Sheria Ya Ndoa

Bongolander

JF-Expert Member
Jul 10, 2007
5,067
2,196
wanaJF kuna mwenye copy ya Sheria ya ndoa hapa, nataka kuijua ki-undani maana kuna issues zinanitatiza sana, kama kuna yoyote anayo naomba msaada na ufafanuzi wake, najua wanasheria wa maana mko hapa.
 
Thanks mwanakijiji naipitia kidogo, nikiwa na maswali i will get back to you!
 
Namba kuuliza kidogo jamani. hivi sheria zote huwa zinaandikwa kwa kiingereza au zipo nakala zake za kiswahili? Nauliza hivi maana wananchi wengi hatujui sheria, kusoma katiba au hata haki zetu. najua baadhi tunaweza kusoma na kuelewa kiingereza hapo lakini sijui mwanandoa wa kule kwentu Nkasi kama anaweza kuelewa kilichoandikwa.
 
ni kweli ndugu hata mimi sina moja ni bora wajuvi waje hapa watujuze,maana mimi nimeolewa ila sijui haki zangu zaidi ya za ndani tu.
 
PART II
(b) Restrictions on Marriage
13.-(1) No person shall marry who, being male, has not attained Minimum the apparent age of eighteen years or, being female, has not attained age the apparent age of fifteen years.

HEBU SOMENI HUU UCHAFU!!!! HIVI VITOTO VINARUHUSIWAJE KUFUNGISHWA NDOA????
 
Namba kuuliza kidogo jamani. hivi sheria zote huwa zinaandikwa kwa kiingereza au zipo nakala zake za kiswahili? Nauliza hivi maana wananchi wengi hatujui sheria, kusoma katiba au hata haki zetu. najua baadhi tunaweza kusoma na kuelewa kiingereza hapo lakini sijui mwanandoa wa kule kwentu Nkasi kama anaweza kuelewa kilichoandikwa.

sheria zote zinaandikwa kwa Kiingereza kwanza. Wakipata muda wanazitafsiri kwa Kiswahili. Hata Bungeni wanalalamika sana kwani wabunge inabidi wapate mtu wa kuhakikisha wanaipata maana ya Kiingereza sawa sawa. Wameombwa mara nyingi kuwapa Baraza la Kiswahili jukumu la kutafsiri sheria hizo lakini hawana kasi, ari, au nguvu ya kufanya hivyo.
 
Lakini nilivyoisoma sheria hii inarejea neno "Tanganyika" badala ya "Tanzania".halafu cha ajabu ni kwamba wakati inasainiwa hiyo sheria ni mwaka 1971 ambapo "Tanganyika" haikuwepo bali ipo "Tanzania" Kwa nini inakuwa hivyo?. jee hii haileti utata wa kwamba sheria hiyo ni Batili kwa sababu inazungumzia nchi isiyokuwepo?
 
Inaonekana kama Tanganyika ilikuwa na maana ya Mainland Tanzania, na inaonekana kama Zanzibar kuna different set of laws.
 
Mwanakijiji and others
I wonder kama mtu umeishi na mwanaume/mwanamke na mna watoto, lakini hakukuwa na sherehe ya ndoa, wala ndoa haijasajiliwa. Isipokuwa kulikuwa na barua ya posa. Mtu akitaka kujikwamua kwenye hii, kwa wote mwananume na mwanamke, what are the legal implications, kwenye mambo ya custody ya watoto na mambo ya kugawana property kama ipo.
 
swali lako ndilo moja wapo ambayo yanataka kufanyiwa marekebisho katika sheria mpya ya ndoa kwani katika sheria zetu kama zilivyo sasa watoto wa nje ya ndoa hawatambuliki kisheria.
 
Inaonekana kama Tanganyika ilikuwa na maana ya Mainland Tanzania, na inaonekana kama Zanzibar kuna different set of laws.

Je kisheria Tanzania Bara inajulikana kama Tanganyika?.

Kuna sheria tofauti ya ndoa kati ya Tanzania bara na Zanzibar?

Kama muswada wa hiyo sheria ulipitishwa bungeni ambapo pia ndani mwake kuna wabunge kutoka Zanzibar, je si ni wazi kuwa hiyo ni sheria ya Tanzania nzima na si Tanzania bara peke yake?

Kama mtu wa Tanzania Bara akioa Mtu kutoka Zanzibar ndoa ikafungwa Dar-es-salaam lakini wakaenda kuishi Unguja, kukitokea matatizo ya kindoa na wakataka kudivorce je zitatumika sheria gani?(iwapo kama zanzibar wana sheria zao tofauti)
 
wabunge wetu, na waziri wa katiba na sheria ni wavivu wa kupitia hizi sheria ambazo zinamgusa mwananchi moja kwa moja. They just seat on the Paliament House to warm the benches. Inauma sana....
 
Sheria ya ndoa kwa kweli ni ovyo sana, na siku hizi kuna hawa watu wanaojiita wa muamsho, Tamwa etc ndio wanavuruga kabisa mambo. Iliyowekwa na waingereza ilikuwa nzuri sana, lakini naona sasa ni kama imevurugwa, nimejaribu kupitia sijaona kama iko wazi kuhusu mtanzania anayeolewa na mgeni, mgeni anayeoa Mtanzania hayako wazi...labda tusome zaidi ili tuielewe
 
... kuhusu mtanzania anayeolewa na mgeni, mgeni anayeoa Mtanzania hayako wazi...labda tusome zaidi ili tuielewe

Ninavyofahamu (sikumbuki nimesoma wapi) ni kuwa sheria ya Tanzania ina base kiume zaidi, yaani mwanamke akiolewa na mgeni mtoto anayezaliwa anahesabika na wa nchi ya huyo mume. Na pia Mtanzania mwanaume akioa mgeni basi mtoto moja kwa moja anakuwa mtanzania. Mtanzania wa kike akizaa na mgeni (nje ya ndoa) na wakawa nje ya nchi basi yule mtoto bado anakuwa raia wa nchi ya huyo mwanaume.

Nawakumbusha tu mjumbe hauawi, ili msije makanirukia mimi hiyo ndiyo sheria ya Tz na sijayatoa kichwani niloandika.
 
Mwanakijiji and others
I wonder kama mtu umeishi na mwanaume/mwanamke na mna watoto, lakini hakukuwa na sherehe ya ndoa, wala ndoa haijasajiliwa. Isipokuwa kulikuwa na barua ya posa. Mtu akitaka kujikwamua kwenye hii, kwa wote mwananume na mwanamke, what are the legal implications, kwenye mambo ya custody ya watoto na mambo ya kugawana property kama ipo.

kama hawa jamaa wamekaa pamoja kwa kipindi cha miaka miwili au zaidi, hata kama pasingekuwepo na barua ya posa, mahakama itaichukulia kama ndoa halali 'presumption of marriage' Sherehe sio hatua za kuonyesha kuwa kuna ndoa, la hasha. ndoa za kimila bado zinatambulikana na hii sheria, ingawa kuna mwongozo wa kusajiri hizo ndoa za kimila.

hivyo swali lako kimila itakuwa ndoa halali 'presumption of marriage, ila tu tutahitaji kuisajili ili kuondoa utata wa hapo baadaye"
 
PART II
(b) Restrictions on Marriage
13.-(1) No person shall marry who, being male, has not attained Minimum the apparent age of eighteen years or, being female, has not attained age the apparent age of fifteen years.

HEBU SOMENI HUU UCHAFU!!!! HIVI VITOTO VINARUHUSIWAJE KUFUNGISHWA NDOA????

Hee pole yaani ulikuwa haujui kuwa watoto wanaolewa? Ndio sheria best, wanasema sheria ni msumeno, ila wanaharakati wanaipigania sana hili sheria ili ibadilishwe
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom