Sheria ya Uchaguzi Ni Bad Law!, Kuendelea Kuitumia ni Ujinga?, Kuwabebesha Masikini Gharama za Uchaguzi ni Dhambi!. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheria ya Uchaguzi Ni Bad Law!, Kuendelea Kuitumia ni Ujinga?, Kuwabebesha Masikini Gharama za Uchaguzi ni Dhambi!.

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Pascal Mayalla, Dec 15, 2017.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Dec 15, 2017
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,640
  Likes Received: 23,836
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,

  Declaration of Interest.
  Mimi ni miongoni mwa Watanzania wazalendo wa nchi yangu, ambaye sio mwanachama wa Chama chochote cha siasa, kwa sababu siasa za vyama za Tanzania, tunaziona kama ni ujinga Fulani hivi, hivyo nawaomba sana univumilie, ninapoita siasa za ujinga ujinga, hii ni opinion yangu, everybody has the right to his/her own opinion, hivyo tukitofautiana kwenye hili, tutofautiene kwa hoja, mimi nimeleta hoja zangu kuwa siasa zetu kwenye maeneo Fulani Fulani zikiwezo siasa za uchaguzi ni ujinga ujinga kwa hoja, naomba tubishane kwa hoja.

  Watanzania Tufanye Siasa za Ukweli, Tuachane na Siasa za Ujinga Ujinga.
  Tufike mahali sisi Watanzania, wazalendo, wenye nia njema na maendeleo ya taifa hili letu masikini, hatuwezi kukaa kimya kwa kuendelea kukumbatia sheria mbovu, bad laws, za uchaguzi, na kuendelea kuwawabesha masikini wa Tanzania, mzigo wa gharama za uchaguzi wa marudio, kwa sababu za kijinga jinga kabisa, zinazotokana na siasa za ujinga ujinga!. Kitendo hiki cha masikini wa kutupwa wa Tanzania, wanaoishi kwenye lindi la umasikini uliotopea wa kipato cha chini ya dola moja kwa siku, halafu kuja kubebeshwa mzigo wa kugharimia chaguzi za marudio kutokana na sababu za kisiasa za ujinga ujinga, na sababu zenyewe kuwa ni sababu za kijinga kabisa, its not only ni nonsense, but also ni dhambi kwa Mungu, kuwabebesha masikini hawa gharama hizi za ziada kutokana na ujinga tuu wa watu fulani in the name of politics!..

  Kwa Nini Sheria Yetu ya Uchaguzi ni Sheria Mbovu, Bad Law.
  Kifungu 21 cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kinatoa haki ya kila Mtanzania mwenye sifa, kuwa huru kushiriki katika siasa kuanzia serikali za mtaa hadi serikali kuu, bila ubaguzi wowote.

  Uhuru wa kushiriki shughuli za umma Sheria ya 1984 Na.15 ib.6 Sheria ya 1994 Na.34 ya ib.4
  21.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ya 5, ya 39 na ya 67 ya Katiba hii na ya sheria za nchi kuhusiana na masharti ya kuchagua na kuchaguliwa, au kuteua na kuteuliwa kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, ama moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi waliochaguliwa na wananchi kwa hiari yao, kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria.

  Lakini kukatokea kikundi Fulani cha wajinga Fulani, wakaipindua katiba kwa sababu Fulani za kijinga kabisa, wakainyofoa haki hiyo ya raia kwa kulazimisha, ili mtu ugombee nafasi yoyote ya uongozi wa umma, ni lazima udhaminiwe na chama cha siasa!, kiukweli kabisa na ki haki, this is nonsense!.

  Rev. Mtikila alikipinga kifungu hiki na Mahakama Kuu ikatamka bayana kipengele hicho ni batili na kinakiuka katiba ya JMT. Wajinga wale, wakaamua kuihalalisha batili ile, kwa kukipenyeza kipengele hicho batili kwenye katiba, ili kuuhalalisha ujinga wao!.

