Sheria ya Uchaguzi ni mbovu! Kuendelea kuitumia sio Ujinga? Kuwabebesha masikini gharama za Uchaguzi sio Dhambi?

Wanabodi,

Declaration of Interest.
Mimi ni miongoni mwa Watanzania wazalendo wa nchi yangu, ambaye japo ni mwanachama wa chama cha siasa, lakini tunapokuja kwenye kutanguliza mbele maslahi ya taifa, mimi taifa kwanza ndipo chama kinafuata, kwa sababu siasa za vyama vingi za Tanzania, tunaziona katika baadhi ya maeneo kama ni ujinga ujinga fulani hivi, bora turejee kwenye chama kimoja, hivyo nawaomba sana univumilie, ninapoita baadhi ya siasa zetu ni kama siasa za ujinga ujinga fulani kwa baadhi ya vyama na baadhi ya wanasiasa, na nasisitiza, nimesema baadhi, nikimaanisha sii zote na sii wote!.

Tubishane kwa Kutoa Hoja kwa Hoja, Kupangua Hoja kwa Hoja, na Sio Hoja Kwa Viroja!.
Hii ni opinion yangu tuu, and everybody has the right to his/her own opinion, hivyo tukitofautiana kwenye hili, tutofautiane kwa hoja, mimi nimeleta hoja zangu kuwa baadhi ya siasa zetu kwenye baadhi ya maeneo fulani fulani, likiwemo eneo la siasa za uchaguzi, kiukweli ni kama ujinga fulani, na zinavyoendeshwa, kuna maeneo zinaendeshwa kwa ujinga ujinga kabisa!. Hivyo naomba uzisome hoja zangu, ili tukitofautiana, tutofautiane kwa hoja, pangua hoja kwa hoja, kwa kupangua hoja zangu na ama kutetea ama kuleta hoja mbadala, nikiwasisitiza na kuwaomba tubishane kwa hoja na kushindanisha hoja kwa hoja, kupangua hoja kwa hoja mbadala na sio watu tumeleta hoja humu, halafu mtu anakuja kuibishia kwa viroja!.

Ili Tupate Maendeleo ya Kweli, Watanzania Lazima Tufanye Siasa za Ukweli, Tuachane na Siasa za Ujinga Ujinga!.
Nashauri kama ni kweli Tanzania tunataka maendeleo ya kweli ya taifa letu, ni lazima tufike mahali tufanye siasa za ukweli, the real politics na sio hizi siasa za blah blah tunazoendelea nazo. Tufike mahali, sisi Watanzania, wazalendo wa kweli wa nchi hii, wenye nia njema na ya dhati ya maendeleo ya kweli ya taifa hili letu masikini, hatuwezi kukaa kimya na kunyamaza kwa kuendelea kukumbatia sheria mbovu za uchaguzi ambazo Makama Kuu ya Tanzania imeziita kuwa ni "bad laws" na kushauri, zifutwe, "scraped" kutoka katika vitabu vya sheria!, lakini kwa vile sheria hizo mbovu, zinakinufaisha chama changu, then tunaendelea kuzing'ang'ania sheria hizo mbovu za uchaguzi, hata kama matumizi ya sheria hizo mbovu, ni kuwawabesha masikini wa Tanzania, mzigo mkubwa wa gharama za uchaguzi wa marudio, kwa sababu za kijinga jinga tuu kabisa, zinazotokana na siasa za ujinga ujinga!. Kitendo hiki cha masikini wa kutupwa wa Tanzania, wanaoishi kwenye lindi la umasikini uliotopea wa kipato cha chini ya dola moja kwa siku, halafu kuja kubebeshwa mzigo wa gharama za kugharimia uchaguzi za marudio, kutokana na diwani mmoja au mbunge mmoja kuhama chama hiki na kuhamia chama kile kwa sababu za kisiasa tuu, hizi ndizo siasa mimi ninazo ziita ni "siasa za ujinga ujinga!", na sababu zenyewe zinazowafanya wabunge na madiwani hao kuhama chama kimoja kwenda chama kingine, naziita kuwa ni sababu za kijinga jinga na nyingine ni za kijinga kabisa!. Kwa maoni yangu, this, its not only ni nonsense, but also ni dhambi kwa Mungu, kuwabebesha, Watanzania masikini hawa wa kutupwa, gharama hizi za ziada za uchaguzi wa marudio, kutokana na wawakilishi wao kuhama vyama kwa sababu tuu za hizi siasa zetu za ujinga ujinga, mimi nauita huu pia ni ujinga fulani in the name of politics!.

Kwa Nini Sheria Yetu ya Uchaguzi ni Sheria Mbovu, Bad Law.
Kifungu 21 cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kinatoa haki ya kila Mtanzania mwenye sifa, kuwa huru kushiriki katika siasa kuanzia serikali za mtaa hadi serikali kuu, bila ubaguzi wowote.

