Sheria ya Uchaguzi ni mbovu! Kuendelea kuitumia sio Ujinga? Kuwabebesha masikini gharama za Uchaguzi sio Dhambi?

Mimi naomba nitakamke rasimi kuwa hakuna haja ya kutupa misaada ya fedha na mikopo kwasababu sisi mnaotusaidi hatujitambui.

Tumebadili sheria nyingi lakini kubadili sheria ya uchaguzi ili watu wanaojiuzulu ubunge au udiwani wasipoteza nafasi zao hizo kuchaguliwa lengo likiwa ni kutopoteza fedha za kugharamia uchaguzi,tumeona si jambo la msingi hivyo sisi sio watu wa kusaidiwa wala kupewa mikopo na ni bora hizo fedha mkawape watu wa mataifa mengine walio serious na maisha yao.

Hii misaada ni fedha/jasho la walipa kodi wa nchi zenu hivyo jasho hili msilipoteze kwa kuwapa watu ambao hawataki kujisaidia.

Endeleeni kukata misaada yote na hata mikopo msitupe tumezidi ujinga.

Uzalendo sio kuunga mkono ujinga au upuuzi kisa tu unafanywa na watu wakubwa bali ni kuupinga upuuzi huo kwa njia yoyote ile hata kama itakuwa na maumivu.
 
Lakin kaka mayalla hii ishu ninkama ni too late kwakweli. Sababu rais hasikilizi ushauri
. Watu wanatoka kwenye vyama vingine.. moja kwa moja wanapewa vyeo. Bila screening yoyote.
Niliahawahi kusema upinzan unaweza tumia nafasi hii kuongiza mapandikiz ndani ya ccm.. halaf baadae watumike kuvuruga chama wkt huo ni too late tayari
 
Wanabodi,
Kuna kitu nilikisema kwenye bandiko hili sasa kinakwenda kutokea tena kwenye huu uchaguzi wa serikali za mitaa.
Kitu chenyewe ni hiki

  1. Kile kipengele cha kudhaminiwa na chama kiishie kwenye uteuzi tuu, kiongozi akiishachaguliwa, anakuwa kiongozi wa umma. kiongozi wa watu, anaweza kuhama chama bila kupoteza uongozi wake kama ilivyo nchini Kenya.
  2. Tubadili sheria yetu ya uchaguzi, kwa kuondoa kipengele cha kudhaminiwa na vyama ili kila Mtanzania mwenye sifa za kugombea uongozi wa nafasi yoyote, aruhusiwe, ila kwenye urais, tuweke vigezo vya ziada, ili asijetokea tajiri mmoja mwenye ukwasi wa kuwanunua Watanzania wote, tukajikuta tuna rais wa kununuliwa. Ila kwenye ubunge, udiwani na serikali za mtaa, kila mtu awe free kugombea, hivyo tuwe na wagombea huru, na hili likifanyika hata sisi tusio na vyama tutashiriki, mfano mimi, naweza kabisa kugombea jimbo fulani na kulitwaa kama kuokota embe dodo lililojiangukia, ambapo mbunge wa hapo, nitamsukuma kama nimesukuma mlevi!.
  3. Hoja yangu ni mgombea akiishadhaminiwa na chama cha siasa na kupitishwa kuwa mgombea, sasa anakuwa ni mgombea wa umma na sio mgombea wa chama.
  4. Wanaomchagua kuwa Mwenyekiti wa serikali ya mtaa, diwali, mbunge au rais ni wananchi na sio watu wa chama chake.
  5. The power basis ya katiba ni watu, wananchi, "we the people". Watu ndio msingi wa katiba, na uchaguzi unafanyika ili kuwapa fursa watu kuchagua viongozi wao.
  6. Process ya uchaguzi ni kutoa legitimacy kwa kiongozi aliyechaguliwa na watu. Kitendo cha chama cha siasa kumvua uanachama kiongozi wa watu na kupoteza uongozi wa umma kiukweli kabisa huu ni ujinga fulani. Yaani umma wenye katiba umchague mtu kiongozi wao, halafu kije kitokee kidubwana kimfute uanachama na kupoteza uongozi wa umma!, this is awkward!.
  7. Kwenye uchaguzi huu wa serikali za mitaa vyama vya Chadema, ACT na UPDP vimejitoa, lakini Waziri Jaffo katangaza majina yatabandikwa na hakuna kuweka mpira kwapani.
  8. Kuna possibility baadhi ya wagombea wa vyama vilivyojitoa wakachaguliwa kuwa viongozi wa wananchi. Kitakachofuata ni viongozi hao watalazimishwa kujiudhuru na wakigoma watafutwa uanachama hivyo kupoteza uongozi wa umma, na kupelekea uchaguzi wa marudio, hapa nauliza tena kiukweli kabisa huu sio ujinga?.
P
 
Naunga mkono hoja.

Lakini pia mara wanapochaguliwa wasiruhusiwe tena kuwa viongozi katika vyama vyao.

Maana wanakuwa na interest za watu wote kuto vyama tofauti na wasio na vyama.

Mfano leo Mbowe asingekuwa mwenyekiti chadema.
Zitto pale ACT asingekuwa kiongozi mkuu.
Magufuli nae uenyekiti wa ccm angekuwa anausoma tu.

Bila ya kuweka haya haitaweza kuwatenganisha na vyama vyao.
 
Wanabodi,
Kuna kitu nilikisema kwenye bandiko hili sasa kinakwenda kutokea tena kwenye huu uchaguzi wa serikali za mitaa.
Kitu chenyewe ni hiki