  Japo Lengo la Kudhaminiwa na Chama ni Nini, Huu Sii Ujinga Tuu?!.
  Katiba katiba ilisema kila Mtanzania ana haki ya kushiriki uongozi, hili sherti la kudhaminiwa na chama lilitoka wapi, na kwa kwa nini watu walazimishwe kuwa wanachama wa vyama ili wadhaminiwe, ndipo waweze kugombea?. Mfano mimi, sina chama kwa sababu naziona siasa za vyama kwa ni ujinga Fulani hivi, ikitokea nina uwezo wa kuwatumikia wananchi wa eneo langu na kuwaletea maendeleo bila kupitia chama chochote, kwa nini nizuiliwe?!. Kiukweli kabisa, huu ni ujinga, it is nonsense, Watanzania tusikubali ujinga huu uendelee hadi 2020!, tupiganie milango ya wagombea binafsi ifunguliwe, 2020, watu wenye nia ya kugombea, tuwaletee wananchi maendeleo, bila kupitia hizi nonsense za vyama tuingie, tushindane kwa hoja na sio kushindana kuhonga, kama hali inavyoendelea sasa!.


  Kiongozi Akiishachaguliwa, Anakuwa ni Kiongozi wa Watu, na Sio Kiongozi wa Chama, Kwa Sababu Anachaguliwa na Watu na Sio Chama!.
  Ujinga mwingine mkubwa kabisa ni huu, hata kama mgombea amedhaminiwa na chama cha siasa kugombea, akiishapitishwa na Tume ya Uchaguzi kuwa Mgombea, japo anatambulika kama ni mgombea wa chama Fulani, lakini akiishachaguliwa, mwenyekiti wa mtaa, diwani, mbunge au rais, anakuwa sio kiongozi wa chama kilichomdhamini, bali anakuwa ni kiongozi wa wananchi. Mfano baada ya rais Magufuli kuchaguliwa kuwa rais kwa tiketi ya CCM, lakini hakuchaguliwa na wana CCM, amechaguliwa na Watanzania, na sio kiongozi wa CCM bali kiongozi wa Watanzania wote, vivyo hivyo kwa wabunge, madiwani na viongozi wa serikali ya mtaa, kitendo cha kujitoa chama na kupoteza ubunge, udiwani au uongozi wa umma, ni ujinga ambao haupaswi kuvumiliwa. Nini muhimu kati ya umma na chama?. Kuukosesha umma kiongozi waliemchagua kwa sababu za chama, sio tuu sio haki kwa wananchi waliomchagua, bali ni ujinga uliopitiliza, halafu kuja kulipisha wananchi hawa ngarama za uchaguzi wa marudio ni ujinga mwingine na dhambi juu yake ukizingatia kiwango cha umasikini wa nchi yetu.