Uhuru wa kushiriki shughuli za umma Sheria ya 1984 Na.15 ib.6 Sheria ya 1994 Na.34 ya ib.4
21.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ya 5, ya 39 na ya 67 ya Katiba hii na ya sheria za nchi kuhusiana na masharti ya kuchagua na kuchaguliwa, au kuteua na kuteuliwa kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, ama moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi waliochaguliwa na wananchi kwa hiari yao, kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria.

Lakini kukatokea kikundi fulani cha watu, naomba kuwaita ni "wajinga fulani", wakaipindua katiba kwa sababu fulani za kijinga kabisa!, wakainyofoa haki hiyo ya raia kushiriki uongozi kwa uhuru kabisa, na badala yake, kulazimisha ili mtu ushiriki uongozi fulani, au ugombee nafasi fulani fulani ya uongozi wa umma, ni lazima kwanza udhaminiwe na chama cha siasa!, kiukweli kabisa na ki haki, huu ni ujinga!, this is nonsense!. Katiba yetu haikusema hivyo!.

Rev. Mtikila (Mungu amuweke pema peponi) alikipinga kifungu hiki na Mahakama Kuu ya Tanzania, ikatamka bayana kuwa kipengele hicho ni batili na kinakiuka katiba ya JMT hivyo kifutwe kwenye sheria, kila Mtanzania awe huru kugombea nafasi yoyote ya uongozi wa umma, au kwa kupitia vyama vya siasa, au bila kupitia chama chochote. Lakini wajinga wale, wakaamua kuihalalisha batili ile, kwa kukipenyeza kipengele hicho batili ndani ya katiba yetu, ili kuuhalalisha ujinga wao!, hivyo shurti la kudhaminiwa na chama sasa ni la kikatiba!.

Jee Lengo la Kudhaminiwa na Chama ni Nini?, Huu Sii Ujinga Tuu?!.
Katiba ilisema kila Mtanzania yuko huru na ana haki ya kushiriki uongozi, toka serikali za mtaa hadi serikali kuu bila kuwa na chama chochote. Hili sherti la kumlazimisha kudhaminiwa na chama lilitoka wapi?!, na kwa kwa nini watu walazimishwe kuwa wanachama wa vyama ili wadhaminiwe, ndipo waweze kugombea?!. Mfano mimi naishi Kawe, ikitokea nina uwezo wa kuwatumikia wananchi wa eneo langu la Kawe na kuwaletea maendeleo bila kupitia chama chochote, kwa nini nizuiliwe?!. Watanzania tusikubali na tupiganie milango ya wagombea huru na wagombea binafsi ifunguliwe, 2020, watu wenye uwezo wa uongozi, na wenye nia ya kugombea, ili kuwaletea wananchi maendeleo, bila kupitia hizi siasa vyama waingie, and you never know hata sisi kama mimi, tuingie, tushindane kwa hoja na sio kushindana kuhonga, kama hali inavyoendelea sasa!.

Kiongozi Akiishachaguliwa, Anakuwa ni Kiongozi wa Watu, na Sio Kiongozi wa Chama, Kwa Sababu Anachaguliwa na Watu na Sio Chama!.
Ujinga mwingine mkubwa kabisa wa siasa zetu za vyama, ni ujinga ni huu, hata kama mgombea amedhaminiwa na chama cha siasa kugombea, akiishapitishwa na Tume ya Uchaguzi kuwa Mgombea rasmi, japo anatambulika kama ni mgombea wa chama fulani, lakini anachaguliwa kwa kura za wananchi wa eneo lile wote wakiwemo wanachama wa chama chake, akiishachaguliwa, mwenyekiti wa mtaa, diwani, mbunge au rais, sasa anakuwa ni kiongozi wa umma na sio kiongozi wa chama kilichomdhamini, bali anakuwa ni kiongozi wa wananchi wa eneo lile waliomchagua, wasio mchagua hata wasiopiga kura, huyu sasa anakuwa ni kiongozi wa wote na sio kiongozi wa chama chake hata kama alidhaminiwa na chama fulani.. Mfano baada ya rais Magufuli kuchaguliwa kuwa rais kwa tiketi ya CCM, lakini hakuchaguliwa na wana CCM pekee, amechaguliwa na wananchi wote na Watanzania wote, na sasa sio kiongozi tuu wa CCM. kwa sababu ndie Mwenyekiti wao, bali rais Magufuli ni kiongozi wa Watanzania wote,wa vyama vyote, wa watu wote!. Hali ni vivyo hivyo kwa wabunge, madiwani na viongozi wa serikali ya mtaa, kitendo cha kiongozi wa umma, kujitoa chama kilichomdhamini na kupoteza uongozi wa umma, ubunge, udiwani au uongozi wa umma, ni ujinga ambao haupaswi kuvumiliwa na kuendelea kukumbatiwa!. Nini muhimu zaidi kati ya umma na chama?. Kuukosesha umma kiongozi waliemchagua kwa sababu za chama, sio tuu sio haki kwa wananchi waliomchagua, bali ni ujinga uliopitiliza!, halafu wananchi masikini wa Tanzania, kuja kulipisha gharama za kugharimia uchaguzi wa marudio, sio tuu ni ujinga mwingine, bali ni dhambi kuwagharimisha wananchi hawa gharama za kurudia uchaguzi kwa sababu fulani amejiuzulu chama hiki na kitu cha ajabu kabisa, huyo huyo fulani aliyejiuzulu, ndio anakuja kugombea tena kupitia chama kingine!.

