Sheria ya Uchaguzi kupoka haki za raia, Uchaguzi utakua Huru na wa Haki?

chameleon

JF-Expert Member
Dec 4, 2013
555
170
Kama wananchi tumepata kwa mshituko mkubwa sana taarifa za Tume ya Uchaguzi kuhusu sheria ya ubaguzi ya uchaguzi inayompoka wananchi haki yake ya kikatiba . Ni wazi kwamba kwa kumlazimisha Mtanzania apige kura sehemu aliyojiandikisha tu na si kwingineko ndani ya Tanzania ni ubaguzi ambao umeacha watanzania wengi hususani wanavyuo bila haki ya kupiga kura kwani wengi wao walijiandikisha ktk maeneo ya vyuo ambavyo sasa vimefungwa kupisha zoezi la uchaguzi mkuu. Katiba ya JMT Na. 13.(1)-(5) ...inaendelea
 
Katiba ya JMT (1977). Ibara 13 (1) . Watu wote ni sawa mbele ya sheria, na wanayo haki, bila ya ubaguzi wowote, kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sheria.
...inaendelea
 
Unategemea vipi uchaguzi huru wakati tume inayosimamia haiko huru?
 
Katiba ya JMT (1977) Ibara 13 (2). Ni marufuku kwa sheria iliyowekwa na mamlaka yoyote katika Jamhuri ya Muungano kuweka sharti lolote ambalo ni la ubaguzi ama wa dhahiri au kwa taathira yake.
...inaendelea
 
Katiba ya JMT (1977). Ibara 13 (3). Haki za raia, wajibu na maslahi ya kila mtu na jumuia ya watu yatalindwa na kuamuliwa na mahakama na vyombo vinginevyo vya Mamlaka ya Nchi vilivyowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria. ...itaendelea
 
Katiba ya JMT (1977). Ibara 5 (3). Bunge litatunga Sheria ya Uchaguzi na kuweka masharti kuhusu mambo yafuatayo- (a)..., (b)..., (c)Utaratibu wa kumwezesha mpiga kura aliyejiandikisha sehemu moja kupiga kura sehemu nyingine na kutaja masharti ya utekelezaji wa utaratibu huo;
 
Back
Top Bottom