Sheria ya Ndoa: Uliza Ujibiwe

Kitabu

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2011
Messages
290
Points
195

Kitabu

JF-Expert Member
Joined Jan 7, 2011
290 195
Habari Mkuu,nina shemeji yangu ambaye alifiwa na mumewe ambaye walifunga nee ndoa ya kiislam, sasa tokea afe ndugu wa mume wamekuwa wakimsumbua sana mke wa marehemu kuhusiana na mali,huku wakishindwa kutoa msaada wowote kwa watoto, nikamshauri aende mahakamani,mahakama ikaamuru kikao cha ndugu kichague msimsmizi wa mirathi,akachaguliwa kaka wa marehemu ambae ndie msumbufu sana, baada ya hapo mahakama ikamthibitisha yule msimamizi wa mirathi na kuuliza kuwa ugawaji wa mali utafuata sheria gani,msimamizi akasema watafuata sheria za kiislam, mahakama ikakubaliana na hilo na kufunga shauri. Sasa shida ni kuwa hiyo sheria ya kiislam itamfanya mke wa marehemu apate SUMNI(yaani kidogo tu) na wa watoto wanampango wakae nao hao ndugu wa marehemu ambao hawawezi kuwatunza kabisa, Mke wa marehemu amechanganyikiwa hajui cha kufanya, Swali langu ni je huyu mke wa marehemu afanyeje ili abaki na watoto wake na pia abaki na mali alizochuma na mumewe?????
naomba majibu tafadhali
 

Forum statistics

Threads 1,344,042
Members 515,307
Posts 32,805,740
Top