  1. Kile kipengele cha kudhaminiwa na chama kiishie kwenye uteuzi tuu, kiongozi akiishachaguliwa, anakuwa kiongozi wa umma. kiongozi wa watu, anaweza kuhama chama bila kupoteza uongozi wake kama ilivyo nchini Kenya.
  2. Tubadili sheria yetu ya uchaguzi, kwa kuondoa kipengele cha kudhaminiwa na vyama ili kila Mtanzania mwenye sifa za kugombea uongozi wa nafasi yoyote, aruhusiwe, ila kwenye urais, tuweke vigezo vya ziada, ili asijetokea tajiri mmoja mwenye ukwasi wa kuwanunua Watanzania wote, tukajikuta tuna rais wa kununuliwa. Ila kwenye ubunge, udiwani na serikali za mtaa, kila mtu awe free kugombea, hivyo tuwe na wagombea huru, na hili likifanyika hata sisi tusio na vyama tutashiriki, mfano mimi, naweza kabisa kugombea jimbo fulani na kulitwaa kama kuokota embe dodo lililojiangukia, ambapo mbunge wa hapo, nitamsukuma kama nimesukuma mlevi!.
  3. Hoja yangu ni mgombea akiishadhaminiwa na chama cha siasa na kupitishwa kuwa mgombea, sasa anakuwa ni mgombea wa umma na sio mgombea wa chama.
  4. Wanaomchagua kuwa Mwenyekiti wa serikali ya mtaa, diwali, mbunge au rais ni wananchi na sio watu wa chama chake.
  5. The power basis ya katiba ni watu, wananchi, "we the people". Watu ndio msingi wa katiba, na uchaguzi unafanyika ili kuwapa fursa watu kuchagua viongozi wao.
  6. Process ya uchaguzi ni kutoa legitimacy kwa kiongozi aliyechaguliwa na watu. Kitendo cha chama cha siasa kumvua uanachama kiongozi wa watu na kupoteza uongozi wa umma kiukweli kabisa huu ni ujinga fulani. Yaani umma wenye katiba umchague mtu kiongozi wao, halafu kije kitokee kidubwana kimfute uanachama na kupoteza uongozi wa umma!, this is awkward!.
  7. Kwenye uchaguzi huu wa serikali za mitaa vyama vya Chadema, ACT na UPDP vimejitoa, lakini Waziri Jaffo katangaza majina yatabandikwa na hakuna kuweka mpira kwapani.
  8. Kuna possibility baadhi ya wagombea wa vyama vilivyojitoa wakachaguliwa kuwa viongozi wa wananchi. Kitakachofuata ni viongozi hao watalazimishwa kujiudhuru na wakigoma watafutwa uanachama hivyo kupoteza uongozi wa umma, na kupelekea uchaguzi wa marudio, hapa nauliza tena kiukweli kabisa huu sio ujinga?.
P
Hiyo ni Sawa lakini hakuna chama tawala kitakubali mageuzi ya aina hii ambayo mwanachama asiyependwa na chama au kundi la watu lakini anayependwa na watu ashinde Uchaguzi.
 
Wanabodi,

Declaration of Interest.
Mimi ni miongoni mwa Watanzania wazalendo wa nchi yangu, ambaye sio mwanachama wa Chama chochote cha siasa, kwa sababu siasa za vyama za Tanzania, tunaziona katika baadhi ya maeneo kama ni ujinga fulani hivi, hivyo nawaomba sana univumilie, ninapoita baadhi ya siasa zetu ni kama siasa za ujinga ujinga fulani kwa baadhi ya vyama na baadhi ya wanasiasa, na nasisitiza, nimesema baadhi, nikimaanisha sii zote na sii wote!.

Tubishane kwa Kutoa Hoja kwa Hoja, Kupangua Hoja kwa Hoja, na Sio Hoja Kwa Viroja!.
Hii ni opinion yangu tuu, and everybody has the right to his/her own opinion, hivyo tukitofautiana kwenye hili, tutofautiane kwa hoja, mimi nimeleta hoja zangu kuwa baadhi ya siasa zetu kwenye baadhi ya maeneo fulani fulani, likiwemo eneo la siasa za uchaguzi, kiukweli ni kama ujinga fulani, na zinavyoendeshwa, kuna maeneo zinaendeshwa kwa ujinga ujinga kabisa!. Hivyo naomba uzisome hoja zangu, ili tukitofautiana, tutofautiane kwa hoja, pangua hoja kwa hoja, kwa kupangua hoja zangu na ama kutetea ama kuleta hoja mbadala, nikiwasisitiza na kuwaomba tubishane kwa hoja na kushindanisha hoja kwa hoja, kupangua hoja kwa hoja mbadala na sio watu tumeleta hoja humu, halafu mtu anakuja kuibishia kwa viroja!.

Ili Tupate Maendeleo ya Kweli, Watanzania Lazima Tufanye Siasa za Ukweli, Tuachane na Siasa za Ujinga Ujinga!.
Nashauri kama ni kweli Tanzania tunataka maendeleo ya kweli ya taifa letu, ni lazima tufike mahali tufanye siasa za ukweli, the real politics na sio hizi siasa za blah blah tunazoendelea nazo. Tufike mahali, sisi Watanzania, wazalendo wa kweli wa nchi hii, wenye nia njema na ya dhati ya maendeleo ya kweli ya taifa hili letu masikini, hatuwezi kukaa kimya na kunyamaza kwa kuendelea kukumbatia sheria mbovu za uchaguzi ambazo Makama Kuu ya Tanzania imeziita kuwa ni "bad laws" na kushauri, zifutwe, "scraped" kutoka katika vitabu vya sheria!, lakini kwa vile sheria hizo mbovu, zinakinufaisha chama fulani, then tunaendelea kuzing'ang'ania sheria hizo mbovu za uchaguzi, hata kama matumizi ya sheria hizo mbovu, ni kuwawabesha masikini wa Tanzania, mzigo mkubwa wa gharama za uchaguzi wa marudio, kwa sababu za kijinga jinga tuu kabisa, zinazotokana na siasa za ujinga ujinga!. Kitendo hiki cha masikini wa kutupwa wa Tanzania, wanaoishi kwenye lindi la umasikini uliotopea wa kipato cha chini ya dola moja kwa siku, halafu kuja kubebeshwa mzigo wa gharama za kugharimia uchaguzi za marudio, kutokana na diwani mmoja au mbunge mmoja kuhama chama hiki na kuhamia chama kile kwa sababu za kisiasa tuu, hizi ndizo siasa mimi ninazo ziita ni "siasa za ujinga ujinga!", na sababu zenyewe zinazowafanya wabunge na madiwani hao kuhama chama kimoja kwenda chama kingine, naziita kuwa ni sababu za kijinga jinga na nyingine ni za kijinga kabisa!. Kwa maoni yangu, this, its not only ni nonsense, but also ni dhambi kwa Mungu, kuwabebesha, Watanzania masikini hawa wa kutupwa, gharama hizi za ziada za uchaguzi wa marudio, kutokana na wawakilishi wao kuhama vyama kwa sababu tuu za hizi siasa zetu za ujinga ujinga, mimi nauita huu pia ni ujinga fulani in the name of politics!.

Kwa Nini Sheria Yetu ya Uchaguzi ni Sheria Mbovu, Bad Law.
Kifungu 21 cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kinatoa haki ya kila Mtanzania mwenye sifa, kuwa huru kushiriki katika siasa kuanzia serikali za mtaa hadi serikali kuu, bila ubaguzi wowote.

Uhuru wa kushiriki shughuli za umma Sheria ya 1984 Na.15 ib.6 Sheria ya 1994 Na.34 ya ib.4
21.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ya 5, ya 39 na ya 67 ya Katiba hii na ya sheria za nchi kuhusiana na masharti ya kuchagua na kuchaguliwa, au kuteua na kuteuliwa kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, ama moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi waliochaguliwa na wananchi kwa hiari yao, kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria.

