyewe kuwa ni sababu za kijinga kabisa, its not only ni nonsense, but also ni dhambi kwa Mungu, kuwabebesha masikini hawa gharama hizi za ziada kutokana na ujinga tuu wa watu fulani in the name of politics!..

Kwa Nini Sheria Yetu ya Uchaguzi ni Sheria Mbovu, Bad Law.
Kifungu 21 cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kinatoa haki ya kila Mtanzania mwenye sifa, kuwa huru kushiriki katika siasa kuanzia serikali za mtaa hadi serikali kuu, bila ubaguzi wowote.

Uhuru wa kushiriki shughuli za umma Sheria ya 1984 Na.15 ib.6 Sheria ya 1994 Na.34 ya ib.4
21.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ya 5, ya 39 na ya 67 ya Katiba hii na ya sheria za nchi kuhusiana na masharti ya kuchagua na kuchaguliwa, au kuteua na kuteuliwa kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, ama moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi waliochaguliwa na wananchi kwa hiari yao, kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria.

Lakini kukatokea kikundi Fulani cha wajinga Fulani, wakaipindua katiba kwa sababu Fulani za kijinga kabisa, wakainyofoa haki hiyo ya raia kwa kulazimisha, ili mtu ugombee nafasi yoyote ya uongozi wa umma, ni lazima udhaminiwe na chama cha siasa!, kiukweli kabisa na ki haki, this is nonsense!.

Rev. Mtikila alikipinga kifungu hiki na Mahakama Kuu ikatamka bayana kipengele hicho ni batili na kinakiuka katiba ya JMT. Wajinga wale, wakaamua kuihalalisha batili ile, kwa kukipenyeza kipengele hicho batili kwenye katiba, ili kuuhalalisha ujinga wao!.

Japo Lengo la Kudhaminiwa na Chama ni Nini, Huu Sii Ujinga Tuu?!.
Katiba katiba ilisema kila Mtanzania ana haki ya kushiriki uongozi, hili sherti la kudhaminiwa na chama lilitoka wapi, na kwa kwa nini watu walazimishwe kuwa wanachama wa vyama ili wadhaminiwe, ndipo waweze kugombea?. Mfano mimi, sina chama kwa sababu naziona siasa za vyama kwa ni ujinga Fulani hivi, ikitokea nina uwezo wa kuwatumikia wananchi wa eneo langu na kuwaletea maendeleo bila kupitia chama chochote, kwa nini nizuiliwe?!. Kiukweli kabisa, huu ni ujinga, it is nonsense, Watanzania tusikubali ujinga huu uendelee hadi 2020!, tupiganie milango ya wagombea binafsi ifunguliwe, 2020, watu wenye nia ya kugombea, tuwaletee wananchi maendeleo, bila kupitia hizi nonsense za vyama tuingie, tushindane kwa hoja na sio kushindana kuhonga, kama hali inavyoendelea sasa!.


Kiongozi Akiishachaguliwa, Anakuwa ni Kiongozi wa Watu, na Sio Kiongozi wa Chama, Kwa Sababu Anachaguliwa na Watu na Sio Chama!.
Ujinga mwingine mkubwa kabisa ni huu, hata kama mgombea amedhaminiwa na chama cha siasa kugombea, akiishapitishwa na Tume ya Uchaguzi kuwa Mgombea, japo anatambulika kama ni mgombea wa chama Fulani, lakini akiishachaguliwa, mwenyekiti wa mtaa, diwani, mbunge au rais, anakuwa sio kiongozi wa chama kilichomdhamini, bali anakuwa ni kiongozi wa wananchi. Mfano baada ya rais Magufuli kuchaguliwa kuwa rais kwa tiketi ya CCM, lakini hakuchaguliwa na wana CCM, amechaguliwa na Watanzania, na sio kiongozi wa CCM bali kiongozi wa Watanzania wote, vivyo hivyo kwa wabunge, madiwani na viongozi wa serikali ya mtaa, kitendo cha kujitoa chama na kupoteza ubunge, udiwani au uongozi wa umma, ni ujinga ambao haupaswi kuvumiliwa. Nini muhimu kati ya umma na chama?. Kuukosesha umma kiongozi waliemchagua kwa sababu za chama, sio tuu sio haki kwa wananchi waliomchagua, bali ni ujinga uliopitiliza, halafu kuja kulipisha wananchi hawa ngarama za uchaguzi wa marudio ni ujinga mwingine na dhambi juu yake ukizingatia kiwango cha umasikini wa nchi yetu.

