Sheria ya Uchaguzi Ni Bad Law!, Kuendelea Kuitumia ni Ujinga?, Kuwabebesha Masikini Gharama za Uchaguzi ni Dhambi!. | Page 8 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheria ya Uchaguzi Ni Bad Law!, Kuendelea Kuitumia ni Ujinga?, Kuwabebesha Masikini Gharama za Uchaguzi ni Dhambi!.

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Pascal Mayalla, Dec 15, 2017.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Dec 15, 2017
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,643
  Likes Received: 23,839
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,

  Declaration of Interest.
  Mimi ni miongoni mwa Watanzania wazalendo wa nchi yangu, ambaye sio mwanachama wa Chama chochote cha siasa, kwa sababu siasa za vyama za Tanzania, tunaziona kama ni ujinga Fulani hivi, hivyo nawaomba sana univumilie, ninapoita siasa za ujinga ujinga, hii ni opinion yangu, everybody has the right to his/her own opinion, hivyo tukitofautiana kwenye hili, tutofautiene kwa hoja, mimi nimeleta hoja zangu kuwa siasa zetu kwenye maeneo Fulani Fulani zikiwezo siasa za uchaguzi ni ujinga ujinga kwa hoja, naomba tubishane kwa hoja.

  Watanzania Tufanye Siasa za Ukweli, Tuachane na Siasa za Ujinga Ujinga.
  Tufike mahali sisi Watanzania, wazalendo, wenye nia njema na maendeleo ya taifa hili letu masikini, hatuwezi kukaa kimya kwa kuendelea kukumbatia sheria mbovu, bad laws, za uchaguzi, na kuendelea kuwawabesha masikini wa Tanzania, mzigo wa gharama za uchaguzi wa marudio, kwa sababu za kijinga jinga kabisa, zinazotokana na siasa za ujinga ujinga!. Kitendo hiki cha masikini wa kutupwa wa Tanzania, wanaoishi kwenye lindi la umasikini uliotopea wa kipato cha chini ya dola moja kwa siku, halafu kuja kubebeshwa mzigo wa kugharimia chaguzi za marudio kutokana na sababu za kisiasa za ujinga ujinga, na sababu zenyewe kuwa ni sababu za kijinga kabisa, its not only ni nonsense, but also ni dhambi kwa Mungu, kuwabebesha masikini hawa gharama hizi za ziada kutokana na ujinga tuu wa watu fulani in the name of politics!..

  Kwa Nini Sheria Yetu ya Uchaguzi ni Sheria Mbovu, Bad Law.
  Kifungu 21 cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kinatoa haki ya kila Mtanzania mwenye sifa, kuwa huru kushiriki katika siasa kuanzia serikali za mtaa hadi serikali kuu, bila ubaguzi wowote.

  Uhuru wa kushiriki shughuli za umma Sheria ya 1984 Na.15 ib.6 Sheria ya 1994 Na.34 ya ib.4
  21.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ya 5, ya 39 na ya 67 ya Katiba hii na ya sheria za nchi kuhusiana na masharti ya kuchagua na kuchaguliwa, au kuteua na kuteuliwa kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, ama moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi waliochaguliwa na wananchi kwa hiari yao, kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria.

  Lakini kukatokea kikundi Fulani cha wajinga Fulani, wakaipindua katiba kwa sababu Fulani za kijinga kabisa, wakainyofoa haki hiyo ya raia kwa kulazimisha, ili mtu ugombee nafasi yoyote ya uongozi wa umma, ni lazima udhaminiwe na chama cha siasa!, kiukweli kabisa na ki haki, this is nonsense!.

  Rev. Mtikila alikipinga kifungu hiki na Mahakama Kuu ikatamka bayana kipengele hicho ni batili na kinakiuka katiba ya JMT. Wajinga wale, wakaamua kuihalalisha batili ile, kwa kukipenyeza kipengele hicho batili kwenye katiba, ili kuuhalalisha ujinga wao!.

  Japo Lengo la Kudhaminiwa na Chama ni Nini, Huu Sii Ujinga Tuu?!.
  Katiba katiba ilisema kila Mtanzania ana haki ya kushiriki uongozi, hili sherti la kudhaminiwa na chama lilitoka wapi, na kwa kwa nini watu walazimishwe kuwa wanachama wa vyama ili wadhaminiwe, ndipo waweze kugombea?. Mfano mimi, sina chama kwa sababu naziona siasa za vyama kwa ni ujinga Fulani hivi, ikitokea nina uwezo wa kuwatumikia wananchi wa eneo langu na kuwaletea maendeleo bila kupitia chama chochote, kwa nini nizuiliwe?!. Kiukweli kabisa, huu ni ujinga, it is nonsense, Watanzania tusikubali ujinga huu uendelee hadi 2020!, tupiganie milango ya wagombea binafsi ifunguliwe, 2020, watu wenye nia ya kugombea, tuwaletee wananchi maendeleo, bila kupitia hizi nonsense za vyama tuingie, tushindane kwa hoja na sio kushindana kuhonga, kama hali inavyoendelea sasa!.