Lakini kukatokea kikundi fulani cha watu, naomba kuwaita ni "wajinga fulani", wakaipindua katiba kwa sababu fulani za kijinga kabisa!, wakainyofoa haki hiyo ya raia kushiriki uongozi kwa uhuru kabisa, na badala yake, kulazimisha ili mtu ushiriki uongozi fulani, au ugombee nafasi fulani fulani ya uongozi wa umma, ni lazima kwanza udhaminiwe na chama cha siasa!, kiukweli kabisa na ki haki, huu ni ujinga!, this is nonsense!. Katiba yetu haikusema hivyo!.

Rev. Mtikila (Mungu amuweke pema peponi) alikipinga kifungu hiki na Mahakama Kuu ya Tanzania, ikatamka bayana kuwa kipengele hicho ni batili na kinakiuka katiba ya JMT hivyo kifutwe kwenye sheria, kila Mtanzania awe huru kugombea nafasi yoyote ya uongozi wa umma, au kwa kupitia vyama vya siasa, au bila kupitia chama chochote. Lakini wajinga wale, wakaamua kuihalalisha batili ile, kwa kukipenyeza kipengele hicho batili ndani ya katiba yetu, ili kuuhalalisha ujinga wao!, hivyo shurti la kudhaminiwa na chama sasa ni la kikatiba!.

Jee Lengo la Kudhaminiwa na Chama ni Nini?, Huu Sii Ujinga Tuu?!.
Katiba ilisema kila Mtanzania yuko huru na ana haki ya kushiriki uongozi, toka serikali za mtaa hadi serikali kuu bila kuwa na chama chochote. Hili sherti la kumlazimisha kudhaminiwa na chama lilitoka wapi?!, na kwa kwa nini watu walazimishwe kuwa wanachama wa vyama ili wadhaminiwe, ndipo waweze kugombea?!. Mfano mimi, sina chama kwa sababu naziona siasa za vyama kama ni ujinga fulani hivi, ikitokea nina uwezo wa kuwatumikia wananchi wa eneo langu na kuwaletea maendeleo bila kupitia chama chochote, kwa nini nizuiliwe?!. Kiukweli kabisa, huu ni ujinga, it is nonsense!. Watanzania tusikubali ujinga huu uendelee hadi 2020!, tupiganie milango ya wagombea huru na wagombea binafsi ifunguliwe, 2020, watu wenye uwezo wa uongozi, na wenye nia ya kugombea, ili kuwaletea wananchi maendeleo, bila kupitia hizi nonsense za siasa vyama waingie, and you never know hata sisi tusio na vyama kama mimi, tuingie, tushindane kwa hoja na sio kushindana kuhonga, kama hali inavyoendelea sasa!.

Kiongozi Akiishachaguliwa, Anakuwa ni Kiongozi wa Watu, na Sio Kiongozi wa Chama, Kwa Sababu Anachaguliwa na Watu na Sio Chama!.
Ujinga mwingine mkubwa kabisa wa siasa zetu za vyama, ni ujinga ni huu, hata kama mgombea amedhaminiwa na chama cha siasa kugombea, akiishapitishwa na Tume ya Uchaguzi kuwa Mgombea rasmi, japo anatambulika kama ni mgombea wa chama fulani, lakini anachaguliwa kwa kura za wananchi wa eneo lile wote wakiwemo wanachama wa chama chake, akiishachaguliwa, mwenyekiti wa mtaa, diwani, mbunge au rais, sasa anakuwa ni kiongozi wa umma na sio kiongozi wa chama kilichomdhamini, bali anakuwa ni kiongozi wa wananchi wa eneo lile waliomchagua, wasio mchagua hata wasiopiga kura, huyu sasa anakuwa ni kiongozi wa wote na sio kiongozi wa chama chake hata kama alidhaminiwa na chama fulani.. Mfano baada ya rais Magufuli kuchaguliwa kuwa rais kwa tiketi ya CCM, lakini hakuchaguliwa na wana CCM pekee, amechaguliwa na wananchi wote na Watanzania wote, na sasa sio kiongozi tuu wa CCM. kwa sababu ndie Mwenyekiti wao, bali rais Magufuli ni kiongozi wa Watanzania wote,wa vyama vyote, wa watu wote!. Hali ni vivyo hivyo kwa wabunge, madiwani na viongozi wa serikali ya mtaa, kitendo cha kiongozi wa umma, kujitoa chama kilichomdhamini na kupoteza uongozi wa umma, ubunge, udiwani au uongozi wa umma, ni ujinga ambao haupaswi kuvumiliwa na kuendelea kukumbatiwa!. This nonsense must stop!. Nini muhimu zaidi kati ya umma na chama?. Kuukosesha umma kiongozi waliemchagua kwa sababu za chama, sio tuu sio haki kwa wananchi waliomchagua, bali ni ujinga uliopitiliza!, halafu wananchi masikini wa Tanzania, kuja kulipisha gharama za kugharimia uchaguzi wa marudio, sio tuu ni ujinga mwingine, bali ni dhambi kuwagharimisha wananchi hawa gharama za kurudia uchaguzi kwa sababu fulani amejiuzulu chama hiki na kitu cha ajabu kabisa, huyo huyo fulani aliyejiuzulu, ndio anakuja kugombea tena kupitia chama kinhine!. This is nonsense!.

