Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura Na. 343 "Kuhusu kukaa mita 200" Inasema

Mr Chin

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
4,625
1,024
[h=2]
kura.jpg
[/h][h=2]MAZOEA YA KUWEPO UMBALI WA MITA 200 AU 300 KUTOKAKITUO CHA KUPIGIA KURA[/h]

Kumekuwepo na mazoea kwamba, baada ya kupiga kura wafuasiwa vyama hubakia na kukaa kwenye maeneo ya kupigia kuraumbali wa mita 100 au 200 au 300.Jambo hili ni kinyume na Sheria za Uchaguzi. Kwani, katikakifungu cha 104 (1) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura Na. 343kinasema nanukuu

“Hakuna mtu atakayefanya Mkutano siku ya kupiga kura au;ndani ya jengo lolote ambamo upigaji kura katika uchaguziunaendelea, au mahali popote ndani ya eneo la mita miambili yajingo hilo, kuvaa au kuonyesha kadi ya picha yoyote, upendeleoau nembo nyingine inayoonesha kuunga mkono mgombea Fulanikatika uchaguzi”

Mwisho wa kunukuu.

Aidha, kifungu cha 103 (1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali zaMitaa, Sura ya 292 kinasema, Nanukuu:

“hakuna mtu atakayeruhusiwa, katika jengo lolote ambalo upigajikura katika uchaguzi unaendelea, au njia yoyote inayotumiwa naumma ndani ya umbali wa mita mia tatu ya mlango wowote wakuingilia katika jengo, atavaa au kuonyesha kadi, upendeleo au 4nembo yoyote inayoashiria kumuunga mkono mgombea Fulanikatika uchaguzi”Mwisho wa kunukuu.

Kifungu cha 5 cha Sheria ya Adhabu, Sura Na. 16 kinaelezamaana ya njia ya Umma.

Nanukuu:

“Public way includes any highway, market place, square, street,bridge or other way which is lawfully used by the public”

Mwisho wa kunukuu.

Vifungu vya Sheria zote kwa pamoja havisemi wala kutoa fursa aunafasi kwa wananchi kukusanyika bali zinapiga marufuku nakukataza uvaaji wa sare, au nembo au alama za Vyama vya Siasasiku ya kupiga kura kwa umbali kati ya mita 200 na 300.

Hivyo basi ieleweke kwamba umbali huo wa mita 200 mpaka 300sio umbali unaowaruhusu watu kukusanyika kwa kisingizio chakulinda kura.

Aidha, uzoefu unaonesha kwamba, katika kampenizinazoendelea, pale ambapo wafuasi wa vyama tofautiwanapokutana uwezekano wa kutokea vurugu ni mkubwa nasehemu nyingine vurugu zimetokea na kusababisha maafamajeruhi na uharibifu mali.

Source: http://www.nec.go.tz/uploads/documen...20UCHAGUZI.pdf

Wacha tu tulinde kura, kwenye chaguzi za mitaa wezi wa kura walikuwa cdm, walikuwa wanasombana kwa bodaboda kupiga kura mbilimbili, wacha tu tulinde wote tena tubebe na mapanga kabisa, tumeshambiwa kura ni mali.
 
sheria hii hsijasema watu wabaki au wasibaki nje ya mita 200 kamwe. hivo ni hiari ya mtu kubaki ama kutokubaki...tume au serikali hawana mamlaka ya kuwazuia watu kubaki...
 
Ni kipengele gani cha sheria kinachokata nje ya mita 200??

Kama hakuna basi hatuwezi kusema kuwazuia watu ni kwa mujibu wa sheria

Kuelekea uchaguzi ni vema ushauri uliotolewa kwa tume kukaa na viongozi wa vyama vya siasa vinavyoshiriki uchahuzi pamoja na Jeshi la Polisi kupata muafaka wa pamoja wa hekima ya jambo hili ili vyovyote iwavyo isizue vurugu
 
Yaaan watu wengne ni hewa.
Kfungu kimekataza kukaa ndani ya mita 200 na hakjakataza kukaa nje ya mita 200.
Tutalinda kura.
Viva ukawa viva.
 
Kifungu Cha Kwanza Kinakataza Kufanya Mkutano Ndani Ya Mita Miambili, Katika Eneo La Kupigia Kura, Ila Kuanzia Mita Miambili Na Kuendelea Ni Ruhusa, Kifungu Cha Pili Kinazuia Kuvaa Sare Za Chama Ndani Ya Mita Mia Tatu, Hvy Kuanzia Mita Mia Tatu Na Kuendelea Wanaruhusiwa Kuvaa Sare. KUHUSU KIFUNGU CHA KWANZA, KWA KUWA KINAKATAZA KUFANYA MKUTANO NDANI YA MITA MIA MBILI, NA KWA KUWA WATAKAOBAKI WAKISUBIRIA MATOKEO HAWATAKUWA NA MKUTANO,NA KWA KUWA WATAKUWA NJE YA MITA MIA MBILI, NA KWA KUWA HAWATAVAA SARE KWA HOJA HIZO BASI, Ni Halali Kabisa Kusubiria Matokeo Nje Ya Mita Miambili, Na Kwa Wale WATAKAOTAKA KUSUBIRIA MATOKEO WAKIWA WAMEVAA SARE ZA VYAMA VYAO WANAPASWA WAKAE NJE YA MITA MIA TATU KUTOKA ENEO LA KUPIGIA KURA KISHA WAPIGE KAMBI HAPO. Nawatakia Uchaguzi Mwema.
 
