Sheria ya Ndoa: Uliza Ujibiwe

Petro E. Mselewa

Petro E. Mselewa

Verified Member
Joined
Dec 27, 2012
Messages
8,709
Points
2,000
Petro E. Mselewa

Petro E. Mselewa

Verified Member
Joined Dec 27, 2012
8,709 2,000
Wana-JF,

Karibuni hapa kwa maswali mbalimbali yahusuyo Sheria ya Ndoa,1971.Wale wote waliopo kwenye ndoa na wanaotarajia kuwa kwenye ndoa wanakaribishwa hapa kuuliza na kujibiwa. Nitashirikiana na Mawakili Wasomi wenzangu waliopo humu kuwajibu maswali yenu.

Asanteni na karibuni!
 
Blaque

Blaque

Senior Member
Joined
Feb 11, 2011
Messages
113
Points
225
Blaque

Blaque

Senior Member
Joined Feb 11, 2011
113 225
Cheti cha ndoa kina gharama? Na kama kinagharama ni kiasi gani? Je,wanandoa wa dini zote wanacheti cha aina moja?

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Petro E. Mselewa

Petro E. Mselewa

Verified Member
Joined
Dec 27, 2012
Messages
8,709
Points
2,000
Petro E. Mselewa

Petro E. Mselewa

Verified Member
Joined Dec 27, 2012
8,709 2,000
Cheti cha ndoa kina gharama? Na kama kinagharama ni kiasi gani? Je,wanandoa wa dini zote wanacheti cha aina moja?

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Mkuu Blaque, cheti cha ndoa hakina gharama zilizoainishwa kisheria.Lakini, gharama hubebwa na taratibu zilizopo kwa Msajili wa Ndoa anyehusika.Kwa mfano,ndoa za kikristu huambatana na gharama mbalimbali kama kulipa zaka na kadhalika.Cheti kama cheti pia huweza kulipiwa moja kwa moja au kwa mchango unaojitegemea
 
Last edited by a moderator:
Daata

Daata

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2012
Messages
4,480
Points
2,000
Daata

Daata

JF-Expert Member
Joined Dec 24, 2012
4,480 2,000
Kulingana na sheria hiyo tafsiri ya ndoa ni nini
Je waweza kukaa/ishi na mwanamke/mwanaume kwa muda gani itatafsirika kuwa ndoa?
 
Blaque

Blaque

Senior Member
Joined
Feb 11, 2011
Messages
113
Points
225
Blaque

Blaque

Senior Member
Joined Feb 11, 2011
113 225
Ok,nimekusoma.Je,kama nimeoa na mimi nikawa source ya matatizo ndani ya ndoa lakini bado nampenda mwenzangu na mwenzangu(mke) akaitaji tuachane,Je anauwezo wakutoa/kuomba taraka kisheria?!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Petro E. Mselewa

Petro E. Mselewa

Verified Member
Joined
Dec 27, 2012
Messages
8,709
Points
2,000
Petro E. Mselewa

Petro E. Mselewa

Verified Member
Joined Dec 27, 2012
8,709 2,000
Ok,nimekusoma.Je,kama nimeoa na mimi nikawa source ya matatizo ndani ya ndoa lakini bado nampenda mwenzangu na mwenzangu(mke) akaitaji tuachane,Je anauwezo wakutoa/kuomba taraka kisheria?!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
Mkuu,mwanandoa yeyote aweza kuomba kutalikiwa Mahakamani kama atakuwa na sababu na atakuwa amefuata taratibu za Talaka. Sababu zinazoainishwa na Sheria ni uzinzi,mateso na kutelekezwa. Hapo nimeacha kando sababu za kuvunjika mara moja kwa ndoa kama ya mmoja wa wanandoa kuwa mwendawazimu na kadhalika. Taratibu zinaelekeza wanandoa kuanzia kwenye Mabaraza ya Usuluhishi ya Ndoa ambayo yameanzishwa kisheria kabla ya kwenda Mahakamani.
 