Nini Kifanyike, A Way Forward.
Kama nilivyowahi kushauri humu, ukosoaji wenye kujenga, huandamana na ushauri wa nini kifanyike kurekebisha kasoro hizi ili kuundoa ujinga huu unaoendelea nchini mwetu kwa sasa.

  1. Iwekwe faini maalum kwa kila kiongozi wa umma, atakayejiuzulu nafasi yake kwa sababu za kijinga jinga, ikiwemo kukatwa mafao yake na ikibidi kufilisiwa ili kugharimia gharama za uchaguzi wa marudio kwa kulitia hasara taifa.
  2. Viongozi wote wanaojiuzulu, wasiruhusiwe tena kugombea nafasi zile zile walizojiuzulu, kama sababu za kujiuzulu mimi nimeziita ni za kijinga, tusiwakubalie wajinga hawa kugombea tena, ili wasije kutuletea tena ujinga ule ule na kutugharimisha masikini sisi kugharimia uchaguzi wa marudio!.
  3. Tubadili sheria yetu ya uchaguzi, kwa kufuta chaguzi zote ndogo, na tuanzishe mpango wa succession plan mgombea wa chama fulani aliyeshinda, tujenge hoja kuwa huyo aliyeshinda ameshinda kwa sababu ya chama c alichogombea hivyo wananchi wamekipa chama ridhaa, hivyo akijiuzulu, akisita kuwa mbunge, diwani, rais kwa sababu zozote zile, chama chake kiteue mwanachama mwingine kushika nafasi ile!. Hili likifanyika, amini usiamini, hatutasikia tena kiongozi anajiuzulu kwa sababu za kijinga jinga!.
  4. Kama tunaamini aliyechaguliwa ni mtu na sio chama, then diwani au mbunge awe huru kuhama na udiwani wake au ubunge wake kama nchini Kenya.
  5. Mbunge au diwani akijiuzulu au kufariki, tuanzishe kitu kinachoitwa "a proportional representation" kwa mwenye kura nyingi ndiye mshindi, lakini likitokea lolote, akasita kuwa rais, mbunge au diwani, yule aliyemfuatia kwa wingi wa kura katika uchaguzi uliopita ndio anatangazwa mbunge, diwani, rais, na kama hayupo anachukuliwa mtu wa tatu, hadi wa mwisho, kama wote hawapo, ndipo uchaguzi mdogo unafanyika.
  6. Kile kipengele cha kudhaminiwa na chama kiishie kwenye uteuzi tuu, kiongozi akiishachaguliwa, anakuwa kiongozi wa umma. kiongozi wa watu, anaweza kuhama chama bila kupoteza uongozi wake kama ilivyo nchini Kenya.
  7. Tubadili sheria yetu ya uchaguzi, kwa kuondoa kipengele cha kudhaminiwa na vyama ili kila Mtanzania mwenye sifa za kugombea uongozi wa nafasi yoyote, aruhusiwe, ila kwenye urais, tuweke vigezo vya ziada, ili asijetokea tajiri mmoja mwenye ukwasi wa kuwanunua Watanzania wote, tukajikuta tuna rais wa kununuliwa. Ila kwenye ubunge, udiwani na serikali za mtaa, kila mtu awe free kugombea, hivyo tuwe na wagombea huru, na hili likifanyika hata akina sisi tuliolazimika kujiunga vyama fulani vya siasa, tutaachana navyo na tutashiriki, as independent candidates mfano mimi, naweza kabisa kugombea jimbo fulani na kulitwaa kama kuokota embe dodo lililojiangukia, ambapo mbunge wa hapo, nitamsukuma kama nimesukuma mlevi!.
Hitimisho.
Tanzania is too poor spend billions on by elections!, nikimaanisha nchi yetu Tanzania ni masikini wa kutupwa, kuhalalisha matumizi ya mabilioni ya fedha kuendesha chaguzi ndogo marudio kwa sababu za kijinga ni ujinga!. Ili Taifa letu lipate maendeleo ya kweli, ni lazima sisi Watanzania tukubali kuwa wakweli toka ndani ya nafsi zetu, tusikubali ujinga huu wa kuhama vyama, uendelee kutugharimisha sisi masikini wa kutupwa, tunaoishi kwenye lindi la umasikini uliotopea, halafu kuendelea kugharimishwa kurudia uchaguzi kwa sababu tuu za kisiasa zilizosababishwa na ujinga usituumize sisi masikini wa Mungu ambao we have nothing!.

