Sheria ya Ndoa: Maswali na majibu mbalimbali

Mkuu kwani lazima uwe na hatu ya usuruhisho ndo ukubariwe kufungua shauri mahakamani? Ikiwa mwenza wako hakutaka usuruhisho katoroka na hataki kusuruhishwa inakuwaje ? Mahakama inaweza kupokea ombi la taraka?

Ikitokea hali hiyo hapo ndiyo huwa na urahisi wa mahakama kutoa talaka!
Ikithibitika amekutelekeza yani shukuru Mungu maana hapo kupata talaka ni rahisi sana kuliko vinginevyo!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mathayo 19:9 Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini.

Wewe umeelewaje hayo maandiko? Wengi wameyakariri tu!
Hapo Maana yake pale itakapothibitika pasipo shaka kuwa mwanandoa mmoja au wote kuwa wamefanya uasherati maana yake kuachana ni ruksa na kwenda kuolewa na mtu mwingine


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza,talaka ni mwisho wa ndoa.Pili,talaka hutolewa na Mahakama tu na si vinginevyo.Tatu, talaka ina taratibu zake.Kwa mfano,ni lazima kwa mwombaji wa talaka apitie katika Baraza la Usuluhishi la Ndoa kabla ya kwenda Mahakamani kudai talaka. Pia,Baraza husika lazima litoe kibali cha kushindwa kuwasuluhisha wanandoa hao ambao mmoja wao anataka kutalikiwa. Nne, talaka hutolewa tu pale ambapo ndoa hiyo itaonekana kuwa haiwezi tena kubaki a kurekebishika.

Kimsingi,Mahakama hulenga hasa katika kuilinda ndoa.Ndiyo maana,mwombaji wa talaka lazima athibitishe uwepo wa sababu za talaka kwa mfano mateso,kutelekezwa na uasherati wa mwenza wake.Ieleweke kuwa talaka zitolewazo kiislam ni hatua tu.Hii ni kwakuwa ni Sheria ya Ndoa tu ndiyo inayotumika katika suala hilo.
Asante kwa ufafanuzi wako . Hebu nisaidie hili kwa zaidi ya Mara 3 make wangu ameondoka nyumbani pasipo kuaga na amekaa huko kwa zaidi ya Sikh 10 bila hata mawasiliano .Aliporudi akajitenga na chumba hata alipokuwa akilala sipajui kwa zaidi ya week 2 . Kimaadili ya ndoa na uhusiano mm nimechukuliabkuwa this is maximum provocation that means uhusiano hapa hautengamani maana ndani yake kumejaa.dharau. To that extent nilitoa talaka
Je hii talaka kwa ndoa iliyokuwa ya bomani na baadaye kuwa ya Ki Islam unataka kunieleza kuwa si halali . Nini nifanye maana hii ndoa hata mimi SIHITAJI

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari za majukumu!

Kuna shauri lilipelekwa Kanisani (Anglican) kwa ajili ya usuluhishi ikashindikana na kwa kuwa matatizo yao yalishapita kwenye vyombo vingi vya usuluhishi kama vile Mwenyekiti wa Mtaa, Kanisani na Polisi baada ya mwanamke kujeruhiwa kwa vipigo vingi tofafuti na RB zipo zaidi ya tatu kama ushahidi. Mlalamikaji mwanamke akaomba apewe barua kwenda mahakamani kwa hatua zaidi ili aweze kupata talaka.

Mahakama ikampa fomu Na 3 tatu ili kanisa iweze kuijaza ili utaratibu wa kimahakama uweze kuendelea tangu mwezi Novemba, 2018. Mpaka muda huu ninapoandika Kanisani wanadai kuwa hawajakaa kikao chochote bado wako kwenye hatua za awali kulishughulikia jambo hili.

Kisheria hii imekaa je? Nitashukuru kwa ushauri wako ili kujua ni hatua gani za kuchukua.
 