Petro E. Mselewa

Petro E. Mselewa

Verified Member
Joined
Dec 27, 2012
Messages
8,709
Points
2,000
Petro E. Mselewa

Petro E. Mselewa

Verified Member
Joined Dec 27, 2012
8,709 2,000
Kulingana na sheria hiyo tafsiri ya ndoa ni nini
Je waweza kukaa/ishi na mwanamke/mwanaume kwa muda gani itatafsirika kuwa ndoa?
Mkuu Daata, kulingana na Sheria tajwa,ndoa ni muungano wa mwanaume na mwanamke wenye lengo la kuwafanya waishi pamoja katika maisha yao yote na katika kujitenga na wengine wote waliobaki. Ndoa ina taratibu zake Mkuu.Hakuna aina au namna yoyote ya ndoa inayotokana na kuishi na mwanamke au mwanaume kwa muda fulani. Dhanio la ndoa lililopo chini ya kifungu cha 160 cha Sheria ya Ndoa huwahusu wau waliohitilafiana na ambao waliishi kwa miaka miwili au zaidi.
 
Last edited by a moderator:
Daata

Daata

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2012
Messages
4,480
Points
2,000
Daata

Daata

JF-Expert Member
Joined Dec 24, 2012
4,480 2,000
Mkuu Daata, kulingana na Sheria tajwa,ndoa ni muungano wa mwanaume na mwanamke wenye lengo la kuwafanya waishi pamoja katika maisha yao yote na katika kujitenga na wengine wote waliobaki. Ndoa ina taratibu zake Mkuu.Hakuna aina au namna yoyote ya ndoa inayotokana na kuishi na mwanamke au mwanaume kwa muda fulani. Dhanio la ndoa lililopo chini ya kifungu cha 160 cha Sheria ya Ndoa huwahusu wau waliohitilafiana na ambao waliishi kwa miaka miwili au zaidi.
Asante Petro E. Mselewa kwa ufafanuzi
Msingi wa swali langu ni kwamba mara nyungi nimewahi kusikia kuwa ukikaa/ishi na mwanamke kwa miezi sita mfululizo huhesabiwa kama ndoa na huyo mwanamke ana haki ya umiliki wa mali zote mlizochuma pamoja
Je kuna ukweli wowote katika madai haya kulingana na sheria hiyo?
 
Last edited by a moderator:
Petro E. Mselewa

Petro E. Mselewa

Verified Member
Joined
Dec 27, 2012
Messages
8,709
Points
2,000
Petro E. Mselewa

Petro E. Mselewa

Verified Member
Joined Dec 27, 2012
8,709 2,000
Asante Petro E. Mselewa kwa ufafanuzi
Msingi wa swali langu ni kwamba mara nyungi nimewahi kusikia kuwa ukikaa/ishi na mwanamke kwa miezi sita mfululizo huhesabiwa kama ndoa na huyo mwanamke ana haki ya umiliki wa mali zote mlizochuma pamoja
Je kuna ukweli wowote katika madai haya kulingana na sheria hiyo?
Hakuna ukweli wowote hapo Mkuu Daata. Kifungu cha 160 cha Sheria husika kinatoa Dhanio la Ndoa.Hili huwepo pale ambapo mwanamke na mwanaume huishi kama mke na mume kwa miaka miwili au zaidi.Wakati wa kuishi kwao na kupata heshima ya jamii kama mke na mume wanaweza kuchuma mali mbalimbali.Sasa katika kuhitilafiana kwao,mwanamke hataondoka mikono mitupu. Hiyo ni dhana tu ya Dhanio la Ndoa na hutumika hivyo na si vinginevyo
 
Makamee

Makamee

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2013
Messages
2,019
Points
1,250
Age
30
Makamee

Makamee

JF-Expert Member
Joined Nov 29, 2013
2,019 1,250
Sheria inazungumziaje uhusiano uliopo kati ya ndoa na talaka?
Talaka ni nini
Aina za talaka
Ipi talaka halali
 
S

Sangomwile

JF-Expert Member
Joined
Aug 17, 2012
Messages
3,083
Points
1,250
S

Sangomwile

JF-Expert Member
Joined Aug 17, 2012
3,083 1,250
Mkuu,naweza kuuliza kuhusu suala la mali kwa wanandoa?
 
