Sheria ya Uchaguzi ni mbovu! Kuendelea kuitumia sio Ujinga? Kuwabebesha masikini gharama za Uchaguzi sio Dhambi?

Shida yako mayalla wewe ni kigeugeu,hata ikitokea siku umeandika kitu cha maana bado tutaona unafanya ukigeu geu.Mwanaume lazima uwe na msimamo katika maisha sio unakuwa wa uvugu vugu.
Mimi siamini kama yeye ni kigeugeu Ila naona ni mtu mwenye" keen intuitive power "na anaitumia ipasavyo.

Kuna muda anatumia sarcasm anakusifia kwa umbo la nnje na umbo la ndani anakuponda, na kuna muda anakuwa moja kwa moja nk.

Kila mada inakuwa na lengo maalum na hadhira iliyokusudiwa.

Ili umfahamu mtu vizuri mfanyie analysis ya muda mrefu ,msome sana si kwa mada moja au mbili ,ikibidi zote,pia kama haitoshi msikilize akiwa anaongea ktk mada mbali mbali na aina ya maswali anayouliza utaweza mfahamu.
 
Nafikiri alikuwa anaongelea urais kwamba tangu Perot hajasikia independent candidates

Ralph Nader je?

Marekani huwa hadi kuna wagombea wa chama cha Kisoshalist ambao hugombea urais.

Hadi write-in candidates huwa wapo na wapo kwenye ngazi zote hadi urais.

Uzuri wa Marekani madhali mtu umetimiza vigezo vya kikatiba kugombea ni rukhsa.

Halafu sijui watu hudhani kuwa Marekani wagombea urais huwa ni wawili tu wakati ukweli wa mambo huwa ni wengi.
 
mkuu mayalla ningependa pia ujaribu ku-predict nini kitatokea kama vyama pinzani vitadhoofishwa na kukosa nguvu kwa juhudi hizi zinazoendelezwa hapa nchini na utawala tulionao

ningependa pia kuona gharama za uchaguzi wa marudio zikigharamiwa na kiongozi aliyejiudhuru
 
wanaoliingiza taifa hasara na kukimbilia CHICHEMI na kusababisha kodi kuteketezwa tena kwa kurudia chaguzi za kuwachagua vibwengo haohao, na bado kuwakumbatia na kuwapongeza huku ukisema karibuni kodi za kurudia uchaguzi zipo na wakati uchaguzi wa diwani mmoja ni milioni 700, je huyu anayewakumbatia na kuwafiriji watu hawa si sehemu ya mafisadi wanaoteketeza kodi za mafukara wa mlo mmoja ?
Zanzibar heroes oyo oyoo !
 
Baada ya chama kikuu cha upinzani kujiondoa katika uchaguzi wa marudio katika majimbo ya Singida Kaskazini , Longido na Songea Mjini

Ukweli ni kwamba hapo ccm itashinda majimbo yote na washindi wameshapatikana .

Ushauli wangu fedha ambazo zilikuwa zimeandaliwa kwa ajiri ya kampeni na tume kuandaa uchaguzi ni vyema

Zingepelekwa kwa vijana wasio na ajira katika majimbo hayo wapewe kama mtaji wa biashara.
 
Watazishukua na kununua wengine....ili azma ya kuongeza....miaka 7...itatimiaa!! Akipiga 7 x 2....miaka 14....roho yake kukomesha watanzania ndio itatimiaa!!
 
Inavyoonekana chaguzi za marudio za udiwani na ubunge awamu hii zitakuwa nyingi sana kutokana na wanaojiuzulu kwasababu mbali mbali ukiacha zile za kawaida kama za kutenguliwa kimahakama au vifo. Ni chaguzi ambazo zitagharimu mabilioni ya shilingi. Tayari chaguzi za kata 43 zimefanyika na kutafina kiasi kikubwa cha pesa.

