Sheria ya ubakaji...

Mbonea

JF-Expert Member
Jul 14, 2009
640
20
Wadau, leo asubuhi nilikuwa nikisikiliza BBC swahili ambapo walikumbushia sheria ya mwaka 1998 ya ubakaji ambapo mwanaume ndiye anahukumiwa... Sasa kutokana na mwanamke mmoja kufungwa kifungo cha miaka saba (7) huko Moshi, mkoani Kilimanjaro kwa kosa la "kumbaka" mvulana wa miaka 15, watetezi wa haki za binadamu na wanasheria wamejitokeza na kupendekeza sheria hiyo ibadilishwe na wanawake nao wahukumiwe coz ilikuwa inalenga kumwadhibu mwanaume tu ukijumlisha na ile ya hata kukonyeza...

Je, munaonaje hapo?
 
Iyo iko sawa na yeye kwa mujibu wa utaratibu uwo na yeye pia kabaka
kwa iyo kifungo kilikua kinamuhusu
 
ile sheria ilitungwa kwa jazba na kwa shinikizo la wanharakati amabao kutokana na vuguvugu la ulingo wa beijing (1995) walimchukulia mwanume kuwa mkosaji na mwenye asili ya mkosaji. .......................na kwa kweli toka wakati huo ukisikia maoni ya wanaharakakti yalionyesha aina ya kumlaumu mwanaume kwa kumkandamiza mwanamke kwa kumnyima haki na kuhodhi madaraka ya utawala. .........................mtazamo huu ndio uliopelekea sheria ile ikatungwa kama sehemu ya mkakati wa uwalinda wanawake na watotot wa kikke wapate fursa kadhaa kama vile elimu bila kukatishwa na tamaa na ukatili wa wanajamii wenzao wa jinsia ya kiume. ...................hatua nyingine za klindaa fursa hizi ililkuwa ni pamoja na kuanzisha kikatiba nafasi za upendeleo wa wanawake (affirmative policy/actions) za ubunge, udiwani na nafazi za uongozi na utendaji serikalini na katika mashirika yake..................

haya yalionekana tangu mwanzo waliokuwa na uelewa wa kutosha na waliikosoa tangu wakati huo. sasa utekelezaji wake ndio unaonekana. .........................sio tu haikuzingatia haki za mtoto wa kiume, lakini pia nadiriki kusema kuwa hata haki za wanawake na watoto wa kike hazikuzingatiwa, mfano unapomfunga baba miaka 30 jela, familia yake (ikiwa na mke na hata watoto wengine wa kike) itaishije ikizingatiwa kuwa familia nyingi baba ndiye anayetegemewa kugharimia mkate, masomo, afa nk.... ..............ni sawa na kusema msichana mmoja alindwe kwa gharama ya kuangamiza future ya familia nzima yenye kujumuisha mke (mwanamke) na watoto (wakiwemo wa kike pia.................. adhabu zilizotungwa na seria hizi zilipitiliza maana ya kuadhibu na kuwa ya kukomoa jinsia ya kiume......................
 
Ni kweli muundo wa sheria hii unawabana zaidi wanaume.,hili si la kushangaza sana kwani hata long title ya hii sheria ya SOSPA inaeleza wazi and I quote...
An Act to amend several laws written making special provisions in those
laws with regard to sexual and other offences to further safeguard the
personal integrity, dignity, liberty and security of women and children
.

Kwa hiyo unaweza kuona kuwa ilikuwa imewalenga zaidi wanawake na watoto, kwa utaratibu huo basi ikawaweka wanaume katika kundi la offenders, kuna makosa mengi tu ambayo mwanamke akiyafanya yanashindwa kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria hii, ni vyenma sheria hii ikapitiwa upya kwani imepitwa na wakati, kwani katika ulimwengu wa sasa si lazima mtu awe na kiungo cha kiume (kibakio) ndio aweze kufanya ubakaji.
 
wanawake wanaweza kubaka, na sio mtoto tu, wanaweza kumbaka hata mtu mzima mwenzao.
kuna wanaume waliowekewa vileo wakawa hawajijui waka end up kufanya tendo, na kwa nchi za ulaya wameweza kuwashitaki wanawake kwa kosa la ubakaji.
tanzania si dhani kama ni rahisi kwa mwanmme rijali kwenda kushitaki kuwa amebakwa ( amelazimishwa kufanya tendo la ndoa bila ridhaa)
 
umewahi sikia ni kesi ngapi zipo mahakamani kuwa mwanaume kaendashtaki kama amebakwa?
 
Back
Top Bottom