Nini Kifanyike, A Way Forward.
Kama nilivyowahi kushauri humu, ukosoaji wenye kujenga, huandamana na ushauri wa nini kifanyike kurekebisha kasoro hizi ili kuundoa ujinga huu unaoendelea nchini mwetu kwa sasa.
  1. Iwekwe faini maalum kwa kila kiongozi wa umma, atakayejiuzulu nafasi yake kwa sababu za kijinga jinga, ikiwemo kukatwa mafao yake na ikibidi kufilisiwa ili kugharimia gharama za uchaguzi wa marudio kwa kulitia hasara taifa.
  2. Viongozi wote wanaojiuzulu, wasiruhusiwe tena kugombea nafasi zile zile walizojiuzulu, kama sababu za kujiuzulu mimi nimeziita ni za kijinga, tusiwakubalie wajinga hawa kugombea tena, ili wasije kutuletea tena ujinga ule ule na kutugharimisha masikini sisi kugharimia uchaguzi wa marudio!.
  3. Tubadili sheria yetu ya uchaguzi, kwa kufuta chaguzi zote ndogo, na tuanzishe mpango wa succession plan mgombea wa chama fulani aliyeshinda, tujenge hoja kuwa huyo aliyeshinda ameshinda kwa sababu ya chama c alichogombea hivyo wananchi wamekipa chama ridhaa, hivyo akijiuzulu, akisita kuwa mbunge, diwani, rais kwa sababu zozote zile, chama chake kiteue mwanachama mwingine kushika nafasi ile!. Hili likifanyika, amini usiamini, hatutasikia tena kiongozi anajiuzulu kwa sababu za kijinga jinga!.
  4. Kama tunaamini aliyechaguliwa ni mtu na sio chama, then diwani au mbunge awe huru kuhama na udiwani wake au ubunge wake kama nchini Kenya.
  5. Mbunge au diwani akijiuzulu au kufariki, tuanzishe kitu kinachoitwa "a proportional representation" kwa mwenye kura nyingi ndiye mshindi, lakini likitokea lolote, akasita kuwa rais, mbunge au diwani, yule aliyemfuatia kwa wingi wa kura katika uchaguzi uliopita ndio anatangazwa mbunge, diwani, rais, na kama hayupo anachukuliwa mtu wa tatu, hadi wa mwisho, kama wote hawapo, ndipo uchaguzi mdogo unafanyika.
  6. Kile kipengele cha kudhaminiwa na chama kiishie kwenye uteuzi tuu, kiongozi akiishachaguliwa, anakuwa kiongozi wa umma. kiongozi wa watu, anaweza kuhama chama bila kupoteza uongozi wake kama ilivyo nchini Kenya.
  7. Tubadili sheria yetu ya uchaguzi, kwa kuondoa kipengele cha kudhaminiwa na vyama ili kila Mtanzania mwenye sifa za kugombea uongozi wa nafasi yoyote, aruhusiwe, ila kwenye urais, tuweke vigezo vya ziada, ili asijetokea tajiri mmoja mwenye ukwasi wa kuwanunua Watanzania wote, tukajikuta tuna rais wa kununuliwa. Ila kwenye ubunge, udiwani na serikali za mtaa, kila mtu awe free kugombea, hivyo tuwe na wagombea huru, na hili likifanyika hata sisi tusio na vyama tutashiriki, mfano mimi, naweza kabisa kugombea jimbo fulani na kulitwaa kama kuokota embe dodo lililojiangukia, ambapo mbunge wa hapo, nitamsukuma kama nimesukuma mlevi!.
Hitimisho.
Tanzania is too poor spend billions on by elections for foolish and nonsense reasons!, nikimaanisha nchi yetu Tanzania ni masikini wa kutupwa, kuhalalisha matumizi ya mabilioni ya fedha kuendesha chaguzi ndogo marudio kwa sababu za kijinga ni ujinga!. Ili Taifa letu lipate maendeleo ya kweli, ni lazima sisi Watanzania tukubali kuwa wakweli toka ndani ya nafsi zetu, tusikubali ujinga huu wa kuhama vyama, uendelee kutugharimisha sisi masikini wa kutupwa, tunaoishi kwenye lindi la umasikini uliotopea, halafu kuendelea kugharimishwa na wajinga fulani kurudia uchaguzi kwa sababu tuu za kisiasa zilizosababishwa na ujinga fulani, yaani ujinga wao. usituumize sisi masikini wa Mungu ambao we have nothing!.

Nawatakia Furahi Dei Njema.

Paskali
Rejea.
Rev. Mtikila ashida kesi ya kuruhusu mgombea binafsi mahakama ya ...
Mtikila: Shujaa wa Demokrasia, Mwanamapinduzi halisi na Shujaa ...
Mgombea binafsi Tanzania: Tatizo ni nini? | Page 9 | JamiiForums ...
Swali kwa Wana UKAWA: Is UKAWA for Real or Just A Marriage of ...

Well said
 
Mkuu Pascal, umeongea kitu ambacho mimi naona ni tatizo kubwa sana Tanzania, kufikia mahali nimsema sana kwamba tatizo tulilo Tanzania na nchi masikini ni kuwa na watu wenye akili ndogo kama viongozi, eidha kwa kuteuliwa au kuchaguliwa kwa kura.

Frankly speaking, msimamo unaouweka wazi hapa mie naona kama ni political illiteracy, kwamba tuko tayari hata kumuunga mkono mwendawazimu ambae hataweza kuisaidia Tanzania katika maendeleo yetu, ili mradi tu ni mwanachama wa chama tunachoshabikia?

Hii ni partisanship of the stupidest order, ambayo mimi naona kama tunakuwa hivyo basi hatuna akili sawasawa na tunapaswa kuhurumiwa sana. Ni lazima watu tuelewe kwamba Tanzania is so much bigger than our Mickey Mouse political parties ili tuweze kuendelea, la sivyo tuondoe mfumo wa vyama vingi maana unakuwa counter productive, hautimizi objectives za kuuanzisha. What Nyerere had in mind aliposema tuanzishe mfumo wa vyama vingi sichi hiki kinachoendelea Tanzania.

Ni lini tutawachagua watu kutokana na sifa zao za kuwa voingozi badala ya kuwachagua kwa kuwa wako kwenye chama tunachoshabikia, no matter kiwe kinafanya upumbavu gani?

Ni lini tutaona maoni mazuri juu ya nchi yetu ni mazuri regardless yanatolewa na mtu wa chama tunachoshabikia au la?

NI lini upumbavu kwetu utakuwa ni upumbavu hata kama unafanywa na chama cha siasa tunachoshabikia?

Ni lini tutaacha kumshabikia na kumtetea Lowasa kwa kuwa yuko chama chetu, kumtukana kwa kuwa kahamia upinzani, na kumshabikia kwa kuwa karudi chama chetu? Huu ni unafiki ambao mtu yeyote mwenye akili ataelewa.

Ideallly, ningependa kuona Magufuli na Lissu wote wakiwa viongozi wa serikali ya Tanzania, kwa kuwa wao kuwa katika vyama tofauti ni missed opportunities kwa maendeleo ya nchi yetu. Ndio maana nakuambia it is better tuondoe mfumo wa vyama vingi. Watanzania we are just too immature, politically illiterate kuwa na siasa za vyama vingi. Hata nikiwa mbele ya Magufuli nitamwambia hata yeyey yuko too immature kuwa raisi katika mfumo wa vyama vingi. Hata Ndugai, Tulia, Kabudi nk. Majaliwa ana nafuu. Sijui Lissu, I may not be able kum-judge kwa sasa.
Karibu mitaa hii
P
 
Kwa sababu tarehe 28 October, Watanzania tunakwenda kufanya uamuzi, sasa muda huu kabla ya uchaguzi, najifanyia tathmini nilisema nini kuhusu uchaguzi huu, na baada ya matokeo, nitarejea na kupima kilichotokea na nilichokiona kabla.
Natoa wito kwa Watanzania wenzangu, tujitokeze kwa vingi kupiga kura na kuchagua chama, viongozi tunaowataka ambao watatuletea maendeleo ya kweli. Kwa wanaotaka maendeleo ya kweli, watachagua chama na maendeleo ya kweli, lakini kwa wanaotaka porojo tuu, rukhsa kuchagua porojo ni haki yako ya kidemokrasia kuchagua chama chochote, kiongozi yoyote.
Paskali.
 