  Kiongozi Akiishachaguliwa, Anakuwa ni Kiongozi wa Watu, na Sio Kiongozi wa Chama, Kwa Sababu Anachaguliwa na Watu na Sio Chama!.
  Ujinga mwingine mkubwa kabisa ni huu, hata kama mgombea amedhaminiwa na chama cha siasa kugombea, akiishapitishwa na Tume ya Uchaguzi kuwa Mgombea, japo anatambulika kama ni mgombea wa chama Fulani, lakini akiishachaguliwa, mwenyekiti wa mtaa, diwani, mbunge au rais, anakuwa sio kiongozi wa chama kilichomdhamini, bali anakuwa ni kiongozi wa wananchi. Mfano baada ya rais Magufuli kuchaguliwa kuwa rais kwa tiketi ya CCM, lakini hakuchaguliwa na wana CCM, amechaguliwa na Watanzania, na sio kiongozi wa CCM bali kiongozi wa Watanzania wote, vivyo hivyo kwa wabunge, madiwani na viongozi wa serikali ya mtaa, kitendo cha kujitoa chama na kupoteza ubunge, udiwani au uongozi wa umma, ni ujinga ambao haupaswi kuvumiliwa. Nini muhimu kati ya umma na chama?. Kuukosesha umma kiongozi waliemchagua kwa sababu za chama, sio tuu sio haki kwa wananchi waliomchagua, bali ni ujinga uliopitiliza, halafu kuja kulipisha wananchi hawa ngarama za uchaguzi wa marudio ni ujinga mwingine na dhambi juu yake ukizingatia kiwango cha umasikini wa nchi yetu.

  Nini Kifanyike, A Way Forward.
  Kama nilivyowahi kushauri humu, ukosoaji wenye kujenga, huandamana na ushauri wa nini kifanyike kurekebisha kasoro hizi ili kuundoa ujinga huu unaoendelea nchini mwetu kwa sasa.
  1. Iwekwe faini maalum kwa kila kiongozi wa umma, atakayejiuzulu nafasi yake kwa sababu za kijinga jinga, ikiwemo kukatwa mafao yake na ikibidi kufilisiwa ili kugharimia gharama za uchaguzi wa marudio kwa kulitia hasara taifa.
  2. Viongozi wote wanaojiuzulu, wasiruhusiwe tena kugombea nafasi walizojiuzulu, kama sababu za kujiuzulu mimi nimeziita ni za kijinga, tusiwakubalie wajinga hawa kugombea tena, ili wasije kutuletea tena ujinga ule ule na kutugharimisha masikini sisi kugharimia uchaguzi wa marudio.
  3. Tubadili sheria yetu ya uchaguzi, kwa kufuta chaguzi zote ndogo, na tuanzishe proportional representation kwa mwenye kura nyingi ndiye mshindi, lakini likitokea lolote, akasita kuwa rais, mbunge au diwani, yule aliyemfuatia katika uchaguzi uliopita ndio anatangazwa mbunge, kama hayupo anachuliwa mtu wa tatu, hadi wa mwisho, kama wote hawapo, ndipo uchaguzi mdogo unafanyika.
  4. Kile kipengele cha kudhaminiwa na chama kiishie kwenye uteuzi tuu, kiongozi akiishachaguliwa, anakuwa kiongozi wa watu, anaweza kuhama chama bila kupoteza uongozi wake kama ilivyo nchini Kenya.
  5. Tubadili sheria yetu ya uchaguzi, kwa kuondoa kipengele cha kudhaminiwa na vyama ili kila Mtanzania mwenye sifa za kugombea uongozi wa nafasi yoyote, aruhusiwe, ila kwenye urais, tuweke vigezo vya ziada, ili asijetokea tajiri mmoja mwenye ukwasi wa kuwanunua watanzania wote, tukajikuta tuna rais wa kununuliwa. Ila kwenye ubunge, udiwani na serikali za mtaa, kila mtu awe free kugombea, hivyo tuwe na wagombea huru, na hili likifanyika hata sisi tusio na vyama tutashiriki, mfano mimi, naweza kabisa kugombea jimbo fulani na kulitwaa kama kuokota embe dodo lililojiangukia, ambapo mbunge wa hapo, nitamsukuma kama nimesukuma mlevi!.
  Hitimisho.
  Tanzania is too poor spend billions on by elections for foolish and nonsense reasons, nikimaanisha nchi yetu Tanzania ni masikini wa kutupwa, kuhalalisha matumizi ya mabilioni ya fedha kuendesha chaguzi ndogo kwa sababu za kijinga. Ili Taifa letu lipate maendeleo ya kweli, ni lazima sisi Watanzania tukubali kuwa wakweli toka ndani ya nafsi zetu, tusikubali ujinga huu wa kuhama vyama, uendelee kutugharimisha sisi masikini wa kutupwa, tunaishi kwenye lindi la umasikini uliotopea, halafu kuendelea kugharimishwa na wajinga Fulani kwa sababu za ujinga wao!.