  Nini Kifanyike, A Way Forward.
  Kama nilivyowahi kushauri humu, ukosoaji wenye kujenga, huandamana na ushauri wa nini kifanyike kurekebisha kasoro hizi ili kuundoa ujinga huu unaoendelea nchini mwetu kwa sasa.
  1. Iwekwe faini maalum kwa kila kiongozi wa umma, atakayejiuzulu nafasi yake kwa sababu za kijinga jinga, ikiwemo kukatwa mafao yake na ikibidi kufilisiwa ili kugharimia gharama za uchaguzi wa marudio kwa kulitia hasara taifa.
  2. Viongozi wote wanaojiuzulu, wasiruhusiwe tena kugombea nafasi walizojiuzulu, kama sababu za kujiuzulu mimi nimeziita ni za kijinga, tusiwakubalie wajinga hawa kugombea tena, ili wasije kutuletea tena ujinga ule ule na kutugharimisha masikini sisi kugharimia uchaguzi wa marudio.
  3. Tubadili sheria yetu ya uchaguzi, kwa kufuta chaguzi zote ndogo, na tuanzishe proportional representation kwa mwenye kura nyingi ndiye mshindi, lakini likitokea lolote, akasita kuwa rais, mbunge au diwani, yule aliyemfuatia katika uchaguzi uliopita ndio anatangazwa mbunge, kama hayupo anachuliwa mtu wa tatu, hadi wa mwisho, kama wote hawapo, ndipo uchaguzi mdogo unafanyika.
  4. Kile kipengele cha kudhaminiwa na chama kiishie kwenye uteuzi tuu, kiongozi akiishachaguliwa, anakuwa kiongozi wa watu, anaweza kuhama chama bila kupoteza uongozi wake kama ilivyo nchini Kenya.
  5. Tubadili sheria yetu ya uchaguzi, kwa kuondoa kipengele cha kudhaminiwa na vyama ili kila Mtanzania mwenye sifa za kugombea uongozi wa nafasi yoyote, aruhusiwe, ila kwenye urais, tuweke vigezo vya ziada, ili asijetokea tajiri mmoja mwenye ukwasi wa kuwanunua watanzania wote, tukajikuta tuna rais wa kununuliwa. Ila kwenye ubunge, udiwani na serikali za mtaa, kila mtu awe free kugombea, hivyo tuwe na wagombea huru, na hili likifanyika hata sisi tusio na vyama tutashiriki, mfano mimi, naweza kabisa kugombea jimbo fulani na kulitwaa kama kuokota embe dodo lililojiangukia, ambapo mbunge wa hapo, nitamsukuma kama nimesukuma mlevi!.
  Hitimisho.
  Tanzania is too poor spend billions on by elections for foolish and nonsense reasons, nikimaanisha nchi yetu Tanzania ni masikini wa kutupwa, kuhalalisha matumizi ya mabilioni ya fedha kuendesha chaguzi ndogo kwa sababu za kijinga. Ili Taifa letu lipate maendeleo ya kweli, ni lazima sisi Watanzania tukubali kuwa wakweli toka ndani ya nafsi zetu, tusikubali ujinga huu wa kuhama vyama, uendelee kutugharimisha sisi masikini wa kutupwa, tunaishi kwenye lindi la umasikini uliotopea, halafu kuendelea kugharimishwa na wajinga Fulani kwa sababu za ujinga wao!.

  Nawatakia Furahi Dei Njema.

  Paskali
  Rejea.
  Rev. Mtikila ashida kesi ya kuruhusu mgombea binafsi mahakama ya ...
  Mtikila: Shujaa wa Demokrasia, Mwanamapinduzi halisi na Shujaa ...
  Mgombea binafsi Tanzania: Tatizo ni nini? | Page 9 | JamiiForums ...
  Swali kwa Wana UKAWA: Is UKAWA for Real or Just A Marriage of ...
   
 2. AKASINOZO

  AKASINOZO JF-Expert Member

  #2
  Dec 15, 2017
  Joined: Aug 22, 2016
  Messages: 425
  Likes Received: 595
  Trophy Points: 180
  Na ww mkuu mayala umeliona hili asnte kwa bandiko mjalabu
   
 3. Bepari

  Bepari JF-Expert Member

  #3
  Dec 15, 2017
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 882
  Likes Received: 287
  Trophy Points: 80
  Si huwa mnasema demokrasia ina gharama? Hata hamueleweki mnataka nini aisee...
   
 4. Marlex Jr El

  Marlex Jr El JF-Expert Member

  #4
  Dec 15, 2017
  Joined: Nov 6, 2015
  Messages: 1,298
  Likes Received: 1,427
  Trophy Points: 280
  Paskali waweza kuwa si mwanachama wa chama chochote lakini unakereketwa na "sera, itikadi na imani " ya chama moja wapo hapa Tz.
   
 5. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #5
  Dec 15, 2017
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 28,267
  Likes Received: 48,906
  Trophy Points: 280
  Katiba mbovu wala sio demokrasia.

  Alafu Demokrasia gani inaruhusu kununua wanasiasa?
   