Tume ya uchaguzi imetunga kanuni za uchaguzi ambazo kwa vyovyote vile zinatengeneza mazingira yasiyo rafiki kwa uchaguzi huru na wa haki.

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
 
Kwa sababu tarehe 28 October, Watanzania tunakwenda kufanya uamuzi, sasa muda huu kabla ya uchaguzi, najifanyia tathmini nilisema nini kuhusu uchaguzi huu, na baada ya matokeo, nitarejea na kupima kilichotokea na nilichokiona kabla.
Natoa wito kwa Watanzania wenzangu, tujitokeze kwa vingi kupiga kura na kuchagua chama, viongozi tunaowataka ambao watatuletea maendeleo ya kweli. Kwa wanaotaka maendeleo ya kweli, watachagua chama na maendeleo ya kweli, lakini kwa wanaotaka porojo tuu, rukhsa kuchagua porojo ni haki yako ya kidemokrasia kuchagua chama chochote, kiongozi yoyote.
Paskali.
Chagua wewe unayemtaka, Wengine wote wanajua watakaomchagua.....
 
Wanabodi,

Declaration of Interest.
Mimi ni miongoni mwa Watanzania wazalendo wa nchi yangu, ambaye japo ni mwanachama wa chama cha siasa, lakini tunapokuja kwenye kutanguliza mbele maslahi ya taifa, mimi taifa kwanza ndipo chama kinafuata, kwa sababu siasa za vyama vingi za Tanzania, tunaziona katika baadhi ya maeneo kama ni ujinga ujinga fulani hivi, bora turejee kwenye chama kimoja, hivyo nawaomba sana univumilie, ninapoita baadhi ya siasa zetu ni kama siasa za ujinga ujinga fulani kwa baadhi ya vyama na baadhi ya wanasiasa, na nasisitiza, nimesema baadhi, nikimaanisha sii zote na sii wote!.

Tubishane kwa Kutoa Hoja kwa Hoja, Kupangua Hoja kwa Hoja, na Sio Hoja Kwa Viroja!.
Hii ni opinion yangu tuu, and everybody has the right to his/her own opinion, hivyo tukitofautiana kwenye hili, tutofautiane kwa hoja, mimi nimeleta hoja zangu kuwa baadhi ya siasa zetu kwenye baadhi ya maeneo fulani fulani, likiwemo eneo la siasa za uchaguzi, kiukweli ni kama ujinga fulani, na zinavyoendeshwa, kuna maeneo zinaendeshwa kwa ujinga ujinga kabisa!. Hivyo naomba uzisome hoja zangu, ili tukitofautiana, tutofautiane kwa hoja, pangua hoja kwa hoja, kwa kupangua hoja zangu na ama kutetea ama kuleta hoja mbadala, nikiwasisitiza na kuwaomba tubishane kwa hoja na kushindanisha hoja kwa hoja, kupangua hoja kwa hoja mbadala na sio watu tumeleta hoja humu, halafu mtu anakuja kuibishia kwa viroja!.

Ili Tupate Maendeleo ya Kweli, Watanzania Lazima Tufanye Siasa za Ukweli, Tuachane na Siasa za Ujinga Ujinga!.
Nashauri kama ni kweli Tanzania tunataka maendeleo ya kweli ya taifa letu, ni lazima tufike mahali tufanye siasa za ukweli, the real politics na sio hizi siasa za blah blah tunazoendelea nazo. Tufike mahali, sisi Watanzania, wazalendo wa kweli wa nchi hii, wenye nia njema na ya dhati ya maendeleo ya kweli ya taifa hili letu masikini, hatuwezi kukaa kimya na kunyamaza kwa kuendelea kukumbatia sheria mbovu za uchaguzi ambazo Makama Kuu ya Tanzania imeziita kuwa ni "bad laws" na kushauri, zifutwe, "scraped" kutoka katika vitabu vya sheria!, lakini kwa vile sheria hizo mbovu, zinakinufaisha chama changu, then tunaendelea kuzing'ang'ania sheria hizo mbovu za uchaguzi, hata kama matumizi ya sheria hizo mbovu, ni kuwawabesha masikini wa Tanzania, mzigo mkubwa wa gharama za uchaguzi wa marudio, kwa sababu za kijinga jinga tuu kabisa, zinazotokana na siasa za ujinga ujinga!. Kitendo hiki cha masikini wa kutupwa wa Tanzania, wanaoishi kwenye lindi la umasikini uliotopea wa kipato cha chini ya dola moja kwa siku, halafu kuja kubebeshwa mzigo wa gharama za kugharimia uchaguzi za marudio, kutokana na diwani mmoja au mbunge mmoja kuhama chama hiki na kuhamia chama kile kwa sababu za kisiasa tuu, hizi ndizo siasa mimi ninazo ziita ni "siasa za ujinga ujinga!", na sababu zenyewe zinazowafanya wabunge na madiwani hao kuhama chama kimoja kwenda chama kingine, naziita kuwa ni sababu za kijinga jinga na nyingine ni za kijinga kabisa!. Kwa maoni yangu, this, its not only ni nonsense, but also ni dhambi kwa Mungu, kuwabebesha, Watanzania masikini hawa wa kutupwa, gharama hizi za ziada za uchaguzi wa marudio, kutokana na wawakilishi wao kuhama vyama kwa sababu tuu za hizi siasa zetu za ujinga ujinga, mimi nauita huu pia ni ujinga fulani in the name of politics!.

Kwa Nini Sheria Yetu ya Uchaguzi ni Sheria Mbovu, Bad Law.
Kifungu 21 cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kinatoa haki ya kila Mtanzania mwenye sifa, kuwa huru kushiriki katika siasa kuanzia serikali za mtaa hadi serikali kuu, bila ubaguzi wowote.

Uhuru wa kushiriki shughuli za umma Sheria ya 1984 Na.15 ib.6 Sheria ya 1994 Na.34 ya ib.4
21.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ya 5, ya 39 na ya 67 ya Katiba hii na ya sheria za nchi kuhusiana na masharti ya kuchagua na kuchaguliwa, au kuteua na kuteuliwa kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, ama moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi waliochaguliwa na wananchi kwa hiari yao, kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria.

