Sheria ya Ndoa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheria ya Ndoa

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Kimey, Dec 3, 2009.

 1. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #1
  Dec 3, 2009
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Salaam!
  Kuna kipengele katika sheria ya ndoa kinachosema kua pindi ndoa inapovunjika Mtoto atakaa kwa mama yake mpaka afikishe miaka saba then baba anaweza kumchukua!! Sasa kuna rafiki yangu mmoja ana experience hii kitu so kwa maoni yake anasema hii sheria inabidi ibadilishwe kwani unakuta mtu unaingia gharama kubwa kumtunza mtoto akiwa kwa mama yake na pili kuna wazazi wengine ndo wanafanya mtoto ka fimbo ya kukukomoa!! Sasa kwa maoni yake anaona kipengele hiki kibadilishe kiweze kusomeke kua "ikiwa kama baba ana uwezo basi aruhusiwe kumchukua mtoto pindi tu amalizapo kunyonya na sio baada ya miaka saba!! Wandugu hapo mnasemaje? naomba maoni!
   
 2. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #2
  Dec 3, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Wafanye some editing kwa zamani miaka saba ata darasa la kwanza bado kwa sasa wangefanya miaka 5 inatosha
   
 3. Suzzie

  Suzzie Member

  #3
  Dec 3, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 98
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  wewe walalamika miaka saba? siku hizi kumi na nne (14)
   
 4. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #4
  Dec 3, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Sheria haisemi hivyo, sheria iko wazi kwamba mtoto anaweza kutunzwa na baba au mama wakati wowote :

  The court may, at any time, by order, place an infant in the custody of his or her father or his or her mother or, where there are exceptional circumstances making it undesirable that the infant be entrusted to either parent, of any other relative of the infant or of any association the objects of which include child welfare.

  Hiyo unayosema wewe ni dhana inayopingika "rebuttable pressumption" kwa hiyo huyo rafikiyo alichotakiwa kufanya ni kupinga dhana hiyo kwamba ni vizuri mtoto akakaa na baba yake badala ya mama pamoja na kuwa mtoto ni chini ya miaka saba.

  There shall be a rebuttable presumption that it is for the good of an infant below the age of seven years to be with his or her mother but in deciding whether that presumption applies to the facts of any particular case, the court shall have regard to the undesirability of disturbing the life of the infant by changes of custody.

  Hata hivyo zingatia kuwa kwenye kufikia uamuzi wa aina yoyote mahakama inaangalia vigezo vingi ikiwemo vifuatavyo:

  In deciding in whose custody an infant should be placed the paramount consideration shall be the welfare of the infant and, subject to this, the court shall have regard to–
  (a) the wishes of the parents of the infant;
  (b) the wishes of the infant, where he or she is of an age to express an independent opinion; and
  (c) the customs of the community to which the parties belong.

   
 5. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #5
  Dec 3, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Lakini kwanza tujiulize mswali yafuatayo:
  1. Mtoto ni wa nani? Mama? Baba? Wote?
  2. Kama ni wa wote, ni vipi mmoja wao awe na haki zaid ya kukaa na mtoto kuliko mwingine?

  Suala la mtoto mdogo kukaa na mama sio automatic!Inategemea na mazingira ya huyo mama. Mahakama/sheria inamtizama zaidi mtoto kuliko wazazi. Je mtoto atafaidika (kiafya, malezi nk)zaidi wapi? kwa baba au kwa mama? Kama wote hawafai, wote wanapoteza haki ya kukaa na mtoto!
   
 6. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #6
  Dec 3, 2009
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mkuu thanx ngoja nitamwambia kuhusu hichi kifungu maana si unajua tena si sheria tunazisikia tu juu juu.....
   
 7. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #7
  Dec 3, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Mie naona angekaa tu na mama yake mpaka afikie umri wa kujitambua mwenyewe sasa na kuamua akae na nani
   
 8. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #8
  Dec 3, 2009
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mama anafanya mtoto mtaji na kumkomoa jamaa!!
   
 9. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #9
  Dec 3, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Kumbuka kuwa hii ni sheria ya kizamani kidogo ambayo ilifikiria kuwa mama atakuwa nyumbani kila siku kwa sasa mama ni mbagaizaji kama baba na matunzo ya watoto muda mwingi ni day care centre, nursery school, bording school to university. Kama mtoto anaweza kwenda day care kwa nini asikae na baba hata kama ana miaka 3 au minne??????
   
 10. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #10
  Dec 3, 2009
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145

  Kinachoangaliwa zaidi katika sheria za familia (family laws) hususani pale ndoa inapovunjika au mume na mke kutengana, ni haki za wahusika katika familia hiyo (yaani baba, mama na mtoto). Kama familia ilikuwa na mali iliyochumwa pamoja akiwemo mtoto, sheria inatembeza mgawo kati ya wahusika, miongoni mwa mali za wazazi ni mtoto/ watoto wakati mali ya mtoto ni "matunzo bora".


  Kanuni ya jumla ni kwamba baba ndie mwenye mtoto. Mtoto anakuwa kwa mama pale tu mazingira ya ustawi wake (walfare of the child) yatapothibitishwa kuwa yatalindwa na kumwezesha mtoto huyo kukua vyema.

  Sheria ya ndoa inahusu zaidi wana ndoa na watoto waliopatikana ndani ya ndoa. Kwa wale ambao hawapo kwenye ndoa, bado sheria inatambua kuwa mtoto ni mali ya Baba. Kwa mfano sheria ya "Affiliation" inampa haki mama wa mtoto anayetarajiwa kuzaliwa au aliekwishazaliwa kuwasilisha ombi maalumu katika mahakama (Mahakama ya Wilaya) kutaka utambuzi wa baba wa mtoto husika na kumtaka baba huyo (putative father) kutoa matunzo kwa mtoto aliyezaliwa ambaye kwa mujibu wa sheria hii anatambulika kama mtoto haramu (illegitimate child). Matunzo kwa mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa (out of wedlock) yanaweza kukoma ikwa baba wa mtoto ataiomba mahakama ifanye hivyo kwa kuthibitisha kuwa mtoto ametimiza miaka 14 au mama husika wa mtoto ameolewa au kuingia kwenye mahusiano ya "ki unyumba (cohabitation)" na mwanaume ambaye alikuwa ameacha.

  Pia mahakama ikijiridhisha kwa sababu nyingine. Amri ya mahakama ya kumtaka baba wa mtoto atoe matunzo kwa sheria ya "Affiliation" inapoteza nguvu mara baada ya mtoto kutimiza miaka 16. (kuna dhana kuwa atakuwa ameanza kujitegemea).

  Ni sawia kuwa mtoto akiwa na umri usiozidi miaka saba (7) akakaa kwa mama lakini uzoefu umeonyesha kuwa akina mama wengi wamekuwa wakitumia fursa hiyo kuchuma kupitia mgongo wa mtoto. Utakuta mama ameolewa na mume mwingine au yupo nje ya eneo ambalo mtoto yupo anapiga "uchangu" na ana mbwaga mtoto kwa bibi au ndugu, lakini bado anataka apewe matunzo ya mtoto huyo ambayo hayamfikii mtoto.

  Katika mazingira kama haya, baba wa mtoto anayo haki ya kuomba mahakama apewe hifadhi ya mtoto na matunzo kukatishwa kwani kanuni ya jumla ya mtoto kuwa kwa mama itakuwa imekiukwa!.
   
 11. Nyuki

  Nyuki JF-Expert Member

  #11
  Dec 3, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  kama mama hajiwezi kimaisha ina maana mtoto akateseke wakati baba anauwezo?
   