  Nawatakia Furahi Dei Njema.

  Paskali
  Rejea.
  Rev. Mtikila ashida kesi ya kuruhusu mgombea binafsi mahakama ya ...
  Mtikila: Shujaa wa Demokrasia, Mwanamapinduzi halisi na Shujaa ...
  Mgombea binafsi Tanzania: Tatizo ni nini? | Page 9 | JamiiForums ...
  Swali kwa Wana UKAWA: Is UKAWA for Real or Just A Marriage of ...
   
 2. Idd Ninga

  Idd Ninga JF-Expert Member

  #141
  Jan 31, 2018
  Joined: Nov 18, 2012
  Messages: 2,562
  Likes Received: 965
  Trophy Points: 280
  Mbinu zote sawa,mradi tu kuepuka gharama.
   
 3. W

  Waziri kivuli JF-Expert Member

  #142
  Jan 31, 2018
  Joined: Nov 30, 2016
  Messages: 2,536
  Likes Received: 2,853
  Trophy Points: 280
  Hapo wataingia mitini
   
 4. sblandes

  sblandes JF-Expert Member

  #143
  Jan 31, 2018
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,762
  Likes Received: 1,004
  Trophy Points: 280
  Solution ni kuwacha maigizo ya Pwagu na Pwaguzi.
   
 5. Rekondoboshiki

  Rekondoboshiki JF-Expert Member

  #144
  Jan 31, 2018
  Joined: Nov 24, 2017
  Messages: 231
  Likes Received: 265
  Trophy Points: 80
  hii hamahama ya kijinga ipo tu huku shithole countries
   
 6. Idd Ninga

  Idd Ninga JF-Expert Member

  #145
  Jan 31, 2018
  Joined: Nov 18, 2012
  Messages: 2,562
  Likes Received: 965
  Trophy Points: 280
  tusilalamike sana,tuangalie na suluhu ili isitokee tena.
   
 7. Idd Ninga

  Idd Ninga JF-Expert Member

  #146
  Jan 31, 2018
  Joined: Nov 18, 2012
  Messages: 2,562
  Likes Received: 965
  Trophy Points: 280
  dah ghafla tu kitu kilikuwa jukwaa la siasa ila sasa kimesukumiziwa huku.,aise Mods bhana halafu mnafanya kimya kimya kwanini hivi ?
   