Lakini kukatokea kikundi fulani cha watu, naomba kuwaita ni "wajinga fulani", wakaipindua katiba kwa sababu fulani za kijinga kabisa!, wakainyofoa haki hiyo ya raia kushiriki uongozi kwa uhuru kabisa, na badala yake, kulazimisha ili mtu ushiriki uongozi fulani, au ugombee nafasi fulani fulani ya uongozi wa umma, ni lazima kwanza udhaminiwe na chama cha siasa!, kiukweli kabisa na ki haki, huu ni ujinga!, this is nonsense!. Katiba yetu haikusema hivyo!.

Rev. Mtikila (Mungu amuweke pema peponi) alikipinga kifungu hiki na Mahakama Kuu ya Tanzania, ikatamka bayana kuwa kipengele hicho ni batili na kinakiuka katiba ya JMT hivyo kifutwe kwenye sheria, kila Mtanzania awe huru kugombea nafasi yoyote ya uongozi wa umma, au kwa kupitia vyama vya siasa, au bila kupitia chama chochote. Lakini wajinga wale, wakaamua kuihalalisha batili ile, kwa kukipenyeza kipengele hicho batili ndani ya katiba yetu, ili kuuhalalisha ujinga wao!, hivyo shurti la kudhaminiwa na chama sasa ni la kikatiba!.

Jee Lengo la Kudhaminiwa na Chama ni Nini?, Huu Sii Ujinga Tuu?!.
Katiba ilisema kila Mtanzania yuko huru na ana haki ya kushiriki uongozi, toka serikali za mtaa hadi serikali kuu bila kuwa na chama chochote. Hili sherti la kumlazimisha kudhaminiwa na chama lilitoka wapi?!, na kwa kwa nini watu walazimishwe kuwa wanachama wa vyama ili wadhaminiwe, ndipo waweze kugombea?!. Mfano mimi naishi Kawe, ikitokea nina uwezo wa kuwatumikia wananchi wa eneo langu la Kawe na kuwaletea maendeleo bila kupitia chama chochote, kwa nini nizuiliwe?!. Watanzania tusikubali na tupiganie milango ya wagombea huru na wagombea binafsi ifunguliwe, 2020, watu wenye uwezo wa uongozi, na wenye nia ya kugombea, ili kuwaletea wananchi maendeleo, bila kupitia hizi siasa vyama waingie, and you never know hata sisi kama mimi, tuingie, tushindane kwa hoja na sio kushindana kuhonga, kama hali inavyoendelea sasa!.

Kiongozi Akiishachaguliwa, Anakuwa ni Kiongozi wa Watu, na Sio Kiongozi wa Chama, Kwa Sababu Anachaguliwa na Watu na Sio Chama!.
Ujinga mwingine mkubwa kabisa wa siasa zetu za vyama, ni ujinga ni huu, hata kama mgombea amedhaminiwa na chama cha siasa kugombea, akiishapitishwa na Tume ya Uchaguzi kuwa Mgombea rasmi, japo anatambulika kama ni mgombea wa chama fulani, lakini anachaguliwa kwa kura za wananchi wa eneo lile wote wakiwemo wanachama wa chama chake, akiishachaguliwa, mwenyekiti wa mtaa, diwani, mbunge au rais, sasa anakuwa ni kiongozi wa umma na sio kiongozi wa chama kilichomdhamini, bali anakuwa ni kiongozi wa wananchi wa eneo lile waliomchagua, wasio mchagua hata wasiopiga kura, huyu sasa anakuwa ni kiongozi wa wote na sio kiongozi wa chama chake hata kama alidhaminiwa na chama fulani.. Mfano baada ya rais Magufuli kuchaguliwa kuwa rais kwa tiketi ya CCM, lakini hakuchaguliwa na wana CCM pekee, amechaguliwa na wananchi wote na Watanzania wote, na sasa sio kiongozi tuu wa CCM. kwa sababu ndie Mwenyekiti wao, bali rais Magufuli ni kiongozi wa Watanzania wote,wa vyama vyote, wa watu wote!. Hali ni vivyo hivyo kwa wabunge, madiwani na viongozi wa serikali ya mtaa, kitendo cha kiongozi wa umma, kujitoa chama kilichomdhamini na kupoteza uongozi wa umma, ubunge, udiwani au uongozi wa umma, ni ujinga ambao haupaswi kuvumiliwa na kuendelea kukumbatiwa!. Nini muhimu zaidi kati ya umma na chama?. Kuukosesha umma kiongozi waliemchagua kwa sababu za chama, sio tuu sio haki kwa wananchi waliomchagua, bali ni ujinga uliopitiliza!, halafu wananchi masikini wa Tanzania, kuja kulipisha gharama za kugharimia uchaguzi wa marudio, sio tuu ni ujinga mwingine, bali ni dhambi kuwagharimisha wananchi hawa gharama za kurudia uchaguzi kwa sababu fulani amejiuzulu chama hiki na kitu cha ajabu kabisa, huyo huyo fulani aliyejiuzulu, ndio anakuja kugombea tena kupitia chama kingine!.

Nini Kifanyike, A Way Forward.
Kama nilivyowahi kushauri humu, ukosoaji wenye kujenga, huandamana na ushauri wa nini kifanyike kurekebisha kasoro hizi ili kuundoa ujinga huu unaoendelea nchini mwetu kwa sasa.