 6. Kasimba G

  Kasimba G JF-Expert Member

  #6
  Dec 15, 2017
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,615
  Likes Received: 617
  Trophy Points: 280
  good analysis mzalendo mwenzangu! Nadhani taifa letu sasa linageuka kuwa taifa la wehu! sijajua sababu ni nini haswa!

  Akili za wananchi wenzetu zinaenda kinyume, technology inaongezeka mataifa mengine wanakimbia kwenda mbele na technology yao sisi waTanzania tumegeuka tuna kimbilia nyuumaa!
   
 7. Econometrician

  Econometrician JF-Expert Member

  #7
  Dec 15, 2017
  Joined: Oct 25, 2013
  Messages: 8,662
  Likes Received: 7,965
  Trophy Points: 280
  Shida yako mayalla wewe ni kigeugeu,hata ikitokea siku umeandika kitu cha maana bado tutaona unafanya ukigeu geu.Mwanaume lazima uwe na msimamo katika maisha sio unakuwa wa uvugu vugu.
   
 8. MKWEPA KODI

  MKWEPA KODI JF-Expert Member

  #8
  Dec 15, 2017
  Joined: Nov 28, 2015
  Messages: 20,665
  Likes Received: 44,116
  Trophy Points: 280
  Mkuu Pascal Mayalla Utawala uliofitinika haujali, hutumia mabavu, hupofuka, hausikii, Mpaka Mungu mwenyewe atakapoamua kuusambaratisha kwa aibu kubwa
   
 9. Econometrician

  Econometrician JF-Expert Member

  #9
  Dec 15, 2017
  Joined: Oct 25, 2013
  Messages: 8,662
  Likes Received: 7,965
  Trophy Points: 280
  mapendekezo yako ni sawa umemwaga tone la maji ktk bahari-hamn hata moja linalowezekana kama CCM wanaendelea kuongoza
   
 10. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #10
  Dec 15, 2017
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 4,278
  Likes Received: 4,440
  Trophy Points: 280
  Pascal Mayalla umesema vyema
  Kwa nini Bunge lipo kimya na huu mwendelezo haramu?
  Wanaohama vyama na kujivua ubunge wagharamie uchaguzi kama sivyo washindi wa pili kila jimbo lililoachwa wazi wapewe ubunge au yabaki wazi hadi 2020
  Huu ni upuuzi na upumbavu kuwafanya Wananchi hasa walipa kodi kwamba pesa yao inaweza tumika vile mtu anapenda.
  Wahame lakini walipe gharama zote awe ni ccm au upinzani hili linawahusu wasitufanye hamnazo.
   
 11. mrangi

  mrangi JF-Expert Member

  #11
  Dec 15, 2017
  Joined: Feb 19, 2014
  Messages: 24,955
  Likes Received: 11,181
  Trophy Points: 280
  Umewapiga dongo jamaa wa lumumba
  Uzi wako watauchungulia tu,watauona mchungu ....

  Ova
   
 12. morenja

  morenja JF-Expert Member

  #12
  Dec 15, 2017
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 4,022
  Likes Received: 1,282
  Trophy Points: 280
  Swali je hao waendekeza ujinga wakaugeuza ndio kazi yao ya kupatia riziki watakusikia kweli !!!???
   
 13. PTER

  PTER JF-Expert Member

  #13
  Dec 15, 2017
  Joined: Dec 28, 2014
  Messages: 2,073
  Likes Received: 1,431
  Trophy Points: 280
  Tatizo lipo kwetu wananchi kuendelea kuamini kuwa hawa wanasiasa wajinga wana nia njema sana na sisi hii si kweli hata kidogo wanachopigania ni kuwa madarakani tu hata kama hawana uwezo wa kujenga kesho iliyobora kwetu.

  Tuna kila sababu ya kuamka na kupigania mamlaka yetu kikatiba kama wananchi. Hatuwezi kuendelea kuwa Mali ya serikali na kwamba hata kama tuna mitazamo tofauti na inavyotenda hatuna cha kufanya tukifanya lolote tunakiona cha mtema kuni.

