Sheria ya Ndoa: Maswali na majibu mbalimbali

Sema kwa upande wa ndoa ya Kiislam, Sheria itakayotumika mahakamani ni Sheria ya Kiislam. Kwao hakuna kupitia mabaraza ya usuluhishi.
Mkuu, jisomee tena Sheria ya Ndoa na taratibu zake. Waislamu wanayo Mabaraza ya usuluhishi. Na ni lazima kuanzia huko kabla ya kwenda Mahakamani.
 
Je kama mtu na mke wake wamekubaliana kutalakiana kutokana na sababu ambazo wao wenyewe Sana ndoa wameona hazitaleata tena amani ndani ya nyumba kunahaja ya kupitia balaza LA usuluhishi au hata wakienda mahakamani moja kwa moja kwa ajili ya kuvunja ndoa watapokelewa
 
Je, kwa kesi ya kukutwa na jumbe mbali mbali kwenye cim inaweza kumfanya mtuhumiwa kupelekea kushikiria mali zake wakati kesi haijatolewa hukumu???
 
hivi mme akiwa na watoto wa nje,halafu mimi na yeye tumeoana tukiwa hatuna kitu,then tukafight tukawa matajiri,siku akifa je wanae wa nje wana haki ya kurithi na wanangu wa ndani ya ndoa?
Watoto wa nje hawana haki ya kurithi labda awagawie kabla hajafa ama awagawie kwenye wosia kama anavyoweza kumgawia mtu yeyote.
 
Nina swali, Mwanandoa mmoja akipeleka shauri mahakamani la kutaka talaka na court wakamwita mwenzake na asihudhurie mahakamani zaidi ya mara tatu, Mahakama uchukua hatua gani?
 
Wana-JF,

Karibuni hapa kwa maswali mbalimbali yahusuyo Sheria ya Ndoa,1971.Wale wote waliopo kwenye ndoa na wanaotarajia kuwa kwenye ndoa wanakaribishwa hapa kuuliza na kujibiwa. Nitashirikiana na Mawakili Wasomi wenzangu waliopo humu kuwajibu maswali yenu.

Asanteni na karibuni!

Asante sana,
Mimi swali langu ni hili.

Nimeenda kijijini kutafuta mke wa kuoa, nimemkuta mwanamke akiwa anaishi kwao bila mme, niliulizia nikaambiwa wameachana na mme wake miaka mitano iliyopita.
Nilichumbia kwao nikaoa kwa kutoa mahali.
Je! Mume wake wa awali anaweza kuja kushika ugoni kwa kuwa hakutoa talaka?
 
Ndiyo Mkuu. Ndoa huvunjwa mahakamani kwa utaratibu wa kisheria. Mshauri aanze kufungua shauri la kuvunja ndoa kwanza.
 
Nina swali, Mwanandoa mmoja akipeleka shauri mahakamani la kutaka talaka na court wakamwita mwenzake na asihudhurie mahakamani zaidi ya mara tatu, Mahakama uchukua hatua gani?
Kama ametimiza sharti la kuanzia Baraza la Usuluhishi,atasikilizwa upande wake na uamuzi kutolewa.
 
Je usipohudhuria mara ya kwanza wakati wa kusomewa shitaka kitatokea Nini

UOTE="Petro E. Mselewa, post: 28036059, member: 116264"]Kama ametimiza sharti la kuanzia Baraza la Usuluhishi,atasikilizwa upande wake na uamuzi kutolewa.[/QUOTE]
 
Wakuu. Mke wangu anaomba talaka sababu eti mm ni mzinzi. Aliniacha akaenda kuishi kivyake n.a. tayari amezaa. Je katika mazingira kama hayo kesi ya mzingi ikiisha , je naweza fungua kesi ya kuomba fidia kutokana na yeye kuzaa kabla talaka kutolewa?
 
Mme wangu ananifukiza kwa sababu zisizo na msingi Mara kwa Mara, ila Mara hii nimeamua kuondoka mana ameanza kunipiga,.kuna Mali tumechuma wote,naanzia wapi ili nipate haki zangu?
 
Wanawake muda wote wanawazia mali tu.

Yaani nyie kwenye kuachana mnawaza 50/50 tu

Eti tumechuma wote
 
Mme wangu ananifukiza kwa sababu zisizo na msingi Mara kwa Mara, ila Mara hii nimeamua kuondoka mana ameanza kunipiga,.kuna Mali tumechuma wote,naanzia wapi ili nipate haki zangu?
Nenda Baraza la usuruhishi la kata au ustawi wa jamii Wilaya.Usuruhishi ukishindikana mtapewa barua mwende juu,baada ya hapo unaenda mahakamani kuomba divorce decree.Mahakama ikikubali kutoa taraka ,itaamua namna ya kulea watoto,kuwatunza na vipi mgawane Mali.Mgawanyo si lazima nusu kwa nusu mahakama itaamua kulingana na mlivyochangia kuitafuta hyo Mali.
 
Tena watataka na uthibitisho
Kuishi na mtu tu huku wewe hufanyi matumizi yoyote zaid unakula tu hapo hutapata kitu

Wanawake wengi wakishaona mali wanawaza ufe ili wazichukue au wakiona una ndugu waongeaji watataka talaka mapema ili wapate chakupata
 
Naomba kuuliza.
Nimeishi na mwanamke toka 2000 na tukafunga ndoa mwaka 2007 tumezaa na tuna watoto wawili.
Ila kutokana na tabia zake tulitengana 2015 ili kupeana muda wa kutafakari kwa sababu tulikuwa tumefikia hatua mbaya ila kumbe kulikuwa na mtu aliyekuwa ameingilia ndoa yangu ndo maana tukafikia hali ile.
Tulipotengana kwa muda wakaenda kufunga ndoa ya kwa mkuu wa wilaya na ukumbuke ya kwangu ilikuwa ya kanisani.
Naomba ushauri.
1.Ndoa aliyonayo ni halali?
2.Kisheria nawezaje kupata talaka?
3.je kama kugawana mali tunagawana ipi?ile tuliyokuwa nayo 2015 au tutakayokuwa nayo muda mahakama itakapotoa talaka?
4.Huyo jamaa aliyeingilia ndoa yangu anaweza kuchukuliwa sheria gani?
5.Au naweza kuacha hivyohivyo na mimi nikaenda kufunga ndoa nyingine?
Asante
 
Ngoja waje wataalamu
 
Back
Top Bottom