Nawatakia Furahi Dei Njema.

Paskali
Rejea.
Rev. Mtikila ashida kesi ya kuruhusu mgombea binafsi mahakama ya ...
Mtikila: Shujaa wa Demokrasia, Mwanamapinduzi halisi na Shujaa ...
Mgombea binafsi Tanzania: Tatizo ni nini? | Page 9 | JamiiForums ...

Swali kwa Wana UKAWA: Is UKAWA for Real or Just A Marriage of ...
hongera kwa kulijua Hilo Pascal Mayalla mambo yaliyokaaa kimchongo hayafai
 
wapinzani wengi wala hawakumuelewa Marehemu Mtikila na Watanzania wengi hawakumuelewa Mtikila na kesi yake ya Mgombea Binafsi,ila CCM na watawala walimuelewa vyema adhma yake ndo maana walitumia kila aina ya hila kuifinyangafinyanga kesi yake.
Marehemu Mchungaji Christopha Mtikila ambaye yeo amelala huko kwenye kaburi lililopo mkoa wa Njombe,wilaya ya Ludewa katika kijiji cha Milo aliliona hili tatizo Mapema mno, lakini yeye alichukua hatua kwa kwenda mahakamani kudai madaraka ya wananchi yarudishwe kwa wananchi kwa kupitia kesi yake ya mgombea binafsi, mara ya kwanza alishinda kesi mara ya pili tena mbele ya marafiki wa mahakama wasomi na manguli kabisa wa sheria wakina prof kabudi ukatolewa uamuzi wa kijinga kabisa na waajabu, yaani chombo ambacho kinahusuka na kutafsiri sheria kikaamua kesi hiyo ipelekwe bungeni..kituko hiki.
kwa mazingira ya sasa hawa wagombea si wawakilishi wa wananchi hawa ni wawakilishi wa vyama vyao,wakati wa uchaguzi wanapelekwa kwa wananchi wakapigiwe kura ila wakishashinda tu hana cha kufanya na mwanachi tena, hawezi kumuogopa mwanachi aliyempa kura kwasababu hawana cha kumfanya mpaka wakati wa uchaguzi tena, ila kinyume chake hawa wanakuwa mali ya chama cha siasa kilichomsimamisha. chama chake kinageuka kuwa ndio mtoa amri kwakwe na ndiyo kinampangia nini cha kufanya na nini asifanya,yaani kwa kifupi ndyiyo kinamdhibiti huyu mwenyekiti wa mtaa, diwani, mbunge na raisi wa nchi, mhusika hata akitofautiana na wanachi cheo chake kipo salama kabisa ila siyo kutofautiana na chama chake, sa nyingine wanaweza hata wakawa na ugomvi na mwenyekiti wake au viongozi wake wa chama kwa visa vya kijinga kabisa ambavyo hata havihusiani na wanachi lakini ikawagharimu wanachi kumkosa na kupoteza muda kwa kuingia kwenye uchaguzi kumchagua mtu mwingine. mfano wakati ule wa Zito kabwe wanachi wake bado walikuwa na mahaba naye na bado walikuwa wanataka aendelee kuwa mbunge wao, lakini Zito alikuwa na ugomvi na chama chake, hivyo ugomvi ule ukasababisha Zito apoteze ubunge wake si kwa matakwa ya waliomchagua bali kwa matakwa ya Chama.
hili suala la sheria hii ya uchaguzi linatusumbua sana kiasi kwamba hata wabunge wanashindwa kufanya shughuli zao kwa utashi wao, maamuzi mengi wanayoyafanya bungeni ni maamuzi ya chama, kila ukiona wanaunga mkono jambo fulani basi jua chama chao kimeelekeza iwe hivyo, wabunge wa CCM wamekuwa wahanga sana kwenye hili mpaka imefika wakati hoja zao ambazo zinapingana na msimamo wa chama chao au zinakosoa serikali yao huwa wanawapenyezea wapinzani waziwasilishe, leo hii tunamshangaa Raisi wetu magufuli kuwa mbona anafanya mambo kana kwamba hakuwepo katika bunge, kila jambo anashangaa utafikiri kashushwa leo Tanzania, anafanya maamuzi kwa ukali anakishangaa Chama chake kwa kukumbatia uozo..anazishangaa serikali zilizopita kwa kukumbatioa ufisadi na ufujaji wa mali yauma na usainiji wa mikataba mibovu wakati ye mwenyewe alikuwa ni sehemu ya hizo hizo serikali na alikuwa ni sehemu ya wabunge waliopigia kura ya ndiyo mambo ya hovyo bungeni,HII YOTE NI KWASABABU YA SHERIA HII YA UCHAGUZI.
kwa kweli ifike mahala wananchi tupige kelele ili madaraka yarudishwe kwa wananchi, tuwamiliki hawa viongozi tunaowachagua kwa kura zetu, tumeviachia vyama vya siasa matokeo yake wanatumika kulinda maslahi ya watu fulani ndani ya vyama. leo hii taifa limekubwa na mambo ya kishamba kabisa ya kuhama hama kwa hawa wawakilishi wa uma, tunapoteza rasilimali fedha na tunapoteza rasilimali muda na saa nyingine tunawapoteza hata watu maana wengine hufariki kwa vurugu ya hizi chaguzi ndogo, damu humwagika na wengine hupata ama vilema au makovu ya kudumu kama alivyopata mama Rose kamili kwa kufanyiwa vitu vya ajabu huko Kalenga kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi mdogo.
kuongoza si lazima uwe ndani ya chama cha siasa, mwenyekiti wa mtaa anahitaji chama cha nini? Diwani anahitaji chama cha nini? mbunge anahitaji chama cha nini? raisi anahitaji chama cha nini? huu kweli ni mfumo wa kijinga kabisa. Eti tunamchagua raisi wa nchi ili aongozwe na utashi wa chama chake, leo hii tushukuru katiba ya CCM inampa uenyekiti wa chama mtu aliyechaguliwa kuwa raisi lakini hizo kofia kama zingekuwa mbili basi kuna hatari raisi angekuwa anapewa maagizo na mwenyekiti wa chama.
uraisi ni cheo ambacho kinatakiwa kiwe huru, mtu akiwa raisi aunde baraza lake la mawadhili na adhibitiwe na chombo cha wanachi ambacho ni bunge. hizi nafasi za kuchaguliwa basi yoyote mwenye sifa apewe nafasi ya kugombea na anadi sera zake kama mgombea huru na atayeona anataka kwenda kwenye chama basi aende, wengine sisi ni waumini wa ustawi na maendeleo ya jamii zetu ambao tunaona si lazima kupitia chama ili uwatumikie wanachi, vyama vyenyewe hivi havieleweki kwetu tunaona ni upumbavu tu, kwanini watu kama sisi tunabaguliwa na kunyimwa haki yetu ya kupigiwa kura kama hatuko kwenye vyama?...hapana tupaze sauti zetu
Mnyikungu.
Vyama ni Makampuni.ukitofautiana nao wanakupiga chini
 
