PetterIsuti
Senior Member
- Nov 29, 2014
- 118
- 28
Ngoja watalaamu waje tupate elimuNaomba kuuliza.
Nimeishi na mwanamke toka 2000 na tukafunga ndoa mwaka 2007 tumezaa na tuna watoto wawili.
Ila kutokana na tabia zake tulitengana 2015 ili kupeana muda wa kutafakari kwa sababu tulikuwa tumefikia hatua mbaya ila kumbe kulikuwa na mtu aliyekuwa ameingilia ndoa yangu ndo maana tukafikia hali ile.
Tulipotengana kwa muda wakaenda kufunga ndoa ya kwa mkuu wa wilaya na ukumbuke ya kwangu ilikuwa ya kanisani.
Naomba ushauri.
1.Ndoa aliyonayo ni halali?
2.Kisheria nawezaje kupata talaka?
3.je kama kugawana mali tunagawana ipi?ile tuliyokuwa nayo 2015 au tutakayokuwa nayo muda mahakama itakapotoa talaka?
4.Huyo jamaa aliyeingilia ndoa yangu anaweza kuchukuliwa sheria gani?
5.Au naweza kuacha hivyohivyo na mimi nikaenda kufunga ndoa nyingine?
Asante