Swali langu ni kuwa hayo mabilioni huwa yametengwa kwenye bajeti? Kama sivyo zinatoka wapi?
 
Mayalla hem tuambie unayasema haya kwa dhamira yako halisi au kwa sababu umekosa uteuzi
Sidhan kama ungepewa shavu hata la ukuu wa wilaya ungesema haya

Nadhan unatakiwa ujitananbaishe kama ni kweli unadhamira ya uzalendo uungane na wapambanaji na kama ww ni ni mchumia tumbo pia ujipambanue. Hii kitu ya kila siku kusema huna chama si sawa sana.. na sizani kama itakusafisha na makandokando yako
 
Mimi si msemaji wa yoyote ila nimewahi msoma mahala humu akiandika kuwa vyeo vya ukuu wa wilaya nk si kitu kwake.
Aliendelea kuandika kwamba Kodi ya pango la ofisi ya company yake inaweza kuwa sawa na mshahara wa mkuu wa wilaya, ukiacha mbali watu aliowaajili nk.
Pia nilimsikia pitia TV akiwa Ikulu akiomba awe anapewa mialiko hata ya nnje ya nchi ya waandishi wanaombatana na Ujumbe wa rais kama free journalist na kuhusu gharama za accommodation ni juu yake.
Kwa hiyo hadi hapo nadhani ni sahihi kudhani kwamba yeye si mtu mwenye njaa na anayosema anamaanisha na haitaji fadhila ya vyeo kutoka kwa mamlaka yoyote ili atatue shida zake
 
Tatizo ni kwamba siasa za nchi hii hazipo kwa ajili ya kumtumikia mwananchi bali kuchuma mali na kukusanya utajiri wa haraka......

Kwa mantiki hiyo siasa imekuwa ni biashara yenye faida kubwa ndio maana wanasiasa wako radhi hata wauze mali zao ili wahonge wapate uongozi........

Hicho ni kipengele cha kijinga hasa kwenye nyakati hizi za ukweli na uwazi

Hii imewafanya wanasiasa kuwa watumwa wa vyama vyao badala ya kuwatumikia wananchi.......

Kiongozi anaweka maslahi ya chama badala ya waliompa kura kwa kuwa ndio walioshika ugali wake........hii inatuzalishia wanasiasa waoga........

NB

TUKIWA KAMA WATAWALIWA TUNAWEZA KUBADILI HALI HII KAMA TUKIAMUA.......
 
Mimi si msemaji wa yoyote ila nimewahi msoma mahala humu akiandika kuwa vyeo vya ukuu wa wilaya nk si kitu kwake.
Aliendelea kuandika kwamba Kodi ya pango la ofisi ya company yake inaweza kuwa sawa na mshahara wa mkuu wa wilaya, ukiacha mbali watu aliowaajili nk.
Pia nilimsikia pitia TV akiwa Ikulu akiomba awe anapewa mialiko hata ya nnje ya nchi ya waandishi wanaombatana na Ujumbe wa rais kama free journalist na kuhusu gharama za accommodation ni juu yake.
Kwa hiyo hadi hapo nadhani ni sahihi kudhani kwamba yeye si mtu mwenye njaa na anayosema anamaanisha na haitaji fadhila ya vyeo kutoka kwa mamlaka yoyote ili atatue shida zake
Hv unataka kusema hao wote wanaopapatikia vyeo kila siku unazani hawana hela kulko huyo best ako mayalla?
Who is mayala hadi useme hana shda ya hela..