Advocate J

Advocate J

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2012
Messages
3,890
Points
1,250
Advocate J

Advocate J

JF-Expert Member
Joined May 24, 2012
3,890 1,250
Wana-JF,karibuni hapa kwa maswali mbalimbali yahusuyo Sheria ya Ndoa,1971.Wale wote waliopo kwenye ndoa na wanaotarajia kuwa kwenye ndoa wanakaribishwa hapa kuuliza na kujibiwa. Nitashirikiana na Mawakili Wasomi wenzangu waliopo humu kuwajibu maswali yenu.

Mods, mnaweza kuufanya uzi huu kuwa 'sticky'? Asanteni na karibuni!
ahsante mkuu sasa hiyo sheria ya ndoa ya 1971 haina CAP? hebu naomba full citation mkuu
 
Petro E. Mselewa

Petro E. Mselewa

Verified Member
Joined
Dec 27, 2012
Messages
8,709
Points
2,000
Petro E. Mselewa

Petro E. Mselewa

Verified Member
Joined Dec 27, 2012
8,709 2,000
ahsante mkuu sasa hiyo sheria ya ndoa ya 1971 haina CAP? hebu naomba full citation mkuu
Mkuu Advocate J, full citation ni Law of Marriage Act, Cap.29 R.E.2002.Karibu tena Mkuu
 
Last edited by a moderator:
Petro E. Mselewa

Petro E. Mselewa

Verified Member
Joined
Dec 27, 2012
Messages
8,709
Points
2,000
Petro E. Mselewa

Petro E. Mselewa

Verified Member
Joined Dec 27, 2012
8,709 2,000
hivi mme akiwa na watoto wa nje,halafu mimi na yeye tumeoana tukiwa hatuna kitu,then tukafight tukawa matajiri,siku akifa je wanae wa nje wana haki ya kurithi na wanangu wa ndani ya ndoa?
Mkuu Victoire, kwanza yategemea namna ya ndoa iliyofungwa baina yenu.Kama ni ya kiislam,kwa mfano,watoto wa nje ya ndoa hawawezi kurithi. Kama ni ndoa ya kimila,yategemea mila za kabila lenu husika. Kama ni ndoa ya Bomani, yategemea na makubaliano yenu katika ndoa yenu.Hii ni kwakuwa,kifungu cha 58 cha Sheria ya Ndoa kinaruhusu uwepo wa Makubaliano juu ya umiliki wa mali za ndoa.Umiliki ndio unaelekeza urithi hapo baadaye.

Nataka nieleweke kuwa, kama mali ni binafsi kama inavyoruhusiwa chini ya vifungu vya 56 na 57,urithi waweza kufuata sheria,mila au Wosia.Lakini,kama ni mali ya pamoja watoto wa nje ya ndoa (kwa ndoa za bomani na za kikristo) hurithi kutokana na matakwa ya wanandoa tu na si vinginevyo.
 
Petro E. Mselewa

Petro E. Mselewa

Verified Member
Joined
Dec 27, 2012
Messages
8,709
Points
2,000
Petro E. Mselewa

Petro E. Mselewa

Verified Member
Joined Dec 27, 2012
8,709 2,000
Sheria inazungumziaje uhusiano uliopo kati ya ndoa na talaka?
Talaka ni nini
Aina za talaka
Ipi talaka halali

Kwanza,talaka ni mwisho wa ndoa.Pili,talaka hutolewa na Mahakama tu na si vinginevyo.Tatu, talaka ina taratibu zake.Kwa mfano,ni lazima kwa mwombaji wa talaka apitie katika Baraza la Usuluhishi la Ndoa kabla ya kwenda Mahakamani kudai talaka. Pia,Baraza husika lazima litoe kibali cha kushindwa kuwasuluhisha wanandoa hao ambao mmoja wao anataka kutalikiwa. Nne, talaka hutolewa tu pale ambapo ndoa hiyo itaonekana kuwa haiwezi tena kubaki a kurekebishika.

Kimsingi,Mahakama hulenga hasa katika kuilinda ndoa.Ndiyo maana,mwombaji wa talaka lazima athibitishe uwepo wa sababu za talaka kwa mfano mateso,kutelekezwa na uasherati wa mwenza wake.Ieleweke kuwa talaka zitolewazo kiislam ni hatua tu.Hii ni kwakuwa ni Sheria ya Ndoa tu ndiyo inayotumika katika suala hilo.
 
Forum statistics

Threads 1,295,911
Members 498,475
Posts 31,227,877
Top