 8. Noel C Shao

  Noel C Shao Member

  #147
  Feb 1, 2018
  Joined: Jan 19, 2017
  Messages: 69
  Likes Received: 150
  Trophy Points: 40
  Katika medali za kimichezo ni jambo la kawaida kusikia mchezaji mmoja anatoka klabu moja kwenda jingine kwa kiwango fulani kikubwa cha pesa. Pesa hiyo huitwa “dau la uhamisho”. Ila ni jambo la kuajabisha kusikia mwanasiasa nae anakuwa na dau la uhamisho.
  Katika nchi maskini kama Tanzania, taifa ambalo halijapevuka kiuchumi hasa katika kutatua changamoto mbalimbali jamii, inatumia zaidi ya billioni moja kumuhamisha mbunge tena aliye katika mhimili wa bunge wenye maamuzi, kutoka chama A kwenda chama B.
  Ukimengenya dhana hii unaweza jiuliza elimu tuliyo nayo ni elimu inayo tupa tafakari gani juu ya ukombozi wa fikra zetu au ni elimu kivuli? viongozi tulio nao wana uzalendo na taifa hili au wao ni uvyama na maslai yao binafsi? Ni jambo fikirishi sana.
  Inajadilika vipi mwakilishi aliye pewa dhamana na wananchi kupitia chama X kuamua kujiuzulu nafasi yake mwenyewe bila hata ruhusa au shinikizo la walio mpa dhamana hiyo? Na pasipo matarajio anarejea kupitia chama Y, kutaka nafasi aliyo iachia bila hata kuomba idhini ya wananchi? Kama taifa hebu tujitathimini katika hili.
  Serikali ya awamu ya tano na dhana ya kubana matumizi kwa lengo la kuwatumikia wananchi bila kujali itikadi ya vyama, hebu na hili nalo litazamwe. Inakubalika vipi mbunge wa jimbo moja tu aiingizie serikali hasara ya zaidi ya billioni moja ambazo ni kodi za Watanzania wote, walio wanasiasa na wasio wanasiasa, walio katika majimbo husika na wasio katika majimbo hayo ya uchaguzi?
  Tupingane na makosa ya makusudi ya mtu au chama fulani kutuingiza katika gharama ambazo hazina msingi. Ingekuwa ni kwa sababu zisizo zuilika mathalani vifo, ingekuwa ni hoja tofauti ila kwa mazingira ya sasa ni aibu kuu.
  Ukiwa na zao bora la akili unaweza kuona mamilioni yanayo enda kuteketea katika uchaguzi, pesa ambazo zingeweza elekezwa katika miradi ya maendeleo katika majimbo husika. Ina tia uchungu kuona watu wanatanguliza maslai ya vyama vyao kuliko maslai na maendeleo ya wananchi.
  Ni heri tukasuguana kifkra katika sera, falsafa na itikadi ndani ya kingo za kisiasa ila inapo fika suala la kuwatumikia wananchi, kusongesha gurudumu la maendeleo mbele, mchakato wa kudumisha amani yetu kama taifa, shabaha ya kuujenga uchumi wetu na kusonga mbele kama taifa lazima tutangulize mbele uzalendo na utaifa, na tuseme kwa lugha na sauti moja.
  Katika kona hiyo hakuna sababu ya wengine kupanda milimani kupiga zumari la kuwakinga watu na mvua ilihali hawajui watu wanavyo sombwa na maji mabondeni au kugombania fito ilhali tunajenga nyumba moja.
  Lazima tushikamane katika kutatua kero za wananchi katika majimbo, kero za uhaba wa maji, miundo mbinu, huduma za afya, Elimu, Kilimo, Ukosefu wa mikopo, tatizo la ukosefu wa ajira, na kama pesa ipo ni vema wananchi pia wakapata uhuru wa kulitazama bunge lao moja kwa moja bila visingizio.
  Katika hili tuache zile siasa za mmoja anatoa jibu la 5+5=10 mwingine anasema ni 7, aliye sema 10 anaonekana ni mkosaji, mnafiki, muongo na adui na aliye sema 7 anatafutiwa sababu nyeti za kutetewa. Hatutafika kama taifa. Lazima nchi ijengwe kwa ajili ya vizazi vya sasa na vizazi vya miaka 500 ijayo.

  Ndimi, Noel Shao
   
 9. Mystery

  Mystery JF Gold Member

  #148
  Feb 1, 2018
  Joined: Mar 8, 2012
  Messages: 9,082
  Likes Received: 9,292
  Trophy Points: 280
  Yote hiyo inasababishwa na kuwa na viongozi washamba na malimbukeni.
  By Zitto Kabwe
   
 10. chodotio richie

  chodotio richie JF-Expert Member

  #149
  Feb 9, 2018
  Joined: May 15, 2017
  Messages: 217
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  Wakuu habar ya Leo. Mimi binafsii nakerwaa SNA SNA na tabiaa ya kurudiaa UCHAGUZI wakatii huo kiongozi husikaa yupo hai hajafa.

  Napendaa kushauri serikalii kufikaa mahalii kuonaa kua hii ni matumizi mabayaa ya pesa za umma. Rai yangu ni kuombaa wabunge waliomo humu au viongozii wenyekuezaa kuishaurii serikali kuwezaa kutunga sheriaa inayopigaa marufukuu mchezoo huu Wa kurudiaa UCHAGUZI kwa MTU aliejiuzulu kwa hiyari take mwenyewee. maana ni matumizi mabayaa ya pesa za walipakodii. Haiwezekanii Tanzania ya matatizo hivii chungumzimaa kujifanyaa hayaonekanii na kuanzaa kutumiaa mabilioni kwajilii ya kurudiaa UCHAGUZI ambao bajetii yake ilishapitaa.

  Inaumizaa snaa na naombaa kuwasilishaa wadau. No maonii yanguu tuu jaman.

  Je we we kama mtanzaniaa mzalendo inakupendezaa hiii??
   