Mkuu ZZK, Zitto , pokea baadhi ya nondo, zipime, mkiona zina sifa, zijumuishe katika maazimio ya kikao chenu cha TCD, leo yanayokabidhiwa Kwa kile kikosi kazi, yatue mezani Kwa Mama, ili sheria zifanyiwe mabadiliko kabla ya uchaguzi wa 2025.

Waliosusa waacheni wasuse, maana kama awamu ya 5, la katiba lilikuwepo kwenye ilani ya CCM, na hatukumlazinisha JPM kubadili katiba, sasa la katiba halimo kwenye ilani ya Samia, hivyo kumshiza au kumlazimisha Samia kukamilisha mchakato wa katiba mpya ni kumuonea!. Tunaweza kubadili baadhi ya sheria kandamizi na kuvibadili baadhi ya vipengele kandamizi vya katiba iliyopo, kuwezesha uchaguzi wa 2025, kuwa ni uchaguzi huru na wa haki, halafu mchakato wa katiba mpya ukaendelea, Kwa nafasi baada ya 2025.

Paskali
Pascal kaka, unaweza kuwa sawa ukiutazama mchakato wa mabadiliko ya katiba kwa jicho la aibu, (kuwaonea aibu waliopo madarakani), lakini ukiutazama kwa uhalisia wake hakika inastaajabisha namna tunavyojadili jambo hili, kwa sababu;

1. Mchakato wa mabadiliko ya katiba sio mpya, Mh.Rais (Samia Suluhu Hassan) alikuwa miongoni mwa wenyeviti walioendesha bunge maalum la katiba, (kumtaka amalizie mchakato si kumuonea hata kidogo, ni wajibu wake)

2. Mchakato uliendeshwa na watu wanaoaminika sana, (warioba na timu yake) walifanya kazi yao kwa weredi mkubwa, wakatuletea "maoni ya wananchi juu ya mambo mbali mbali" ikatengenezwa rasimu ya kwanza ya katiba, yakaundwa mabaraza kama sheria (Na. 83) ya mabadiliko ya katiba ilivyotaka, na kutuletea rasimu ya pili!

3. Likaundwa bunge maalum la katiba, likatumia mabilioni ya shilingi, (japo kuna waliotoka ndani ya bunge kwa kutokubaliana ndani ya bunge) lakini haikusimamisha mchakato, uliendelea mpaka tulipoletewa "katiba inayopendekezwa" walioshiriki mchakato ule, wakaifaidi keki ya taifa na kurejea makwao mifuko ikiwa imetuna! Hatukupiga kura kuikubali au kuikataa katiba inayopendekezwa!