Nini Kifanyike, A Way Forward.
Kama nilivyowahi kushauri humu, ukosoaji wenye kujenga, huandamana na ushauri wa nini kifanyike kurekebisha kasoro hizi ili kuundoa ujinga huu unaoendelea nchini mwetu kwa sasa.
  1. Iwekwe faini maalum kwa kila kiongozi wa umma, atakayejiuzulu nafasi yake kwa sababu za kijinga jinga, ikiwemo kukatwa mafao yake na ikibidi kufilisiwa ili kugharimia gharama za uchaguzi wa marudio kwa kulitia hasara taifa.
  2. Viongozi wote wanaojiuzulu, wasiruhusiwe tena kugombea nafasi walizojiuzulu, kama sababu za kujiuzulu mimi nimeziita ni za kijinga, tusiwakubalie wajinga hawa kugombea tena, ili wasije kutuletea tena ujinga ule ule na kutugharimisha masikini sisi kugharimia uchaguzi wa marudio.
  3. Tubadili sheria yetu ya uchaguzi, kwa kufuta chaguzi zote ndogo, na tuanzishe proportional representation kwa mwenye kura nyingi ndiye mshindi, lakini likitokea lolote, akasita kuwa rais, mbunge au diwani, yule aliyemfuatia katika uchaguzi uliopita ndio anatangazwa mbunge, kama hayupo anachuliwa mtu wa tatu, hadi wa mwisho, kama wote hawapo, ndipo uchaguzi mdogo unafanyika.
  4. Kile kipengele cha kudhaminiwa na chama kiishie kwenye uteuzi tuu, kiongozi akiishachaguliwa, anakuwa kiongozi wa watu, anaweza kuhama chama bila kupoteza uongozi wake kama ilivyo nchini Kenya.
  5. Tubadili sheria yetu ya uchaguzi, kwa kuondoa kipengele cha kudhaminiwa na vyama ili kila Mtanzania mwenye sifa za kugombea uongozi, awe free kugombea, hivyo tuwe na wagombea huru, na hili likifanyika hata sisi tusio na vyama tutashiriki, mfano mimi, kuna jimbo Fulani nitagombea kwa kulitwaa kama kuota embe dodo, ambapo mbunge wa hapo, nitansukuma kama nimesukuma mlevi!.
Hitimisho.
Tanzania is too poor spend billions on by elections for foolish and nonsense reasons, nikimaanisha nchi yetu Tanzania ni masikini wa kutupwa, kuhalalisha matumizi ya mabilioni ya fedha kuendesha chaguzi ndogo kwa sababu za kijinga. Ili Taifa letu lipate maendeleo ya kweli, ni lazima sisi Watanzania tukubali kuwa wakweli toka ndani ya nafsi zetu, tusikubali ujinga huu wa kuhama vyama, uendelee kutugharimisha sisi masikini wa kutupwa, tunaishi kwenye lindi la umasikini uliotopea, halafu kuendelea kugharimishwa na wajinga Fulani kwa sababu za ujinga wao!.

Nawatakia Furahi Dei Njema.

Paskali
Rejea.
Rev. Mtikila ashida kesi ya kuruhusu mgombea binafsi mahakama ya ...
Mtikila: Shujaa wa Demokrasia, Mwanamapinduzi halisi na Shujaa ...
Mgombea binafsi Tanzania: Tatizo ni nini? | Page 9 | JamiiForums ...
Swali kwa Wana UKAWA: Is UKAWA for Real or Just A Marriage of ...
Tatizo lipo kwetu wananchi kuendelea kuamini kuwa hawa wanasiasa wajinga wana nia njema sana na sisi hii si kweli hata kidogo wanachopigania ni kuwa madarakani tu hata kama hawana uwezo wa kujenga kesho iliyobora kwetu.

Tuna kila sababu ya kuamka na kupigania mamlaka yetu kikatiba kama wananchi. Hatuwezi kuendelea kuwa Mali ya serikali na kwamba hata kama tuna mitazamo tofauti na inavyotenda hatuna cha kufanya tukifanya lolote tunakiona cha mtema kuni.

Sheria nyingi mbovu mbovu kama hizi zinatunyima fursa kama wananchi ya kuwa na mamlaka hata kwa tunaowachagua badala yake hutufanyia kila mazila wanayoyaweza kuyafanya na tusiwe na lolote la kufanya. Hatuwezi kuendelea kuushuhudia huu upumbavu japo wewr umeuita ujinga Mimi nauona ni upumbavu uliopitiliza unaotufanya tuendelee kugeuzwa mazezeta na wanasiasa wapumbavu wanaotumia rasilimali zetu kipumbavu.

Nini kifanyike.
Tuanzishe harakati ya kufanya mabadiliko mqkubwa kwenye sheria ya uchaguzi kama tumeshindwa katiba ifanyiwe mabadiliko ya haraka tuondokane na huu ushenzi unaofanywa na wanasiasa wapumbavu.

TUTUMIE UPUUZI HUU KUKWEPA UPUUZI UJAO.
 
Kuna wakati najiulizaga hvi hawa tunaowapigia kura kwa mapenzi yote kabisaaaaaa kwann wao wanatuchukia, hawakumbuki hata marupurupu mazuri na mishahara mizuri ni kwa sababu yetu, hawana utu kabisaaa,hawatuonei huruma kabisaaaa,na awamu hii ndo wanatuumiza kweli,mamaangu kijijini anatema a lot of Km kufata maji ambayo sio safi na salama kabisaaa, lkn limtu linakuja na masababu yake ya kipuuzi linajivua ubunge tunarudia uchaguzi, hzo pesa kwann zisiwasaidie wananchi, na wananchi tumejawa uwoga bila Katiba mpya tutalia weeeeeee lkn haitasaidia kitu
 
Shida yako mayalla wewe ni kigeugeu,hata ikitokea siku umeandika kitu cha maana bado tutaona unafanya ukigeu geu.Mwanaume lazima uwe na msimamo katika maisha sio unakuwa wa uvugu vugu.
Shida yako unafuata msafara wa chama fulani bila kuhoji. Ukiwa na tabia ya kuhoji, ni ngumu sana kuwa na msimamo na chama chochote Tanzania, vyote vimejaa ujinga ujinga tu.................
 
60 Reactions
Reply
Back
Top Bottom