 11. wambagusta

  wambagusta JF-Expert Member

  #150
  Feb 9, 2018
  Joined: Nov 28, 2014
  Messages: 1,728
  Likes Received: 463
  Trophy Points: 180
  Tupo pamoja mkuu !
   
 12. swissme

  swissme JF-Expert Member

  #151
  Feb 9, 2018
  Joined: Aug 15, 2013
  Messages: 13,109
  Likes Received: 16,845
  Trophy Points: 280
  Sisonje polepole na serikali ya ccm atapata sifa wapi?maana nchi imewashinda wameshindwa kuwapatia watanzania maendeleo na sasa wameona ni bora kuchota pesa azina na kununua wapinzani ili wampe sifa sisonje.


  Poor them


  Swissme
   
 13. chodotio richie

  chodotio richie JF-Expert Member

  #152
  Feb 9, 2018
  Joined: May 15, 2017
  Messages: 217
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  Sasa mkuu tufanyejee. Manaa hii imekuaa dondaa suguu kiukwel
   
 14. chodotio richie

  chodotio richie JF-Expert Member

  #153
  Feb 9, 2018
  Joined: May 15, 2017
  Messages: 217
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  OK mkuu
   
 15. j

  jabulani JF-Expert Member

  #154
  Feb 9, 2018
  Joined: Aug 1, 2015
  Messages: 3,166
  Likes Received: 4,149
  Trophy Points: 280
  Hawatakuelewa zimetengwa bilioni 18 kuhonga wapinzani ili kubadili katiba.
   
 16. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #155
  Feb 9, 2018
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,737
  Likes Received: 7,507
  Trophy Points: 280
  WAzo zuri; lakini unafanyaje kuhusu kumpata mtu mwingine kuchukua nafasi ya yule aliyejiuzulu? au unapendekeza watu wasiwe na wawakilishi kwa vile mtu kajiuzulu.
   
 17. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #156
  Feb 9, 2018
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 80,463
  Likes Received: 117,261
  Trophy Points: 280
  Ni kweli kila jimbo/ kata linahitaji kuwa na muwakilishi lakini si kwa mwendo huu wa kununuliwa kisha urushwe kugombea tena nafasi ile ile kupitia MACCM. Kumuunga mkono Magu hakuhitaji kujiuzulu na kujiunga na MACCM. Subiri awamu yako iishe ujiunge na MACCM badala ya kuwabebesha walipa kodi gharama chungu nzima za mabilioni pesa ambazo zingeweza kuelekezwa kwenye mambo ya tija kwa Watanzania badala ya hizi chaguzi UCHWARA.

   
 18. denoo49

  denoo49 JF-Expert Member

  #157
  Feb 9, 2018
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 5,981
  Likes Received: 5,962
  Trophy Points: 280
  Atafutwe aliyekuwa anamkaribia kwa kura, ndio achukue nafasi ya uwakilishi. Na huu ndio utakuwa mwarobaini, sijui kama kuna atakayekuwa tayari kujiuzulu.
   
 19. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #158
  Feb 9, 2018
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,643
  Likes Received: 23,839
  Trophy Points: 280
  Naunga mkono hoja.
  Sheria ya Uchaguzi Ni Bad Law!, Kuendelea Kuitumia ni Ujinga?, Kuwabebesha Masikini Gharama za Uchaguzi ni Dhambi!.

  Shurti la kudhaminiwa na chama kugombea uchaguzi, ni shurti batili kwa mujibu wa Katiba, linatutia hasara, tulifute!.

  P
   
 20. Auz

  Auz JF-Expert Member

  #159
  Feb 9, 2018
  Joined: Apr 6, 2016
  Messages: 3,156
  Likes Received: 1,952
  Trophy Points: 280
  Serikali unayoieleza inahusika kwa asilimia 100 juu ya hilo swala. Hakuna anayejali pesa za umma, kwa kuwa zipo, wao wanazifuja tu!
   
 21. c

  cumins JF-Expert Member

  #160
  Feb 9, 2018
  Joined: Dec 25, 2013
  Messages: 982
  Likes Received: 416
  Trophy Points: 80
  Hiyo imekaa vizuri.
  Ili kukomesha kabisa tabia hii ungeongezea na kuiomba selikali isitishe kutoa ruzuku kwa vyama vyote ili kila chama kitumie pesa za uchaguzi kutoka kwenye vyanzo vyake.
  Natumai kero hii au matumizi mabaya ya pesa za umma itapotea kabisa, na hao wanaojiita wapinzani Sijui kama watakuwepo.
  Ngumu kumeza, ngumu kutema.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...