Kwanini isiwe kuihuisha sheria ya mabadiliko ya katiba ili mchakato ufikie mwisho badala ya kuanza kupakana mafuta kwa mgongo wa chupa kwamba mchakato usubiri kwanza 2025...pesa zetu zulizopotea kwa mabilioni nani anawajibika kuzilipa?

Kwa maoni yangu bora hata tungehitimisha kwa kuipigia kura katiba inayopendekezwa, kuliko hii danadana inayopigwa na kutoa sababu zisizo na mashiko kwamba mchakato wa katiba usubiri kwanza, kana kwamba ndo tunaanza wakati tulishafika mbali sana tu!

4. Wote tunajua tulipata Rais mchapa kazi kweli kweli, JPM lakini uchapa kazi wenye kupuyanga puyanga tu, alikuwa haeleweki hata anataka kulifanyia nini taifa zaidi zaidi alitaka kujimilikisha nchi na kutaka abakie madarakani kwa miaka mingi zaidi ya matakwa ya katiba yetu!

Mwisho, kaka Pascal Mayalla, tuisaidieni nchi yetu, hii habari ya kutosema ukweli wa mambo tunajenga jamii ya ajabu sana, haiwezekani nchi yetu masikini hivi ipoteze mabilioni ya shilingi kizembe zembe tu na bado tuone ni sawa!
 
Ilikuwa sawa mchakato kuishia pale ulipoishia, maana baada ya hapo ilikuwa ni kupiga kura ya maoni ya wananchi yaliyochakachuliwa. Tungepoteza pesa nyingi kwenye kura na bado haya yangeweza kutokea
1. Wananchi kuikataa katiba ile na hivyo kurudi kwenye katiba ya sasa (unnecessary cost)
2.Wananchi kuhujumiwa kuwa wamekubali katiba mpya wakati haina tofauti kubwa na ile ya zamani (another unnecessary cost).
Mchakato mpya uanzie kwenye katiba iliyopendekezwa kutokana na maoni ya wananchi siyo ile iliyopendekezwa na wabunge.
Pili wajumbe wa bunge la katiba wasiwe hawa wabunge wa sasa. Iwe ni marufuku kwa wabunge kuwa wajumbe ili kuondoa mgongano wa maslahi (mtakumbuka mwakilishi wa kundi fulani alivyoacha kutetea maoni ya wanachama wake akaanza kutetea maoni ya chama tawala kwa kuwa alitarajia kuwa mgombea). Na wawakilishi katika bunge la katiba na ndugu zao wa karibu, wasiruhusiwe kuwa wagombea wa vyeo vya kisiasa kwa miaka 10 inayofuata ili kuondoa mgongano wa maslahi
 
Pascal kaka, unaweza kuwa sawa ukiutazama mchakato wa mabadiliko ya katiba kwa jicho la aibu, (kuwaonea aibu waliopo madarakani), lakini ukiutazama kwa uhalisia wake hakika inastaajabisha namna tunavyojadili jambo hili, kwa sababu;

1. Mchakato wa mabadiliko ya katiba sio mpya, Mh.Rais (Samia Suluhu Hassan) alikuwa miongoni mwa wenyeviti walioendesha bunge maalum la katiba, (kumtaka amalizie mchakato si kumuonea hata kidogo, ni wajibu wake)

2. Mchakato uliendeshwa na watu wanaoaminika sana, (warioba na timu yake) walifanya kazi yao kwa weredi mkubwa, wakatuletea "maoni ya wananchi juu ya mambo mbali mbali" ikatengenezwa rasimu ya kwanza ya katiba, yakaundwa mabaraza kama sheria (Na. 83) ya mabadiliko ya katiba ilivyotaka, na kutuletea rasimu ya pili!

3. Likaundwa bunge maalum la katiba, likatumia mabilioni ya shilingi, (japo kuna waliotoka ndani ya bunge kwa kutokubaliana ndani ya bunge) lakini haikusimamisha mchakato, uliendelea mpaka tulipoletewa "katiba inayopendekezwa" walioshiriki mchakato ule, wakaifaidi keki ya taifa na kurejea makwao mifuko ikiwa imetuna! Hatukupiga kura kuikubali au kuikataa katiba inayopendekezwa!

Kwanini isiwe kuihuisha sheria ya mabadiliko ya katiba ili mchakato ufikie mwisho badala ya kuanza kupakana mafuta kwa mgongo wa chupa kwamba mchakato usubiri kwanza 2025...pesa zetu zulizopotea kwa mabilioni nani anawajibika kuzilipa?

Kwa maoni yangu bora hata tungehitimisha kwa kuipigia kura katiba inayopendekezwa, kuliko hii danadana inayopigwa na kutoa sababu zisizo na mashiko kwamba mchakato wa katiba usubiri kwanza, kana kwamba ndo tunaanza wakati tulishafika mbali sana tu!

4. Wote tunajua tulipata Rais mchapa kazi kweli kweli, JPM lakini uchapa kazi wenye kupuyanga puyanga tu, alikuwa haeleweki hata anataka kulifanyia nini taifa zaidi zaidi alitaka kujimilikisha nchi na kutaka abakie madarakani kwa miaka mingi zaidi ya matakwa ya katiba yetu!