[h=2]
kura.jpg
[/h][h=2]MAZOEA YA KUWEPO UMBALI WA MITA 200 AU 300 KUTOKAKITUO CHA KUPIGIA KURA[/h]

Kumekuwepo na mazoea kwamba, baada ya kupiga kura wafuasiwa vyama hubakia na kukaa kwenye maeneo ya kupigia kuraumbali wa mita 100 au 200 au 300.Jambo hili ni kinyume na Sheria za Uchaguzi. Kwani, katikakifungu cha 104 (1) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura Na. 343kinasema nanukuu

“Hakuna mtu atakayefanya Mkutano siku ya kupiga kura au;ndani ya jengo lolote ambamo upigaji kura katika uchaguziunaendelea, au mahali popote ndani ya eneo la mita miambili yajingo hilo, kuvaa au kuonyesha kadi ya picha yoyote, upendeleoau nembo nyingine inayoonesha kuunga mkono mgombea Fulanikatika uchaguzi”

Mwisho wa kunukuu.

Aidha, kifungu cha 103 (1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali zaMitaa, Sura ya 292 kinasema, Nanukuu:

“hakuna mtu atakayeruhusiwa, katika jengo lolote ambalo upigajikura katika uchaguzi unaendelea, au njia yoyote inayotumiwa naumma ndani ya umbali wa mita mia tatu ya mlango wowote wakuingilia katika jengo, atavaa au kuonyesha kadi, upendeleo au 4nembo yoyote inayoashiria kumuunga mkono mgombea Fulanikatika uchaguzi”Mwisho wa kunukuu.

Kifungu cha 5 cha Sheria ya Adhabu, Sura Na. 16 kinaelezamaana ya njia ya Umma.

Nanukuu:

“Public way includes any highway, market place, square, street,bridge or other way which is lawfully used by the public”

Mwisho wa kunukuu.

Vifungu vya Sheria zote kwa pamoja havisemi wala kutoa fursa aunafasi kwa wananchi kukusanyika bali zinapiga marufuku nakukataza uvaaji wa sare, au nembo au alama za Vyama vya Siasasiku ya kupiga kura kwa umbali kati ya mita 200 na 300.

Hivyo basi ieleweke kwamba umbali huo wa mita 200 mpaka 300sio umbali unaowaruhusu watu kukusanyika kwa kisingizio chakulinda kura.

Aidha, uzoefu unaonesha kwamba, katika kampenizinazoendelea, pale ambapo wafuasi wa vyama tofautiwanapokutana uwezekano wa kutokea vurugu ni mkubwa nasehemu nyingine vurugu zimetokea na kusababisha maafamajeruhi na uharibifu mali.

Source: http://www.nec.go.tz/uploads/documen...20UCHAGUZI.pdf

Dah aisee lakini ww jamaa ni bonge la msomi, kwa hiyo km kituo cha kupigia kura kiko mita 200 kutoka sokoni polisi wakiwakuta watu sokoni iwapige mabomu maana wamekusanyika bila sheria sio!?
 
Kinachonisshanagaza ni ccm na tume wako buzy kuwataka wananchi waende nyumbani ili fisi abaki na bucha alinde nyama! Haijawahi kutokea! Tume ya kwao, wasimamizi wa uchaguzi wa kwao, polisi wa kwao! Mnasikitisha na imekula kwenu
 
Kituo chetu ni ndani ya zahanati, barabara na nyumba za kuishi ziko kama mita 5 hadi 10 kutoka zahanati. Hapa busara itumike au sivyo naona kipigo tu.
 
Ndo akili gani hiyo, nchi hii tuna watu wanaojifanya wamesoma wakati hawana uwezo wa kupambanua mambo. Lengo la sheria yoyote ni public interest au maslahi ya jamii. Maslahi ya jamii kwa uchaguzi huu ni kulinda kura zidi ya wezi au wapiga BAO LA MKONO. Mengine ni wizi.
 
Mleta mada mwaka 2010 tulisubiri kura umbali wa mita 200 ubungo na hakuna vurugu zilizotokea,mwishowe haki ikatendeka!usituletee uzoefu wa nchi nyingine,uzoefu wa Tanzania unaonesha pale wananchi wanaposubiri matokeo wasimamizi wa uchaguzi hulazimika kutoa matokeo sahihi!
 