Uzalendo wa mayala unaupimaje?
Nadhan badala ya kumtetea sana mwache mwenyewe aje ajibu, maana mengine huez yajua kwa sabab hajateukiwa, lait angeteuliwa cheo chochote alafu akatae uteuz ningesema yees.. Ila yote anayoongea haya ni kutokana na kukosa kuteuliwa
 
Mayalla hem tuambie unayasema haya kwa dhamira yako halisi au kwa sababu umekosa uteuzi
Sidhan kama ungepewa shavu hata la ukuu wa wilaya ungesema haya

Nadhan unatakiwa ujitananbaishe kama ni kweli unadhamira ya uzalendo uungane na wapambanaji na kama ww ni ni mchumia tumbo pia ujipambanue. Hii kitu ya kila siku kusema huna chama si sawa sana.. na sizani kama itakusafisha na makandokando yako
Mkuu Chater Master, kwanza ni kweli mimi sina chama, pili naomba nikueleze
Nimesoma Tambaza darasa moja na mtoto wa Mkapa, he is a friend, hivyo mimi nakwenda kumsalimia Mkapa kama baba fulani, na sio kama rais wa nchi!, ingekuwa issue ni uteuzi si ningelobby!.

Nimesoma UDSM na Riz1, he is a friend, ingekuwa ni kusaka uteuzi, ningeingia CCM na kumuomba Riz anisukumie pale kwa mshua wake!.

Magu ndio usiseme, kwanza ni homeboy wangu, pili kila nikiwa Chato, nafikia kwake, na kunasiku niifika na wageni wazungu, mpishi akashinda kuwapikia special menu yao, Mama Janet mwenyewe in person, aliingia jikoni!, hivyo kama ni lobbying, ningelobby!.

Mimi ni muumini wa katiba ya Warioba, ma DC ni redundant na wastage of time, money and resources.
Mimi ni mzalendo wa kweli, and if God wishes, soon hata wewe hili utalitambua na utakubaliana na mimi kuwa taifa hili litakombolewa na wazalendo wa kweli na sio wachumia tumbo.

Paskali
 
Hv unataka kusema hao wote wanaopapatikia vyeo kila siku unazani hawana hela kulko huyo best ako mayalla?
Who is mayala hadi useme hana shda ya hela..
Mkuu ChaterMaster, kwanza hakuna mtu ambaye hana shida ya pesa, tena please usiite shida ya pesa, bali ita mahitaji, hakuna binadamu yoyote ambaye hana mahitaji, wala mimi sio tajiri kusema sina shida ya pesa, mimi ni masikini wa kutupwa ila ni masikini jeuri, pango tuu ninalolipa NHC ni Zaidi ya mshahara wa DC, hivyo niutafute u DC ili nipate nini?.

Amini usiamini, kazi kubwa na muhimu kuliko zote ni kazi ya urais, kuna Watanzania kibao, wanauwezo wa kuwa rais mzuri kwa Tanzania mara kumi ya Magufuli, lakini huo urais hata bure hawautaki!. Kuna watu kibao wako kama mimi, japo ni masikini kuliko DC, lakini huo uDC hata bure hawaufikirii, they are just happy doing what they do, they live happy with the little they make kwa kujituma wenyewe na sio kuwa proud na kazi za kutumwa!.

Paskali
 
Na hili ni moja ya makosa yetu kutegemea opinions za watawala kwenye masuala nyeti yanayoamua mustakhabali wa Taifa to the other grounds mass mobilization is inevitable.

suluhu ya huu uhuni ni kama watajitokeza wanasheria wazuri waaandae hoja hawa wabunge woote washatakiwe kwa kosa la uhujumu uchumi! sababu zipo wazi za kuwatia hatiani na hata wakishinda, mara nyingine mtu atafikiria mara mbili kabla ya kujiuzuru kwa sababu za kipuuuuzi!
 
Katiba mbovu wala sio demokrasia.
Alafu Demokrasia gani inaruhusu kununua wanasiasa?
Yes, katiba ni tatizo, lakini katiba ni ya Wananchi, kwa nini Watanzania tunakubali kuendelea kukubali kutumika kwa sharia mbovu zinazotugharimu?, huu sio ujinga?!, we have to say no to bad laws, lets wake up and say no!.

Paskali
 
60 Reactions
Reply
Back
Top Bottom