Mwisho, kaka Pascal Mayalla, tuisaidieni nchi yetu, hii habari ya kutosema ukweli wa mambo tunajenga jamii ya ajabu sana, haiwezekani nchi yetu masikini hivi ipoteze mabilioni ya shilingi kizembe zembe tu na bado tuone ni sawa!
Ni litaka kukupa 5 kwa ujinga huu hapana umekuja kuharibu hapa
 
Ilikuwa sawa mchakato kuishia pale ulipoishia, maana baada ya hapo ilikuwa ni kupiga kura ya maoni ya wananchi yaliyochakachuliwa. Tungepoteza pesa nyingi kwenye kura na bado haya yangeweza kutokea
1. Wananchi kuikataa katiba ile na hivyo kurudi kwenye katiba ya sasa (unnecessary cost)
2.Wananchi kuhujumiwa kuwa wamekubali katiba mpya wakati haina tofauti kubwa na ile ya zamani (another unnecessary cost).
Mchakato mpya uanzie kwenye katiba iliyopendekezwa kutokana na maoni ya wananchi siyo ile iliyopendekezwa na wabunge.
Pili wajumbe wa bunge la katiba wasiwe hawa wabunge wa sasa. Iwe ni marufuku kwa wabunge kuwa wajumbe ili kuondoa mgongano wa maslahi (mtakumbuka mwakilishi wa kundi fulani alivyoacha kutetea maoni ya wanachama wake akaanza kutetea maoni ya chama tawala kwa kuwa alitarajia kuwa mgombea). Na wawakilishi katika bunge la katiba na ndugu zao wa karibu, wasiruhusiwe kuwa wagombea wa vyama vya siasa kwa miaka 10 inayofuata ili kuondoa mgongano wa maslahi
Good
 
a sababu zenyewe zinazowafanya wabunge na madiwani hao kuhama chama kimoja kwenda chama kingine, naziita kuwa ni sababu za kijinga jinga na nyingine ni za kijinga kabisa!. Kwa maoni yangu, this, its not only ni nonsense, but also ni dhambi kwa Mungu, kuwabebesha, Watanzania masikini hawa wa kutupwa, gharama hizi za ziada za uchaguzi wa marudio, kutokana na wawakilishi wao kuhama vyama kwa sababu tuu za hizi siasa zetu za ujinga ujinga, mimi nauita huu pia ni ujinga fulani in the name of politics!.
Usiziite za ujingaujinga Mayala, ziite ni umalaya! wanaume mnakubali kuwa Ma- kaka poa ni dhambi sana!
 
Sasa anaumia nani? KWA kutokuwa na katiba, ni chadema au nnccr au wananchi wote mkiandika mtumiage akili kidogo,

Haya Hali ngumu ya maisha kipindi hikiinayosababishwa na Serikali dhaifu, bunge dhaifu unailaumu chadema?
Hii ya hali ngumu ya maisha kupanda msitafute kick za kizombo. Mama kakuta hazina imekaushwa, aliamza upya, miradi mikubwa ya reli, bwawa, umeme na maji kwa wote vikiwa vinatakiwa kuendelea, COVID-19 na vita ya Ukraine na Urusi vinahisika sana. Hata Ulaya wanalia kwa kupanda bei ya maisha.
 
Mpaka Sasa watanzania wameshaanza kupotea Imani na wagombea wa vyama vya upinzani kwa ngazi zote. Hapa naongelea ngazi za urais, ubunge na udiwani, hasa kutokana na uwezo wao wa kuhamia Chama tawala wakati wowote. Hebu ona wagombea kama Lyatonga, Slaa, Lipumba, Ngoyai, Membe, Sumaye, Lamwai, wabunge na madiwani wanaorudi CCM bila kujali nguvu na jasho la waliowaigia na kulinda kura zao
 
Chadema na NCCR wamekunja ngumi na kuificha kwenye mifuko yao ya mapajama waliovaa wakati wa kulala usiku, ngumi hizi wanangojea waone wapi pa kuzichomolea na kuzirusha kwa waliemkusudia, kususia ni kumuonea mama bila sababu. Vitendo hivi vya kung'ng'ania lazima muungano uwe wa serikali tatu ndivyo vilivyokwamisha mchakato mzima wa katiba hadi leo. Katiba ile ingekuwa na muungano wa serikali mbili lakini Tume huru ya uchaguzi. Kususa kulisababisha kukosekana kwa serikali tatu lakini na tume huru ya uchaguzi.
Katiba pendekezwa haikuwa na tume huru ya uchaguzi.