  1. Iwekwe faini maalum kwa kila kiongozi wa umma, atakayejiuzulu nafasi yake kwa sababu za kijinga jinga, ikiwemo kukatwa mafao yake na ikibidi kufilisiwa ili kugharimia gharama za uchaguzi wa marudio kwa kulitia hasara taifa.
  2. Viongozi wote wanaojiuzulu, wasiruhusiwe tena kugombea nafasi zile zile walizojiuzulu, kama sababu za kujiuzulu mimi nimeziita ni za kijinga, tusiwakubalie wajinga hawa kugombea tena, ili wasije kutuletea tena ujinga ule ule na kutugharimisha masikini sisi kugharimia uchaguzi wa marudio!.
  3. Tubadili sheria yetu ya uchaguzi, kwa kufuta chaguzi zote ndogo, na tuanzishe mpango wa succession plan mgombea wa chama fulani aliyeshinda, tujenge hoja kuwa huyo aliyeshinda ameshinda kwa sababu ya chama c alichogombea hivyo wananchi wamekipa chama ridhaa, hivyo akijiuzulu, akisita kuwa mbunge, diwani, rais kwa sababu zozote zile, chama chake kiteue mwanachama mwingine kushika nafasi ile!. Hili likifanyika, amini usiamini, hatutasikia tena kiongozi anajiuzulu kwa sababu za kijinga jinga!.
  4. Kama tunaamini aliyechaguliwa ni mtu na sio chama, then diwani au mbunge awe huru kuhama na udiwani wake au ubunge wake kama nchini Kenya.
  5. Mbunge au diwani akijiuzulu au kufariki, tuanzishe kitu kinachoitwa "a proportional representation" kwa mwenye kura nyingi ndiye mshindi, lakini likitokea lolote, akasita kuwa rais, mbunge au diwani, yule aliyemfuatia kwa wingi wa kura katika uchaguzi uliopita ndio anatangazwa mbunge, diwani, rais, na kama hayupo anachukuliwa mtu wa tatu, hadi wa mwisho, kama wote hawapo, ndipo uchaguzi mdogo unafanyika.
  6. Kile kipengele cha kudhaminiwa na chama kiishie kwenye uteuzi tuu, kiongozi akiishachaguliwa, anakuwa kiongozi wa umma. kiongozi wa watu, anaweza kuhama chama bila kupoteza uongozi wake kama ilivyo nchini Kenya.
  7. Tubadili sheria yetu ya uchaguzi, kwa kuondoa kipengele cha kudhaminiwa na vyama ili kila Mtanzania mwenye sifa za kugombea uongozi wa nafasi yoyote, aruhusiwe, ila kwenye urais, tuweke vigezo vya ziada, ili asijetokea tajiri mmoja mwenye ukwasi wa kuwanunua Watanzania wote, tukajikuta tuna rais wa kununuliwa. Ila kwenye ubunge, udiwani na serikali za mtaa, kila mtu awe free kugombea, hivyo tuwe na wagombea huru, na hili likifanyika hata sisi tusio na vyama tutashiriki, mfano mimi, naweza kabisa kugombea jimbo fulani na kulitwaa kama kuokota embe dodo lililojiangukia, ambapo mbunge wa hapo, nitamsukuma kama nimesukuma mlevi!.
Hitimisho.
Tanzania is too poor spend billions on by elections!, nikimaanisha nchi yetu Tanzania ni masikini wa kutupwa, kuhalalisha matumizi ya mabilioni ya fedha kuendesha chaguzi ndogo marudio kwa sababu za kijinga ni ujinga!. Ili Taifa letu lipate maendeleo ya kweli, ni lazima sisi Watanzania tukubali kuwa wakweli toka ndani ya nafsi zetu, tusikubali ujinga huu wa kuhama vyama, uendelee kutugharimisha sisi masikini wa kutupwa, tunaoishi kwenye lindi la umasikini uliotopea, halafu kuendelea kugharimishwa kurudia uchaguzi kwa sababu tuu za kisiasa zilizosababishwa na ujinga usituumize sisi masikini wa Mungu ambao we have nothing!.

Nawatakia Furahi Dei Njema.

Paskali
Rejea.
Rev. Mtikila ashida kesi ya kuruhusu mgombea binafsi mahakama ya ...
Mtikila: Shujaa wa Demokrasia, Mwanamapinduzi halisi na Shujaa ...
Mgombea binafsi Tanzania: Tatizo ni nini? | Page 9 | JamiiForums ...

Swali kwa Wana UKAWA: Is UKAWA for Real or Just A Marriage of ...
This justifies the need for a new constitution. A constitution that calls for a total overhaul of the entire governance and the ruling system. A constitution that decentralizes the mentors of power into the hands of the citizens and not the president.
 
Kwenye demokrasia geresha(sham democracy) ndio kuna mambo ya mapingamizi na kuengua wagombea ili kuondoa ushindani.

Sheria na kanuni zote zinazoipa tume mamlaka ya kupokea mapingamizi na kuengeua wagombea kwa sababu yoyote ile zinapaswa kufutwa kabisa kwa sababu zinakiuka msingi mzima wa demokrasia ya vyama vingi na ushindani.

Sheria inapaswa kuwa kwamba wagombea waenguliwe kama sio raia au ni whalifu tena kupitia mahakama na sio tume au kamati.
 
Wanabodi,
Nini Kifanyike, A Way Forward.
Kama nilivyowahi kushauri humu, ukosoaji wenye kujenga, huandamana na ushauri wa nini kifanyike kurekebisha kasoro hizi ili kuundoa ujinga huu unaoendelea nchini mwetu kwa sasa.

  1. Iwekwe faini maalum kwa kila kiongozi wa umma, atakayejiuzulu nafasi yake kwa sababu za kijinga jinga, ikiwemo kukatwa mafao yake na ikibidi kufilisiwa ili kugharimia gharama za uchaguzi wa marudio kwa kulitia hasara taifa.
  2. Viongozi wote wanaojiuzulu, wasiruhusiwe tena kugombea nafasi zile zile walizojiuzulu, kama sababu za kujiuzulu mimi nimeziita ni za kijinga, tusiwakubalie wajinga hawa kugombea tena, ili wasije kutuletea tena ujinga ule ule na kutugharimisha masikini sisi kugharimia uchaguzi wa marudio!.
  3. Tubadili sheria yetu ya uchaguzi, kwa kufuta chaguzi zote ndogo, na tuanzishe mpango wa succession plan mgombea wa chama fulani aliyeshinda, tujenge hoja kuwa huyo aliyeshinda ameshinda kwa sababu ya chama c alichogombea hivyo wananchi wamekipa chama ridhaa, hivyo akijiuzulu, akisita kuwa mbunge, diwani, rais kwa sababu zozote zile, chama chake kiteue mwanachama mwingine kushika nafasi ile!. Hili likifanyika, amini usiamini, hatutasikia tena kiongozi anajiuzulu kwa sababu za kijinga jinga!.
  4. Kama tunaamini aliyechaguliwa ni mtu na sio chama, then diwani au mbunge awe huru kuhama na udiwani wake au ubunge wake kama nchini Kenya.
  5. Mbunge au diwani akijiuzulu au kufariki, tuanzishe kitu kinachoitwa "a proportional representation" kwa mwenye kura nyingi ndiye mshindi, lakini likitokea lolote, akasita kuwa rais, mbunge au diwani, yule aliyemfuatia kwa wingi wa kura katika uchaguzi uliopita ndio anatangazwa mbunge, diwani, rais, na kama hayupo anachukuliwa mtu wa tatu, hadi wa mwisho, kama wote hawapo, ndipo uchaguzi mdogo unafanyika.
  6. Kile kipengele cha kudhaminiwa na chama kiishie kwenye uteuzi tuu, kiongozi akiishachaguliwa, anakuwa kiongozi wa umma. kiongozi wa watu, anaweza kuhama chama bila kupoteza uongozi wake kama ilivyo nchini Kenya.
  7. Tubadili sheria yetu ya uchaguzi, kwa kuondoa kipengele cha kudhaminiwa na vyama ili kila Mtanzania mwenye sifa za kugombea uongozi wa nafasi yoyote, aruhusiwe, ila kwenye urais, tuweke vigezo vya ziada, ili asijetokea tajiri mmoja mwenye ukwasi wa kuwanunua Watanzania wote, tukajikuta tuna rais wa kununuliwa. Ila kwenye ubunge, udiwani na serikali za mtaa, kila mtu awe free kugombea, hivyo tuwe na wagombea huru, na hili likifanyika hata akina sisi tuliolazimika kujiunga vyama fulani vya siasa, tutaachana navyo na tutashiriki, as independent candidates mfano mimi, naweza kabisa kugombea jimbo fulani na kulitwaa kama kuokota embe dodo lililojiangukia, ambapo mbunge wa hapo, nitamsukuma kama nimesukuma mlevi!.
Mkuu ZZK, Zitto , pokea baadhi ya nondo, zipime, mkiona zina sifa, zijumuishe katika maazimio ya kikao chenu cha TCD, leo yanayokabidhiwa Kwa kile kikosi kazi, yatue mezani Kwa Mama, ili sheria zifanyiwe mabadiliko kabla ya uchaguzi wa 2025.