  Sheria nyingi mbovu mbovu kama hizi zinatunyima fursa kama wananchi ya kuwa na mamlaka hata kwa tunaowachagua badala yake hutufanyia kila mazila wanayoyaweza kuyafanya na tusiwe na lolote la kufanya. Hatuwezi kuendelea kuushuhudia huu upumbavu japo wewr umeuita ujinga Mimi nauona ni upumbavu uliopitiliza unaotufanya tuendelee kugeuzwa mazezeta na wanasiasa wapumbavu wanaotumia rasilimali zetu kipumbavu.

  Nini kifanyike.
  Tuanzishe harakati ya kufanya mabadiliko mqkubwa kwenye sheria ya uchaguzi kama tumeshindwa katiba ifanyiwe mabadiliko ya haraka tuondokane na huu ushenzi unaofanywa na wanasiasa wapumbavu.

  TUTUMIE UPUUZI HUU KUKWEPA UPUUZI UJAO.
   
 14. Bepari

  Bepari JF-Expert Member

  #14
  Dec 15, 2017
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 882
  Likes Received: 287
  Trophy Points: 80
  Ndiyo muache kuwanunua wanasiasa!
   
 15. Clkey

  Clkey JF-Expert Member

  #15
  Dec 15, 2017
  Joined: May 29, 2014
  Messages: 4,112
  Likes Received: 10,064
  Trophy Points: 280
  Kuna wakati najiulizaga hvi hawa tunaowapigia kura kwa mapenzi yote kabisaaaaaa kwann wao wanatuchukia, hawakumbuki hata marupurupu mazuri na mishahara mizuri ni kwa sababu yetu, hawana utu kabisaaa,hawatuonei huruma kabisaaaa,na awamu hii ndo wanatuumiza kweli,mamaangu kijijini anatema a lot of Km kufata maji ambayo sio safi na salama kabisaaa, lkn limtu linakuja na masababu yake ya kipuuzi linajivua ubunge tunarudia uchaguzi, hzo pesa kwann zisiwasaidie wananchi, na wananchi tumejawa uwoga bila Katiba mpya tutalia weeeeeee lkn haitasaidia kitu
   
 16. Kingo

  Kingo JF-Expert Member

  #16
  Dec 15, 2017
  Joined: May 12, 2009
  Messages: 805
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 60
  Andiko lina mantiki kisiasa, kidemokrasia, kuiwakilishi na kikatiba.
   
 17. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #17
  Dec 15, 2017
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 37,374
  Likes Received: 16,338
  Trophy Points: 280
  Pasco ameleta thread ni individual opinion, sasa unapoandika "eti huwa mnasema" hao wanaosema ni kina nani? Na ni nani hapa ni muwakilishi wa hao.

  Hizi ni tabia za kikahaba kabisa jiangalie.
   
 18. wilbald

  wilbald JF-Expert Member

  #18
  Dec 15, 2017
  Joined: Dec 17, 2007
  Messages: 1,569
  Likes Received: 878
  Trophy Points: 280
  Sometimes you speak the truth but not in spirit... So try to reverse your thoughts to earn more likes.
   
 19. Deodat

  Deodat JF-Expert Member

  #19
  Dec 15, 2017
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 1,279
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Shida yako unafuata msafara wa chama fulani bila kuhoji. Ukiwa na tabia ya kuhoji, ni ngumu sana kuwa na msimamo na chama chochote Tanzania, vyote vimejaa ujinga ujinga tu.................
   
 20. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #20
  Dec 15, 2017
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 28,267
  Likes Received: 48,906
  Trophy Points: 280
  Vitu vitatu ninavyovichukia zaidi katika huu Ulimwengu:cha kwanza CCM, cha pili CCM, cha tatu CCM.

  Hawa watu na lichama lao ndio wametufikisha hapa.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...