Kifungu Cha Kwanza Kinakataza Kufanya Mkutano Ndani Ya Mita Miambili, Katika Eneo La Kupigia Kura, Ila Kuanzia Mita Miambili Na Kuendelea Ni Ruhusa, Kifungu Cha Pili Kinazuia Kuvaa Sare Za Chama Ndani Ya Mita Mia Tatu, Hvy Kuanzia Mita Mia Tatu Na Kuendelea Wanaruhusiwa Kuvaa Sare. KUHUSU KIFUNGU CHA KWANZA, KWA KUWA KINAKATAZA KUFANYA MKUTANO NDANI YA MITA MIA MBILI, NA KWA KUWA WATAKAOBAKI WAKISUBIRIA MATOKEO HAWATAKUWA NA MKUTANO,NA KWA KUWA WATAKUWA NJE YA MITA MIA MBILI, NA KWA KUWA HAWATAVAA SARE KWA HOJA HIZO BASI, Ni Halali Kabisa Kusubiria Matokeo Nje Ya Mita Miambili, Na Kwa Wale WATAKAOTAKA KUSUBIRIA MATOKEO WAKIWA WAMEVAA SARE ZA VYAMA VYAO WANAPASWA WAKAE NJE YA MITA MIA TATU KUTOKA ENEO LA KUPIGIA KURA KISHA WAPIGE KAMBI HAPO. Nawatakia Uchaguzi Mwema.

Usichokijua ni kuwa sheria ya Uchaguzi inasema siku ya kupiga kura hakutakuwa na mikusanyiko ya kisiasa.Mikusanyiko yote ya kisiasa mwisho wake ni siku ya mwisho wa kampeni ambayo ni tarehe 24 octoba 2015.Ukikusanya watu wako siku hiyo ya uchaguzi wawe wana UKAWA au CCM wakajikusanya mahali ni kosa kisheria.

Pili kwa mujibu wa sheria zinazohusu mikusanyiko ni lazima kutoa taarifa polisi kuwa kutakuwa na mkusanyiko mahali fulani na kwa lengo gani. Hivyo kama kurtakuwa na watu wenye lengo la kukusanyika popote inabidi wawasilishe maombi yao polisi wakijieleza wao ni akina nani ili wapewe ulinzi wa polisi

Tatu kuna sheria ya ardhi.Unaposema utakusanyika hapo kwenye mita 200 hilo eneo ni mali ya baba yako au mama yako? Huyo mwenye miliki ya hiyo ardhi karidhia? Hivyo kama kuna watu watakaotaka kukusanyika ni lazima wapeleke kibali cha mwenye eneo kuwa karidhia eneo lake litumike kwa mikusanyiko.Na kwamba mikusanyiko hiyo haitakuwa kero wala bugudha kwa wakazi wa eneo husika,majirani n.k Maana kama watu watajiamulia kukusanyika hiyo mita mia 200 bila mwenye eneo lake kuridhia ina maana ni uvamizi wa ardhi ya mtu bila ridhaa yake.Na huo ni uvunjifu wa amani kwenye eneo la watu.Hivyo Mahakama lazima iangalie maslahi ya wenye maeneo maeneo yao yasije vamiwa SIKU YA KUPIGA KURA NA KUKALIWA KWA MABAVU na hao wanaojiita walinda kura.

Polisi kwa kuliona hilo kuwa kutakuwa na uvunjaji sheria kwa watu kuvamia maeneo ya watu na kujikusanya wakasema kila mtu aende kwake asubirie kwake.Sababu vituo vya kupigia kura haviko mbali na makazi ya watu.Kwa nini watu wakae kwenye viwanja vya watu?

Kwangu sikubali mtu akusanyike WALA KUWEKA MAKALIO YAKE KWENYE ENEO LANGU NITAITA DEFENDER NA GARTI LA WASHA WASHA HARAKA WAJE NA MABOMU NA VIRUNGU WAONDOE WAVAMIZI KWENYE ENEO LANGU.

Hawa akina KIBATALA wanataka kuleta vurugu na ugomvi kati ya wenye maeneo na hao watu anaotaka wakusanyike hizo mita mia mbili sababu sio kwao ni kwa watu.

Eti bila haya lowasa na mbowe wanatoa amri mkimaliza kura kaeni mita 200.Hilo eneo wanaloamrisha watu wakae ni la baba yake au mama yake lowasa au mbowe.Sheria ya ardhi iheshimiwe majaji msimamie hilo kwa maslahi ya wenye maeneo yao.Mkiwakubalia mnawaweka wenye maeneo matatizoni.
 
Serikali itangaze hali ya hatari.kituo chetu kipo sokoni na soko letu ni la kila siku sasa tuache biashara zetu kisa uchaguzi?sheria nyingine mgando haziendani na uhalisia wa mazingira.
 
sheria hii hsijasema watu wabaki au wasibaki nje ya mita 200 kamwe. hivo ni hiari ya mtu kubaki ama kutokubaki...tume au serikali hawana mamlaka ya kuwazuia watu kubaki...
Zipo sheria zinazosimamia mikutano na mikusanyiko ya kisiasa.
 
Serikali itangaze hali ya hatari.kituo chetu kipo sokoni na soko letu ni la kila siku sasa tuache biashara zetu kisa uchaguzi?sheria nyingine mgando haziendani na uhalisia wa mazingira.
Wewe jifanye kijogoo
 
Back
Top Bottom