Waliosusa waacheni wasuse, maana kama awamu ya 5, la katiba lilikuwepo kwenye ilani ya CCM, na hatukumlazinisha JPM kubadili katiba, sasa la katiba halimo kwenye ilani ya Samia, hivyo kumshiza au kumlazimisha Samia kukamilisha mchakato wa katiba mpya ni kumuonea!. Tunaweza kubadili baadhi ya sheria kandamizi na kuvibadili baadhi ya vipengele kandamizi vya katiba iliyopo, kuwezesha uchaguzi wa 2025, kuwa ni uchaguzi huru na wa haki, halafu mchakato wa katiba mpya ukaendelea, Kwa nafasi baada ya 2025.

Chadema na NCCR wamekunja ngumi na kuificha kwenye mifuko yao ya mapajama waliovaa wakati wa kulala usiku, ngumi hizi wanangojea waone wapi pa kuzichomolea na kuzirusha kwa waliemkusudia, kususia ni kumuonea mama bila sababu. Vitendo hivi vya kung'ng'ania lazima muungano uwe wa serikali tatu ndivyo vilivyokwamisha mchakato mzima wa katiba hadi leo. Katiba ile ingekuwa na muungano wa serikali mbili lakini Tume huru ya uchaguzi. Kususa kulisababisha kukosekana kwa serikali tatu lakini na tume huru ya uchaguzi.
 
Wanabodi,
Kuna kitu nilikisema kwenye bandiko hili sasa kinakwenda kutokea tena kwenye huu uchaguzi wa serikali za mitaa.
Kitu chenyewe ni hiki

  1. Kile kipengele cha kudhaminiwa na chama kiishie kwenye uteuzi tuu, kiongozi akiishachaguliwa, anakuwa kiongozi wa umma. kiongozi wa watu, anaweza kuhama chama bila kupoteza uongozi wake kama ilivyo nchini Kenya.
  2. Tubadili sheria yetu ya uchaguzi, kwa kuondoa kipengele cha kudhaminiwa na vyama ili kila Mtanzania mwenye sifa za kugombea uongozi wa nafasi yoyote, aruhusiwe, ila kwenye urais, tuweke vigezo vya ziada, ili asijetokea tajiri mmoja mwenye ukwasi wa kuwanunua Watanzania wote, tukajikuta tuna rais wa kununuliwa. Ila kwenye ubunge, udiwani na serikali za mtaa, kila mtu awe free kugombea, hivyo tuwe na wagombea huru, na hili likifanyika hata sisi tusio na vyama tutashiriki, mfano mimi, naweza kabisa kugombea jimbo fulani na kulitwaa kama kuokota embe dodo lililojiangukia, ambapo mbunge wa hapo, nitamsukuma kama nimesukuma mlevi!.
  3. Hoja yangu ni mgombea akiishadhaminiwa na chama cha siasa na kupitishwa kuwa mgombea, sasa anakuwa ni mgombea wa umma na sio mgombea wa chama.
  4. Wanaomchagua kuwa Mwenyekiti wa serikali ya mtaa, diwali, mbunge au rais ni wananchi na sio watu wa chama chake.
  5. The power basis ya katiba ni watu, wananchi, "we the people". Watu ndio msingi wa katiba, na uchaguzi unafanyika ili kuwapa fursa watu kuchagua viongozi wao.
  6. Process ya uchaguzi ni kutoa legitimacy kwa kiongozi aliyechaguliwa na watu. Kitendo cha chama cha siasa kumvua uanachama kiongozi wa watu na kupoteza uongozi wa umma kiukweli kabisa huu ni ujinga fulani. Yaani umma wenye katiba umchague mtu kiongozi wao, halafu kije kitokee kidubwana kimfute uanachama na kupoteza uongozi wa umma!, this is awkward!.
  7. Kwenye uchaguzi huu wa serikali za mitaa vyama vya Chadema, ACT na UPDP vimejitoa, lakini Waziri Jaffo katangaza majina yatabandikwa na hakuna kuweka mpira kwapani.
  8. Kuna possibility baadhi ya wagombea wa vyama vilivyojitoa wakachaguliwa kuwa viongozi wa wananchi. Kitakachofuata ni viongozi hao watalazimishwa kujiudhuru na wakigoma watafutwa uanachama hivyo kupoteza uongozi wa umma, na kupelekea uchaguzi wa marudio, hapa nauliza tena kiukweli kabisa huu sio ujinga?.
P
Eti huyu jamaa ndo alisema kama chadema hawarekebisha katiba yao hakuna haja ya kuandika katiba mpya wa wananchi wote. Njaa inasumbua Sana vijana wetu
 
Chadema na NCCR wamekunja ngumi na kuificha kwenye mifuko yao ya mapajama waliovaa wakati wa kulala usiku, ngumi hizi wanangojea waone wapi pa kuzichomolea na kuzirusha kwa waliemkusudia, kususia ni kumuonea mama bila sababu. Vitendo hivi vya kung'ng'ania lazima muungano uwe wa serikali tatu ndivyo vilivyokwamisha mchakato mzima wa katiba hadi leo. Katiba ile ingekuwa na muungano wa serikali mbili lakini Tume huru ya uchaguzi. Kususa kulisababisha kukosekana kwa serikali tatu lakini na tume huru ya uchaguzi.
Sasa anaumia nani? KWA kutokuwa na katiba, ni chadema au nnccr au wananchi wote mkiandika mtumiage akili kidogo,

Haya Hali ngumu ya maisha kipindi hikiinayosababishwa na Serikali dhaifu, bunge dhaifu unailaumu chadema?
 
Back
Top Bottom