Kifupi mchakato ule uliirudisha katiba mpya in a new pdf doc tu
 
Ina maana unataka kusema tupitishe kipengele ambacho kinasema hata Bakhressa/mengi/manji/dewji akiamua anagombea uchguzi wa raisi kama mgombea binafsi?.
Tanzania ni changa sana kwenye suala zima la demokrasia!..labda naomba unipe mfano wa nchi ambayo inafanya huo uchaguzi wa mgombea binafsi!!..
Haujasoma uzi ukauelewa.
 
Hili ni bandiko la 2017, hoja zake bado ni valid, ile siku Rais Samia anaruhusu mikutano ya siasa, alizungumzia kuziangalia baadhi ya sheria zetu kandamizi tuzifanyie mabadiliko, moja ya sheria hizo ni sheria hii ambayo mimi bado nalia nayo!. Madudu haya ya ajabu ya kisheria yaliweza kufanyika vipi wakati tuna Wanasheria?
Hayo nilioita ni madudu ya ajabu ndio sheria hiyo!.
P
Endapo maoni haya kwenye Katiba mpya yatafanyiwa kazi, tutakuwa tumepiga hatua.
 
Hili ni bandiko la 2017, hoja zake bado ni valid, ile siku Rais Samia anaruhusu mikutano ya siasa, alizungumzia kuziangalia baadhi ya sheria zetu kandamizi tuzifanyie mabadiliko, moja ya sheria hizo ni sheria hii ambayo mimi bado nalia nayo!. Madudu haya ya ajabu ya kisheria yaliweza kufanyika vipi wakati tuna Wanasheria?
Hayo nilioita ni madudu ya ajabu ndio sheria hiyo!.
P
Kuruhusu mgombea binafsi bila kulazimika kupitia mavyama haya ni muhimu sana. Kwani tunaogopa nini kusita kuruhusu mgombea binafsi?

Tuwe na njia za wazi za kupiga kura ili kila mtu achaguliwe na kushindwa kwa wazi kutokana na sera zake. Lakini tuwe na uwezo pia wa kuweza kumdhibidi kiongozi yeyoyote yule asieongoza kwa mujibu wa makubaliano (katiba) yetu. Yaani tuwe na njia za wazi za kumdhibiti kiongozi wa kuchaguliwa wakati wowote aliyeukanyaga mstari mwekundu tuliojichorea sisi wenyewe kama taifa.
 
Kuruhusu mgombea binafsi bila kulazimika kupitia mavyama haya ni muhimu sana. Kwani tunaogopa nini kusita kuruhusu mgombea binafsi?

Tuwe na njia za wazi za kupiga kura ili kila mtu achaguliwe na kushindwa kwa wazi kutokana na sera zake. Lakini tuwe na uwezo pia wa kuweza kumdhibidi kiongozi yeyoyote yule asieongoza kwa mujibu wa makubaliano (katiba) yetu. Yaani tuwe na njia za wazi za kumdhibiti kiongozi wa kuchaguliwa wakati wowote aliyeukanyaga mstari mwekundu tuliojichorea sisi wenyewe kama taifa.
Mimi naona kuwepo kwa ukomo wa ubunge na udiwani , kwani mtu anadumu miaka 40, hii inanyima haki kileleni kipengele cha kila raia mwenye sifa ana haki ya kuchagua na kuchaguliwa. Hiyo ya mtu kukaa muda mrefu kuweza kupelekea rushwa kukua.
 
Wanabodi,

Declaration of Interest.
Mimi ni miongoni mwa Watanzania wazalendo wa nchi yangu, ambaye japo ni mwanachama wa chama cha siasa, lakini tunapokuja kwenye kutanguliza mbele maslahi ya taifa, mimi taifa kwanza ndipo chama kinafuata, kwa sababu siasa za vyama vingi za Tanzania, tunaziona katika baadhi ya maeneo kama ni ujinga ujinga fulani hivi, bora turejee kwenye chama kimoja, hivyo nawaomba sana univumilie, ninapoita baadhi ya siasa zetu ni kama siasa za ujinga ujinga fulani kwa baadhi ya vyama na baadhi ya wanasiasa, na nasisitiza, nimesema baadhi, nikimaanisha sii zote na sii wote!.
Hivi binadam wengi awawezi kuishi kabisa kwenye wanacho kiamini. Kaka mleta post ulikua mmoja ya wale walioshangiria makosa yaliyofanyika kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa wakati wa utawala wa JPM. Tupo tuliopinga hiyo tabia na hayo matuimizi mabaya ya dola na katiba ingawa wewe na genge lako mlikua mstari wa mbele kusema kinachofanywa ni sahihi kabisa. Nataka kusema nini hapa? Wewe na genge lako una moral authority na legitimacy kusema wala kushauri hilo
Mkuu Bishweko , asante kwa mchango wako, ila kuna watu ukishawajua ni makada wa kile chama chetu pekee, unadhani wote ni wa kereketwa au wafurukutwa, wengine ni makada wazalendo, wanasimama na haki bin haki, kada mimi ni mmoja wapo, angalia mada zangu hizi kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa 2019.
P
 
Back
Top Bottom