Naomba kuuliza.
Mimi ni Mtanzania lakini nilibahatika kupata marafiki na sasa nchini mwao kuna machafuko ya kivita. Wameniuliza kama inawezekana kwao kuja kufunga NDOA hapa Tanzania, hivyo ningependa kujua kama sheria zinaruhusu na utaratibu upi ufuatwe ili waweze kuja.
Ahsante.
 
Naomba kuuliza.
Mimi ni Mtanzania lakini nilibahatika kupata marafiki na sasa nchini mwao kuna machafuko ya kivita. Wameniuliza kama inawezekana kwao kuja kufunga NDOA hapa Tanzania, hivyo ningependa kujua kama sheria zinaruhusu na utaratibu upi ufuatwe ili waweze kuja.
Ahsante.
 
Wana-JF,


Karibuni hapa kwa maswali mbalimbali yahusuyo Sheria ya Ndoa,1971.Wale wote waliopo kwenye ndoa na wanaotarajia kuwa kwenye ndoa wanakaribishwa hapa kuuliza na kujibiwa. Nitashirikiana na Mawakili Wasomi wenzangu waliopo humu kuwajibu maswali yenu.

Asanteni na karibuni!
Nisadie ksi hii tafadhali nakuomba. nitupie inbox, najua unayo maana lazima uwe na TLR kama hii
SARJIT SINGH v SEBASTIAN CHRISTOM 1988 TLR 24 (HC) Court High Court of Tanzania - Dar Es Salaam
Judge Kyando J
 
SWALI LIPO MWISHONI BAADA YA STORI HII :

-Mwanaume alishahama ndani ya nyumba na kwenda kupanga nje ni zaid ya miez 6 sasa

-Mwanamke amebaki ndani ya nyumba hajahama

-Mwanaume anadai kamfumania mkewe (ugoni wa kutunga) eneo la biashara analofanyia mkewe biashara zake mchana kweupe barabarani kulikua na wateja zaidi ya sita na wengineo ivo wapo katika kesi ya talaka na mgao wa mali kwasasa


-Mwanaume anamtumia mkewe watu kumtishia kumtoa mwanamke ndani ya nyumba kua hakuweka tofali hata moja ivo siku talaka ikitoka atamtoa na defender ndani ili aje akae yeye kiuhuru

-Mwanamke alipoolewa alikuta nyumba ambayo haijaisha yan ilikua na chumba kimoja tu ivo wakaimalizia wote vyumba vingine wakaishi miaka 11 na kuzalia watto wao wote pale

-Wakajenga nyumba nyingine na kuhamia kwenye nyumba yao ya pili napo wakaishi miaka 20 ndipo ugomvi ulipoibuka

-wameishi ndani ya ndoa miaka 31 na watto wao wote ni above 18

-mwanaume kafoji mkataba ukielezea kua alishamkabidhi mwanamke mgao wa mali miaka mingi kisa ana watto wa nje wasije kumsumbua ivo kamtoa katika mgao wa mali na hana cha kumdai huyo mwanamke... Mkataba ni handwritten mwanzo mwisho ukiwa na mwandiko wa mwanaume tu akithibitisha kutoa pesa mil. 60 na kumpatia mkewe.. Lakini hakuna sehemu ambayo mwanamke kathibitisha kupokea izo pesa lakn kuna sahihi na kidole gumba tu anachodai ni cha mkewe na mkataba huo umethibitishwa na wakili mhuri upo (miaka minne imepita tangia wafanye huo mkataba) ndo yakaja kuibuka haya... It means mwanaume anataka kufanya dhuluma kwa mwanamke ya mali kupitia njia hyo



QUESTION
1. KATI YA MWANAUME NA MWANAMKE NI NANI ANAESTAHILI KUTOLEWA NDANI YA NYUMBA BAADA YA TALAKA KUTOLEWA ?? NA KWA KUTUMIA KIFUNGU KIPI CHA SHERIA?