 12. kitalolo

  kitalolo JF-Expert Member

  #12
  Dec 3, 2009
  Joined: Dec 4, 2006
  Messages: 1,846
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  thats why i like jf
   
 13. kitalolo

  kitalolo JF-Expert Member

  #13
  Dec 3, 2009
  Joined: Dec 4, 2006
  Messages: 1,846
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  mara nyingi tumekuwa na migogoro ya hapa na pale ndani ya nyumba na nimekuwa nikifikiri kuwa endapo itatokea ikafikia tunaachana nini hatima ya mtoto nimekuwa nikitafuta suluhu kwasababu ya mtoto wetu, mwanzoni mamaa alikuwa ananiambia anaondoka na alikuwa nataka kuondoka na mtoto na kwasababu nampenda sana mtoto wangu na sitaki ateseke nimekuwa nikimzuia mamaa asiondoke ila mara ya mwisho amabpo tukuwa na utata mama alikuwa tayari kuondoka na kuniachia mtoto kutokana na kwamba nilimtishia usalama wa mtoto iwapo ataondoka naye ingawa tulifika muafana na bado tuko pamoja ila nimeamua kwasasa akilianzisha n itamruhusu aondoke na aniachie mtoto kwasababu nina hakika hana uwezo wa kumtunza
   
 14. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #14
  Dec 3, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Asante sana mkuu kwa ufafanuzi wa kisheria. Ila pia nitapenda utuuleze kuwa kwa mfano baba aliwatelekeza au kutelekeza mtoto na mama kwa kuda mrefu bila sababu ya msingi. Na hasa pale ambako hakuzuiwa kuwaona au kumwoana mtoto na mzazi mweziwe. Na kuwa mama huyo anatunza mtoto/watoto peke yake in everything. Je naomba usaidie yafuatayo:

  1. Baba huyo anaweza kuomba custody ya mtoto hata kama ni over 7 or 14 years na akakubaliwa wakati hana upendo na interest na mtoto/watoto?

  2. Kwa kisheria mtoto/watoto hao watakuwa chini ya nani?


  3. Je haiwezekani akina baba wa aina hiyo wakanyang'anywa ile haki ya kuwa bilogical father? Naamini baba unaheshimika kwa kumtunza mtoto na si kumzaa na kumtelekeza kwa makusudi

  4. Je na talaka inaweza kutolewa kwa baba ambaye kaitelekeza familia kwa kuwa amepata kimada na kwa kuwa anataka aoe kimada kile basi anawahi mahakamani kupata talaka. Je mke huyo hawezi kuweka pingamizi kwa kuwa mume huyo not innocent as he descerted the family?

  Mkuu leta utaalam hapa ili tuisaidie jamii. Kuna ndoa na akina mama wanapata shida na hawajui sheria itawasaidiaje.
   
 15. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #15
  Dec 4, 2009
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Mkuu pata ufafanuzi huu wa kina na bure kabisa. Kama kuna zaidi usisite kurudi JF kuuliza hii ndo huduma kwa mteja, ukiridhika kumbuka kuchangia JF ili iendelee kuwepo na kuwahudumia wadau wake:

  <U>
  </U>
   
 16. H

  Hashim Mohamed Member

  #16
  Dec 8, 2009
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 29
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Haiwezekani kukukomoa kwani hata mahakama au ustawi wa jamii wenyewe wanazingatia kipato chako kabla ya kukupangia kiasi cha kutoa matunzo. Na isitoshe kama mama anao uwezo hapaswi kupewa chochote. Na zaidi ya hayo mtoto anapokuwa ameacha kunyonya mama akikataa kukaa nae na ikiwa ana uwezo wa kifedha anpaswa kutoa pesa za matunzo kwa baba....
   
 17. Lemunyake

  Lemunyake Senior Member

  #17
  Dec 11, 2009
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  I love this . Hivi kuna website ambapo tunaweza kupata more information? It makes for some very good reading.
   
Loading...