Daata
JF-Expert Member
- Dec 24, 2012
- 4,639
- 1,794
Mkuu Daata, kulingana na Sheria tajwa,ndoa ni muungano wa mwanaume na mwanamke wenye lengo la kuwafanya waishi pamoja katika maisha yao yote na katika kujitenga na wengine wote waliobaki. Ndoa ina taratibu zake Mkuu.Hakuna aina au namna yoyote ya ndoa inayotokana na kuishi na mwanamke au mwanaume kwa muda fulani. Dhanio la ndoa lililopo chini ya kifungu cha 160 cha Sheria ya Ndoa huwahusu wau waliohitilafiana na ambao waliishi kwa miaka miwili au zaidi.
Asante Petro E. Mselewa kwa ufafanuzi. Msingi wa swali langu ni kwamba mara nyungi nimewahi kusikia kuwa ukikaa/ishi na mwanamke kwa miezi sita mfululizo huhesabiwa kama ndoa na huyo mwanamke ana haki ya umiliki wa mali zote mlizochuma pamoja
Je kuna ukweli wowote katika madai haya kulingana na sheria hiyo?
Last edited by a moderator: