ChaterMaster
JF-Expert Member
- Aug 17, 2009
- 1,622
- 791
Ooky thx kwa ufafanuz na historia yko binafsi... btw ni muda muafaka wa kuunganisha nguvu zako ktk kikundi au union/organization fulaani ambayo itamuvu forwad agenda unazoziamini..Mkuu ChaterMaster, kwanza hakuna mtu ambaye hana shida ya pesa, tena please usiite shida ya pesa, bali ita mahitaji, hakuna binadamu yoyote ambaye hana mahitaji, wala mimi sio tajiri kusema sina shida ya pesa, mimi ni masikini wa kutupwa ila ni masikini jeuri, pango tuu ninalolipa NHC ni Zaidi ya mshahara wa DC, hivyo niutafute u DC ili nipate nini?.
Amini usiamini, kazi kubwa na muhimu kuliko zote ni kazi ya urais, kuna Watanzania kibao, wanauwezo wa kuwa rais mzuri kwa Tanzania mara kumi ya Magufuli, lakini huo urais hata bure hawautaki!. Kuna watu kibao wako kama mimi, japo ni masikini kuliko DC, lakini huo uDC hata bure hawaufikirii, they are just happy doing what they do, they live happy with the little they make kwa kujituma wenyewe na sio kuwa proud na kazi za kutumwa!.
Paskali
Pia uhakikishe unakuwa na msimamo ktk unayoyaamini hii ni pamoja na kuacha kuwa na double standard ya mambo.
Sijui unajisafishaje ktk hili linalolalamikiwa na wengi hapa kuwa ni ndumilakuwili. Hii si SIFA nzuri hasa kwa wanaojiita wazalendo/wapambanaji. Utakuwa huna tofauti na Zitto ambaye ni mjenga hoja mzur ila kiukwel wengi wanambeza na kumpuuza sababu ya undumilakuwili wake.
Please define your Way of Life, hii itakupa heshima badala ya dharau. Ukushindwa bora uwe kimya maana wengi watakuupuuza pale usemapo.
Lastly, natamani uteuliwe kisha nithibitishe kuwa wew huna njaa za kijinga kama walizonazo wengii