2. MGAO WA MALI KWA WANANDOA UNAWEZA KUFANYIKA KABLA YA NDOA KUVUNJIKA ILI PASIWEPO NA MGAO BAADA YA NDOA KUVUNJIKA MIAKA YA MBELENI INCASE KWA MWANANDOA MMOJA ASIDAI KITU CHOCHOTE MBELENI ??

3.WAKILI ANA MAMLAKA YA KUFANYA MGAO WA MALI KWA WANANDOA?? sheria na kifungu kipi kama kipo...
Hiyo nyumba wawape watoto wairithi mme na mke waondoke

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante sana kwa darasa nzuri sana. Nimejifunza mengi sana kwenye darasa hili.
 
Je kama mm mwanaume ni mfanyakazi halafu nikawa naishi na mwanamke bila kufunga ndoa kwa miaka miwili .Halafu nikachukua mkopo benki nikanunua kiwanja .je siku tukiachana hicho kiwanja tutakigawana ? Wakati mimi bado deni benki wanalikata kwenye mshahara.hapo inakuweje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini,kama ni mali ya pamoja watoto wa nje ya ndoa (kwa ndoa za bomani na za kikristo) hurithi kutokana na matakwa ya wanandoa tu na si vinginevyo.
Mheshimiwa ina maana mke wa ndoa ana HAKI ya kukataa watoto wa nje ya ndoa wa mme wake wasirithi mali?
 
Kama ni mali zako binafsi,haziwezi kuwa machumo ya ndoa. Hivyobasi,hazitagawanywa. Lakini,hakikisha zinakuwa kweli mali zako binafsi kwa kutunza nyaraka za uthibitisho wa hilo.
Mkuu naomba Ufafanuzi hapa, labda ni kwa kutojua sheria hasa kwa mke anaposhirikiana na mme wake katika matumizi nyumbani kiasi kwamba kipato chake chote kinatumika kwa mfano chakula, matibabu, mavazi nk halafu mume yeye ananunua viwanja na kujenga ama anaanzisha kampuni au kitega uchumi chochote kisha hivyo vyote anaandikisha kwa jina lake. Je hapa mke anakuwa na haki ya umiliki? Wakiachana mke watagawana mali au mke ataondoka mikono mitupu? Urithi je, ana haki ya urithi!/ umiliki wa mali hizi?
Asante.
 
Muheshimiwa Petro E. Mselewa kama mme wa ndoa amezaa nje ya ndoa halafu mme anataka kumchukua huyo mtoto kuishi naye, je mke wa ndoa ana haki ya kukataa kumpokea/ kulea mtoto huyo?
 
Presumption of marriage sec 160 of law of marriage act sheria imesema ni miaka 2 inakuwa ndoa na jamii inayo wazunguka itambue kuwa mnaishi km mke& Mme na hio ndoa haina taraka Ila INA mgao WA Mali na maintenance of children and custody km ikivunjika (broken down irreparably) obiter dictum#
...kwa hiyo hapa Mkuu Kasabuku ina maana kuwa mnaweza kuishi hata miaka 15 pamoja kwa hiyo mantiki ya kwamba baada ya miaka mi2 tu mmefahamika kama wanandoa...lakini baada ya hiyo miaka 15 mmoja wa wanandoa hao akaamua tu ku move on, habanwi na chochote wala yule aliyebaki hana Say yoyote katika hili??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
...kwa hiyo hapa Mkuu Kasabuku ina maana kuwa mnaweza kuishi hata miaka 15 pamoja kwa hiyo mantiki ya kwamba baada ya miaka mi2 tu mmefahamika kama wanandoa...lakini baada ya hiyo miaka 15 mmoja wa wanandoa hao akaamua tu ku move on, habanwi na chochote wala yule aliyebaki hana Say yoyote katika hili??

Sent using Jamii Forums mobile app
Salamu Mkuu Kasabuku.
Kama bado upo humu nitakushukuru sana ukinitolea ufafanuzi wa hili...
 
Back
Top Bottom